Daktari Mtanzania afariki kutokana na maambukizi ya Ebola Uganda
Daktari raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 37 ambaye amekuwa akisomea Shahada ya Uzamili ya Udaktari katika Upasuaji katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola, Chama cha Madaktari wa Upasuaji Uganda kimetangaza.
Moja kwa moja
Habari za hivi punde, Urusi yasema wanajeshi wake wametoroka katika mji muhimu wa mashariki wa Lyman
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Ukraine wafika Lyman
Wizara ya ulinzi
ya Urusi imesema imewaondoa wanajeshi wake katika mji wa kimkakati wa Lyman
mashariki mwa Ukraine.
"Kwa sababu
ya tishio la kuzingirwa askari washirika wameondolewa kutoka Krasnyi Lyman hadi
kwenye sehemu nzuri," inasema, ikinukuliwa na mashirika ya habari ya
serikali ya Urusi.
Krasnyi
(Nyekundu) Lyman lilikuwa jina la zamani la Soviet la Lyman, ambalo vikosi vya Ukrain
vinasema waameingia.
Urusi inawaita
wanajeshi wake "walioshirikiana" na wapiganaji wa ndani wanaoungwa
mkono na Moscow.
Mwanamuzi Chike: ‘Mimi sio zilionea au bilionea’
Chanzo cha picha, Michael Tubes Creations
Maelezo ya picha, Mwanamuziki wa Nigeria Chike
Mwimbaji wa Nigeria Chike amezungumza na kipindi cha BBC cha
This is Africa radio kuhusu shinikizo la kifedha analokumbana nalo baada ya
mafanikio yake kimuziki na kutoa albamu yake, The Brother's Keeper.
Familia yake inamgeukia wakati maamuzi makubwa yanahitajika
kufanywa kwa sababu "yeye atalipa", alisema.
"Mimi sio bilionea au bilionea, mbali na hilo,"
aliongeza, akisema ana furaha.
Kwa hakika, jina la albamu yake mpya ni rejeleo la moja kwa
moja la jinsi uhusiano wake na marafiki na familia umebadilika kufuatia
mafanikio yake kama msanii wa muziki.
Chike alikuja kujulikana kupitia maonyesho ya talanta ikiwa
ni pamoja na The Voice Nigeria, na katika hali isiyo ya kawaida, ameweza
kujitengenezea taaluma yake mwenyewe baadae, na nyimbo kadhaa zilizovuma kwa
jina lake zimeshinda tuzo ya albamu ya kwanza, Boo of the Booless.
Lakini pamoja na mafanikio makubwa huja wajibu mkubwa
anasema: "Kwa maisha haya mapya sina budi kumtazama kila mtu aliye karibu
nami. Huo ndio ukweli sasa hivi."
Idadi ya walioambukizwa Ebola Uganda yafikia 38 - Wizara ya afya
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Ebola
Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya ebola kufikia sasa
imefikia watu 38
Kulingana na ripoti mpya ya wizara ya afya nchini Uganda, aidha
idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo imefikia 8 baada ya watu
wengine watatu kufariki.
Watu hao waliofariki wameripotiwa kutoka eneo la Mubende.
Daktari Mtanzania aliyekuwa akisoma nchini Uganda ni
miongoni mwa waliofariki kutokana na virusi vya Ebola.
Raia huyo huyo mwenye umri wa miaka 37 alikuwa akisomea
Shahada ya Uzamili ya Udaktari katika Upasuaji, akiwa mwanafunzi wa kimataifa.
Chama cha madaktari wa upasuaji nchini Uganda kimetoa risala
za rambirambi kwenye akaunti zao za Twitter.
Mapema wiki hii, wizara ya afya ilisema kuwa wahudumu sita
wa afya walipimwa na kukutwa na virusi vya Ebola. Inasemekana wengine
waligusana na muathiriwa wa kwanza wa ebola
Wahudumu wengi wa afya walioshughulikia kesi ya kwanza
walikuwa wanafunzi. Baadaye walitangaza kuwa walikuwa kwenye mgomo, wakitaja
ukosefu wa vifaa vya kujikinga na marupurupu yakujiweka hatarini..
Siku ya Ijumaa, wizara ilitangaza kuwa mlipuko wa Ebola
ulikuwa umeenea hadi wilaya ya nne.
Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa jumla ya kesi
zilizothibitishwa zimefikia thelathini na tano, na vifo vinane.
Watu wawili hadi sasa wamepona ugonjwa huo wa virusi,
kulingana na mamlaka ya afya.
Rais Yoweri Museveni amefutilia mbali kufungiwa kwa maeneo
yaliyoathiriwa.
Mlipuko wa Ebola nchini Uganda unahusisha aina adimu ya
virusi vya Sudan ambayo hakuna chanjo yake.
Bilionea wa teknolojia Elon Musk azindua aina mpya ya roboti yenye umbo la binaadamu
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe, 1
Roboti ya Optimus iliokuwa jukwaani katika hafla hiyo ilionekana ikipungia watu mkono na kunyanyua magoti yake.
Afisa mkuu mtendaji amesema roboti hiyo inaendelea kufanyiwa kazi lakini huenda ikauzwa kwa umma katika miaka michache ijayo.
Roboti za Tesla zitafanyiwa majaribio katika kazi za mkono kwenye viwanda vya kutengeneza magari, wahandisi wa kampuni hiyo wanasema.
Roboti hiyo ilisukumwa kwenye jukwaa katika hafla ya kila mwaka ya kampuni ya Tesla kwenye maonyesho ya intelijensia bandia.
Watu walionyeshwa video ya Optimu akifanya kazi nyepesi kama vile kumwagilia mimea maji, akibeba maboxsi na kunyanyua vyuma.
Musk amesema roboti hizo zitaundwa kwa wingi kwa bei ya chini ya $20,000 (£17,900), na zitapatikana sokoni katika muda wa miaka mitatu hadi mitano ijayo.
Mmiliki huyo wa kampuni ya Tesla amezungumzia "mustakabli wenye neema".
"Ni mageuzi muhimu ya ustaarabu kama tunavyooufahamu," aliongeza kusema.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe, 2
Erik ten Hag: 'Ninamuamini Maguire'
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Maguire
Meneja wa Manchester United Erik ten Hag anasema bado
anamuamini Harry Maguire licha ya beki huyo kukosolewa
Maguire amekuwa akidhihakiwa na baadhi ya mashabiki wake
kwenye majukumu ya klabu na nchi msimu huu na alifanya makosa katika ufungaji
wa mabao mawili ya Ujerumani katika sare
ya 3-3 ya England siku ya Jumatatu.
"Ninamuunga
mkono kwa sababu ninamwamini," alisema Ten Hag.
"Inamhusu.
Nina hakika anaweza kufanya hivyo. Ataligeuza hili. Nina hakika sana kuhusu
hilo."
Ten Hag
amewapendelea Lisandro Martinez na Raphael Varane kama safu yake ya ulinzi ya
kati, huku mchezaji Bruno Fernandes akivalia kitambaa cha unahodha mbele ya
Maguire katika wiki za hivi karibuni.
Maguire amecheza
mechi tatu pekee za Premier League msimu huu.
"Hata baada
ya kutokuwa kwenye timu, alifanya mazoezi vizuri," alisema mkufunzi Ten
Hag kuhusu mchezaji huyo mwenye wa umri
wa miaka 29 .
"Lakini
muhimu zaidi, ubora ulikuwepo. Unaona kazi yake, takribani mechi 50 akiwa na
England. Amefanya vizuri sana kwa Leicester na Manchester United. Unachokiona
ni kwamba ana uwezo wa juu."
Luke Shaw,
mchezaji mwenza wa Manchester United na Uingereza, alisema mapema wiki hii
kwamba Maguire amekosolewa "zaidi ya nilivyowahi kuona hapo awali kwenye
soka".
Wanajeshi wa UKraine wauzingira mji uliotekwa na Urusi
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Urusi Lyman
Kundi kubwa la Wanajeshi wa Urusi huko Lyman
"limezingirwa" na makazi karibu na mji huo yamekombolewa tena,
anasema Serhiy Cherevatyi, msemaji wa vikosi vya Ukraine mashariki.
Aliiambia TV ya Ukraine "data zetu zinaonyesha kwamba
karibu wanajeshi 5,000 hadi 5,500 wa Urusi waliokuwa Lyman wamezingirwa na
vikosi vya Ukraine", lakini alisema idadi hiyo ilikuwa chini kwa kwa
sababu ya mashambulizi ya hivi karibuni ambapo wanajeshi "wengi" wa Urusi
waliuawa au kujeruhiwa.
Cherevatyi alisema majaribio yote yanayoendelea ya wanajeshi
wa Urusi "yameshindwa". Pia alizungumza juu ya umuhimu wa Lyman, ambao,
iwapo utachukuliwa na wanajeshi wa
Ukraine, ingewaruhusu kusonga mbele kwenye Kreminna na Severodonetsk, ambazo
zote ni ngome kuu zinazoshikiliwa na Urusi.
"Pia ni muhimu sana kisaikolojia, kwa sababu - kama
Rais Zelensky alivyosema jana - vikosi vya Ukraine vinaanza kuingia kwa nguvu
katika maeneo yaliotekwa - na sio kutetea tu."
Hata hivyo operesheni ya kijeshi "bado haijaisha,"
alihitimisha.
Video sasa imeibuka inayodaiwa kuwaonyesha wanajeshi wa Ukraine wakiinua bendera ya taifa ya nchi hiyo yenye rangi ya buluu na njano kwenye lango la mji huo, ambapo maelfu ya wanajeshi wa Urusi wanaripotiwa kuzingirwa.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Habari za hivi punde, Ecowas yalaani mapinduzi ya kijeshi Burkina Faso
Majirani wa Burkina Faso wamelaani mapinduzi ya wazi ya
Ijumaa, wakisema "haikuwa sawa" kwa waasi wa jeshi kunyakua mamlaka
wakati nchi hiyo ilipokuwa ikitafuta utawala wa kiraia.
Kundi la eneo la Ecowas lilielezea kuondolewa kwa kiongozi
Luteni Kanali Paul-Henri Damiba kama "kinyume cha katiba".
Hii ni mara ya pili mwaka huu jeshi la nchi hiyo kunyakua
madaraka.
Mara zote mbili, viongozi wa mapinduzi walisema walilazimika
kuingilia kati kwa sababu usalama wa taifa ulikuwa mbaya sana.
Burkina Faso inadhibiti 60% pekee ya eneo lake, wataalam wanasema, na
ghasia za Kiislamu zinazidi kuwa mbaya.
Akiwa amezungukwa na wanajeshi waasi, kiongozi huyo wa jeshi alitangaza kwenye TV ya taifa Ijumaa
jioni kwamba wamemfukuza kiongozi wa kijeshi Lt Kanali Paul-Henri Damiba,
kuivunja serikali na kusimamisha katiba.
Ibrahim Traoré alisema kushindwa kwa Luteni Kanali Damiba
kukabiliana na waasi wa Kiislamu ndio sababu ya mapinduzi hayo .
Biden: "Marekani imejiandaa kikamilifu kutetea kila inchi moja ya eneo la Nato".
Chanzo cha picha, reuters
Maelezo ya picha, Biden amuonya Putin
Rais Joe Biden ameionya Urusi kwamba Marekani haitatishwa na
vitisho vya kizembe baada ya Vladmir Putin kutangaza kunyakua maeneo manne ya
Ukraine inayokaliwa kwa mabavu.
Rais Biden alilaani "maneno ya kizembe na vitisho"
vya mwenzake wa Urusi, lakini akaongeza kuwa Putin "hatatutisha".
"Marekani na washirika wake hawatatishika," Biden
alisema katika Ikulu ya White House.
Kisha alizungumza na kiongozi wa Urusi moja kwa moja,
akinyoosha kidole chake kwenye kamera, na kusema kwamba "Marekani
imejiandaa kikamilifu, pamoja na washirika wetu wa Nato, kutetea kila inchi
moja ya eneo la Nato".
"Bwana Putin, usielewe vibaya ninachosema: kila
inchi."
Muda mfupi baadaye, afisa mkuu wa usalama wa taifa wa Biden
alisema kulikuwa na nafasi ya Moscow kutumia silaha za nyuklia, lakini
hakuonekana kuwa na tishio la karibu.
Daktari Mtanzania afariki kutokana na maambukizi ya Ebola Uganda
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe, 1
Daktari Mtanzania aliyekuwa akisoma nchini Uganda amefariki
kutokana na virusi vya Ebola, waziri wa afya wa Uganda Dkt Jane Ruth Aceng
amethibitisha.
Raia huyo huyo mwenye umri wa miaka 37 alikuwa akisomea
Shahada ya Uzamili ya Udaktari katika Upasuaji, akiwa mwanafunzi wa kimataifa.
Chama cha madaktari wa upasuaji nchini Uganda kimetoa risala
za rambirambi kwenye akaunti zao za Twitter.
Haijabainika jinsi Dkt Mohammed Ali aliambukizwa lakini kifo chake kinajiri saa
chache baada ya Wizara ya Afya siku ya Ijumaa kutangaza kwamba idadi ya
waliofariki kutokana na mlipuko wa Ebola nchini imeongezeka hadi saba.
“Ni kwa masikitiko makubwa tumepokea taarifa za kufariki kwa
Dk Mohammed Ali, raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 37 ambaye alikuwa
akisomea Shahada ya Uzamili ya Upasuaji katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha
Kampala. Dk. Ali alishindwa katika vita dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Ebola,”
Chama cha Madaktari wa Upasuaji Uganda kiliandika kwenye Twitter Jumamosi.
Waziri wa Afya, Dk Jane Ruth Aceng alisema Dk Ali alipimwa
na kuwa na Ebola Septemba 26, 2022 na alifariki dunia alipokuwa akipatiwa
matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Fort Portal. Alikufa saa 3
asubuhi siku ya Jumamosi.
“Dk Ali ndiye Daktari wa kwanza, na mhudumu wa afya wa pili
kuugua Ebola. Wa kwanza alikuwa mkunga kutoka Kliniki ya St Florence, kisa
kinachowezekana, kwa sababu alifariki kabla ya kupimwa,” Dkt Aceng alituma ujumbe wa Twitter Jumamosi.
Lakini mapema wiki hii, wizara ya afya ilisema kuwa wahudumu
sita wa afya walipimwa na kukutwa na virusi vya Ebola. Inasemekana wengine