Mzozo wa DRC: Rais Tshisekedi adai jeshi la kikanda linashirikiana na waasi
Rais Felix Tshisekedi amedokeza wanajeshi hao wanaweza kuondoka mwishoni mwa Juni.
Moja kwa moja
Yanga mguu mmoja fainali? yaichapa Marumo 2-0 kwa Mkapa
Chanzo cha picha, CAF
Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga imeichapa Marumo Gallants ya Afrika Kusini mabao 2-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, uliofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mechi hiyo ilianza kwa kasi, huku pande zote mbili zikijaribu kupata mabao ya haraka, ingawa ulikuwa wa kupoa na kupata kasi tena.
Ulikuwa mchezo wa wazi, kila timu ikitengeneza nafasi za wazi kadhaa lakini ni Yanga ndiyo iliyoweza kunufaika zaidi kwa nafasi mbili.
Mzunguko wa pili utahitimisha kujua kama Yanga itafuzu kwa mara ya kwanza fainali ya michuano hiyo mwaka huu.
Mechi ya marejeano itapigwa Royal Bafokeng Stadium Rustenburg Mei 17 nchini Afrika Kusini.
Mafuriko DRC: Watoto wachanga wawili wakutwa hai wakielea siku tatu baada wazazi wao kusombwa na mafuriko
Chanzo cha picha, KALEHE CIVIL SOCIETY
Watoto wawili wameokolewa wakielea karibu na ufukwe wa ziwa Kivu siku chache baada ya mafuriko kuua zaidi ya watu 400 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
"Ni muujiza, sote tulishangaa," kiongozi wa jumuiya ya eneo hilo Delphin Birimbi aliambia BBC. Wazazi wao wamefariki lakini jamii inawasiliana na watu wanaoweza kuwalea, Bw Birimbi anaongeza.
Haijabainika jinsi watoto hao wachanga walinusurika kwa karibu siku tatu katika ziwa hilo, lakini mashuhuda wanasema waliwaona wakielea kwenye vifusi.
Watoto hao waliokolewa Jumatatu - mmoja huko Bushushu na mwingine Nyamukubi, vijiji viwili vilivyoathiriwa zaidi na mafuriko yaliyotokea wiki jana, Bw Birimbi anasema.
Mkasa huo umesababisha hisia za kuhuzunisha katika vijiji hivyo vyenye mrundikano wa maiti zilizofunikwa kwa blanketi.
Wabunge Tanzania waonywa kuvua nguo bungeni
Chanzo cha picha, Parliament
Wabunge wa Tanzania wameonywa kutovua nguo zozote wanapokuwa bungeni.
Spika Tulia Ackson alitoa onyo hilo baada ya Mbunge Mwita Waitara kuvua koti na tai wakati wa mjadala.
Alikuwa akionyesha kutoridhishwa na na majibu ya serikali - kuhusu fidia kwa wapiga kura wake walioko kwenye maeneo ya uchimbaji madini.
Alivua mavazi hayo huku akitoka nje ya ukumbi.
Kwa mujibu wa Spika, hakukerwa na namna ya kuondoka kwake, bali alikiuka kanuni za mavazi ya ubunge, ambayo yanahitaji uvaaji rasmi ndani ya ukumbi wa Bunge.
Alielezea kitendo chake ni kilikuwa ni "utovu wa nidhamu".
"Tabia hii hairuhusiwi ndani ya bunge na isijirudie tena," alisema Bi Ackson.
Mvulana wa miaka 8 anusurika kwa kula theluji baada ya kutoweka kwa siku mbili
Chanzo cha picha, MICHIGAN STATE POLICE
Mvulana wa
miaka minane aliyepotea katika misitu ya mbali ya Michigan alinusurika kwa siku
mbili kwa kula theluji na kujificha chini ya magogo.
Nante Niemi
alitoweka siku ya Jumamosi alipokuwa akipiga kambi na familia yake katika mbuga
ya serikali ya Milima ya Porcupine.
Alipotea
wakati akitembea kutafuta kuni, na hivyo kuzua jitihada za watu 150 kumtafuta
ili kumwokoa.
Siku ya Jumatatu alipatikana chini ya gogo moja
"akiwa na afya njema", kama maili mbili kutoka kambi yake.
"Alikuwa amevumilia hali ngumu kwa kujikinga chini ya gogo ambapo hatimaye
alipatikana," Polisi wa Jimbo la Michigan walisema katika taarifa.
Mvulana huyo
aliwaambia polisi kwamba "alikula theluji safi kwa ajili ya maji".
Mara tu
baada ya habari kuenea kuhusu kutoweka kwake Jumamosi, mama yake aliwashukuru
watu kwa usaidizi wao lakini akawasihi kila mtu "tafadhali kaa mbali
itafanya iwe vigumu kumpata".
Polisi wa
serikali walisema eneo hilo "liko mbali sana na lenye vilima na maji mengi
ya kusimama kutokana na wakati wa mwaka". Barabara nyingi hazipitiki
kutokana na wingi wa theluji.
Timu hiyo
ililenga eneo la takriban maili 40 za mraba (km 100 za mraba) katika bustani
hiyo, na hatimaye kumpata mvulana huyo.
Amekutanishwa
tena na familia yake, polisi walisema.
Alfie Halaand: Babake Erling Halaand aliondolewa kwenye kiti chake baada ya kuwakera mashabiki wa Real Madrid
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Alfie Halaanda ni babake mshambuliaji wa Manchester City Erling Braut Halaand
Alfie
Haaland anasema alisindikizwa kutoka kiti chake Bernabeu kwa sababu mashabiki
wa Real Madrid "hawakufurahishwa" na sherehe zake baada ya Kevin de
Bruyne kuisawazishia Manchester City katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya
Ligi ya Mabingwa.
Video kwenye
mitandao ya kijamii inaonekana kumuonyesha babake Erling Haaland akiwakejeli
mashabiki wa nyumbani kabla ya kuondolewa katika eneo lake.
Haaland
alitweet: "Sawa. RM hakufurahi tulikuwa tukisherehekea bao la KDB.
"Zaidi
ya hayo tulilazimika kuhama kwa sababu mashabiki wa RM hawakufurahishwa na
1-1."
De Bruyne alifunga dakika ya 67 na kusawazisha bao la kuongoza la Vinicius Junior.
Haaland alipunga mkono kwa mikono miwili huku akitabasamu
kwa umati wa watu waliokuwa chini yake, akitega masikio yake kwa mashabiki wa
Real Madrid na kufanya ishara, huku ripoti nchini Uhispania zikipendekeza kuwa
aliwarushia chakula wafuasi hao.
Kiungo huyo wa zamani wa Manchester City na Leeds ni mtu
wa kawaida kwenye mechi za City, ambapo mwanawe amefunga mabao 51 hadi sasa
msimu huu.
Miamba wa Uhispania Madrid wametwaa taji la Ligi ya
Mabingwa - mashindano ambayo City bado hawajashinda - mara tano tangu 2014 na
kuwaondoa mabingwa hao wa Ligi ya Premia katika hatua ya nusu fainali mwaka
jana.
Mnamo Oktoba ripoti zilipendekeza kwamba kandarasi ya
Haaland ina kipengele maalum cha kuachiliwa kwake ili ajiunge na Real Madrid
mnamo 2024, ambayo bosi wa City Pep Guardiola alisema baadaye "sio
kweli".
Kiongozi wa kanisa la kufunga hadi kufa Paul Mackenzie kusalia kizuizini kwa siku 30 zaidi
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, .Kiongozi wa kanisa la kufunga hadi kufa paul Mackenzie
Kiongozi wa madhehebu ya Shakahola Paul Mackenzie
atasalia rumande kwa siku 30 zaidi, mahakama ya Mombasa iliamua Jumatano.
Hakimu Mkuu
wa Shanzu Yusuf Shikanda alichukua uamuzi wa kuwazuilia Mackenzie, mkewe Rhoda
Maweu na washukiwa wengine 16 akitaja uchunguzi unaoendelea.
Bw Shikanda
zaidi alisema usalama na usalama wa washukiwa huenda ukawa hatarini iwapo
wataachiliwa kwa dhamana katika hatua hii.
Kiongozi
huyo wa madhehebu ya Kilifi anaaminika kuwahadaa makumi ya wafuasi wake hadi
kufa kwa njaa.
Marekani yathibitisha mfumo wake uliliangusha kombora 'lisiloharibika' la Urusi
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mfumo wa kulinda anga wa patriot
Katika
mkutano na Jeshi la Wanahewa Brigedia Jenerali Pat Ryder, msemaji wa Idara ya
Ulinzi ya Marekani, alithibitisha kwamba kombora la Kirusi la Kinzhal la
hypersonic lilidunguliwa juu ya anga yam ji wa Kiev mnamo Mei 4 kwa kutumia
mfumo wa Patriot uliopatikana hivi karibuni na jeshi la Ukraine.
Kombora la Kinzahl
lililodaiwa kutowezekana na Urusi lilizinduliwa wiki iliyopita katika shambulio
kubwa la kombora la Urusi.
Hapo awali,
mifumo ya Patriot ilitumiwa dhidi ya makombora ya kawaida ya balestiki, na
uwezo wa kurusha makombora ya hypersonic ulikuwa wa kinadharia tu.
Ijapokuwa
wanajeshi wa Ukraine walipata mabaki ya kombora hilo, mamlaka zilichelewa kutoa
maelezo hadi iliporipotiwa mahali pengine, kwani inaaminika kuwa kombora hilo
haliwezi kuharibika.
Baada ya
hapo, habari hiyo ilithibitishwa na kamanda wa Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine,
Luteni Jenerali Nikolai Oleshchuk.
"Ndio,
tulipiga risasi" isiyo na kifani "Kinzhal"! Hii ilitokea wakati
wa shambulio la usiku Mei 4 katika anga ya mkoa wa Kiev. Kombora la X-47
lilirushwa na MiG-31K kutoka eneo la Urusi," aliandika.
Taarifa hii
ya Jumanne iliungwa mkono na uthibitisho rasmi kutoka Pentagon.
Mzozo wa DRC: Rais Tshisekedi adai jeshi la kikanda linashirikiana na waasi
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Rais Felix Tshisekedi alisema wanajeshi hao wanaweza kuondoka mwishoni mwa Juni
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi amesema Jeshi la Kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF) litaondolewa mashariki mwa nchi hiyo iwapo litashindwa kutekeleza majukumu yake ya kuleta amani ifikapo Juni.
"Tutaamua kutoa kikosi hiki ... na kuwashukuru," alisema Jumanne nchini Botswana, ambako yuko katika ziara ya serikali.
EACRF ilipelekwa katika eneo hilo mwezi Machi ili kusaidia kukabiliana uasi wa Waasi M23 lakini tangu wakati huo imekosolewa kwa kushindwa kuwaondoa waasi katika eneo hilo.
Rais Tshisekedi pia alionyesha kuchoshwa na jeshi la kikanda, ambalo alisema halifanyi kazi kama ilivyotarajiwa DR Congo na inadaiwa kuwa lilikuwa likishirikiana na waasi.
"Katika baadhi ya mikoa, jeshi la kikanda linaishi pamoja na magaidi wa M23.
Hii haikuwa sehemu ya mpango huo. "Makubaliano yalikuwa kuondoa vikosi vya M23 na kusitisha mapigano" aliongeza.
Kauli yake ilikuja siku moja baada ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) kukubali kupeleka wanajeshi mashariki mwa DR Congo.
Kiongozi huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pia alikosoa mamlaka ya Kenya kwa kujiuzulu na kuchukua nafasi ya kamanda wa kikosi cha kwanza, Jenerali Jeff Nyagah, kutokana na "vitisho" ambavyo havijabainishwa.
Paul Mackenzie: Kiongozi wa dhehebu tata la Kenya kufikishwa mahakamani, uchunguzi unaendelea
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Polisi wanataka kuendelea kumzuilia Paul Nthenge Mackenzie.
Kiongozi wa dhehebu tata la kidini linalohusishwa na tuhuma ya mauaji ya waumini wake nchini Kenya leo anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa mara nyingine tena.
Huku hayo yakijiri polisi wanandelea kuchunguza vifo vya zaidi ya wafuasi 130 wa dhehebu hilo la kidini lenye utata.
Wanataka kuendelea kumzuilia Paul Nthenge Mackenzie, anayedaiwa kuamuru wafuasi wake kufunga hadi kufa ili wafike mbinguni haraka zaidi.
Uchimbaji wa makaburi ya pamoja katika msitu wa Shakahola huko Kilifi pwani ya Kenya unaendelea - miili mingine 21 ilifukuliwa Jumanne.
Mamia watu hawajulikani walipo.
Pia unaweza kusoma:
Madhehebu ni nini na kwa nini watu hujiunga nayo?
Paul Makenzi:Mhubiri huyu alianzaje safari tata ya kuwashawishi watu kufunga hadi kufa?
Matukio ya ibada hatari zaidi ulimwenguni
Buhari arefusha safari yake London ili kupata matibabu ya meno
Chanzo cha picha, get
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameongeza muda wa kukaa London kwa wiki moja kwa matibabu ya meno, msaidizi wake amesema.
Awali rais huyo alikuwa amesafiri kwenda Uingereza wiki iliyopita kuhudhuria kutawazwa kwa Mfalme Charles III.
Alipangiwa kurejea Nigeria wiki hii lakini sasa atasalia "kwa amri ya daktari wake wa meno, ambaye ameanza kumhudumia".
"Mtaalamu anahitaji kuonana na rais katika siku nyingine tano kwa ajili ya utaratibu ambao tayari umeanza," msemaji wa rais Femi Adesina alisema katika taarifa iliyotolewa Jumanne usiku.
Kukaa kwa muda mrefu kwa rais huyo mjini London kumezua shutuma kutoka kwa baadhi ya Wanigeria, wanaosema kwamba anapaswa kuyapa kipaumbele masuala ya ndani na kushughulikia changamoto za usalama zinazoikabili nchi hiyo.
Bw Buhari amesafiri hadi Uingereza mara kadhaa katika kipindi chake cha urais kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi huku kukiwa na uvumi kuhusu afya yake. Ameratibiwa kumkabidhi Rais Mteule Bola Tinubu tarehe 29 Mei.
Uturuki yaongeza mishahara ya wafanyikazi wa umma kwa 45%
Chanzo cha picha, ge
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameangaza nyongeza ya asilimia 45 ya mshahara kwa wafanyikazi wa umma 700,000 siku tano kabla ya uchaguzi mkuu.
Haya yanajiri wakati uchumi wa nchi hiyo ukiyumba kutokana na athari za matetemeko makubwa ya ardhi mwezi Februari.
Erdogan, ambaye alichaguliwa kuwa rais wa Uturuki mwaka 2014, atawania muhula mwingine katika uchaguzi wa rais na wabunge mnamo Mei 14.
Kura za maoni zinaonyesha Erdogan anakabiliwa na kinyang'anyiro kikali kutoka mgombea urais wa upinzani, Kemal Kilicdaroglu.
Uchumi wa Uturuki ni suala muhimu kuelekea uchaguzi wa Jumapili.
Hatua ya Erdogan ya kupunguza kwa viwango vya riba kusiko kwa kawaida kulisababisha kushuka kwa thamani ya lira ya Uturuki mwishoni mwa 2021 na kufanya mfumuko wa bei kufikia asilimia 85.5 mwaka jana, kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa ndani ya miaka 24.
Kenya: 'Yesu wa Tongaren' kuhojiwa katika msako dhidi ya madhehebu tata ya kidini
Mhubiri mwenye utata nchini Kenya ametakiwa kufika polisi kwa mahojiano huku serikali ikikabiliana na kile inachokiita makanisa yenye utata na viongozi wa kidini wenye msimamo mkali.
Eliud Wekesa, almaarufu "Yesu wa Tongaren", kiongozi wa dhehebu la New Jerusalem, aliitwa siku ya Jumanne ili kuhojiwa kuhusu mafundisho yake ya kidini yanayotiliwa shaka.
Amewaongoza waumini wa kanisa lake kuamini kuwa yeye ni Yesu.
Anatarajiwa kufika mbele ya polisi katika kaunti ya magharibi ya Bungoma siku ya Jumatano.
Mhubiri huyo, hata hivyo, anasema hajafanya chochote kibaya kutakachomfanya akamatwe, akiongeza kuwa anaeneza injili pekee, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.
Haya yanajiri huku wachunguzi wakifukua miili 21 zaidi katika kaunti ya Kilifi pwani, ya Kenya na kufanya jumla ya waliofariki katika mauaji ya Shakahola kufikia 133.
Mchungaji Paul Mackenzie, kiongozi wa Kanisa la Good News International lenye makao yake makuu mjini Kilifi, anasubiri kufikishwa mahakamani, kwa tuhuma za kuwasihi wafuasi wake kufunga hadi kufa ili ''waende mbinguni''.
Mamia ya wengine wameripotiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha.
Rais William Ruto ameunda tume ya uchunguzi kuchunguza vifo vya Shakahola katika kaunti ya Kilifi.
Polisi katika jimbo jirani la Kwale siku ya Jumatatu waliwaokoa watu 200 wakiwemo watoto 50 kutoka msituni katika kisa kinachoshukiwa cha utekaji nyara wa kidini.
Mwandishi wa Australia azuiliwa siku 1,000 jela nchini China kwa sababu isiyojulikana
Chanzo cha picha, Contributed photo
"Siku elfu moja ni muda mrefu sana kizuizini," anasema Nick Coyle.
Anazungumzia kilichokuta mpenzi wake, mwandishi wa habari wa Australia Cheng Lei, ambaye bado anazuiliwa katika gereza la China.
Maelezo kuhusu mashtaka dhidi yake bado yamewekwa siri na hajahukumiwa.
Kama marafiki na familia nyingine za Bi Cheng, Bw Coyle anasema hailewi kwa nini Cheng anapitia madhila kama haya.
"Nitoa wito kwa mamlaka husika nchini China kutatua hali hii mbaya haraka iwezekanavyo," anaiambia BBC.
Cheng Lei alikuwa akifanya kazi kama mwandishi wa taarifa za biashara katika kituo cha televisheni cha taifa cha China cha CGTN alipokamatwa ghafla na maafisa wa usalama wa serikali tarehe 13 Agosti 2020, na baadaye kushutumiwa kwa "kutoa siri za serikali nje ya nchi kinyume cha sheria".
Miezi yake sita ya kwanza alizuiliwa katika kifungo cha upweke, akidhibitiwa vikali ingawa alihojiwa bila kuwa na wakili.
Tangu wakati huo, amekuwa akizuiliwa pamoja na wafungwa wengine.
Kesi yake ilifanyika faraghani mwezi Machi mwaka jana.
Balozi wa Australia nchini China Graham Fletcher alinyimwa kuingia mahakamani.
Lakini hukumu yake imeahirishwa mara kwa mara.
Juhudi za BBC kuwasiliana na maafisa wa kwa Mahakama ya Beijing, ambako kesi yake ilifanyika, hazikufaulu.
Bw Coyle - mtendaji mkuu wa zamani wa Chama cha Wafanyabiashara wa China-Australia - sasa ameondoka Beijing lakini anaendelea kufuatilia suala hilo kutoka ng'ambo wa ajili ya kuachiwa kwake.
Wizara ya mambo ya nje ya China imejaribu kupunguza wasiwasi wa kimataifa kuhusu kesi hiyo.
Vita vya Ukraine: Mwandishi wa habari wa Ufaransa auawa karibu na Bakhmut
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mwandishi wa habari wa Ufaransa aliyeuawa akitabasamu na paka begani
Mwandishi wa habari wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 32 ameuawa alipokuwa akiripoti kutoka eneo la vita mashariki mwa Ukraine.
Arman Soldin, ambaye alifanya kazi katika shirika la habari la AFP, alifariki Jumanne baada ya kupigwa na roketi karibu na Chasiv Yar, magharibi mwa Bakhmut.
Timu ya waandishi wa habari ilishambuliwa mwendo wa saa 16:30 (13:30 GMT) wakiwa na kundi la wanajeshi wa Ukraine.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitoa pongezi kwa kazi ya Soldin kwenye mstari wa mbele wa vita.
"Tunaungana na wapendwa wake na wenzake," aliandika kwenye ujumbe wa Twitter.
Mwenyekiti wa AFP, Fabrice Fries, alisema shirika la habari "limehuzunishwa" na kifo cha Soldin, ambacho alisema "ni ukumbusho mbaya wa hali hatari wanazokabiliana nazo waandishi wa habari kila siku wanapoangazia mzozo wa Ukraine".
Mkurugenzi wa shirika hilo la Ulaya, Christine Buhagiar, alimkumbuka Soldin kama "mwenye shauku, mwenye nguvu na jasiri", na kuongeza kuwa "amejitolea kabisa kwa uwelediwake".
Wabunge walisimama katika Bunge la Kitaifa la Ufaransa na kutoa heshima kwa Soldin.
Trump apatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono
Chanzo cha picha, Getty Images
Jopo la majaji
katika kesi ya madai limempata Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump n ahatia
ya kumnyanyasa kingono mwandishi wa jarida katika duka moja kuu la New York
miaka ya 1990.
Ni mara ya
kwanza kwa Bw Trump kupatikana na hatia ya kuhusika na unyanyasaji wa kingono.
Lakini Bw Trump
hakupatikana na hatia ya kumbaka E Jean Carroll katika chumba cha kubadilishia nguo
cha Bergdorf Goodman.
Mahakama pia
ilimpata Bw Trump na hatia ya kuharibia jina kwa kuyaita madai ya mwandishi
huyo "Uvumi na uwongo".
Mahakama ya
Manhattan iliamuru Bw Trump amlipe takriban dola milioni milioni tano kama
fidia.
Jopo hilo la
majaji tisa ilifikia uamuzi wao baada mashaurinao ya chini ya saa tatu siku ya Jumanne.
"Leo,
ulimwengu hatimaye unajua ukweli," Bi Carroll alisema katika taarifa
iliyoandikwa kufuatia uamuzi huo.
"Ushindi
huu sio kwangu tu bali kwa kila mwanamke ambaye ameteseka kwa sababu
hakuaminiwa."
Wakili wa Bw
Trump alisema rais huyo wa zamani anapanga kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Maelezo zaidi:
Ni nini kilichotokea kati ya Stormy Daniels na Donald Trump?
Kwa nini simulizi hii ya Trump na Daniels ni muhimu
Katika picha: Donald Trump alivyofikishwa mahakamani