Urusi na Ukraine: Wapiganaji 1,000 wamendoka katika kiwanda cha chuma Mariupol - Urusi
Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema kuwa wapiganaji wa Ukraine kutoka Mariupol wamepelekwa katika eneo linalodhibitiwa na Urusi tangu Jumatatu.
Moja kwa moja
Je, ni nini hatma ya wapiganaji 1000 wa Ukraine wanaoshikiliwa na Urusi?

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Mamia ya wapiganaji wa Ukraine wamepelekwa kwa mabasi maeneo yaliyojitenga yanaoungwa mkono na Urusi Karibu wapiganaji 1,000 wa Ukraine ambao wamezuiliwa katika kiwanda cha vyuma Azovstal huko Mariupol wamepelekwa katika eneo linalodhibitiwa na Urusi, Urusi inasema.
Ni nini kitatokea kwao baadaye haijulikani, huku Ukraine ikitoa wito wa kubadilishana wafungwa lakini baadhi nchini Urusi wakipendekeza wafunguliwe mashtaka.
Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema wanajeshi hao watashughulikiwa "kulingana na sheria husika za kimataifa", lakini kuna wasiwasi juu ya nini kitatokea kwao ikiwa wataendelea kuzuiliwa na Moscow.
"Wahalifu wa Nazi hawapaswi kubadilishana," spika wa bunge la chini la Urusi, Vyacheslav Volodin, alisema Jumanne.
"Tunapaswa kufanya kila kitu kuhakikisha wanawekwa kwenye mashtaka."
Urusi inadai, bila ushahidi wowote, kwamba Ukraine ni kitovu cha Wanazi, na mojawapo ya malengo makuu ya operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine ni "kuondoa Unazi".
Na Kikosi cha Azov - ambacho wanachama wake ni miongoni mwa wale waliohamishwa kutoka Mariupol - ndicho kinacholengwa mara kwa mara na madai ya Moscow kwamba kinapigana dhidi ya Wanazi.
Mzozo wa Ukraine: Mwanajeshi wa Urusi akiri kuua raia katika kesi ya kwanza ya uhalifu wa kivita

Chanzo cha picha, Reuters
Mwanajeshi wa Urusi anayekabiliwa na kesi ya uhalifu wa kivita nchini Ukraine amekiri kosa la kumuua raia ambaye hakuwa na silaha.
Vadim Shishimarin, 21, anatuhumiwa kwa kumpiga risasi mzee wa miaka 62 siku chache baada ya vita nchini Ukraine kuanza.
Waendesha mashtaka wanasema kesi zaidi zinakuja, baada ya kubaini kuna uwezekano wa uhalifu mwingine wa kivita umefanywa na wanajeshi wa Urusi.
Moscow imekanusha kuwa wanajeshi wake wamewalenga raia.
Kesi hiyo ni ya kwanza ya aina yake tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ulipoanza mwezi Februari.
Imefanyika Kyiv, Ukraine, huku mkalimani akitafsiri kesi katika lugha ya Kirusi kwa mshtakiwa.
"Je, unakubali hatia yako?" hakimu aliuliza. "Ndiyo," Shishimarin alijibu.
"Kabisa?" "Ndiyo," aijibu
Anatuhumiwa kumuua raia huyo, ambaye inadaiwa alikuwa kwenye baiskeli, karibu na kijiji cha Chupakhivka katika eneo la mashariki la Sumy tarehe 28 Februari, siku nne baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Waendesha mashtaka wanasema Bw Shishimarin alikuwa akiendesha gari lililoibwa akiwa na wanajeshi wengine katika eneo la kaskazini-mashariki la Sumy walipokutana na mwendesha baiskeli mwenye umri wa miaka 62 akitumia simu.
Aliamriwa kumpiga risasi raia huyo ili kuzuia kuwaambia watetezi wa Ukraine kuhusu eneo lao, hiyo ni kwa mujibu wa waendesha mashtaka.
Idrissa Gueye adaiwa kukataa kuvaa jezi ya PSG yenye alama ya kuunga mkono wapenzi wa jinsia moja

Chanzo cha picha, Getty Images
Idrissa Gueye mchezaji wa Paris St-Germain na Senegal alikataa kucheza mechi dhidi ya Montpellier siku ya Jumamosi ili kuepuka kuvaa jezi yenye alama ya upinde wa mvua inayoashiria kuunga mkono haki za wapenzi wa jinsia moja (LGBTQ+.)
Kiungo huyo wa zamani wa Aston Villa na Everton mwenye umri wa miaka 32 hakuwepo kwenye mechi hiyo iliyowapatia ushindi wa goli 4-0.
Bosi wa PSG Mauricio Pochettino alisema tu kwamba Gueye alikosa mchezo kwa "sababu binafsi".
Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF) limeripotiwa kumtaka Gueye aeleze kwa nini hakuwepo katika mchezo wa Jumamosi.
Cheikhou Kouyate wa Crystal Palace na Ismaila Sarr wa Watford wamechapisha kwenye mitandao ya kijamii wakionyesha kuunga mkono msimamo wa mwenzao wa Senegal.
Kouyate alichapisha picha yake akiwa pamoja na Gueye kwenye Instagram, na nukuu ikimuita Gueye "mwanaume halisi". Winga wa Watford Sarr alichapisha picha yake na Gueye iliyoambatana na emoji tatu za moyo na kuandika "100%".
Mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria nchini Senegal na unaweza kuadhibiwa kwa vifungo cha hadi miaka mitano.
Hata hivyo rais wa Senegal Macky Sall aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa imani ya dini ya mchezaji huyo iheshimiwe.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Vilabu vya ligi kuu ya Ufaransa vilivaa jezi zenye nambari za rangi ya upinde wa mvua ili kuonyesha kuunga mkono haki za LGBTQ Tanzania yazindua chanjo ya Polio kwa watoto,

Serikali ya Tanzania imezindua rasmi kampeni ya kitaifa ya utoaji wa chanjo ya matone ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa polio.
Zaidi ya watoto milioni kumi wanalengwa katika zoezi hilo litakalochukua siku nne.
Katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dodoma, waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Tanzania nayo iko hatarini baada ya nchi jirani kama vile Malawi, Msumbiji na Zambia kuthibitisha kuwepo kwa ugonjwa huo.
Kilele cha kampeni hiyo itakuwa ni tarehe 21 mwezi huu.
Ummy Mwalimu ambae ni wazir wa Afya nchini Tanzania, amesema lengo la kampeni hii ni pamoja na kuimarisha kinga, kuzuia na kukinga kusambaa kwa virusi vya polio katika jamii.
Kampeni hii ambayo itanyika kwa muda wa siku nne, itapita majumbani, vituo vya huduma za afya, pamoja na kuwafuata watoto walipo ikiwemo mashuleni.
Ikumbukwe kwamba, hatua hii ni utekelezaji wa mwongozo wa shirika la afya duniani WHO ambapo pia unatekelezwa na nchi jirani kama vile Malawi, Zambia na Msumbiji.
Mwaka 2015 kupitia WHO na mwaka 2020 kupitia Jumuia ya Afrika, Tanzania ilipewa cheti cha kuthibitishwa kutokuwa na ugonjwa wa polio.
Unaweza pia kusoma
- Mafanikio ya Afrika katika kupambana na polio
- Polio: 'Sikuiamini chanjo mpaka mtoto wangu alipopata polio'
Washirika wa Nato wanapaswa kuheshimu maamuzi ya Uturuki – Erdogan

Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa Uturuki ametishia kwamba Uturuki inaweza kupinga maombi ya mataifa ya Sweden na Finland kujiunga na NATO.
Rais Erdogan alisema leo asubuhi kwamba anatarajia washirika wa Nato kuelewa hisia za Uturuki kuhusu usalama.
Katika hotuba yake kwa wabunge wa chama chake tawala, pia alirudia maoni yake kwamba wajumbe wa Uswidi na Finland wasijisumbue kuja Uturuki kujadili masuala hayo.
Na alisema Sweden haipaswi kutarajia Uturuki kuidhinisha nia yake ya uanachama wa Nato bila kurejesha "magaidi".
Uturuki inayashutumu mataifa hayo mawili ya Nordic kwa kuwapa hifadhi wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Kurdistan (PKK), kikundi ambacho inakiona kama chama cha kigaidi, na wafuasi wa Fethullah Gulen, ambaye Ankara inamtuhumu kuandaa jaribio la mapinduzi ya 2016.
Kulingana na shirika rasmi la habari la Uturuki, Finland na Uswidi zimekataa maombi kadhaa ya kuwarejesha wanamgambo wa Kikurdi ambao Uturuki inawataja kuwa magaidi.
Bila uungwaji mkono wa wanachama wote wa Nato, Uswidi na Finland haziwezi kujiunga na muungano huo wa kijeshi, ingawa Rais wa Marekani Joe Biden alisema jana kuwa ana imani makubaliano yanaweza kufikiwa.
Nyati mweupe adimu aonekana katika mbuga ya wanyama Tanzania

Chanzo cha picha, Wizara ya Maliasili/TZ
Nyati mweupe adimu ameonekana katika Hifadhi ya Kitaifa ya Tarangire kaskazini mwa Tanzania.
Nyati huyo alionekana kwa mara ya kwanza katika mbuga hiyo siku ya Jumatatu, na kuvutia watalii wengi waliotaka kumuona mnyama huyo, wizara ya maliasili na utalii ilisema.
Nyati hao walikuwa wakubwa kuliko nyati wengine, gazeti la ndani la The Citizen liliripoti, likisema alionekana akichanganyika kwa uhuru na kundi lingine.
Inabainisha kwamba kando na kuwa nadra, nyati weupe huonwa kuwa watakatifu miongoni mwa jamii fulani.
Hifadhi ya Tarangire iko kanda ya kaskazini kusini mwa Ziwa Manyara.
Urusi yawafukuza wanadiplomasia zaidi ya 30 wa Ufaransa

Chanzo cha picha, Getty Images
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema inawatimua wanadiplomasia 34 wa Ufaransa katika hatua ya 'tit-for-tat'.
Inawapa wiki mbili kuondoka nchini.
Mnamo Aprili, Ufaransa iliwafukuza Warusi 35 wenye hadhi ya kidiplomasia - ilikuwa ni sehemu ya wimbi la kufukuzwa kutoka miji mikuu ya Ulaya ambayo ilishuhudia Warusi zaidi ya 300 wakirudishwa nyumbani.
Baadaye mwezi huo, wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ilitangaza mawakala sita wa Urusi wanaojifanya wanadiplomasia kama "persona non grata" - ambayo kwa kawaida inamaanisha kuwa hadhi yao ya kidiplomasia imebatilishwa.
Hii ilikuwa baada ya idara za ujasusi za Ufaransa kuwashawishi Warusi kufanya kazi kinyume na matakwa ya kitaifa ya Ufaransa. Zana za kushiriki makala
Unaweza pia kusoma:
- Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
- Urusi na Ukraine: Usaidizi wa kijeshi ambao nchi za Magharibi zitatuma kwa serikali ya Ukraine (na mabadiliko ya msimamo wa Ujerumani)
- Kuanzia asubuhi hadi usiku, siku ya Rais Putin inakuaje?
Ghadhabu zazuka baada ya balozi kupeperusha bendera za kuunga mkono wapenzi wa jinsia moja Zambia

Chanzo cha picha, Sweden in Zambia
Balozi za Sweden na Finland nchini Zambia zinakabiliwa na mzozo nchini humo baada ya kuinua bendera ya upinde wa mvua pamoja na bendera zao za kitaifa kwenye majengo yao siku ya Jumanne.
Mahusiano ya watu wa jinsia moja yameharamishwa nchini Zambia, ambapo sheria za wakati wa ukoloni wa Uingereza kuhusu mapenzi ya jinsia moja bado zinatumika.
Ubalozi wa Sweden nchini Zambia ulituma kwenye ukurasa wake wa Twitter bendera ya upinde wa mvua kwa kutumia alama ya #Idahot2022, ambayo inawakilisha Siku ya Kimataifa ya Kupambana unyanyapaa wa wapenzi wa jinsia moja.
"Haki za LGBTIQ ni haki za binadamu - siku zote na kila mahali," waliandika kupitia twitter.
Ubalozi wa Finland pia aliandika"kusimama pamoja kwa ajili ya haki za binadamu".
Mwanadiplomasia wa zamani wa Zambia Emmanuel Mwamba amedai majibu kutoka kwa wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo, tovuti ya The Lusaka Times inaripoti.
"Inashangaza kwamba balozi hizi zilichagua kupeperusha bendera hizi katika majengo yao bila kuzingatia sheria na hisia za kitamaduni za Wazambia na Zambia kuhusu suala hilo," alinukuliwa akisema.
Mnamo Desemba 2019, Amerika ilimwita balozi wake nchini Zambia juu ya mzozo wa kidiplomasia baada ya kukosoa kufungwa kwa wanandoa wa jinsia moja.
Serikali ya Zambia ilikuwa imemshutumu balozi huyo kwa kujaribu kuamuru.
Hifadhi ya wanyama ya Marekani kuonyesha ng’ombe wa Ankole wanaopatikana zaidi nchini Uganda
Hifadhi ya Wanyama ya Philadelphia nchini Marekani imeanza onyesho la ng’ombe wenye pembe ndefu wanaofugwa zaidi nchini Uganda wanaofahamika kama Ankole.
Ng’ombe wa Ankole, wanaofahamika kama ‘’mifugo wa wafalme’’, ni kizazi chenye asili ya Afrika na wanafahamika kwa kuwa na pembe kubwa na ndefu ambazo hukua kadri myama huyo anavyoendelea kukua , ambapo hatimaye pembe hukua na kufikia uzito wa takriban kilo saba (15lbs).
“Tumefurahi kuleta kizazi hiki katika hifadhi ya Wanyama kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka yetu 163. Tunaamini wataimarisha uzoefu wa wageni wetu huku tukiangazia kazi ya usaidizi wa uhifadhi wa wanyama nchini Uganda ,” hifadhi ya Wanyama ya Philadelphia ilisema katika taarifa yake.
Hifadhi ya Wanyama ya Philadelphia ilianzisha onyesho la Yamaani, Gaaju na Kutekaana – majina ambayo watu wa kabila la Banyakole la Uganda huwaita kwa misingi ya tofauti za rangi zao.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Habari za hivi punde, Urusi na Ukraine: Wapiganaji takriban 1,000 wa Azovstal wamesajisalimisha, Urusi yasema

Wapiganaji karibu1,000 wa Ukraine waliozingirwa katika kiwanda cha chuma cha Azovstal kilichopo katika Mariupol sasa wamejisalimisha, kulingana na wizara ya ulinzi ya Urusi.
Urusi imesema wapiganaji 694 kutoka jeshi la Ukraine na batalioni ya Azov wamejisalimisha katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
Wizara hiyo inasema jumla ya wale ambao wamejisalimisha ni 959 (idadi hii inajumuisha wanajeshi wengine 265 ambao ilisema waliondoka katika awamu ya kwanza ya kuwaondoa katka eneo hilo Jumatatu).
Wale wanaoondoka katika kiwanda cha chuma wanapelekwa katika eneo linalodhibitiwa na Warusi.
Maafisa wa Ukraine hawajapewa taarifa za hivi karibuni kuhusu jinsi wapiganaji wengi walivyoondoka Azovstal leo.
Unaweza pia kusoma:
- Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
- Urusi na Ukraine: Usaidizi wa kijeshi ambao nchi za Magharibi zitatuma kwa serikali ya Ukraine (na mabadiliko ya msimamo wa Ujerumani)
- Kuanzia asubuhi hadi usiku, siku ya Rais Putin inakuaje?
Uganda inasema itaondoa wanajeshi wake kutoka DRC

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Uganda iliwapeleka wanajeshi wake 1700 katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congomwezi Disemba Jeshi la Uganda linasema litawaondoa mamia ya wanajeshi wake iliyowapeleka mwaka jana kuisaidia nchi jirani ya Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo kukabiliana na kundi la uasi la Kiislamu.
Kamanda wa majeshi ya ardhini Muhoozi Kainerugaba amesema kwamba Operesheni Shujaa ililenga tu kudumu kwa muda wa miezi sit ana itamalizika katika mwezi ujao iwapo hapatakuwa na makubaliano ya kuongezwa muda kwa uwepo wa wanajeshi hao katika DRC.
Maafisa katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamesema kuwa nchi zote zitahitaji kujadili kanuni na muda wa kuondoka kwa wanajeshi wa Uganda.
Mwezi Disemba, Uganda iliwapeleka wanajeshi wake 1,700 kushiriki katika operesheni ya pamoja na vikosi vya Congo dhidi ya waasi wanaofahamika kama Allied Democratic Forces ( ADF)
ADF wanashutumiwa kufanya uvamizi na mauji ya kikatili katika maeno ya mshariki mwa DRC na kulipua mabomu yaliyowauwa watu nchini Uganda.
Finland na Uswidi zawasilisha rasmi maombi ya kujiunga na Nato, je Urusi itachukua hatua gani?

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Mabalozi katika Nato kutoka Uswidi na Finland waliwasilisha maombi yao kwa katibu mkuu wa Muungano wa Nato (katikati) asubuhi hii Uswidi na Finland zimewasilisha rasmi maombi yake ya kujiunga na nato asubuhi hii.
Katibu mkuu wa Muungano huo Jens Stoltenberg anasema ni " kipindi cha kihistoria, ambacho ni lazima tukitumie", akiongeza kuwa uanachama wa ‘’nchi za Scandnavia ‘ ' utaongeza usalama.
Tangazo la viongozi wa mataifa haya mawili kuhusu azma yao ya kuwasilisha maombi ya uanachama wa muungano wa Nato siku ya Jumapili, limekuja kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Bunge la Uswidi lilipiga kura kuunga mkono hatua hiyo, huku Finland ikifanya hivyo jana.
Finland inapana na Urusi katika mipaka yake ya ardhini na nchi kavu. Finland na jirani yake Uswidi ziliendelea kutounga mkono upande wowote katika kipindi chote cha vita baridi kwahiyo maombi yake ya kujiunga na Nato yanaonyesha mabadiliko muhimu katika misimamo yake.
Mchakatowa kujiunga na Nato unaweza kuharakishwa na kuchukua wiki mbili tu, lakini utahitaji uungwaji mkono wa wajumbe wote 30, uidhinishaji ambao unaweza kuchukua hadi mwaka mmoja. Serikali ya Uturuki imekwisha kuelezea upinzani wake.
Rais wa Finland Sauli Niinisto na waziri mkuu wa Uswidi Magdalena Andersson wanatarajia kukutana na Rais wa Mareknai Joe Biden katika Ikulu ya White House Kesho kujadili mada zikiwemo athari za Nato, Usalama wa Ulaya na usaidizi kwa ajili ya Ukraine.
Unaweza pia kusoma:
- Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
- Urusi na Ukraine: Usaidizi wa kijeshi ambao nchi za Magharibi zitatuma kwa serikali ya Ukraine (na mabadiliko ya msimamo wa Ujerumani)
- Kuanzia asubuhi hadi usiku, siku ya Rais Putin inakuaje?
Habari za hivi punde, Zelensky: Urusi Inarusha makombora kwa sababu ya ukosefu wa mafanikio ardhini

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, . Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amedai kuwa Urusi inarusha makombora ya masafa marefu katika miundombinu ya raia na ile ya kijeshi ya Ukraine kwa sababu jeshi lake haliwezi kuonyesha mafanikio yoyote muhimu.
Katika hotuba yake ya video iliyotolewa jana usiku, Zelensky alisema kumekuwa na ufyatuaji wa makombora katika maeneo ya Lviv, Sumy na Chernihiv, mashambulizi ya anga katika eneo la Luhansk na "shughuli za hujuma" katika maeneo ya mpakani.
"Haya yote sio tu kuleta mvutano kwa jimbo letu, sio tu kujaribu nguvu zetu," Zelensky anasema.
"Hili ni jaribio la jeshi la Urusi kufidia safu ya kushindwa mashariki na kusini mwa nchi yetu.
"Hawawezi kuonyesha mafanikio kwa hatua za jumla za kijeshi katika maeneo wanayojaribu kusonga mbele. Kwa hiyo wanajaribu kuonyesha mafanikio kupitia makombora yao na shughuli nyingine. Bila mafanikio pia."
Unaweza pia kusoma:
- Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
- Urusi na Ukraine: Usaidizi wa kijeshi ambao nchi za Magharibi zitatuma kwa serikali ya Ukraine (na mabadiliko ya msimamo wa Ujerumani)
- Kuanzia asubuhi hadi usiku, siku ya Rais Putin inakuaje?
Njaa inasababisha kifo ’kila sekunde 48’ Katika Afrika Mashariki

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameonya juu ya njaa kali inayosababisha utapiamlo inayohusiana na mzozo, mzozo wa hali ya hewa, na mfumuko wa bei za chakula. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameonya katika eneo lote la mataifa ya Ethiopia, Kenya na Somalia, mtu mmoja hufariki kila sekunde 48 kutokana na njaa ya muda mrefu inayosababishwa na mzozo, mzozo wa hali ya hewa na kuongezeka kwa gharama ya chakula.
Ripoti ya mashirika ya misaada Oxfam na Save the Children inakadiria kuwa takriban watu milioni 181 kote duniani wanapitia uzoefu viwango vya mzozo wa njaa, huku wanawake wakiathiriwa zaidi.
Mashirika hayo yanasema njaa kali ni kushindwa kisiasa.
Yanakosoa jamii ya kimataifa kwa kuchelewa sana kushugulikia tatizo la njaa na kutozuia dharura "zinazojirudia na kutabirika " .
Kanali mstaafu atoa picha ya tofauti kuhusu vita vya Ukraine kwenye Televisheni ya Urusi

Vyombo vya habari vya kawaida vya Urusi vinatoa mtazamo wa vita vya Ukraine ambavyo havifanani na chochote kinachoonekana kutoka nje ya nchi. Kwa kuanzia, hata hawaiti vita.
Lakini mhariri wetu wa Urusi anaakisi matangazo ya nadra kwenye TV ya serikali. Ilikuwa ni kipande cha mazungumzo ya televisheni cha ajabu.
Kipindi kilikuwa cha Dakika 60, kipindi cha mazungumzo ya mara mbili kwa siku kwenye Televisheni ya serikali ya Urusi: mjadala wa studio ambao unaitangaza Kremlin kwa kila kitu, pamoja na kile kinachoitwa "operesheni maalum ya kijeshi" ya Rais Putin nchini Ukraine.
Kremlin bado inashikilia msimamo kuwa mashambulizi ya Urusi yanakwenda kwa namna ilivyopangwa. Lakini Jumatatu usiku, mgeni wa studio Mikhail Khodarenok, mchambuzi wa kijeshi na kanali mstaafu, alitoa picha tofauti sana.
Alionya kwamba "hali [ya Urusi] itazidi kuwa mbaya zaidi" huku Ukraine ikipokea usaidizi wa ziada wa kijeshi kutoka Magharibi na kwamba "jeshi la Ukraine linaweza kuwapa silaha watu milioni moja".
Akirejelea askari wa Ukrainia, alisema: "shauku ya kutetea nchi yao ipo sana. Ushindi wa mwisho kwenye uwanja wa vita unaamuliwa na ari ya juu ya wanajeshi ambao wanamwaga damu kwa mawazo ambayo wako tayari kuyapigania.
"Tatizo kubwa la hali ya kijeshi na kisiasa ya [Urusi]," aliendelea, "ni kwamba tumetengwa kabisa kisiasa na ulimwengu mzima unatupinga, hata kama hatutaki kukubali.
Tunahitaji kutatua hii hali. "Hali hiyo haiwezi kuchukuliwa kuwa ya kawaida dhidi yetu, kuna muungano wa nchi 42 na wakati rasilimali zetu, kijeshi-kisiasa na kiufundi-kijeshi, ni chache."
Ni nadra kusikia uchambuzi wa kweli wa matukio kwenye TV ya Kirusi. Nadra. Lakini si ya kipekee. Katika wiki za hivi karibuni, maoni muhimu yameonekana kwenye runinga hapa.
Mnamo Machi, kwenye kipindi kingine maarufu cha mazungumzo ya TV, mtengenezaji wa filamu wa Kirusi alimwambia mtangazaji: "Vita vya Ukraine vinatoa picha ya kutisha, vina ushawishi wa kukandamiza sana jamii yetu."
Kwa hivyo ni nini kilifanyika kwa Dakika 60? Je, hii ilikuwa ni simulizi ya ghafla, isiyotarajiwa kwa Ukraine ambayo iliteleza kwenye wavu? Au ilikuwa ni mlipuko wa ukweli uliopangwa tayari ili kuandaa umma wa Kirusi kwa habari mbaya juu ya maendeleo ya "operesheni maalum ya kijeshi"? Ni vigumu kusema.
Lakini kama wavyosema kwenye televisheni, kaa karibu na Runinga ya Urusi kwa ishara zaidi.
Unaweza pia kusoma:
- Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
- Urusi na Ukraine: Usaidizi wa kijeshi ambao nchi za Magharibi zitatuma kwa serikali ya Ukraine (na mabadiliko ya msimamo wa Ujerumani)
- Kuanzia asubuhi hadi usiku, siku ya Rais Putin inakuaje?
Urusi na Ukraine: Ukraine inafanya kila liwezekanalo kuwanusuru wapiganaji wapiganaji waliosalia Mariupol

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Takriban mabasi mengine saba yalionekana yakiondoka kutoka kwenye eneo la Azovstal Jumanne na baadaye kuwasili katika kijiji kinacpodhibitiwa na wasi wanaoungwa mkono na Urusi, limeripoti Shirika la habari la Reuters. Ukraine inafanya ‘’kila liwezekanalo na lisilowezekana ’’ kuwanusuru wapiganaji wengine waliobaki ambao wamekwama katika kiwanda cha chuma kilichopo Mariupol, amesema afisa wa ngazi ya juu.
Naibu Waziri wa ulinzi Hanna Maliar amesema kuwa kyiv inafahamu ni wanajeshi wake wangapi ambao bado wamekwama katika kiwanda hicho, lakini akasisitiza kwamba hiyo ni ‘’taarifa ya siri’’.
Jumatatu, wapiganaji 264-wengi wao wakiwa wameumia vibaya-waliokolewa na kupelekwa katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.
Jumanne, mabasi mengine saba, yalionekana yakiondoka katika eneo hilo, limesema shirika la habari la Reuters.
Iliongeza kuwa msafara huo baadaye uliwasili katika kijiji cha Olenivka, kilichotekwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi kilichopo katika jimbo la mashariki la Donbas.
Unaweza pia kusoma:
- Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
- Urusi na Ukraine: Usaidizi wa kijeshi ambao nchi za Magharibi zitatuma kwa serikali ya Ukraine (na mabadiliko ya msimamo wa Ujerumani)
- Kuanzia asubuhi hadi usiku, siku ya Rais Putin inakuaje?
Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu mubashara leo ikiwa ni tarehe 18.05.2022
