Vita vya Ukraine: Ukraine yaanzisha uchunguzi wa uhalifu baada ya mashambulio ya makombora ya Urusi

Ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu nchini Ukraine imeanzoshisha uchunguzi kwa ajili ya mashitaka kuhusina na mashambulio ya makombora ya Urusi yaliyopiga katika miji na vijiji kwenye majimbo ya Ukraine ya Donetsk na Zaporozhye

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa taarifa zetu za moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho panapo majaaliwa.

  2. Vita vya Ukraine: Muasisi wa Wagner atoa hesabu kamili kuhusu pesa wanazohitaji kudhibiti mji muhimu Bakhmut

    screenshot

    Chanzo cha picha, screenshot

    Muasisi wa kikundi cha mamluki cha Wagner, Yevgeny Prigozhin, amechapisha video nyinginekutoka Bakhmut, ambapo alizungumzia kuhusu ni kiasi gani mashambulio ya mwezi ya kikundi chake yanaweza kugarimu.

    Akijibu swali kuhusu iwapo yeye binafsi anaweza kununua silaha muhimukwa ajili ya mamluki, uhaba wasilaha katika eneo la Bakhmut ambako mamluki wamekuwa wakilalamika tangu mwishoni mwa Disemba , Prigozhin alisema kwamba kikundi cha mamluki wake kilihitaji “takriban tani 10,000 za risasi kwa mwezi.”

    “Kilo moja ya risasi inagarimu dola $50, tani 10,000 zinagarimu dola milioni 500. Kama ukiongeza "silaha zinazolenga kwa usahihi ",vifaru, machine gani, makombora ya masafa na silaha nyinginezo -unapata dola nyingine milioni 500 kwa ujumla dola bilioni 1”, Prigozhin alikokotoa mahesabu .

    Hata kama mfanyabiashara ana bilioni ya kununua risasi, taifa ambalo lina gesi halimpatii, hii basi inakuwa sio biashara, bali utawala wa taifa. Kwasababu sina matyamanio ya kisiasa, nipe risasi.”aliongeza.

    Prigozhin alirekodi video nyingine kutoka juu yap aa la jengo la gorofa tisa katika mtaa wa Shchedra sehemu ya kusini mwa wa Bakhmut.

    BBC imetambua kijiografia eneo alipopiga vido yake: Nyuma yake kuna kanisa la Kiinjilisti katika mtaa wa Gorky Street yapata mita 700 meters feneo alipochukua video, mahala unapotitirikia Mto Bakhmutka

    Mwishoni mwa mwezi wa Februari, Prigozhin alichapisha video kadhaa alipokuwa katika eneo Artyomovsk huku alifungua champagne ya ushindi akisherehekea kasi ya ushindi wa mamluki wake katika eneo hilo.

    Wakati hayo yakijiri katika taarifa zake za mara kwa mara kuhusu vita vya Ukraine, mapema hii leo ,shirika la ujasusi la Uingereza liliripoti kuwa kwa kipindi cha siku nne, mamluki wa Urusi wameweza kuchukua udhibiti wa mengi kati ya maeneo ya mashariki mwa Bakhmut, hukujeshi la Ukraine likishikilia eneo la magharibi mwa mji huo , linalogawanya mto Bakhmutka.

    Unaweza pia kusoma:

    • Kiongozi wa mamluki Urusi asema mji wa Bakhmut
    • Bakhmut: Mapigano yanaendelea barabarani lakini Urusi haidhibiti - naibu meya
    • Vita vya Ukraine: Mkuu wa Wagner alishtumu jeshi la Urusi kwa 'usaliti' katika vita vya Bakhmut
  3. Ni nini alichosema Mkurugenzi Mkuu wa BBC Tim Davie said kuhusiana na Gary Lineker, mtangazaji maarufu wa soka?

    g

    Kufuatia kusimamishwa kwa utangazaji wa kipindi cha moja kwa moja cha soka -Match of the Day, kwa Gary Lineker kutokana na maoni aliyotoa akishutumu sera mpya ya serikali kuhusu wahamiaji.

    Mkurugenzi mkuu wa BBC Tim Davie ametoa kauli mbali mbali kama ifuatavyo:

    • Davie aliomba msamaha kwa walipakodi kwa kuvurugwa kwa mangilio wa michezo baada ya mtangazajiwengine kukataa kwenda hewani kwa kumuunga mkono Lineker
    • "Tunafanya kazi kwa bidi kutatua hali hii," alisema
    • "Mafanikio kwangu ni kutejesha hewani Gary," Daviealiongeza
    • Hapajakuwepo na "uenezaji " wa chama chochote cha kisiasa

    Awali BBC ilieleza kuwa maoni yake Lineker "katika siku za hivi karibuni kwenye mtandao wa kijamii yanakwenda kinyume na muongozo wa shirika hili". iliongeza kuwa "hastahili kuonekana kuwa na msimamo kuhusu masuala ya kisiasa au mizozo ya kisiasa ".

    BBC ilimtaka Lineker akae kando baada ya "majadiliano marefu na Gary na kikosi chake katika siku za hivi karibuni". "Na hadi pale kutakuwa na msimamo uliokubalika na wa wazi kuhusu matumizi yake ya mitandao ya kijami" ilisema taarifa ya BBC na kuendelea kusema kuwa : "Inapokuja kuhusu kuongoza utangazaji wa soka na michezo, Gary hana mfano. "Hatusemi kuwa Gary hastahili kuwa na maoni au kwamba hawezi kuwa na maoni kuhusu masuala yanayomuhusu.

  4. Utafiti 'tata' wa mayai ya uzazi yanayotengenezwa kwa seli za kiume

    utafiti

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mtafiti wa Kijapan amesema kuwa ameweza kutengeneza mayai ya uzazi kwa kutumia seli za kiume za panya.Hayash ameyasema hayo katika mkutano wa kimataifa kuhusu jeni za urithi mjini London..

    Utafiti huo ambao uko katika hatua zake za mwanzo, unahusisha kubadili kile kinachoitwa kisayansi jinsia ya XY Kromosomu ( XY sex chromosomes) kutoka kuwa ya kiume na kuwa ya kike au kutoka kwa mayai ya uzazi ya kike.

    Profesa Katsuhiko Hayashi kutoka chuo kikuu cha Osaka nchini Japan anasema anaendelea na juhudi za kutengeneza tiba ya kutokuwa na uwezo wa kuzaa au kuzalisha.

    Taarifa ya utafiti huu ambayo imechapishwa kwenye jarida la masuala ya kisayansi Nature, imeibua mjadala huku wengi wakisema kuwaiwapo utafiti huu utakuwa na ufanisi kuna uwezekano wa "wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja" wa jamii ya LGBTQ wanaweza kuwa na watoto kwa njia hiyo.

    Profesa George Daley wa Chuo kikuu cha tiba cha Harvard Medical , ambaye hakuhusika katika utafiti huu, alisema kuwa bado utafiti huu una safari ndefu kabla ya jamii kukubali uamuzi wa aina hiyo.

    "Kazi ya Katsuhiko Hayashi haijachapishwa lakini ni ya kufurahisha. Itakuwa vigumu kuwafanya watu kama panya," alisema. Hatujaelewa bado kuhusu baiolojia ya seli za binadamu(kuhusu uundwaji wa tishu za uzazi) iwapo zinaweza kutengenezwa saw ana kazi ya Hayashi katika panya .''

    Maelezo ya utafiti huu yaliwasilishwa katika mkutano wa uhariri wa jeni za binadamu uliofanyika katika taasisi ya Crick mjini London.

  5. Urusi kuipatia Iran ndege aina ya Su-35 - Vyombo vya habari

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Urusi itaipatia Iran ndege za mapigano aina ya Su-35. Serikali ya Iran imetangaza kuwa hayo yalikuwa makubaliano yaliyofikiwa baina ya utawala wa Tehran na Moscow, hata hivyo upande wa Urusi bado haujatoa tangazo rasmi kuthibitisha mkataba huu.

    ''Ndege za vita Su-35 kiufundi zinafaa kutumiwa na Iran, na Iran hatimaye imeidhinisha makubaliano kuhusu ununuzi wake ," kampuni ya televisheni na terio ya Iran, IRIB ilinumnukuu mfanyakazi ambaye hakutajwa jina wa oubalozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa akisema.

    Chanzo cha habari cha vyombo vya habari vya Iran hakikumtaja kiasi cha fedha kitakachotumiwa kununua na hakikutoa maelezo zaidi. Aliongeza kuwa Iran pia inataka kununua ndege za kijeshi kutoka mataifa mengine mbali mbali.

    Kikosi cha anga cha Iran kina ndege chache tu za mapigano – ambazo ni za Urusi na nyingine ni zaKimarekani zenye mtindo wa kizamani, masalia ya tangu enzi ya mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ya mwaka 1979.

    Mnamo mwaka 2018, Iran ilitangaza kwamba ilikuwa imeanza utengenezaji wa ndege zake za kivita aina zaKowsarjet. Baadhi ya wataalamu wanasema Kowsar is ni nakala ya F-15, ambayo ilianza kutengenezwa nchini Marekani katika miaka ya 1960.

  6. Watu wanane wafa maji wakichimba dhahabu magharibi mwa Tanzania

    Wachimbaji wadogo nane wamepoteza maisha Magharibi mwa Tanzania baada ya shimo waliloingia kuchimba dhahabu kujaa maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha katika mkoa wa Geita.

    Aidha mmoja alinusurika huku vikosi vya uokoaji vikifanikiwa kuopoa miili nane kutoka kwenye shimo hilo jana.

    Mamlaka zinasema wachimbaji hao waliingia kinyume cha sheria kutafuta dhahabu katika handaki lisilokuwa salama ambalo lilikuwa na leseni ya shughuli za utafiti pekee.

    Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Safia Jongo aliiambia BBC kuwa kazi ya uokoaji ilifungwa jana ambapo walipata miili nane na mtu mmoja alitoka akiwa hai.

    "Walichokifanya ni kuhatarisha maisha yao, na watu wengi, haswa vijana huchukua hatari kama hizi kwa kuingia maeneo hatarishi bila kujali athari...

    "...huwa tunawasihi wasiingie kwenye mashimo ikiwa hawana leseni ya shughuli hiyo. Tahadhari za usalama huwekwa wakati mtu ana leseni ya kufanya kazi, vinginevyo unapovamia unakuwa katika hatari kubwa," alisema kamanda huyo.

    Kamanda huyo pia amewaonya wachimbaji ambao wamekuwa wakivamia mashimo yenye miliki kuacha kwa sababu ni kinyume na sheria.

    Geita ni miongoni mwa maeneo yanayoripotiwa kuwa na akiba kubwa ya dhahabu katika upande wa magharibi mwa Tanzania.

    Soma taarifa zaidi kuhusu ajali za migodi tanzania:

    • Wachimbaji mgodi 15 waliokwama ardhini waokolewa Tanzania
    • Nyarugusu wapongezwa kwa uokozi
  7. Mwanamuziki wa Afrika Kusini Costa Titch afariki akiwa jukwaani

    g

    Chanzo cha picha, Costa Ditch/Twitter

    Mwanamuziki wa muziki wa rap nchini Afrika kusini Costa Titch ameripotiwa kufariki huku akiwa jukwaani , vimeripoti vyombo vya habari.

    Mwanamuziki huyo ambaye jina lake halisi ni Costa Tsobanoglou ameripotiwa kuanguka na kufa hapo hapo wakati alipokuwa akitumbuiza jukwaani katika tamasha la muziki Jumamosi usiku.

    Costa ambaye pia ni mchezaji densi alizaliwa mwaka 1995 katika jimbo la Mpumalanga anafahamika kwavibao vyake maarufu mkiwemo kile cha Nkalakatha na Activate.

    Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na mtangazaji wa taarifa za burudani nchini humo Phil Mphela kwenye ukurasa wake wa Twitter, usiku na kufuatiwa na jumbe za rambirambi zilizotiririka kwenye ukurasa huo:

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

    Mwanamuziki wa Tanzania Ommy Dimpoz pia amemuomboleza Costa Tich kupitia kurasa wake Instagram:''kabla ya kufanikiwa kwenye Uimbaji alikuwa a very talented Dancer nitamkumbuka na nashukuru kwa mchango wake chanya kwenye video yangu ya Wanjera!

    Rest With Angels Brother! Bongo Fleva itakukumbuka kwa Mchango wako'', aliandika Dimpoz

    Ruka Instagram ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa Instagram ujumbe

  8. Israel yashuhudia mojawapo ya maandamano makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Suala la mageuzi ya mfumo wa mahakama linaigawanya sana jamii ya Waisraeli

    Maelfu kwa maelfu ya Waisraeli wanashiriki maandamano ambayo baawanayataja kuwa maandamano makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo.

    Maandamano dhidi ya mipango ya serikali ya kufanya mageuzi makubwa ya mfumo wa mahakama yamekuwa yakeendelea kwa wiki 10.

    Idadi kubwa ya waandamanaji wamejitokeza katika miji kama vile Haifa, hukutakriban waandamanaji 200,000 wakiaminiwa kuandamana katika mitaa ya mji mku Tel Aviv.

    Wakosoaji wanasema mageuzi yatadhoofisha demokrasia lakini Waziri mkuu Benjamin Netanyahu anasema mabadiliko yaliyopangwa ni bora kwa wapiga kura.

    Waandalizi wanasema waandamamanaji wanaounga mkono demokrasia wameandamana katika mitaa mbali mbali kote Jumamosi, katika kile gazeti la IsraeliIsraeli Haaretz limeita maandamano makubwa zaidi ya demokrasia katika historia ya nchi".

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Waandamanaji wapatao 200,000 wameripotiwa kuandamana katika mitaa ya tel Avit
  9. Vita vya Ukraine:Ukraine yaanzisha uchunguzi wa uhalifu baada ya mashambulio ya makombora ya Urusi

    shambulio

    Chanzo cha picha, Ukrainian general prosecutor's office

    Maelezo ya picha, Athari za mashambulizi ya makombora katika Zaporozhye

    Ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu nchini Ukraine imeanzoshishauchunguzi kwa ajili ya mashitakakuhusina na mashambulio ya makombora ya Urusi yaliyopiga katika miji na vijijikwenye majimbo yaUkraine ya Donetsk na Zaporozhye

    Katika jinbo la Donetsk , kulingana na abari za hivi punde, vikosi vya Urusi vilitumia makomboraaina kubwa za bunduki ambazo kwa kawaida hufyatua vilipuzi vya kemikali na Uragan MLRS. Mji wa Konstantinovka na vijiji viwili vilipigwa na kuungua. Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 51 ailiuawa huku raia wengine wanne wakijeruhiwa.

    Kutokana na mashambulio ya Zaporozhye, uchunguzi wa kesi ya uhalifu imeanzishwa kutokana kuhusiana na iwapo kulikuwa na ukikaji wa sheria na taratibu za vita.

    Ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu inaamini kuwa makombora mawili ya masafa aina ya S-300 yalitumika katika mashambulio katika jimbo la Zaporozhye Matikeo yake , majingo ya kiwanda yaliangamizwa na bomba la gesi likaharibiwa.

    Ukrainian general prosecutor's office

    Chanzo cha picha, Ukrainian general prosecutor's office

    Urusi na Ukraine: Mengi zaidi:

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  10. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo Jumapili tarehe 12.03.2023