Kijana wa kimisri ajinyakulia mamilioni katika mashindano ya Qur’an nchini Tanzania
Raia wa Misri Omar Mohammad Hussein ameibuka kidedea katika mashindano ya Afrika ya kuhifadhi Qur’an yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hii leo.
Moja kwa moja
Mwanaharakati wa Urusi aliyefichua maelezo ya mazishi ya mamluki wa Wagner waliouawa Ukraine atoroka Urusi

Chanzo cha picha, VITALY VOTANOVSKY
Vitaly Votanovsky, ambaye alianza kuweka kumbukumbu za vifo vya wanajeshi wa Urusi nchini Ukraine kwa kufuatilia makaburi katika eneo lake la nyumbani, alitoroka nchi humo tarehe 4 Aprili baada ya kupokea vitisho vingi vya kuuawa.
Alizungumza na BBC kutoka mji mkuu wa Armenia Yerevan.
Mwaka jana, Vitaly alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 50 katika jela.
Mwanaharakati huyo kutoka eneo la kusini mwa Urusi la Krasnodar, alikamatwa na kufungwa jela tarehe 24 Februari 2022, siku ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Afisa huyo wa zamani wa jeshi la Urusi alikuwa ametoka kuandamana siku hiyo akiwa amevalia nguo zilizoandikwa maneno "Hapana kwa Putin!" na "Hapana kwa vita!"
Picha za Vitaly akiwa amevalia mavazi yake zimejumuishwa kwenye nyaraka rasmi za mahakama ambazo Vitaly aliionyesha BBC.
"Kwa sababu ya koti hilo nilipatikana na hatia na kuzuiliwa jela kwa siku 20!", anasema.
Katika eneo la Krasnodar, Vitaly hijulikani kwa maandamano ya mitaani, lakini kwa kumbukumbu za makaburi.
Alikuwa mtu wa kwanza kugundua kaburi ambalo sasa lina sifa mbaya katika kijiji kidogo cha Bakinskaya katika Mkoa wa Krasnodar, tangu kujulikana kama makaburi ya Wagner.
Hapa ndipo kundi la mamluki linalojulikana kwa ukatili linawazika wafu wake wengi kutoka Ukraine - wanaume ambao ama hawana jamaa au miili yao haijadaiwa.
Imekua kutoka kwa kaburi ndogo la kijiji hadi makaburi mengi, na maeneo kadhaa mapya ya kushughulikia idadi inayoongezeka ya wafu.
Walinzi sasa wanashika doria katika kituo hicho.
Maia na Rina Dee: Dada wawili waliouawa katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa wamezikwa

Chanzo cha picha, PA Media
Dada wawili Maia na Rina Dee wa Uingereza wenye asili ya Israel waliouawa kwa kupigwa risasi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu wamezikwa.
Dada hao waliuawa siku ya Ijumaa alasiri karibu na Makutano ya Hamra kaskazini mwa Bonde la Yordani, walipokuwa wakiendesha gari kuelekea Tiberia.
Walikuwa ni watoto wa Rabi Leo Dee, mwenye asili ya London, ambaye aliwataja kuwa "wa kipekee".
Mama yao, Leah, bado yuko katika hali mbaya hospitalini.
Rabi Dee alisema risasi mbili zilitolewa kwenye uti wa mgongo na shingo ya mkewe wakati wa upasuaji.
Maia alikuwa na umri wa miaka 20 na alijitolea kwa huduma ya kitaifa katika shule ya upili, huku dada mdogo Rina akiwa na umri wa miaka 15.
Gari lao lilitolewa nje ya barabara baada ya kupigwa risasi na watu wenye silaha huku baba yao akiendesha gari tofauti.
Akizungumza na BBC, aliwataja binti zake kuwa warembo, werevu na maarufu.
Alisema hakuweza kulala tangu vifo vyao. "Kila wakati, niliota ndoto mbaya na kuamka," alisema, "lakini ukweli ulikuwa mbaya zaidi kuliko ndoto, kwa hivyo nilirudi kulala. Ndoto mbaya za mara kwa mara ... ndivyo ilivyokuwa."
Alisema Maia alikuwa "mzuri, mrembo, alikuwa na marafiki wengi ... alikuwa na hamu sana ya kufanya mwaka wa pili wa kujitolea". Rina, alisema, alikuwa "mrembo, mcheshi, mwerevu sana, alipata alama za juu katika kila somo, maarufu sana kwa marafiki, mwanamichezo...aliyewajibika sana, angewajibika kwa mambo mengi".
Habari za hivi punde, Kijana wa kimisri ajinyakulia mamilioni katika mashindano ya Qur’an nchini Tanzania,

Raia wa Misri Omar Mohammad Hussein ameibuka kidedea katika mashindano ya Afrika ya kuhifadhi Qur’an yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hii leo.
Hussein amewashinda washiriki wenzake 23 kutoka nchi 23ndani na nje ya bara la Afrika na kujizolea zawadi ya shilingi milioni 23 ambazo ni sawa na dola elfu 10 za kimarekani.
Wakati huo huo, watanzania wawili ambao wameweza kuibuka katika tano bora ni Adurahim Abubakar Masoud, ambae ameshika nafasi ya tatu na Bakari Juma Hamadi nafasi ya tano.
Mashindano hayo ya 23 yameshuhudiwa na maelfu ya wananchi waliojitokeza kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na nje ya nchi.
Soma zaidi:

Pia, kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo, kuna washiriki kutoka bara la Asia kama Saudi Arabia lakini vile vile Marekani na Uingereza.
Awali, hofu ilitanda ya uwezekano wa kuharibika kwa shughuli hiyo baada ya Mvua kubwa kunyesha, hata hivyo baadae wananchi walionekana kupata ujasiri wa kuvumilia mpaka tamati.
Mbali na washindi hao, pia kuna waliopata zawadi ya kuwa na sauti nzuri katika usomaji huku Salahdeen Katerega mwenye miaka 13 kutoka Uganda akipata zawadi ya dola mia tano kwa kuwa mshiriki mdogo kuliko wote miaka 13.
Rais wa Zanzibar Dk Hissein Mwinyi ndiye aliyekuwa mgeni rasmi akimwakilisha rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Algeria: Imam Walid Mahsas ambaye hakukatiza Swala ya Taraweeh licha ya Paka kumrukia mabegani atunukiwa tuzo

Chanzo cha picha, The Official Page Of Sheikh Walid Mehsas
Maelezo ya picha, Paka akiwa amepanda kwenye mabega ya Imam Walid Mehsas Unakumbuka, siku chahce zilizopita, kulitokea tukio la paka kumrukia Imam na kupanda hadi mabegani kwake wakati akiwa anaswalisha swala ya Taraweeh.
Imam huyo hakuvunja sala wala hakumshusha paka, badala yake alimruhusu paka afanye biashara yake, na yeye akaendelea na kuswalisha. Video hiyo ilisambaa katika mitandao ya kijamii duniani kote.
Imam huyo Walid Mahsas wa msikiti mmoja kule nchini Algeria ametunukiwa tuzo na serikali ya Algeria chini ya ofisi ya masuala ya dini kwa kuonyesha kwake ile picha ya Uislmau ya huruma na upendo kwa wanyama.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Tazama jinsi paka huyo alivyopanda juu ya mabega ya ImamWalid Mahsas
Ukraine kuuza tena umeme nje baada ya miezi ya uvamizi wa Urusi

Chanzo cha picha, Reuters
Ukraine sasa in uwezo wa kuuza umeme nje ya nchi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi sita huku miundombinu yake ya nishati ikirejea katika hali ya kawaida kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya Urusi yaliyodumu kwa miezi kadhaa.
Urusi ilianza mashambulizi yake ya muda mrefu na ya makusudi kwenye miundombinu ya nishati ya Ukraine Oktoba, 2022.
Hali hiyo Ilisababisha kukatika kwa umeme na kuweka mgawo wa umeme, na kuiacha miji na majiji gizani wakati wa msimu wa baridi.
Ukraine ililazimika kusitisha mauzo ya umeme nje - lakini sasa itaweza kuuza tena nishati ya ziada.
Waziri wa Nishati Herman Halushchenko alitia saini waraka wa kuidhinisha mauzo ya nishati nje, ingawa7 wateja wa ndani wanabakia kuwa kipaumbele.
Alisema mfumo huo umekuwa ukitoa uwezo wa ziada kwa karibu miezi miwili na kwamba raia wa Ukraine hawakukabiliwa na upungufu.
"Kipindi cha baridi kali zaidi kimepita," Bw. Halushchenko alisema Ijumaa.
"Hatua inayofuata ni kuanza kusafirisha umeme nje, ambayo itatuwezesha kuvutia rasilimali za ziada za kifedha kwa ajili ya ujenzi muhimu wa miundombinu ya nishati iliyoharibiwa."
Pia alipongeza "kazi kubwa ya wahandisi na washirika wa kimataifa kurejesha mfumo huo. Mwezi uliopita, wakaazi katika maeneo mengi ya Ukraine waliiambia BBC kwamba vifaa vya umeme vilikuwa vya kutegemewa zaidi.
"Jiji limebadilika," Inna Shtanko, mzazi kijana huko Dnipro alisema.
"Mwishowe, taa za barabarani zinawaka, na haiogopeshi tena kutembea kwenye mitaa ya jiji".
Soma zaidi:
Israel yashambulia maeneo mengi Syria baada ya kurusha roketi usiku kucha

Chanzo cha picha, Reuters
Israel imeshambulia maeneo mengi ya kijeshi nchini Syria baada ya kurusha makombora katika maeneo inayodhibiti usiku kucha, jeshi la Israel limesema.
Israel imesema mizinga na ndege zisizo na rubani vilitumika kushambulia kambi ya jeshi la Syria na kurusha roketi baada ya kurusha roketi sita kuelekea milima ya Golan.
Maafisa walisema roketi tatu zimeingia katika ardhi ya Israel. Mbili zilishambulia eneo la wazi na ya tatu ilizuiliwa. Katika chapisho kwenye ukurasa Facebook, wizara ya ulinzi ya Syria ilithibitisha mashambulizi hayo.
Maafisa wa ulinzi walidai kuwa walinzi wa anga walijibu shambulio hilo na kufanikiwa kuzuia baadhi ya makombora. Iliongeza kuwa hakuna hasara iliyoripotiwa, na kwamba ni uharibifu wa vifaa tu uliosababishwa na shambulio hilo.
Wakati huo huo, vyombo vya habari vya serikali ya Syria viliripoti milipuko karibu na mji mkuu wa Syria, Damascus.
Awali, milio ya mashambulizi ya anga ilisikika katika milima ya Golan baada ya kurushwa kwa roketi kutoka eneo la Syria, lakini hakuna vifo au uharibifu ulioripotiwa.
Vyombo vya habari vya Lebanon viliripoti kwamba Brigedi ya Al-Quds, ambalo ni tawi la kijeshi la kundi la Jihad ya Kiislamu ya Palestina linaloungwa mkono na Irani - limedai kuhusika na mashambulizi hayo.
Katika taarifa mapema Jumapili, vikosi vya Ulinzi vya Israel vilisema "wanaona hali ya Syria inawajibika kwa matukio yote ndani ya ardhi yake na haitaruhusu majaribio yoyote ya kukiuka mamlaka ya dola la Israel".
Israel iliteka eneo la military ya Golanlenye kilomita za mraba 1,200 lililokuwa likidhibitiwa hapo awali na Syria, wakati wa vita vya siku
Sita mwaka 1967 na kulitwaa mwaka 1981, hatua ambayo hata hivyo, haitambuliwi na wengi katika jumuiya ya kimataifa.
Mashambulizi hayo yanakuja huku kukiwa na hali ya wasiwasi katika eneo hilo.
Siku ya Ijumaa, Israel ilishambulia maeneo kadhaa ya kusini mwa Lebanon ambayo yanadhibitiwa na kundi la wapiganaji wa Palestina Hamas, ambalo linatuhumiwa kuhusika na msururu wa maroketi 34, yaliyorushwa kaskazini mwa Israel siku ya Alhamisi.
Pia unaweza kusoma:
Mashindano makubwa ya usomaji Qur’an yanayojumuisha nchi za nje yanaendelea Tanzania,

Mamia wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na viunga vyake wamejitokeza katika uwanja wa Taifa kushuhudia mashindano makubwa ya usomaji Qur’an.
Mashindano hayo ya 23 yanajumuisha jumla ya washiriki 23 kutoka nchi 23 ndani na nje ya bara la Afrika.
Miongoni mwa nchi hizo ni za Afrika Mashariki pamoja na za Afrika Magharibi kama vile Nigeria.
Pia, kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo, kuna washiriki kutoka bara la Asia kama Saudi Arabia lakini vile vile Marekani na Uingereza.

Atakaeibuka kidedea katika mashindano haya atajizolea zawadi ya kitita cha fedha taslimu milioni 23 za kitanzania ambazo ni sawa na dola elfu 10 za kimarekani.
Mshindi wa pili hadi wa tano watapata kuanzia milioni 15 hadi milioni 4.
Licha ya mvua kubwa inayonyesha idadi kubwa wa wananchi walionyesha utulivu mkubwa kufuatilia mashindano hayo huku wakinyeshewa.
Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi ndio anamwakilisha mgeni rasmi ambae ni rais Samia Suluhu Hassan
UFC 287: Israel Adesanya ampa kipigo cha nguvu Alex Pereira na kushinda tena taji lake la uzani wa kati

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Adesanya alipata ushindi wake wa 13 katika mapambano 15 ya UFC Israeli Adesanya hatimaye amerejea katika ubora wake.
Baada ya kupoteza mara mbili katika mchezo wa kickboxing mnamo 2016 na 2017, na kwenye UFC 281 mnamo Novemba, alijizatiti na kulipiza kisasi katika hafla kuu ya Jumamosi usiku ya UFC 287 huko Miami, Florida, na kumwangusha Mbrazil huyo.
Ulikuwa ushindi muhimu sana kwa raia huyo wa New Zealand mzaliwa wa Nigeria kunyakua kwake tena taji la UFC uzito wa kati.
"Wanasema kulipiza kisasi ni kutamu, na ikiwa unanijua, nina jino tamu," alisema katika mahojiano yake baada ya pambano.
Raundi ya ufunguzi ilikuwa ya majaribio kidogo, na mateke mengi ya miguu yakipigwa kati yao kuliko kitu kingine chochote.
Mambo yaliendelea vyema katika raundi ya pili.
Poatan alikuwa tayari zaidi kuruhusu mikono yake kwenda, na tayari alikuwa akipiga mguu wa kuongoza wa Izzy.
Pereira alimfanya Adesanya abanishwe kwenye uzio na kuanza kushusha mapigo makali, lakini Adesanya alikuwa na kitu kwenye mkono wake.
Izzy alikabiliana na mkono wa kulia ambao ulimshtua Pereira, na kisha akafuata na ngumi mbili ambazo zilimtia baridi.
Na hatimaye Adesanya alilipiza kisasi kwa UFC 287.
Adesanya alikutana na Pereira kwa mara ya kwanza kwenye ulingo wa masumbwi mwaka wa 2016 na akapoteza kwenye uamuzi ulioleta utata.
Kisha walikutana mwaka mmoja baadaye, na Pereira alinusurika na hofu ya mapema ya kumtoa Adesanya katika raundi ya tatu na ya mwisho.
Hatimaye walikutana chini ya sheria za MMA kwenye UFC 281 Novemba mwaka jana huko New York City, huku Adesanya akidhibiti tena mechi nyingi kabla ya kupata kipigo kikali katika raundi ya tano na matokeo yake akapoteza mkanda wake.
Mambo yalianza kuwa tofauti haraka kwenye UFC 287.
Hakukuwa na shaka kwamba Adesanya alikabiliana na mchuano mgumu sana—tulijua Pereira angeweza kumpiga na kumpiga vibaya—lakini bingwa huyo wa zamani alikuwa angalizo tangu alipoingia ulingoni.
Hakika alionekana kuwa imara mara tu pambano lilipoanza.
Katika UFC 287, Adesanya alionyesha upande tofauti wa mchezo wake. Wakati Pereira alipokuwa akisonga mbele kwa sehemu kubwa ya raundi ya kwanza na ya pili, Adesanya hakuruhusu bingwa huyo kumsumbua na mara kwa mara alijisogeza mbele katika juhudi za kuvuruga mdundo wa adui yake.
Hatimaye alipata matokeo aliyotaka katika dakika za mwisho za wakati Pereira alipoanza kujiamini.
Makumi ya watu wauawa katika mashambulizi ya 'kinyama' Burkina Faso

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Mkuu mpya wa jeshi la Burkina Faso ameapa kuongeza juhudi za kukabiliana na ghasia za wanajihadi nchini humo Takriban watu 44 wameuawa baada ya mashambulizi mawili mabaya kaskazini mwa Burkina Faso siku ya Alhamisi, maafisa wamesema.
Mashambulizi hayo mawili yalitokea katika vijiji vya Kourakou na Tondobi katika eneo la Sahel, karibu na mpaka wa Niger.
Hakuna kundi lililokiri kufanya mashambulizi hayo, lakini ghasia za wanajihadi ni za kawaida katika eneo hilo na maafisa wamelaumu "makundi ya kigaidi yenye silaha".
Makundi ya wapiganaji wanaohusishwa na al-Qaeda na Islamic State (IS) yanajulikana kufanya kazi katika eneo hilo.
Luteni-Gavana wa eneo la Sahel, Rodolphe Sorgho, alisema washambuliaji waliendesha "shambulio la kuchukiza na la kinyama".
Wanakijiji wengine waliripotiwa kujeruhiwa katika mashambulizi hayo, lakini haijulikani ni wangapi. Bw Sorgho alisema "hatua za kuleta utulivu eneo hilo zinaendelea".
Mkazi mmoja aliliambia shirika la habari la AFP kwamba "idadi kubwa ya magaidi waliingia kijijini" na kwamba alisikia milio ya risasi usiku kucha.
"Ilikuwa Ijumaa asubuhi ambapo tuliona kwamba kulikuwa na watu kadhaa waliokuwa wamefariki dunia," alisema.
AFP pia imeripoti kwamba mauaji hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa wanajihadi wawili ambao walijaribu kuiba ng'ombe siku chache zilizopita.
Mauaji ya Alhamisi usiku yalitokea karibu na kijiji cha Seytenga, ambapo makumi ya watu waliuawa Juni mwaka jana.
Burkina Faso na majirani zake wamekabiliwa na uasi wa muda mrefu wa wanajihadi tangu 2013.
Maelfu ya watu wameuawa wakati wa mzozo huo na zaidi ya milioni mbili wametoroka makazi yao.
Ghasia hizo zimesababisha msukosuko mkubwa wa kisiasa nchini humo.
Jeshi - likiongozwa na Lt Kanali Paul-Henri Damiba - lilichukua mamlaka nchini humo Januari mwaka jana, na kuahidi kukomesha ghasia.
Lakini alishindwa kukomesha mashambulizi, na aliondolewa katika mapinduzi ya pili na Kapteni Ibrahim Traoré Septemba iliyofuata.
Capt Traoré ameahidi kushinda tena eneo kutoka kwa wanajihadi, na kufanya uchaguzi wa kidemokrasia mnamo Julai 2024.
Mkuu wake mpya wa kijeshi, Kanali Celestin Simpore, aliapa mapema wiki hii kuongeza "uvamizi mkali" ili kukabiliana na wanajihadi.
Lakini Kapteni Traoré pia amewataka wanajeshi wa Ufaransa kuondoka nchini humo na kumekuwa na uvumi mkubwa kwamba huenda akaanza kufanya kazi na mamluki wa Urusi.
Marekani yaitaka China ijizuie wakati wa mazoezi yake ya kijeshi Taiwan

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Meli ya kivita ya China yashiriki katika mazoezi karibu na Visiwa vya Matsu vinavyodhibitiwa na Taiwan China imefanya mazoezi ya kijeshi ya majini kwa siku ya pili kuzunguka Taiwan, huku hali ya wasiwasi ikiendelea kuongezeka baada ya ziara ya Rais Tsai Ing-wen nchini Marekani wiki iliyopita.
Mazoezi hayo - ambayo Beijing imeyaita "onyo kali" kwa Taipei - yametumia vikosi vya majini na anga kuiga kuzingira kisiwa hicho.
Taiwan ilisema makumi ya ndege za Kichina ziliruka kwenye kisiwa hicho siku ya Jumapili, wakati meli tisa pia zilionekana.
Operesheni hiyo iliyopewa jina la "Upanga wa Pamoja" na Beijing, itaendelea hadi Jumatatu.
Maafisa wa Taiwan wamekasirishwa na operesheni hiyo, na siku ya Jumamosi maafisa wa ulinzi huko Taipei waliishutumu Beijing kwa kutumia ziara ya Bi Tsai - ambapo alikutana na spika wa Bunge la Merika Kevin McCarthy - kama "kisingizio cha kufanya mazoezi ya kijeshi, ambayo yamedhoofisha sana amani, utulivu na usalama katika eneo hilo".
Siku ya Jumamosi moja ya meli za China ilirusha duru kutoka kwenye sitaha yake ilipokuwa ikisafiri karibu na kisiwa cha Pingtan, eneo la karibu zaidi la China na Taiwan, shirika la habari la Reuters liliripoti.
Soma zaidi:
Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja
