Rais Museveni apitisha sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja Uganda
Spika wa Bunge la Uganda ametangaza kuwa Rais Museveni ameutia saini muswada wa kupinga mapenzi ya jinsia moja kuwa sheria.
Moja kwa moja
Mapambano yajitokeza Sudan kabla ya kusitishwa kwa mapigano,

Chanzo cha picha, AFP
Kumekuwa na mapigano makali nchini Sudan, saa chache kabla ya kumalizika kwa usitishaji mapigano wa siku saba ambao umekuwa ukivunjwa mara kwa mara.
Wakazi wa kusini na magharibi mwa Omdurman, karibu na mji mkuu Khartoum wanasema jeshi na vikosi pinzani vya Rapid Support Forces vimekuwa vikishambuliana kwa lengo la kupata eneo.
Marekani na Saudi Arabia ambao walianzisha mapatano hayo wamezitaka pande zote mbili kusaini kuongeza muda.
Umoja wa Mataifa na mashirika ya misaada yanasema yamejitahidi kupata vibali vya dhamana ya usalama kusafirisha misaada inayohitajika kote nchini.
Takribani watu milioni 1.4 wamelazimika kuyahama makazi yao tangu vita vilipozuka wiki sita zilizopita.
Bola Tinubu: Rais mpya wa Nigeria afutilia mbali ruzuku ya mafuta

Chanzo cha picha, Reuters
Rais mpya wa nchi yenye demokrasia kubwa zaidi barani Afrika, Nigeria, ametumia hotuba yake ya kuapishwa kutoa tangazo kubwa la sera.
Bola Tinubu, 71, alishinda uchaguzi ulizua pingamizi wa Februari kwa ahadi ya kurejesha matumaini - lakini anakabiliwa na changamoto ngumu za kiuchumi na kiusalama.
Alitangaza kumalizika kwa ruzuku ya miongo kadhaa kwa bidhaa za petroli.
"Ruzuku ya mafuta imetoweka," aliuambia umati uliojaa katika mji mkuu, Abuja.
Haijabainika ni lini sera ya petroli itaanza kutekelezwa lakini kukomesha ruzuku kutasababisha kupanda kwa bei ya petroli na kunaweza kuwa na athari kwa bei za bidhaa nyingine.
Bw Tinubu aliapishwa katika hafla iliyofanyika katika mji mkuu, Abuja baada ya kushinda uchaguzi wa Februari.
Anachukua hatamu kutoka kwa Rais wa mihula miwili Muhammadu Buhari huku kukiwa na mfumuko wa bei ya juu, viwango vya juu vya deni na kuongezeka kwa visa vya utekaji nyara kwa ajili ya fidia.
Ushindi wa Bw Tinubu unapingwa mahakamani na wapinzani wake wawili wa karibu.
Wanasema matokeo yalibadilishwa.
Lakini Bw Tinubu, ambaye alisema "ananyoosha mkono wake katika kumaliza mgawanyiko wa kisiasa", alitaja uchaguzi huo kuwa uliokuwa vita vikali na kusema ulikuwa wa ubora zaidi kuliko ule wa awali.
Viongozi kutoka bara zima wakiwemo marais Paul Biya wa Cameroon, Macky Sall wa Senegal na Mohamed Bazoum wa Niger walikuwa kwenye sherehe hiyo.
Bw Tinubu anaweza kuwa na muda mchache wa kusherehekea.Wananchi wa Nigeria wanatarajia hatua za haraka.
Mfumuko wa bei unaendelea kwa kiwango cha juu zaidi kwa karibu miaka 18, mtu mmoja kati ya watatu hawana ajira na pato la sekta muhimu ya mafuta linapungua.
Atalazimika kuchukua hatua za haraka katika maeneo yote ili kuwashawishi watu ambao hawakumpigia kura kuwa yuko tayari kutekeleza majukumu yake.
Alikubali haya katika hotuba yake, akisema timu yake itatoa ramani yake ya kiuchumi baada ya wiki lakini alisema kuwa viwango vya riba vilikuwa vya juu sana.
Pia alisema wanawake na vijana watajitokeza sana katika utawala wake na kudokeza kuajiri askari zaidi wa usalama ili kukabiliana na changamoto za nchi.
Kama gavana wa awamu mbili wa Lagos, alifufua kituo cha kibiashara cha Nigeria - hakuna kazi rahisi - na anafahamu vyema masuala hayo.
Lakini wapinzani wa rais huyo mpya wanasema amepoteza msisimko wake aliokuwa akiutumia kuifanya Lagos kuwa ya kisasa.
Tangu uchaguzi ufanyike amesafiri nje ya nchi mara mbili, hivyo kuzua maswali kuhusu afya yake.Mnamo 2021 alitumia miezi kadhaa huko London akitibiwa ugonjwa ambao haukutajwa.
Amepuuzilia mbali ukosoaji huo, akisema kazi hiyo haihitaji uthabiti wa mwanariadha wa Olimpiki - na washirika wake ni wepesi kukumbusha kila mtu kwamba Rais wa Marekani Joe Biden ni mzee, ana miaka 80.
Lakini ikiwa wagombea walioshika nafasi ya pili na ya tatu - Atiku Abubakar na Peter Obi - katika uchaguzi wa urais wa Februari watafaulu katika mkondo wanaochukua basi Bw Tinubu huenda asiwe madarakani kwa muda mrefu.
Mahakama ya uchaguzi inatarajiwa kuanza kusikiliza hoja kuu siku ya Jumanne na matokeo ya kesi hiyo yanapaswa kujulikana ndani ya miezi sita ijayo.
Unaweza pia kusoma:
- Kuapishwa kwa Tinubu: Changamoto tano zinazomsubiri rais mpya wa Nigeria
Mauaji ya Delhi: Mwanaume ashikiliwa baada ya kumuua msichana kikatili hadharani

Maelezo ya picha, Picha za CCTV za uhalifu huo zilisambaa Polisi katika mji mkuu wa India, Delhi, wamemkamata kijana mwenye umri wa miaka 20 kwa kumdunga kisu kikatili na kumuua rafiki wa kike mwenye umri wa miaka 16 hadharani.
Picha za shambulio hilo zinaonyesha mwanamume huyo akimdunga kisu msichana mara kadhaa na kumponda kichwa kwa jiwe kubwa.
Video hiyo, ambayo imesambaa mitandaoni na kusababisha hasira nchini India, inaonyesha watu wengi wakitazama shambulio hilo au wakitembea.
Polisi wamewahusisha kimapenzi wanandoa hao na kusema walizozana saa kadhaa kabla ya mauaji siku ya Jumapili.
Msichana huyo alikuwa anaenda kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa kwa mtoto wa rafiki yake aliposhambuliwa, afisa mkuu wa polisi Ravi Kumar Singh aliambia shirika la habari la ANI.
Alimtaja mshukiwa kuwa ni Sahil na akasema alikamatwa kutoka karibu na wilaya ya Bulandshahr katika jimbo jirani la Uttar Pradesh.
Bw Singh aliongeza kuwa uchunguzi unaendelea na kwamba polisi hawakuweza kufichua maelezo zaidi kwa sasa.
Baada ya kusambaa kwa video za mauaji hayo ya kutisha, wengi walijitokeza kwenye mitandao ya kijamii kueleza hasira na ghadhabu.
Hashtagi kama vile mauaji ya Delhi na uhalifu wa Delhi zilikuwa zikivuma kwenye Twitter pamoja na Shahbad Dairy, jina la eneo ambalo uhalifu ulitokea.
Katika ujumbe wa Twitter , Waziri Mkuu wa Delhi Arvind Kejriwal alielezea mauaji hayo kama "ya kusikitisha sana" na akasema kwamba "wahalifu wamekuwa hawaogopi, hakuna hofu ya polisi".
Marekani yafutilia mbali viza ya Spika wa Bunge la Uganda kuhusu sheria dhidi ya mapenzi ya jinsia moja

Chanzo cha picha, Anita Annet Among/Twitter
Marekani imefutilia mbali visa vya Spika wa Bunge la Uganda, Anita Among huku mbunge Asuman Basalirwa akisema yeye ndiye mwathirika wa kwanza wa uwezekano wa kuwekewa vikwazo baada ya taifa hilo la Afrika Mashariki kuhalalisha sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja , LGBTQ.
"Viza ya sasa ya spika imefutwa na hii inathibitishwa katika barua pepe," Basalirwa ambaye aliwasilisha Mswada huo alisema.
Akinukuu barua pepe hiyo muda mfupi baada ya kujulikana kuwa Rais Museveni alipuuzilia mbali shinikizo la nchi za Magharibi na mashirika ya kutetea haki za binadamu kusaini Mswada wa kupinga mapenzi ya jinsia moja kuwa sheria, Basalirwa aliongeza kuwa:
"Serikali ya Marekani imebatilisha viza yako (Among) ya sasa kuhusu taarifa zilizopatikana baada ya kutolewa kwako mara ya mwisho," alisema alipokuwa akionyesha chapisho la barua hiyo kwa waandishi wa habari Bungeni.
"Kuanzia Mei 12, 2023, wewe (Among) huna viza halali ya Marekani ingawa unakaribishwa kutuma ombi tena," alisema alipokuwa akionyesha chapisho la barua hiyo kwa wanahabari bungeni.
Kulingana na Basalirwa, spika amehimizwa kupeleka paspoti yake kwa Ubalozi wa Marekani kupitia wizara ya fedha kwa ajili ya marekebisho muhimu ya viza yake.
"Nadhani walikuwa wanatafuta visa yangu ya Marekani lakini hawakuipata.Kwa hivyo, mwathiriwa wa kwanza ni spika,” Mbunge huyo wa Manispaa ya Bugiri aliona.
Chini ya sheria mpya, wale wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wanakabiliwa na adhabu kali ambazo zinaweza kujumuisha kifungo cha maisha.
Mapema Jumatatu, Among alikuwa ameweka wazi kwamba "Bunge litasimamia na kuendeleza maslahi ya watu wa Uganda daima."
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Hospitali ya Afrika Kusini yachunguzwa kwa kuwaweka watoto wachanga kwenye masanduku ya boksi
Mamlaka ya Afrika Kusini inachunguza tukio ambapo watoto wachanga waliwekwa kwenye masanduku ya kadibodi, badala vitanda maalum vya watoto wachanga katika jimbo la Kaskazini Magharibi.
Tukio hilo katika sehemu ya watoto wachanga katika Hospitali ya Mkoa wa Mahikeng lilidhihirika siku ya Jumamosi baada ya chapisho la Facebook kuonyesha watoto wakiwa wamevikwa blanketi za hospitali za zambarau na mirija ya puani na kuwekwa kwenye masanduku ya kahawia, vyombo vya habari vya ndani vilisema.
Mkuu wa afya Kaskazini Magharibi Madoda Sambatha alisema wanachunguza suala hilo ili kubaini ni muda gani watoto hao walikaa kwenye masanduku hayo.
Bw Sambatha aliomba msamaha na akaomba utulivu wakati suala hilo likichunguzwa.
Alisema, kwa dharura, utaratibu ulifanywa ili vitanda vya ziada vipelekwe hospitalini.
Meneja wa hospitali hiyo ameripotiwa kusimamishwa kazi.
Waziri wa Afya Joe Phaahla mnamo Jumatatu alielezea tukio hilo kama usimamizi duni wa wale wanaosimamia kituo hicho.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Vita vya Ukraine: Mashambulizi mapya dhidi ya Kyiv baada ya mashambulizi makali ya droni

Chanzo cha picha, VITALI KLITSCHKO
Makombora ya Urusi yamepiga mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, kufuatia mashambulio makali ya ndege zisizo na rubani kwa siku mbili.
Yote yameripotiwa kupigwa risasi na hakuna taarifa za majeruhi.
Vifusi vinavyowaka moto kutoka kwa makombora yaliyozuiliwa vilitua katika maeneo ya makazi katikati mwa Kyiv.
Urusi imeanzisha mashambulizi 16 ya anga kwenye mji mkuu wa Ukraine mwezi huu.La hivi punde, hata hivyo, halikuwa la kawaida kwa sababu lilifanyika mchana - na lilionekana kulenga katikati mwa jiji.
Mashambulizi mengine yote ya anga kwenye mji mkuu hadi sasa mnamo Mei yamefanyika usiku na yalionekana kuelekezwa katika miundombinu muhimu ya kitaifa na ulinzi wa anga nje kidogo.
Msemaji wa Jeshi la Wanahewa Yuri Ihnat alisema kuwa makombora ya balistiki ya Iskander yalitumiwa katika shambulizi la hivi punde na kwamba inawezekana makombora ya S-300 na S-400 pia yalirushwa.
Ving'ora vya mashambulizi ya anga viliripotiwa pia katika maeneo mengine kadhaa ya Ukraine.
Makamanda wa kijeshi wa eneo la Kyiv waliishutumu Urusi kwa kubadilisha mbinu zake na kuwalenga raia kimakusudi.Inaonekana kwamba Moscow inataka kuongeza shinikizo lake kwa Ukraine hata zaidi kabla ya mashambulizi yoyote ya kukabiliana nayo.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Rais Museveni apitisha sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja Uganda

Chanzo cha picha, Uganda State House
Spika wa Bunge la Uganda ametangaza kuwa Rais Museveni ameutia saini muswada wa kupinga mapenzi ya jinsia moja kuwa sheria.
Spika Anita Among , amesema Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, ametekeleza majukumu yake ya kikatiba kama ilivyoainishwa na Ibara ya 91 (3) (a) ya Katiba. Ameidhinisha Sheria ya Kupinga mapenzi ya jinsia moja, aliandika katika taarifa yake aliyoituma kwenye mtandao wa Twitter.
''Kama Bunge la Uganda, tumejibu kilio cha wananchi wetu. Tumetunga sheria ili kulinda utakatifu wa familia kulingana na Kifungu cha 31 cha Katiba ya Uganda''.
''Tumesimama kidete kutetea utamaduni wetu na matarajio ya watu wetu kulingana na malengo ya 19 & 24 ya malengo ya kitaifa na kanuni za maagizo ya sera ya serikali. Namshukuru Mheshimiwa Rais, kwa hatua yake thabiti kwa maslahi ya Uganda.'', aliandika Spika Anita Among.
Aliongeza kuwa ''Kwa Mungu na Nchi yangu, Daima tutasimamia na kuendeleza maslahi ya watu wa Uganda''
Aliwashukuru wananchi wa Uganda kwa ''maombi na kutia moyo tulipotekeleza wajibu wetu'' kwa mujibu wa Ibara ya 1 na 79 ya Katiba.
Amewataka watekelezaji kutekeleza mamlaka waliyopewa kisheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja.
Ikulu ya Uganda katika ukurasa wake wa Twitter imetuma picha ya Museveni kuthibitisha kuwa rais huyo ametia saini muswada:
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Je Muswada dhidi ya wapenzi wa jinsia moja unasemaje?
Uhusiano wa jinsia moja umeharamishwa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Lakini mswada wa Kupinga mapenzi ya jinsia moja unalenga kwenda mbali zaidi na kuwafanya watu kuwa wahalifu kwa msingi wa utambulisho wao wa kijinsia.
- Mtu anayepatikana na hatia ya kulea au kusafirisha watoto kwa madhumuni ya kuwashirikisha katika vitendo vya wapenzi wa jinsia moja anakabiliwa na kifungo cha maisha jela.
- Watu binafsi au taasisi zinazounga mkono au kufadhili shughuli au mashirika ya haki za LGBT, au kuchapisha, kutangaza na kusambaza nyenzo na fasihi za vyombo vya habari vinavyounga mkono wapenzi wa jinsia moja, pia watakabiliwa na mashtaka na kufungwa gerezani.
Chini ya sheria iliyopendekezwa, marafiki, familia na wanajamii watakuwa na wajibu wa kuripoti watu walio katika mahusiano ya jinsia moja kwa mamlaka.
Unaweza pia kusoma:
- Utafungwa maisha gerezani kwa kusema unashiriki mapenzi ya jinsia moja Uganda
- Bunge la Uganda lapitisha tena muswada wa kupinga mapenzi ya jinsia moja
- Mtazamo: Vita vya Afrika Mashariki kuhusu utamaduni na mapenzi ya jinsia moja
Viongozi wa Afrika wawasili Nigeria kwa ajili ya kuapishwa kwa Tinubu

Chanzo cha picha, Ofisi ya rais/Afrika Kusini
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ni miongoni mwa viongozi wa Afrika wanaohudhuria sherehe hizo
Marais kadhaa wa Afrika na viongozi wengine wa kigeni wamewasili nchini Nigeria kwa ajili ya kuapishwa kwa Bola Tinubu kuwa rais wa 16 wa taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani humo.
Harakati za kuzunguka Eagle Square huko Abuja, mahali pa kukabidhi na kuzindua gwaride, zimezuiwa hadi Jumanne.
Vyombo vya habari vya ndani vinasema takriban viongozi 20 wa Afrika wanatarajiwa mjini Abuja.
Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune ni miongoni mwa viongozi waliowasili Jumapili.
Pia huko Abuja kuna Samia Suluhu Hassan, Denis Sassou Nguesso, Umaro Sissoco Embaló na Julius Maada Bio.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Rais wa Chad Mahamat Deby, Rais wa Jamhuri ya Niger Mohamed Bazoum na Rais Nana Akufo-Ado wa Ghana.
Katibu mkuu wa baraza la mawaziri nchini Kenya Musalia Mudavadi atawakilisha Rais William Ruto.
Ujumbe wa watu tisa kutoka Marekani na maafisa wa China wakiongozwa na mwanachama mkuu wa Chama cha Kikomunisti pia wamewasili kwa hafla hiyo.
Ushindi wa Bw Tinubu katika uchaguzi unapingwa na wapinzani wa upinzani.
Siku ya Jumanne, mahakama itaanza kusikiliza hoja kuu katika ombi la uchaguzi.
Waziri Lavrov awasili Kenya kwa ziara ambayo haikutangazwa

Chanzo cha picha, MFA Urusi/Twitter
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov amewasili nchini Kenya kwa safari ambayo haijatangazwa.
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Moscow ilitangaza kuwasili kwa Bw Lavrov jijini Nairobi Jumatatu asubuhi, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu ziara hiyo.
Ubalozi wa Urusi mjini Nairobi kwenye Twitter yake ilisema hii itakuwa "wiki yenye matunda mengi kwa uhusiano baina ya Urusi na Kenya".
Rais wa Kenya William Ruto hakuhudhuria kuapishwa kwa Rais mteule wa Nigeria Bola Tinubu hii leo Jumatatu.
Ziara ya Bw Lavrov inajiri siku chache baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba kufanya ziara ya Afrika wiki jana.
Nyama ya nguruwe kujumuishwa kwenye chakula katika shule za Rwanda

Chanzo cha picha, Getty Images
Mipango inaendelea kuwezesha shule kujumuisha nyama ya nguruwe katika ratiba ya chakula nchini Rwanda kama njia ya kutokomeza utapiamlo, Olivier Kamana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Rasilimali Wanyama amenukuliwa na gazeti la New Time nchini humo akisema.
"Tunaziomba shule kuanzisha miradi ya ufugaji wa nguruwe ili kuweza kumudu nyama ya nguruwe," alisema.
Mnamo mwaka wa 2019, mpango wa lishe shuleni ulitekelezwa katika shule za sekondari (zinazosaidiwa na serikali na za serikali) huku wanafunzi 680,000 wakipokea ruzuku ya Serikali ya chakula cha shule.
Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa shule za msingi na sekondari ziliongezeka kutoka 2,877 mwaka 2017 hadi 2,963.
Mnamo 2021, Rwanda ilizalisha tani 185,989 za nyama. Idadi ya nguruwe imeongezeka kutoka 989,000 mnamo 2012 hadi takriban milioni 1.5 mnamo 2021.
Nchi hiyo iilizalisha wastani wa tani 23,000 za nyama ya nguruwe kwa katika mwaka 2019 na inalenga kuongeza uzalishaji wa nyama hiyo hadi kufikia tani 68,000 ifikapo 2024.
“Tunashughulikia mpango wa kutumia vyanzo mbadala vya protini kulisha mifugo badala ya mahindi. Hii itasaidia kuongeza idadi ya wafugaji wa nguruwe na uzalishaji wa nguruwe,” Kamana alisema.
Vita vya Ukraine: Zelensky ataka Iran iwekewe vikwazo kwa miaka 50

Chanzo cha picha, EPA
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliwasilisha muswada unaopendekeza kuanzishwa kwa vikwazo vya kisekta dhidi ya Iran kwa miaka 50.
Muswada huo unapendekeza kupiga marufuku kabisa shughuli za biashara zinazohusiana jeshi la Wairan, na pia "vizuizi vya biashara za huduma " kama vile usambazaji, uuzaji, uhamishaji, uzalishaji au matumizi ya bidhaa hizo.
Mapendekezo mengine ni pamoja na kupiga marufuku uhamishaji wa teknolojia na haki miliki kwa wakazi wa Iran, marufuku ya uwekezaji nchini Iran na kwa ajili ya wakazi wa nchi hiyo, na kusitishwa kwa huduma za malipo ya kielektroniki zinazotolewa na wakazi wa Iran.
Baraza la Mawaziri, Huduma ya Ujasusi wa Kigeni, Huduma ya Usalama, Benki ya Kitaifa ya Ukraine na vyombo vingine vya serikali vinatakiwa kuteuliwa kuwajibika kwa utekelezaji na ufuatiliaji wa vikwazo hivyo, kulingana na mapendekezo hayo.
Tarehe ya kupiga kura ya Bunge la Ukraine juu ya muswada huo bado haijawekwa.
Ukraine na nchi za Magharibi zina imani kuwa Iran inaipatia Urusi zana za kijeshi, zikiwemo ndege zisizo na rubani za Shahed, ambazo hutumika kuishambulia miundombinu ya kiraia na kijeshi ya Ukraine. Iran na Urusi zinakanusha hili.
Mapema wiki hii, Volodymyr Zelensky aliwataka watu wa Iran kuacha kuiunga mkono Urusi, akibainisha kuwa hii pia inasababisha kutengwa zaidi kwa Iran yenyewe.
Kulingana naye, zaidi ya ndege 1,150 za Iran zilirushwa nchini Ukraine wakati wa vita, na 900 kati ya hizo zilidunguliwa.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Tinubu aapishwa kuwa rais wa Nigeria

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Rais mteule wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu Bola Tinubu ameapishwa kuwa rais mpya wa Nigeria katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa Eagle Square mjini Abuja, kushangiliwa na umati wa watu.
Mkewe, Oluremi Tinubu, alisimama kando yake alipokuwa akila kiapo chake na kutia sahihi nyaraka.
Tinubu amesema kuwa "makabidhiano ya amani kutoka serikali moja hadi nyingine" sasa ni "mila" ya nchi hiyo, baada ya kula kiapo chake cha kuhudumu katika uwanja wa Eagle Square mjini Abuja.
Alisema Nigeria sasa "imeimarishwa" kama demokrasia alipochukua hatamu kutoka kwa mtangulizi wake na mwanachama mwenzake wa chama Muhammadu Buhari.
"Makabidhiano haya yanaashiria imani yetu kwa Mungu, imani yetu ya kudumu katika serikali ya uwakilishi na imani yetu katika uwezo wetu wa kuunda upya taifa hili kuwa jamii ambayo siku zote ilikusudiwa kuwa'. Rais Tinubu alisema.
Pia alitoa pongezi kwa Bw Buhari na kusema kuwa vita vya uchaguzi vilipiganwa vikali na alishinda kwa haki na aliwakilisha matakwa ya Nigeria.
Hata hivyo, wagombea wakuu wa upinzani wanapinga ushindi wake mahakamani.
Muda mchache hapo awali, Makamu wake wa Rais Kashim Shettima aliapishwa.
Kashim Shettima pia ameapishwa kama makamu wa rais mpya wa Nigeria katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa Eagle Square mjini Abuja.
Alikuwa pembeni ya mke wake na maafisa wa mahakama alipokuwa akila kiapo na kutia saini nyaraka.
Unaweza pia kusoma:
- Kuapishwa kwa Tinubu: Changamoto tano zinazomsubiri rais mpya wa Nigeria
Uchaguzi wa Uturuki: Nini cha kutarajia katika utawala mpya wa Erdogan?

Recep Tayyip Erdogan anaweza kuwa aliwachangamsha wafuasi wake kwa kuimba nyimbo zisizo na msingi baada ya ushindi wake - lakini yuko sawa linapokuja suala la kupigania uchaguzi.
Aliwasoma wapiga kura vizuri kuliko wapiga kura na wachambuzi, ambao walisema kuwa anaweza kushindwa na upinzani. Lakini ukweli ni kwamba, sio wakati huu.
Mpinzani wake - Kemal Kilicdaroglu - alikuwa nyuma yake kwa asilimia nne tu. Bila shaka Rais Erdogan atakuwa akiyatafakari hayo anapoanza muhula wake wa tatu madarakani.
Taifa hili la kimkakati la Nato limechagua njia yake, wapiga kura wengi wakichagua kiongozi wa kidemokrasia wa msimu badala ya mwanademokrasia ambaye hajajaribiwa kama Bw Kilicdaroglu.
Kiongozi huyo wa upinzani aliendesha kampeni yake kama Bw Nice Guy, akiahidi mwanzo mpya kwa Uturuki.
Baadaye alikwepa kulia, na kuapa kuwarudisha wakimbizi wote nyumbani. Hilo lilipata uungwaji mkono wake wa ziada kutoka kwa wazalendo, lakini haitoshi.
Kiongozi wa Kiislamu wa Uturuki Bw Erdogan ana uhusiano na wafuasi wake ambao unarudi nyuma miaka 20 iliyopita.
Wengi ni wahafidhina wa kidini kama yeye. Wameshikamana naye katika hali ngumu - na mfumuko wa bei – na kumpa miaka mitano zaidi.
Huku matokeo ya uchaguzi wa marudio yakitangazwa, mitaa ya mji mkuu Ankara ilikuwa na bendera za Uturuki, honi za magari zinazovuma, na wafuasi wa Erdogan wakishangilia.
Idadi kubwa ya watu walimiminika kwenye ikulu yake ya rais iliyojengwa maalum na vyumba 1,000 vya ziada. Mpinzani wake alikuwa ameahidi kuiweka hadharani.
Unaweza pia kusoma:
- Athari za hamaki katika uchaguzi wa Uturuki baada ya tetemeko la ardhi
- Kwa nini uchaguzi wa Uturuki unafuatiliwa kwa karibu barani Afrika
Vita vya Ukraine: Zelensky apongeza jeshi la anga baada ya shambulio lingine kubwa zaidi la droni la Urusi

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Afisa wa zimamoto katika eneo la kiwanda cha tumbaku kilichoharibiwa wakati wa shambulio la ndege isiyo na rubani Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amevipongeza vikosi vya ulinzi wa anga vya nchi yake baada ya shambulio kubwa zaidi la ndege zisizo na rubani la Urusi dhidi ya Kyiv kuwahi kushuhudiwa tangu vita kuanza.
"Nyinyi ni mashujaa," alisema Bw Zelensky, baada ya makamanda wa kijeshi kusema kwamba ndege nyingi zisizo na rubani za kamikaze zilizorushwa na Urusi ziliangushwa.
Hata hivyo watu wawili waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na vifusi vya majengo.
Urusi imeongeza kuwa mashambulio yake dhidi ya Kyiv katika wiki za hivi karibuni, ikitaka kuuharibu mji mkuu huo.
Shambulio la Urusi la anga la usiku wa tarehe 14 mwezi huu mjini Kyiv - lilikuja wakati watu wa mji mkuu wakijiandaa kusherehekea Siku ya Kyiv, ukumbusho wa kuanzishwa kwa jiji hilo zaidi ya miaka 1,500 iliyopita.
Katika onyesho la ajabu la ujasiri, watu walienda kwenye bustani, baa na mikahawa katika mji mkuu kusherehekea siku hiyo.
Meya wa Kyiv Vitaliy Klitschko alielezea shambulio hilo la usiku kama "kubwa", akisema ndege zisizo na rubani zilikuwa "zikishambulia kutoka pande kadhaa mara moja".
Baadhi ya majengo kikiwemo kiwanda cha tumbaku yameteketea kwa moto baada ya kugongwa na vipande vya ndege zisizo na rubani zilizoanguka.
Kwingineko, katika jiji la Zhytomyr kaskazini-magharibi mwa Ukraine, angalau majengo 26 ya makazi yaliharibiwa pamoja na shule na vitengo vya matibabu, kulingana na tovuti ya habari za mtandaoni ya Ukrayinska Pravda.
Lakini makamanda wa kijeshi walisema vikosi vya ulinzi wa anga vya Ukraine vimeangusha ndege 58 kati ya 59 zilizotengenezwa na Iran zilizorushwa na Urusi.
Akisifu jeshi lake la anga, Bw Zelensky alisema: "Kila mara mnaporusha ndege zisizo na rubani na makombora ya adui, maisha yanaokolewa... ninyi ni mashujaa."
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Hujabo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni tarehe 20.05.2023
