Marubani wapitiwa na usingizi angani na kuzua 'kizaazaa' wakati wa kutua

Marubani wawili walipitiwa na usingizi ndege ikiwa juu kwa umbali wa futi 37,000 (11,000m), na kupitiliza njia ya kutua ndege, chapisho moja la masuala ya anga limeripoti.

Moja kwa moja

  1. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu kwa hii leo.

  2. Waziri Mkuu achukuliwa vipimo vya dawa za kulevya kutokana na kupenda 'kujirusha'

    Marin

    Waziri mkuu wa Finland amesema amefanyiwa vipimo vya dawa za kulevya, baada ya video mpya kuibuka zikimuonyesha kiongozi huyo akicheza muziki na mwigizaji wa pop wa Finland.

    Sanna Marin, 36, alikashifiwa wiki hii baada ya video kuvuja ikimuonyesha 'akijirusha', huku baadhi ya wanasiasa wakisema anafaa kupimwa kama anatumia dawa za kulevya.

    Katika mkutano na wanahabari leo siku ya Ijumaa, Bi Marin alisema amefanya vipimo hivyo na anatarajia kupokea majibu ya vipimo hivyo wiki ijayo.

    Marin

    Waziri mkuu alirudia kukanusha kuwa hajawahi kutumia dawa za kulevya. "Sikufanya chochote kinyume cha sheria," aliwaambia waandishi wa habari huko Helsinki.

    "Hata katika ujana wangu sijatumia aina yoyote ya dawa," Bi Marin alisema, akiongeza kuwa alichukua kipimo cha dawa kama hatua ya ziada ya kupunguza wasiwasi walionao watu.

    Waziri mkuu pia alisisitiza kwamba ana haki ya kudhaniwa kuwa hana hatia.

    Marin, aliyewahi kuwa kiongozi mkuu wa serikali mwenye umri mdogo zaidi duniani - cheo ambacho sasa kinashikiliwa na Rais wa Chile Gabriel Boric - amekuwa hafichi 'kujirusha', na mara nyingi amekuwa akipigwa picha akiwa kwenye sherehe mbalimbali za muziki.

    Video mpya ya sasa imezua mjadala mkali nchini humo.

  3. Bilionea Xiao Jianhua afungwa miaka 13 jela nchini China

    Xiao Jianhua, picha hii ni kutoka maktaba

    Chanzo cha picha, CUHK

    Maelezo ya picha, Xiao Jianhua, picha hii ni kutoka maktaba

    Bilionea wa China mwenye uraia wa Canada amehukumiwa kifungo cha miaka 13 jela nchini China na kampuni yake kutozwa faini ya zaidi ya $8bn (£6.7bn).

    Xiao Jianhua na kampuni yake ya Tomorrow Holdings walishtakiwa kwa ubadhirifu na hongo, mahakama ya Shanghai ilisema.

    Xiao - mmoja wa watu tajiri zaidi wa Uchina - alionekana mara ya mwisho akifukuzwa kutoka hoteli ya kifahari huko Hong Kong mnamo 2017.

    Hakukuwa na neno rasmi kutoka kwake tangu wakati huo, hadi ubalozi wa Canada uliposema mnamo Julai kuwa atakabiliwa na kesi.

    Kesi hiyo ilisemekana kuanza tarehe 4 Julai.

    Xiao na kampuni yake walipatikana na hatia ya ‘’kufyonza amana za umma kinyume cha sheria, kuvunja imani katika matumizi ya mali waliyokabidhiwa... [na] matumizi haramu ya fedha,’’ taarifa kutoka mahakama ya Shanghai iliyonukuliwa na AFP ilisema.

    Pia ilisema kampuni ya Tomorrow Holdings ilikuwa na hatia ya ‘’uhalifu wa hongo’’.

    Iliongeza kuwa Xiao na kampuni yake ‘’wamekiuka sana agizo la usimamizi wa fedha’’ na kuumiza usalama wa kifedha wa serikali’’.

    Mahakama ilisema Xiao na kampuni yake walikubali hatia na walitoa ushirikiano kwa mamlaka na hivyo adhabu yao ilipunguzwa.

  4. Jeshi la Urusi lajiandaa kukata mtambo wa nyuklia kutoka kwa gridi ya taifa - Ukraine inasema

    Mtambo wa nyuklia wa Zaporizhzhia

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Mtambo wa nyuklia wa Zaporizhzhia

    Kama tumekuwa tukiripoti, kampuni ya nishati ya nyuklia ya Ukraine Enerhoatom imesema kwamba wanajeshi wa Urusi wanaodhibiti kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhya huenda wanapanga kukitenganisha na njia zinazoingiza nishati katika mfumo wa nishati wa Ukraine katika siku za usoni.

    Enerhoatom amechapisha kwenye mtandao wa Telegram ikionya kwamba jeshi la Urusi kwa sasa linatafuta wasambazaji wa mafuta wa ‘’jenereta za dizeli, ambazo zinatarajiwa kuwashwa baada ya vitengo vya nguvu za umeme kuzimwa’’.

    Inapendekeza jenereta hizi zingehitajika kuweka nguvu zinazotolewa kwa mifumo ya kupoesha kwa mafuta ya nyuklia yaliyotumika.

    Kampuni hiyo iliendelea kudai kwamba Warusi wamepiga picha walipokuwa wao wenyewe wanarusha makombora kwenye eneo hilo, kwa lengo la kusambaza picha hizo na kulaumu vikosi vya Ukraine.

    Hata hivyo, BBC News imeshindwa kuthibitisha madai haya.

    Katika siku za hivi karibuni pande zote mbili zimekuwa zikishutumiana eti upande mwingine unakaribia kufanya ‘’chokozi’’ kwenye kiwanda hicho.

    ‘’Kwa mara nyingine tena tunatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua zote muhimu haraka iwezekanavyo ili kuondoa umiliki wa Zaporizhzhya [kinu cha kuzalisha umeme] kwa sababu usalama wa nyuklia na mionzi ya wanadamu wote uko hatarini,’’ kampuni ya Enerhoatom ilisema.

    Soma zaidi:

  5. Almanusura kusababisha ajali baada ya Marubani kushikwa na usingizi angani

    Plane

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Marubani wawili walipitiwa na usingizi ndege ikiwa juu kwa umbali wa futi 37,000 (11,000m), na kupitiliza njia ya kutua ndege, chapisho moja la masuala ya anga limeripoti.

    Muongoza ndege kwenye uwanja wa ndege wa Addis Ababa nchini Ethiopia walijaribu kuwasiliana na marubani hao bila mafanikio baada ya kona ndege ikipitiliza kwneye njia iliyopaswa kutua.

    Hata hivyo marubani hao wa Shirika la Ndege la Ethiopia hatimaye waliamshwa na kengele maalumu (alarm) ya kujiendesha na kufanikiwa kutua kwenye njia ya pili katika uwanja huo huo, shirika la Aviation Herald lilisema.

    Ndege ya abiria, Jumatatu iliondoka kutoka uwanja wa ndege wa Khartoum nchini Sudan. Ndege hiyo aina ya Boeing 737, yenye uwezo wa kubeba viti 154, kwa kawaida huchukua chini ya saa mbili katika safari yake kati ya nchi hizo jirani.

    Muitikio wa watu kuhusu marubani hao kulala kazini zilichukulia kwa huruma na watu kutokana na ratiba ngumu ya kazi ya marubani.

    "Siwezi kuwatupia lawama wafanyakazi wa Shirika la Ethiopia haswa hapa - hili ni jambo ambalo linaweza kumtokea mfanyakazi yoyote duniani na pengine ilitokea... Lawama ziko kwa shirika na wasimamizi," moja ya maoni yalisomeka kwenye Tovuti ya Aviation Herald.

    "Uchovu wa marubani si jambo geni, na unaendelea kuwa tishio moja kubwa kwa usalama wa anga - kimataifa," alitweet mchambuzi wa masuala ya anga, Alex Macheras. BBC imewasiliana na Ethiopian Airlines kwa maoni.

  6. Mwanamuziki BNXN wa Nigeria atuhumiwa kumtemea mate usoni afisa Polisi

    BNXN

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mwimbaji wa Nigeria BNXN, inayotamkwa Benson, amekana kumtemea mate afisa wa Polisi, huku kukiwa na utata kwamba amefanya tukio hilo.

    BNXN, ambaye jina lake halisi ni Daniel Benson, alijigamba kwneye mtandao wake wa Twitter kwamba amemtemea afisa wa polisi mate usoni, katika tweet ambayo hata hivyo ilifutwa muda mfupi. Msemaji wa polisi wa jimbo la Lagos alisema nyota huyo "hakika atajibu kwa shambulio lake dhidi ya afisa wa polisi".

    BNXN alirejea kwenye maoni yake ya wali, akisema hakuwahi kumtemea afisa yeyote mate usoni na watu hawapaswi kuchukua maoni yake ya hapo awali kwa uzito au halisi.

    "Twitter yangu ya awali kwamba nilimtemea polisi usoni ilikuwa ni usemi wa kipuuzi kusema kwamba nilimdharau afisa wa polisi na sio jinsi watu walivyochukulia kwenye mitandao ya kijamii. Siungi mkono unyanyasaji au unyanyasaji dhidi ya polisi, kwa namna yoyote ile,” alitweet.

    "Nilikuwa katika hali ya kutishia maisha hali iliyonifanya nipigwe vijembe kutokana na kushambuliwa kimwili na baadhi ya polisi ambao sasa wamefikishwa mahakamani," aliendelea. Pia aliendelea kuwashukuru maafisa wa polisi kwa kuingilia kati.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  7. Erdogan 'kuteta' na Putin kuhusu kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia

    Putin

    Chanzo cha picha, Reuters

    Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan amesema kuwa atazungumza na rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusu suala la kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia baada ya kufanya mazungumzo yake na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

    Zelensky aliomba Urusi iondoe shuguhuli zake zote karibu na kiwanda hicho wakati wa mkutano huo, Erdogan aliwaambia waandishi wa habari akiwa kwenye ndege yake akirejea kutoka Ukraine ambako viongozi hao wawili walikutana siku ya Alhamisi.

    "Tutajadili suala hili na Putin na kumuomba haswa Urusi kufanya kile inachopaswa kama hatua muhimu kwa amani ya ulimwengu," alisema.

    Ziara ya Erdogan nchini Ukraine ilikuwa ya kwanza kwake nchini humo tangu Urusi ilipovamia nchi hiyo mapema mwaka huu. Siku ya Alhamisi, alikutana na Zelensky na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.

    Nuclear

    Chanzo cha picha, Getty Images

    "Hatutaki yatukute yaliyotokea Chernobyl," alisema baada ya mkutano huo. Erdogan - ambaye ameweka mistari ya kidiplomasia wazi na Moscow - anajiona kama msuluhishi wa pande hizo mbili, waandishi wa habari wanasema.

    Urusi yenyewe kupitia kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Ryabkov, aliyenukuliwa na shirika la habari la Reuters, anasema wanajeshi wanaodhibiti kinu hicho wanalenga kuzuia maafa yaliyotokea Chernobyl" mwaka 1986 yasitokee tena - ambayo yanachukuliwa kuwa ajali mbaya zaidi ya nyuklia duniani.

  8. Mwili wa mtalii aliyezama Mto Nile Uganda kumuokoa mtoto wake wapatikana

    Robert Kaweesi

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Polisi nchini Uganda wameupata mwili wa raia wa Uingereza alifariki kwa kuzama kwenye mto Nile siku ya Jumatano.

    Robert Kaweesi, 48, kutoka Birmingham, alikuwa na mkewe, Justine Katantazi, na watoto wao wanne na wakifikia kwenye moja ya hoteli iliyoko kando ya kingo za mto huko Pakwach. Mwanawe mwenye umri wa miaka 12 alienda kuogelea mtoni lakini alipopatwa na matatizo, babake aliruka ili kumsaidia.

    Hata hivyo Mvulana huyo aliokolewa na watu waliokuwa karibu lakini Bw Kaweesi hakuweza kuonekana, polisi walisema awali.

    Mwili wake ulipatikana Ijumaa asubuhi kufuatia msako wa wapiga mbizi wa polisi na watu wa kujitolea wa eneo hilo. Kamanda wa polisi wa eneo aliambia BBC kwamba uchunguzi wa maiti utafanywa kabla ya mwili kukabidhiwa kwa familia.

    Bw Kaweesi, raia wa Uingereza mwenye asili ya Uganda, na mpenzi wake wa muda mrefu Justine Katantazi walikuwa walifunga ndoa nchini Uganda mapema Agosti. Bi Katantazi alimtaja Kaweesa kama mtu mcheshi na rafiki yake mkubwa.

    Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza ilisema inaisaidia familia hiyo na ilikuwa inawasiliana na mamlaka za ndani.

  9. Baada ya watu 36 kuuawa, Walinda amani wa UN waondoka Butembo, DRC

    Monusco

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) vimeondoka katika mji wa mashariki wa Butembo kufuatia maandamano mabaya ya mwezi uliopita kuhusu kushindwa kwao kukomesha ghasia za waasi, afisa wa serikali amesema.

    “MONUSCO' tayari wameondoka, kuhusu vifaa ambavyo bado vipo mjini tunaenda kukutana Goma na wasimamizi wa misheni kuona namna ya kuvihamisha, pamoja na watumishi wachache waliobaki Butembo,” alisema Mkuu wa mkoa wa Jimbo la Kivu Kaskazini, Jenerali Constant Kongba Ndima.

    Msemaji wa MONUSCO, Ndeye Khady Lo, alisema kuwa "ujumbe huo umeendelea na kusambaza kwa muda wafanyakazi wake nje ya Butembo, baada ya mashauriano na mamlaka za mitaa na kitaifa".

    Maandamano dhidi ya ujumbe wa kulinda amani yalifanyika Kivu Kaskazini mwishoni mwa Julai. Waandamanaji hao walitaka wanajeshi hao kuondoka nchini humo. Serikali ya Kongo ilisema watu 36 waliuawa na wengine 170 walijeruhiwa katika maandamano hayo.

  10. kundi la 10 la wahamiaji kutoka Libya lawasili Rwanda

    Kundi la 10 la watu 103 wanaotakafuta uhamiaji waliookolewa kutoka Libya limewasili Alhamisi salama nchini Rwanda.

    Watapewa hifadhi katika kituo cha makazi ya muda cha Gashora katika wilaya ya Bugesera nchini Twanda, kulingana na ujumbe wa Twitter ya wizara ya Rwanda inayohusika na udhibiti wa dharura.

    Kituo hicho kwa sasa ni makazi ya wakimbizi 421 na wahamiaji waliookolewa kabla.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Unaweza pia kusoma:

    • Wahamiaji 117 waliozuiliwa Libya wawasili Rwanda
    • Wahamiaji 66 walio hatarini zaidi kutoka Libya wamewasili nchini Rwanda
    • Safari ya wahamiaji wa Uingereza kupelekwa Rwanda 'yaota mbawa', Mahakama yaingilia kati
    • Kutupeleka Rwanda haukutuzuia kufika Ulaya
  11. Polisi wawasiliana na waziri wa Afrika Kusini kuhusu unyanyasaji wa kingono

    Getty

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Enoch Godongwana aliteuliwa kama Waziri wa fedha Agosti 2021

    Waziri fedha wa Afrika Kusini Enoch Godongwana aliwasiliana na polisi Alhamisi kuhusiana na malalamiko ya unyanyasaji wa kingono yaliyowasilishwa dhidi yake, ananukuliwa akisema katika vyombo vya habari nchini humo.

    Malalamiko ya unyanyasaji huo yalitolewa na mwanamke ambaye ameajiriwa katika hoteli ambako Waziri huyo aliishi na mke wake katika jimbo la magharibi la Mpumalanga mapema mwezi huu.

    Bw Godongwana anakana kufanya kosa lolote.

    Polisi Alhamisi walimfahamisha Waziri kuhusu malalamishi dhidi yake.

    “Nina afueni hatimaye nimewasiliana na polisi na kupewa fursa ya kusikia ni nini ninachoshumiwa. Pia nashukuru kuwa na fursa ya kurekodiwa kwa maelezo yangu ya kukana. Ninachukulia madai haya kwa uzito mkubwa ,” waziri ananukuliwa akisema

    Pia alisema hawezi kujiuzulu kama waziri wa fedha.

  12. Afrika kwa picha wiki hii: Baadhi ya picha kutoka matukio mbali mbali ya Afrika

    Legio

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Kina hisia za juu Jumapili mjini Kisumu Kenya Jumapili, huku mwanaume akijaribu kumsaidia mwanamke asianguke katika maombi ya kanisa la Legio Maria ..
    Regio

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Siku iliyofuatia waumini wa Legio Maria, tawi lililojitenga na Kanisa Katoliki, wakishiriki katika ibada ya usiku katika mji wa Kisumu magharibi mwa Kenya
    Kenya

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Jumatatu mjini Nairobi, Kenya mwanaume akiwa amekaa mbele ya moto huku wafuasi wa muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya wakiandamana baada ya kutangazwa kuwa William Ruto alikuwa ameshinda uchaguzi wa urais na kumshinda mshindani wake Raila Odinga...
    miss

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Mlimbwende anayeondoka wa Afrika Kusini, Lalela Mswane, akitabasamu mbele ya kamera huku akipigwa picha katika shindano la urembo
    AFP

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Katika eneo la Mutoto, Uganda Jumamosi , mvulana anashiriki katika sherehe ya kitamatuni ya kutahiriwa inayoitwa Imbalu kwa ajili ya wavulana wanaopewa mafunzo ya kuingia utu uzima katika jamii ya Bagisu...
    Judo

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Wakati huo huo Jumamosi hiyo hiyo, Msenegal Gaye Serigne Amsatou akikabiliana na Muiran Mohammadreza Sedighi wakati wa mechi ya Judo
  13. Kesi ya R. Kelly: Shuhuda asema alinyanyaswa kingono na muimbaji

    Kelly

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mwanamke wa pili katika kesi ya pili ya shirikisho dhidi ya R. Kelly ametoa ushahidi kuwa mwimbaji wa muziki wa R&B alifanya ngono na yeyemara "mia moja" kabla atimize umri wa miaka 18.

    Mwanamke huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 37, anayefahamika kama "Jane", alisema mawasiliano yasiyo sahihi baina yake na Kelly yalianza wakati alipokuwa na umri wa miaka 13.

    Muimbaji huyo anashitakiwa katika Chicago kwa ponografia ya watoto, kuzuia utekelezwaji wa sheria na mashtaka mengine.

    Wakili wake alisisitiza kuwa yeye sio "zimwi" na anastahili kuwa na kesi ya haki.

    Kelly, ambaye jina lake kamili ni Robert Sylvester Kelly, anakabiliwa na mashitaka 13 ya uhalifu yakiwemo kubuni na kupokea ponografia za watoto, kuweka pingamizi kwa sheria na kuwalaghai watoto kuingia katika shughuli za ngono.

    Tayari anatumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kuwasafirisha watu kwa ajili ya ngono na alishitakiwa tena katika mahakama nyingine tofauti mjini New York mwaka jana.

    Unaweza pia kusoma:

    • R. Kelly: Nyota aliyehukumiwa kwa kuwanyanyasa kingono wasichana
    • Robert Kelly: Nyota wa muziki wa R&B nchini Marekani maarufu R. Kelly apatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono
    • R. Kelly ahukumiwa miaka 30 jela katika kesi ya unyanyasaji wa kingono
  14. Polisi Nigeria yagundua miili 20 katika eneo linaloshukiwa kuwa 'takatifu'

    Nigeria

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Polisi wamewakamata watu watatu kuhusiana na miili iliyokaushwa

    Polisi kusini mwa Nigeria wamewakamata watu watatu kufuatia ugunduzi wa miili 20 iliyokaushwa karibu na mji wa Benin katika jimbo la Edo.

    Miili hiyo ilipatikana katika jengo linaloshukiwa kutumiwa kama kaburi la voodoo.

    Msemaji wa polisi, Chidi Nwabuzor, ameiambia BBC kwamba maiti 15 za wanaume, wanawake watatu na watoto wawili zimegundulika.

    Haijawa wazi ni kwa muda gani zimekuwa pale.

    Aliongeza kuwa maafisa wa polisi wenye silaha na walinzi wa eneo walikuwa wamevamia jengo hilo lililopo nje tu ya mji kufuatia taarifa waliyopewa kwa siri.

    Ugunduzi wa miili hiyo umewashitua watu nchini Nigeria na wakazi wa eneo hilo wanasema wametishwa na tukio hilo.

    Wengi wanauliza ni kwa vipi miili hiyo iliweza kufichwa pale bila majirani kufahamu.

    Unaweza pia kusoma:

    • Maiti ya kale iliyopo makumbusho ya Misri, mtu huyu alikufaje?
    • Misri ya Kale: Mafarao walizikwa pamoja na wahudumu wao wakiwa hai kama kafara ya maisha ya baadaye
  15. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara ya leo tarehe 19.08.2022