Uchaguzi Nigeria 2023: Shughuli ya kupiga kura yaanza katika uchaguzi muhimu
Mamilioni ya Wanigeria wakipiga kura katika uchaguzi wenye ushindani mkali zaidi wa urais tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi.
Moja kwa moja
Maelfu ya wafungwa wenye tatoo katika gereza kubwa zaidi la El Salvador
Kundi la kwanza la wafungwa wanaoshukiwa kuwa wajumbe wa genge katika El Salvadorwamehamishiwa katika gereza kubwa, huku ambalo limeandaliwa na rais wa nchi hiyo Nayib Bukele kwa ajili ya vita dhidi ya uhalifu
Maelfu kwa maelfu ya washukiwa wa magenge ya uhalifu wamekuwa wakizingirwa kufuatia hali ya dharura ya kitaifa iliyotangazwa baadaya kuongezeka kwa kiwango cha juu cha mauaji na ghasia nyingine za uhalifu.

Chanzo cha picha, Reuters
Hatimaye gereza lilikuwa na wafungwa zaidi ya 40,000.
Picha zinaonyesha kikundi cha wafungwa wengi – wenye michoro ya tatoo bila viatu – wakiongozwa kuingia ndani ya gereza.

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, Reuters
Wafungwa wanaondoka mahala walipokuwa wameketi sakafuni huku mikono yao ikiwa nyuma ya vichwa vyao vilivyokatwa nywele, wakiwa wamekaribiana pamoja, kabla ya kupelekwa katika mahabusu zao.

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, Reuters
Rais Bukele alituma ujumbe wa Twitter kwamba kundi la kwanza la watu 2,000 walisafirishwa "alfajiri, katika operesheni moja" kuelekea katika kituo cha kuwafunga magaidi, ambacho amesemani jela kubwa zaidi kuliko jela zote za Marekani.
"Hii itakuwa nyumba yao mpya, ambamo wataishi kwa miongo, wote wakiwa wamechanganyika, ambapo hawataweza kufanya madhara yoyote kwa watu."

Chanzo cha picha, Reuters
Uchaguzi Mkuu Nigeria 2023: Kwa picha
Raia wa Nigeria wamekuwa wakijitokeza kupiga kura katika uchaguzi muhimu nchini mwao.
Shughuli ya kupiga kura imeanza kote nchini Nigeria, huku mamilioni ya Wanigeria wakipiga kura katika uchaguzi wenye ushindani mkali zaidi wa urais tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi. Raia zaidi ya milioni 87 wana haki ya kupiga kura.
Hizi ni baadhi ya picha za shughuli ya uchaguzi kutoka kwa waandishi mbali mbali wa BBC walioko katika maeneo mbalimbali ya nchi:


Maelezo ya picha, Francis Nwogu , ambaye alipiga kura katika uchaguzi uliopita, ana wasi wasi kura yake huenda isihesabiwe. Anataka serikali na tume ya uchaguzi kuheshimu chaguo la watu. 
Chanzo cha picha, BBC/ Gift Ufuoma
Maelezo ya picha, Kulikuwa na jazba jijini Lagosi baada ya kucheleweshwa kwa upigaji kura 
Chanzo cha picha, BBC/ Gift Ufuoma

Chanzo cha picha, BBC/Simi Jolaos
Maelezo ya picha, Baadhi ya waangalizi wa uchaguzi ya Nigeria (Inec), wameelezea kuwa matatizo ya ukosefu wa vifaa ilikuwa ni moja ya sababu zilizosababishwa kuchelewa kwa upigaji kura katika kituo alichopigia kura mgombea wa urais Bola Tinubu 
Chanzo cha picha, BBC/Yemisi Adegoke
Maelezo ya picha, Hadiza Abubakar (pichani), 40,ni mama wa watoto wanane na anasema uchaguzi huu ni muhimu kwasababu anataka kurejea nyumbani , baada ya kufurushwa na wanamgambo wa jihadi . kwa sasa anaishi katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Adamawa kaskazini mwa Nigeria Soma zaidi kuhusu uchaguzi wa Nigeria:
- Mamilioni ya Wanigeria wapiga kura katika uchaguzi wenye ushindani mkali zaidi kuwahi kushuhudiwa
- Uchaguzi wa Nigeria 2023: Ni nani yuko kwenye kinyang'anyiro cha kuiongoza Nigeria?
‘Kikao cha fedha’ cha G20 huenda kikamalizika bila taarifa ya mwisho kutokana na mzozo wa lugha ya vita

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Janet Yellen anasema kutolaani vita katika taarifa ya mwisho ya G20 itakua ni hatua ya kuelekea mwelekeo mbaya Kulaaniwa kwa vita vya Urusi ni muhimu katika taarifa ya pamoja kufuatia mkutano wa G20 wa wakuuwa masuala ya fedha na benki,amesema waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen.
Ninaamini kuwa taarifa ya mwisho ya kikao hicho lazima iwe taarifa inayolaani vita vya Urusi. Tumefanya hili katika nyakati za nyumba, katika Bali, na hili ndilo ninaloliangalia kama jambo muhimu sana,” alisema Janet Yellen.
Kauli yake inakuja huku kukiwa na uwezekano wa kutokubaliana katika maneno yanayopaswa kuandikwa katika kauli ya mwisho ya kikao hicho.
India, ambayo ni mwenyekiti wa G20,inasisitiza kuhusu umuhimu wa kuondoa neno ‘’vita’’ katika taarifa ya mwisho wameliambia shirika la habari la Reuters wajumbe wa wan chi hiyo.
Serikali ya Delhi imekuwa na msimamo wa kutokuwa na mafungamano yoyote kuhusu vita huku ikiongeza ununuzi wa mafuta yake kutoka Urusi.
Sawa na Uchina, India ilikuwa ni miongoni mwa nchi ambazo zilikataa kupigia kura wito wa Umoja wa Mataifa unaoitaka Urusi kumaliza uhasama na kuondoa vikosi vyake Ukraine.
Wengi wa wawakilishi wa G20 wanalaani vikali vita nchini Ukraine, taarifa ilisema. “Kulikuwa na maoni tofauti na tathmini tofauti ya hali na vikwazo,” ilisema. Urusi kama mwanachama wa G20 inapinga taarifa hiyo.
Mkutano huo uliofanyika Bangalore India unamalizika leo Jumamosi jioni.
Habari za hivi punde, Urusi na Ukraine: Uvamizi wa anga kote Ukraine
Jumamosi asubuhi, milio ya mashambulio ya anga imesikika kkote nchini Ukraine, kulingana na wavuti rasmi unaowapasha habari raia.
Mapema, maafisa wa Ukaraine waliripoti kwamba Urusi imeongeza mara dufu idadi ya meli zake za kivita katika Bahari nyeusi.
Kulingana na jeshi, meli nane za kijeshi zipo kwa sasa baharini, ikiwa ni pamoja na zana za kivita na makombora ya aina ya masafa ya Caliber.
Hii kulingana na kamanda wa Majeshi ya Ukraine, huenda inaashiria maandalizi ya shambulio jipya la Urusi dhidi ya Ukraine.
Soma zaidi taarifa kuhusu uvamizi wa Ukraine:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Vita vya Ukraine: Zelensky ataka mkutano na Xi Jinping kufuatia mpango wa amani wa China

Chanzo cha picha, AFP VIA GETTY IMAGES
Rais wa Ukraine Ukraine Volodymyr Zelensky amesema anapanga kukutana na kiongozi wa Uchina Xi Jinping kujadiliana naye kuhusu mapendekezo ya Beijing kuhus namna ya kumalizika kwa viyta nchini Ukraine.
Akizungumza katika maadhimisho ya kwanza ya uvamizi kamili wa Urusi nchini kwake, Bw Zelensky alisema pendekezo linaonyesha kuwa Uchina inajihusisha katika kutafuta amani.
"Kusema kweli ninataka kuamini kwamba Uchina haitaipatia silaha Urusi,"alisema.
Mpango wa Uchina unatoa wito wa mazungumzo ya amani na kuheshimu hadhi ya taifa.
Hatahivyo, waraka wa pendekezo hilo wenye vipengele vinne hausemi lolote kwa Urusi inapaswa kuondoa wanajeshi wake Ukraine, na haulaani matumizi ya"vikwazo vya jumla", katika kile kinachoonekana kama ni kufunikwa kwa ukosoaji wa washirika wa Ukraine wa Magharibi.
Maafisa nchini Uchina bado hadi sasa hawajajibu wazi wito wa Zelensky wa mkutano na Bw Xi.
Wakati huo huo, Urusi ilisifu mapendekezo ya amani ya Uchina. "Tuna mitizamo inayofanana na wa Beijing," ilisema taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Urusi.
Unaweza pia kusoma:
- Vita vya Ukraine: China inaisaidia Urusi kwa msaada gani?
Uchaguzi Nigeria 2023: Shughuli ya kupiga kura yaanza katika uchaguzi muhimu

Chanzo cha picha, AFP
Shughuli ya kupiga kura imeanza kote nchini Nigeria, huku
Mamilioni ya Wanigeria wakipiga kura katika uchaguzi wenye ushindani mkali zaidi wa urais tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi.
Miongoni mwa masuala muhimu yanayozingatiwa na wapiga kura katika uchaguzi huu ni suala la mafuta.
Wapigakura katika Port Harcourt amkako ni kitovu cha mavuta kusini mwa Nigeria wameiambia BBC kwamba wanataka kuona mabadiliko katika nchi yao
Benibo,ambaye ni mpigaji kura wa mara ya kwanza (katika picha hapa chin),ameazimia kupiga kura yake kuleta mabadiliko chanya kama anavyosema “mahangaiko yamepita kiasi”.

Chanzo cha picha, BBC/Karina Igonikon
Francis Nwogu (chini), ambaye alipiga kura katika uchaguzi uliopita, ana wasi wasi kura yake huenda isihesabiwe. Anataka serikali na tume ya uchaguzi kuheshimu chaguo la watu .

Chanzo cha picha, BBC/Karina Igonikon
Victoria Briggs (chini) anataka serikali mpya kufanya bei za chakula ziwe rahisi, kuwasaidia wastaafu na kutoa fursa za ajira kwa vijana.

Chanzo cha picha, BBC/Karina Igonikon

- Taarifa zaidi kuhusu uchaguz mkuu wa Nigeria 2023:
- Uchaguzi wa Nigeria 2023: Ni nani yuko kwenye kinyang'anyiro cha kuiongoza Nigeria?
- Mamilioni ya Wanigeria wapiga kura katika uchaguzi wenye ushindani mkali zaidi kuwahi kushuhudiwa
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo Jumamosi 25.03.2023
