Mtoto wa Museveni aapa kuwa atakuwa rais Uganda
Mtoto wa Rais wa muda mrefu wa Uganda Yoweri Museveni kwa mara nyingine tena amezua tetesi kuwa yuko katika mstari wa kumrithi baba yake.
Jenerali Muhoozi Kainerugaba ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba "atalipa fadhila kwa nchi yake" kwa kuwa rais.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Bw Museveni amekuwa mamlakani tangu 1986 na kuna tetesi za mara kwa mara kwamba Jenerali Kainerugaba anaandaliwa kumfuata.
Mnamo Mei mwaka huu, mwanajeshi huyo aliuliza kwenye Twitter ikiwa watu walidhani anafaa kugombea urais na mapema mwezi huu aliandika: "Kwa upinzani wa Uganda, baada ya baba yangu, nitawashinda vibaya katika uchaguzi wowote, Waganda wananipenda zaidi kuliko nyinyi''
Jenerali huyo mwenye umri wa miaka 48 si mgeni kwenye mabishano kwenye Twitter.
Mwanzoni mwa Oktoba, alitishia katika ujumbe wake wa Twitter kuivamia nchi jirani ya Kenya, na hivyo kusababisha kuomba radhi kwa umma na mikutano ya kidiplomasia ili kuthibitisha uhusiano huo.
Kisha baadae Rais Museveni kuagiza kwamba akome kutoa maoni yake kuhusu masuala ya serikali kwenye Twitter, Jenerali Kainerugaba alisema kwamba "hakuna mtu atakayempiga marufuku kwa chochote".









