Prigozhin awaambia mamluki wa Wagner kurejea kambini 'kuepuka umwagaji damu'

Vikosi vya Wagner vimesitisha hatua ya kusonga mbele huko kuelekea Moscow

Moja kwa moja

Ambia Hirsi and Abdalla Seif Dzungu

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja. Kwaheri.

  2. Habari za hivi punde, Prigozhin awaambia mamluki wa Wagner kurejea kambini 'kuepuka umwagaji damu'

    TH

    Chanzo cha picha, Reuters

    Vikosi vya Wagner vimesitisha hatua ya kusonga mbele kuelekea Moscow.

    Kiongozi wa mamluki wa Wagner Yevgeny Prigozhin ametuma ujumbe kwenye kituo chake cha Telegram akisema amekubali "kusimamisha" harakati za wanajeshi wake wanaosonga mbele kuelekea mji mkuu wa Urusi.

    Rais wa Prigozhin na Belarus walikubali 'kupunguza hali ya taharuki'

    Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amefanya mazungumzo na mkuu wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin wakati ambapo Prigozhin alikubali kusimamisha wanajeshi wake na "kuondoa hali hiyo," kituo cha habari cha Rossiya 24 kilisema.

    "Prigozhin alikubali pendekezo la Lukashenko la kusimamisha harakati za Wagner katika eneo la Urusi na kwa hatua zaidi za kupunguza mvutano," Rossiya 24 ilisema, ikinukuu huduma ya vyombo vya habari ya Lukashenko.

    Pia ilisema ilikuwa inathibitisha "inawezekana kupata njia inayokubalika ya kupunguza [hali] kwa hakikisho la usalama kwa wapiganaji wa Wagner PMC".

    Rossiya 24 ilisema mazungumzo hayo yamekubaliwa na Putin.

    Mamluki walifika ndani ya kilomita '200 kutoka Moscow'

    Imekuwa ni nusu saa ya kushangaza na habari za ghafla kwamba askari wa Wagner wataacha kuelekea hadi Moscow.

    Hii hapa taarifa kamili kutoka kwa mkuu wa Wagner, Yevgeny Prigozhni:

    "Walitaka kuvunja kampuni ya kijeshi ya Wagner. Tulianza maandamano ya haki tarehe 23 Juni.

    Katika masaa 24, tulifika ndani ya kilomita 200 kutoka Moscow.Kwa wakati huu hatukumwaga hata tone moja la damu ya wapiganaji wetu.

    Sasa wakati umefika ambapo damu inaweza kumwagika.Kuelewa wajibu [kwa uwezekano ] kwamba damu ya Warusi itamwagika upande mmoja, tunageuza misafara yetu na kurudi kwenye kambi kama ilivyopangwa."

    Kauli ya Prigozhni imetazamwa kwenye chaneli yake ya Telegram zaidi ya mara milioni tatu.

    Pia unaweza kusoma:

    • Putin aapa kuwaadhibu mamluki wa Wagner wanaotuhumiwa kwa uasi
    • "Sote 25,000 tuko tayari kufa" - Prigozhin
    • Je, haya ni mapinduzi? Prigozhin anafanya nini nchini Urusi?
    • Fahamu mzozo unaoendelea kati ya Wagner na Wizara ya Ulinzi ya Urusi
  3. Habari za hivi punde, Wakazi wa Moscow watahadharishwa, huku mamluki wa Wagner wakielekea mji mkuu wa Urusi

    Meya wa Moscow

    Chanzo cha picha, EPA

    Meya wa Moscow, Sergei Sobyanin, ameweka ujumbe kwenye mtandao wa Telegram kutangaza kwamba "operesheni ya kukabiliana na ugaidi imeanzishwa katika jiji la Moscow" na kwamba Jumatatu watu "hawataenda kazini" ili "kupunguza hatari".

    Ametoa wito kwa wakazi wa Moscow "kujizuia kutembea jijini".

    "Huduma za jiji ziko katika hali ya tahadhari," alisema.

    Mamluki wa Wagner wameoonekana kuhamia kaskazini kutoka mikoa ya kati ya Urusi, kuelekea mji mkuu.

    Meya huyo pia amesema "Hali ni ngumu," katika taarifa yake iliyotumwa kwenye Telegram.

    Aliongeza kuwa huenda baadhi ya barabara au vitongoji vya jiji hili zikafungwa.

    ''Operesheni ya kukabiliana na ugaidi'' iliyotangazwa hapo awali na mamlaka ya Urusi katika jiji la Moscow, mkoa wa Moscow, na mkoa wa Voronezh kuelekea kusini, inaipa mamlaka maalum ikiwa ni pamoja na:

    • Kudhibiti shughuli za watu na usafiri
    • Kufuatilia au kuzuia mawasiliano
    • Haki ya kukamata watu na magari
    • Kuhamisha watu ikiwa inahitahajika kufanya hivyo

    Pia unaweza kusoma:

    • Putin aapa kuwaadhibu mamluki wa Wagner wanaotuhumiwa kwa uasi
    • "Sote 25,000 tuko tayari kufa" - Prigozhin
    • Je, haya ni mapinduzi? Prigozhin anafanya nini nchini Urusi?
    • Fahamu mzozo unaoendelea kati ya Wagner na Wizara ya Ulinzi ya Urusi
  4. Latvia yafunga mpaka na Urusi

    Ulimengu unafuatilia kwa karibu mzozo unaofukuta nchini Urusi - majirani zake wa karibu wakichukua hatua madhubuti.

    Latvia - ambayo ilishuhudia mmiminiko wa wakimbizi wa Urusi wakati vita nchini Ukraine vilipoanza mwaka jana - imefunga mpaka wake na Urusi.

    Katika ujumbe wa Twitter, Waziri wa Mambo ya Nje alisema mtu yeyote anayekuja "kutokana na matukio ya sasa" hataruhusiwa kuingia.

    Estonia pia imesema inaimarisha usalama katika mpaka wake, huku Waziri Mkuu Kaja Kallas akiongeza kuwa "anawasiliana kwa karibu" na wenzake wa Latvia, Lithuania na Finland.

    Nchi zingine - ikiwa ni pamoja na Poland, Uingereza na Marekani - pia zimesema zinafuatilia kwa karibu hali hiyo.

    Ramani
  5. Ramani ya Urusi: Ni maeneo yapi yanayokumbwa na uasi wa mamluki?

    Ramani

    Kiongozi wa kundi lenye nguvu la mamluki la Wagner, Yevgeny Prigozhin, ametoa wito wa uasi nchini Urusi na kuzindua kile anachokiita "maandamano ya haki".

    Wizara ya Ulinzi ya Uingereza (MoD) inasema wapiganaji wake "bila shaka wanalenga kufika Moscow".

    Inasema kwamba mapema za Jumamosi, vikosi vya Wagner vilivuka mpaka kutoka Ukraine, ambako wamekuwa wakipigana upande wa Warusi, na kuchukua udhibiti wa mji wa Rostov-on-Don.

    Hili ni tatizo kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin na vita vyake, kwani ni makao makuu ya uvamizi wa Urusi huko Ukraine - kamandi ya Urusi ya Wilaya ya Kijeshi ya Kusini - iko katika jiji hilo.

    Vyanzo vya habari vya BBC Idhaa ya Kirusi pia vinasema mamluki wa Wagner wameteka vituo vya kijeshi huko Voronezh, ambayo ni nusu kati ya Rostov na Moscow - mlipuko mkubwa umesikika karibu na jiji hilo.

    Katika dakika chache zilizopita, kitengo chetu BBC kimethibitisha video inayoonyesha msafara wa magati ya Wagner yakisafiri kwenye barabara kuu ya M4, inayounganisha Voronezh na Moscow kupitia eneo la Lipetsk.

    Maelezo zaidi:

    • Putin aapa kuwaadhibu mamluki wa Wagner wanaotuhumiwa kwa uasi
    • "Sote 25,000 tuko tayari kufa" - Prigozhin
    • Je, haya ni mapinduzi? Prigozhin anafanya nini nchini Urusi?
    • Fahamu mzozo unaoendelea kati ya Wagner na Wizara ya Ulinzi ya Urusi
  6. Wanajeshi wa Urusi washambulia msafara wa Wagner, Prigozhin asema

    BBC

    Kiongozi wa kundi la Wagner Yevgeny Prigozhin amelishutumu jeshi la Urusi kwa kushambulia wapiganaji wake wanaosonga mbele.

    Katika chapisho lililopita (hapa chini), tuliripoti juu ya msafara wa Wagner ambao ulionekana kaskazini mwa Voronezh, jiji ambalo Wagner ameripotiwa kuteka vituo vya kijeshi.

    "Tulifyatuliwa risasi: kwanza mizinga ya risasi, na kisha kutoka kwa helikopta," Prigozhin alisema katika chapisho la Telegraph, bila kutoa ushahidi au kubainisha ni wapi shambulio linalodaiwa lilitokea.

    Pia unaweza kusoma:

    • Putin aapa kuwaadhibu mamluki wa Wagner wanaotuhumiwa kwa uasi
    • "Sote 25,000 tuko tayari kufa" - Prigozhin
    • Je, haya ni mapinduzi? Prigozhin anafanya nini nchini Urusi?
    • Fahamu mzozo unaoendelea kati ya Wagner na Wizara ya Ulinzi ya Urusi
  7. Habari za hivi punde, Msafara wa Wagner waonekana katika mkoa wa kusini mwa Moscow

    Wagner

    Chanzo cha picha, Twitter

    Kitengo chetu cha BBC Verify kimethibitisha video inayoonyesha msafara wa magari yenye silaha ya mamluki wa Wagner yakisafiri kwenye barabara kuu ya M4, inayounganisha Voronezh na Moscow kupitia eneo la Lipetsk

    Picha hiyo hapo juu imechukuliwa kutoka kwa video. Kama tulivyoripoti hapo awali, gavana wa mkoa wa Lipetsk amewataka wakazi kusalia majumbani na kusitisha safiri, iwe ni kutumia magari ya umma au ya kibinafsi.

    Mamlaka za mkoa huko Lipetsk zimesema kuwa huduma zote za basi katika mkoa huo zimehairishwa hadi hali itakapokuwa shwari.

    Voronezh ni moja ya miji miwili - mwingine ukiwa Rostov-on-Don, kusini ya mbali - ambapo mamluki wa Wagner wameripotiwa kuteka maeneo muhimu.

    Matukio katika eneo hilo yananabadikika kwa kasi. Tutakuletea habari zaidi pindi tutakapozipokea.

    Pia unaweza kusoma:

    • Putin aapa kuwaadhibu mamluki wa Wagner wanaotuhumiwa kwa uasi
    • "Sote 25,000 tuko tayari kufa" - Prigozhin
    • Je, haya ni mapinduzi? Prigozhin anafanya nini nchini Urusi?
    • Fahamu mzozo unaoendelea kati ya Wagner na Wizara ya Ulinzi ya Urusi
  8. 'Unadhani ni nini kinaweza kutokea' - majibu ya baadhi ya wakazi wa Moscow

    Usalama umeimarishwa mjini Moscow, huku magari ya kivita yakionekana mitaani.

    Lakini je, wakazi wa Moscow wanasemaje kuhusu yale yanayojiri mjini humo?

    Haya hapa ni baadhi ya maoni

    Nikolai

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Nikolai
    Galina

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Galina
    Sergei

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Sergei
  9. Udhaifu wa Urusi uko wazi - Zelensky

    Volodymyr Zelensky

    Chanzo cha picha, Ukrainian Handout

    Maelezo ya picha, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky

    Sasa tunaelekee nchini Ukraine, ambako Rais Volodymyr Zelensky ametoa kauli yake kuhusiana na matukio ya hivi punde nchini Urusi.

    Zelensy, ameweka ujumbe kwenye mtandao wake wa Telegram, anasema mtu yeyote "anayechagua njia ya uovu hujiangamiza", na kwamba "udhaifu wa Urusi ni dhahiri".

    Ingawa hakumtaja Rais wa Urusi Putin kwa jina, Zelensky anaonekana kumkosoa kiongozi huyo wa Urusi kwa "kuwaingiza maelfu ya watu" vitani.

    Kadiri Urusi inavyoendelea kuwaweka wanajeshi wake na mamluki nchini Ukraine, "ndivyo itakavyokumbwa na machafuko," Zelensky anasema.

  10. Kiongozi wa Wagner Prigozhin amjibu Putin

    Prigozhin

    Chanzo cha picha, Reuters

    Ujumbe wa sauti sasa umechapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Telegram wa kundi la Wagner.

    Unaonekana kuwa jibu la moja kwa moja na la dharau kutoka kwa Yevgeny Prigozhin, mkuu wa kikundi cha mamluki, mara baada ya hotuba ya awali ya Rais Vladimir Putin.

    Sauti ya kiume inayofanana na ya Prigozhin inasikika ikisema: "Kuhusu uhaini wa nchi, rais alikosea sana. "Sisi ni wazalendo wa nchi yetu, tumekuwa tukipigana na tunapigana hata sasa.

    "Na hakuna mtu atafanya - kama anavyotaka rais, FSB (huduma ya usalama ya Urusi) au mtu mwingine yeyote - tukubali makosa yetu.

    "Kwa sababu hatutaki nchi yetu iendelee kuishi katika ufisadi, uwongo na urasimu."

    Katika hotuba yake Jumamosi asubuhi, Putin alishutumu Wagner kwa uhaini mkubwa.

    Soma:

    • Putin aapa kuwaadhibu mamluki wa Wagner wanaotuhumiwa kwa uasi
    • "Sote 25,000 tuko tayari kufa" - Prigozhin
    • Je, haya ni mapinduzi? Prigozhin anafanya nini nchini Urusi?
    • Fahamu mzozo unaoendelea kati ya Wagner na Wizara ya Ulinzi ya Urusi
  11. Ni nini kimechochea uasi nchini Urusi

    Wapiganaji wa Wagner wamesimama karibu na gari la kivita huko Rostov-on-Don

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wapiganaji wa Wagner wamesimama karibu na gari la kivita huko Rostov-on-Don

    Mamlaka nchini Urusi na mkuu wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin zinaonyesha haziko tayari kulegeza kamba katika mzozo ambao sasa unaelekea kutishia nchi hiyo.

    Lakini uasi huu umechochewa na nini?

    Mara kwa mara Prigozhin amemwelekezea lawama Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu vikosi vya jeshi la nchi hiyo vikishindwa kwenye uwanja wa vita huko Ukraine.

    "Vita vilihitajika... ili Shoigu aweze kuwa mkuu wa jeshi, ili aweze kuwa shujaa wa pili ... vita havikuwa vya kudhibiti shughuli za kijeshi au kuiondoa Ukraine. Ilihitajika kwa malengo ziada," Prigozhin alisema.

    Pia alilaumu vita dhidi ya watu mashuhuri wa Urusi, akilaani "ukoo ambao kiuhalisia unatawala Urusi leo".

    Kauli yenye utata inaonekana kuwa madai ya Prizoghin kwamba kambi ya Wagner nchini Ukraine ilishambuliwa na jeshi la Urusi mapema wiki hii.

    Wizara ya Shoigu inakanusha hili. Wachambuzi wa Kremlin pia wanaashiria chuki ya kibinafsi ya muda mrefu kati ya Prigozhin na Shoigu, ambao majenerali wao wanamwona mkuu wa Wagner kama mgeni mwenye uchu wa madaraka.

    Lakini mpaka sasa, Prigozhin - aliyepewa jina la utani "mpishi wa Putin" kwa mikataba ya upishi ya zamani kutoka Kremlin - haijaelekeza changamoto ya moja kwa moja kwa utawala wa Putin.

    • Je, haya ni mapinduzi? Prigozhin anafanya nini nchini Urusi?
    • Fahamu mzozo unaoendelea kati ya Wagner na Wizara ya Ulinzi ya Urusi
    • Yevgeny Prigozhin: Je ni nani huyu mshirika wa Putin na mwanzilishi wa kundi la Wagner ?
  12. "Tuko tayari kufa" - Kiongozi wa kundi la Wagner Yevgeny Prigozhin

    Yevgeny Prigozhin amesema yeye na vikosi vyake "wako tayari kufa" kama sehemu ya hatua yake

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Yevgeny Prigozhin amesema yeye na vikosi vyake "wako tayari kufa" kama sehemu ya hatua yake

    Katika ujumbe uliotumwa kwenye mtandai wa Telegram Jumamosi asubuhi, Yevgeny Prigozhin alisema kwamba wanachama wote wa kundi lake la mamluki la Wagner walikuwa "tayari kufa" katika hatua yake dhidi ya jeshi la Urusi.

    "Sote tuko tayari kufa. Wote 25,000, na wengine 25,000," alisema katika ujumbe wa sauti, akiongeza hatua hiyo inachukuliwa "kwa niaba ya watu wa Urusi".

    Pia unaweza kusoma:

    • Putin aapa kuwaadhibu mamluki wa Wagner wanaotuhumiwa kwa uasi
    • "Sote 25,000 tuko tayari kufa" - Prigozhin
    • Je, haya ni mapinduzi? Prigozhin anafanya nini nchini Urusi?
    • Fahamu mzozo unaoendelea kati ya Wagner na Wizara ya Ulinzi ya Urusi
  13. Yevgeny Prigozhin ni nani?

    Yevgeny Prigozhin (kushoto) akimkabidhi chakula Rais wa Urusi Vladimir Putin

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Yevgeny Prigozhin (kushoto) akimpa chakula Rais wa Urusi Vladimir Putin

    Yevgeny Prigozhin leo anagonga vichwa vya habari. Kufuatia miezi kadhaa ya kutoridhika na jinsi vita vya Ukraine vinavyoendeshwa, ametoa wito wa uasi dhidi ya jeshi - ingawa amekanusha jaribio la mapinduzi.

    Lakini yeye ni nani, na kwa nini ni muhimu sana?

    Ameibuka kama mhusika mkuu katika uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine, akisimamia jeshi la kibinafsi la mamluki - linalofahamika kama Kundi la Wagner - linaloongoza mashambulizi ya Urusi katika maeneo muhimu ya vita.

    Anatoka St Petersburg, mji wa nyumbani kwa Vladimir Putin.

    Kufuatia kifungo cha muda gerezani kwa wizi, Prigozhin alianzisha maduka mengi ya kuuza mbwa huko St Petersburg.

    Biashara ilifanya vizuri na ndani ya miaka michache, katika miaka ya 1990 Prigozhin aliamua kufungua migahawa ya mikubwa katika jiji hilo.

    Baadaye, kampuni ya upishi ya Prigozhin ya Concord ilipewa kandarasi ya kupeleka chakula Kremlin, na ikampa jina la utani "mpishi wa Putin".

    Baada ya miaka ya kukanusha uwepo wa kundi la Wagner, tarehe 27 Julai 2022 vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na Kremlin vilikiri ghafla kwamba ilikuwa ikipigana mashariki mwa Ukraine.

  14. Putin aapa kuwaadhibu mamluki wa Wagner wanaotuhumiwa kwa uasi

    Putin

    Chanzo cha picha, EPA/Shutterstock

    Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya kuwa "adhabu isiyoepukika" itachukuliwa dhidi ya wale wanaogawanya jamii ya Urusi na kuongeza vikosi vya kukabiliana na ugaidi sasa viko katika mji mkuu wa Moscow na mikoa mingine kadhaa nchini humo.

    Katika hotuba yake kwa taifa kupitia Televisheni,Rais Putin anasema mustakabali wa Urusi uko hatarini, akielezea vitendo vya waasi kama "usaliti".

    Bila kumtaja kiongozi wa kundi la Wagner Yevgeny Prigozhin, Putin anasema "matamanio" makubwa ya baadhi ya watu yamesababisha "uhaini mkubwa".

    Kiongozi huyo anasema baadhi ya Warusi "wamedanganywa na kuingizwa katika tukio la uhalifu" - bila kutaja wapiganaji waasi wa Wagner.

    Maelezo zaidi:

  15. Mvutano unatokea wapi?

    Rostov-on-Don, ambapo magari ya kijeshi ya kivita yameonekana mitaani, iko zaidi ya kilomita 1,100 (maili 680) kusini mwa Moscow.

    Yevgeny Prigozhin, mkuu wa kundi la mamluki la Wagner, anasema vikosi vyake sasa vinaudhibiti mji huo.

    Wakazi wa eneo la Rostov linalopakana na Ukraine wametakiwa kusalia majumbani kwa sababu vikosi vya usalama vinafanya kazi katika eneo hilo.

    Ramani

    Mkuu wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin ameapa kuondoa uongozi wa jeshi la Urusi na kusema kuwa vikosi vyake vimevuka hadi Urusi kutoka Ukraine.

  16. Habari za hivi punde, Putin kuhutubia taifa

    Rais wa Urusi Vladimir Putin anatarajiwa kulihutubia taifa kwa njia ya televishenimuda mfupi ujao, shirika la habari la Tass limemnukuu msemaji wa Kremlin akisema.

  17. Katika picha: Wapiganaji wa kundi la Wagner mjini Rostov-on-Don kusini mwa Urusi

    Wagner

    Chanzo cha picha, Reuters

    Shirika la habari la Reuters limewasilisha baadhi ya picha za wapiganaji wa Wagner katika mji wa kusini mwa Urusi wa Rostov-on-Don, ambao kiongozi wa Wagner Yevgeny Progozhin anasema majeshi yake sasa yanaudhibiti.

    Wagner

    Chanzo cha picha, Reuters

    Wagner

    Chanzo cha picha, Reuters

    Wagner

    Chanzo cha picha, Reuters

  18. Hatua za usalama zawekwa mjini Moscow, mkuu wa Wagner ashutumiwa kwa uasi

    Meya wa jiji la Moscow ametangaza hatua za kupambana na ugaidi zinachukuliwa ili kuimarisha usalama katika mji mkuu.

    Katika chapisho kwenye Telegram Sergey Sobyanin aliandika: "Kuhusiana na yale yanayojiri, hatua za kupambana na ugaidi zinachukuliwa huko Moscow zinazolenga kuimarisha hatua za usalama.

    "Udhibiti wa ziada wa barabara umeanzishwa.

    "Hali hii inaweza kuathiri shughuli za umma. Tafadhali zingatia hatua zilizochukuliwa kwa makini."

    Maelezo zaidi:

  19. Hujambo na karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumamosi 24.06,2023.