Vita vya Ukraine: Sweden yathibitisha kuomba kujiunga na NATO

Tarehe ya maombi rasmi bado haijulikani kwa sababu Sweden itatuma maombi yake pamoja na Finland, anasema waziri mkuu wa Sweden

Moja kwa moja

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja. Hadi kesho kwaheri.

  2. Biden aidhinisha kurejeshwa kwa wanajeshi wa Marekani nchini Somalia

    Utawala wa Rais Biden unataka kuweka ulinzi bora zaidi dhidi ya al-Shabab

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Utawala wa Rais Biden unataka kuweka ulinzi bora zaidi dhidi ya al-Shabab

    Mamia ya wanajeshi wa Marekani huenda wakarejeshwa nchini Somalia baada ya Rais Joe Biden kuidhinisha kupelekwa kwao nchni humo katika hatua iliyobatilisha uamuzi wa mtangulizi wake , Donald Trump.

    Biden pia ameidhinisha ombi la Pentagon la kuwalenga viongozi wa kundi la al-Shabab,gazeti la New York Times linaripoti..

    "Uamuzi huo ulifanywa ili kuongeza usalama na ufanisi wa vikosi vyetu na kuwawezesha kutoa usaidizi bora zaidi kwa washirika wetu," msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa Adrienne Watson alinukuliwa akisema, akiongeza kwamba itawezesha " mapambano yenye tija zaidi dhidi ya al-Shabab”.

    Hatua hii inajiri baada ya wabunge wa Somalia kumchagua rais mpya, Hassan Sheikh Mohamud, siku ya Jumapili.

    Soma:

  3. Sweden yathibitisha kuomba kujiunga na NATO

    w

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, waziri mkuu wa Sweden Magdalena Andersson

    Waziri Mkuu wa Uswidi Magdalena Andersson katika mkutano wake na waandishi wa habari Anaanza kwa kuthibitisha kwamba Uswidi itaomba uanachama wa Nato.

    Na hivyo kuondoa historia ya muda mrefu ya kutoegemea upande wowote kijeshi.

    Waziri Mkuu huyo anaongeza kuwa ana uhakika kwamba kuna msaada kwa hili kati ya watu wa Uswidi.

    Tarehe ya maombi rasmi bado haijulikani kwa sababu Uswidi itatuma maombi yake pamoja na Ufini, anasema.

    Anaongeza kuwa haoni tishio lolote la moja kwa moja la kijeshi dhidi ya Uswidi.

    Ulf Kristersson, kiongozi wa chama cha upinzani cha Wastani, pia anazungumza katika mkutano na waandishi wa habari na anaunga mkono uamuzi wa kuomba uanachama wa Nato."Huu ni uamuzi wa kihistoria," anasema.

    Sio juu ya siasa za vyama lakini juu ya kuchukua jukumu la pamoja kwa usalama wa nchi, anaongeza.

  4. Wakenya wakejeli msongamano katika barabara kuu mpya

    Barabara ya mwendokasi ilifunguliwa kwa umma mwishoni mwa juma

    Chanzo cha picha, BBC/Peter Mwangangi

    Maelezo ya picha, Barabara hiyo ilifunguliwa kwa umma mwishoni mwa juma

    Wakenya mtandaoni wamekuwa wakilalamikia msongamano katika barabra kuu mpya iliyojengwa katika jiji kuu la Nairobi.

    Baadhi ya picha zilizoshirikishwa mtandaoni zinaonesha foleni ya magari kuelekea katika eneo la kulipia ada ya kutumia barabra hiyo ya juu kwa juu inayopitia katikati mwa jiji.

    Baaadhi yao wamekejeli hali hiyo, huku wengine wakighadhabishwa na msongamano mkubwa wa magari ambao ulitarajiwa kusuluhishwa na ujenzi wa barabara hiyo.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Barabara hiyo kuu ya umbali wa kilomita 27 (maili 16) ilijengwa na kampuni ya China ilifunguliwa kwa umma siku ya Jumamosi kwa “awamu ya majaribio” ikisubiri ufunguzi rasmi katika miezi michache ijayo.

    Wiki mbili zilizopita Rais Uhuru Kenyatta alisema kwamba awamu hiyo ya kwanza itakuwa ya majaribio ya utumizi wake na "kumalizia sehemu ambazo hazijakamilika”.

    Pia alisema barabara hiyo “itasaidia kukabiliana na msongamano mkubwa wa magari unaokumba jiji la Nairobi.

  5. Kenya yamtakia heri njema rais mpya wa Somalia

    Wasomali katika nchi jirani ya Kenya wameungana kumtakia heri njema kiongozi mpya wa nchi hiyo Rais, Hassan Sheikh Mohamud.

    Rais Uhuru Kenyatta amemtakia mwenzake "afya njema anapochukua hatamu ya uongozi , na kumhakikishia kuwa Kenya itaendelea kuwa msharika wa karibu",Ikulu ya Rais ilisema kupitia mtandao wa Twitter.

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Kenya ina mpaka mrefu na Somalia na imekuwa mhasiriwa wa mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa al-Shabab lenye makao yake nchini Somalia.

    Nchi hiyo pia inachangia wanajeshi katika kikosi cha Umoja wa Afrika kinachounga mkono serikali ya shirikisho ya Somalia katika mapambano yake dhidi ya al-Shabab.

    Mafanikio ya serikali ya Mogadishu katika kukabiliana na wanamgambo hao yana athari za moja kwa moja kwa Kenya.

    Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, Moussi Faki Mahamat, pia ametuma pongezi zake:

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

  6. Sweden kutuma wanadiplomasia nchini Uturuki kuishawishi iunge mkono kujiunga kwao na NATO

    RE

    Chanzo cha picha, Reuters

    Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan alisema haitaona vyema Sweden na Finland kujiunga na Nato.

    Sweden inatuma wanadiplomasia nchini Uturuki ili kujaribu kushinda pingamizi la nchi hiyo kwa mpango wake wa kujiunga na Nato.

    Haya yanajiri huku Sweden ikitarajiwa kufanya uamuzi rasmi kuhusu ombi lake la kujiunga na muungano wa kijeshi leo. Finland pia imethibitisha kuwa itaomba kujiunga na Nato.

    Hata hivyo, Uturuki, ambayo ni mshirika wa nchi zote mbili, ilisema haitatazama maombi ya Sweden na Finland vyema, huku rais wake, Tayyip Erdogan, akisema "Nchi za Skandinavia ni nyumba za wageni za mashirika ya kigaidi".

    Uturuki ilisema ilitaka nchi za Nordic kusitisha uungaji mkono kwa makundi ya wapiganaji wa Kikurdi waliopo kwenye eneo lao, na kuondoa marufuku ya uuzaji wa baadhi ya silaha kwa Uturuki.

    Uamuzi wowote wa kuongeza nchi ndani ya Nato unahitaji idhini ya wanachama wote 30 wa muungano na mabunge yao, lakini wanadiplomasia walisema Erdogan atawekewa shinikizo kukubaliana, kwani Finland na Uswidi zitaimarisha sana Nato katika Bahari ya Baltic.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mzozo wa Ukraine: "Siioni Urusi kama adui": Waukraine wanaounga mkono uvamizi wa Urusi katika eneo la mzozo la Donbas
    • Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
    • Urusi na Ukraine: Usaidizi wa kijeshi ambao nchi za Magharibi zitatuma kwa serikali ya Ukraine (na mabadiliko ya msimamo wa Ujerumani)
  7. Mlinda amani wa Zambia amuasili mtoto mchanga kutoka Jamhuri ya Afrika ya kati (CAR)

    BBC / Kennedy Gondwe

    Chanzo cha picha, BBC / Kennedy Gondwe

    Mwanajeshi wa Zambia kapteni Mwila Chansa amezungumzia kuhusu mapambano yake ya kumuasili mtoto mchanga ambaye alikutana naye kwa mara ya kwanza alipokuwa katika kazi ya kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

    Mama yake mtoto huyo mchanga alikuwa ana ujauzito wa mapacha , lakini akapata matatizo ya kiafya na kufariki baada ya kujifungua mtoto wa kwanza Novemba mwaka 2020. Mtoto wa pili alifariki kabla ya kuzaliwa.

    Kapteni Chansa aliytembelea eneo la Birao, lililopo karibu na mpaka baina ya Sudan na Chad, katika mwaka 2021 wakati aliposikia hadithi ya mtoto huyo mchanga - ambaye wakati huo alikuwa chini ya uangalizi wa wauguzi katika kambi ya Zambia.

    Alifanya uamuzi wa kumuasili, lakini urasimu wa mchakato huo uligeuka kuwa mrefu katika katika kufuatilia sheria ya Kiislamu.

    "Nilikwenda Google, kujaribu kuangalia namna ya kumuasili, mtoto kutoka CPR. Taarifa zote zilikuwa kuhusu USAidna jinsi ilivyo rahisi kwa Wamarekani kwa ujumla kuwaasili watoto. Lakini hapakuwa na taarifa zozote kuhusu jinsi ya Mzambia anavyoweza kuasili mtoto ," aliiambia BBC.

    Mwila Chansa

    Chanzo cha picha, Mwila Chansa

    Kapteni alisema "utashi mkubwa " ulimfanya afanye juhudi kubwa "kuzungumza na mamlaka ili kuhakikisha mtoto mchanga awasili hapa [katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka]".

    "Inanikumbusha tu mengi sana ya historia ya kibiblia ya Moses,” alisema.

    “Kumuasili mtoto ni kama kumpenda mtu kimapenzi . Unawaona wanaume wengi sana , wanawake wengi sana lakini unamchagua mmoja tu ."

    Rais wa ZambiaHakainde Hichilema alimsifu Kapteni Captain Chansa kwa kuonyesha utu katika kazi yake.

    Kapteni ana mipango mengi kwa mtoto wake mchanga wa kikeambao amemuitaThabo.

    “Ningependa awe rais wa jamuhuri ya Afrika ya kati. Ninasema wasi wasi,” alisema.

  8. Majenerali 35 kustaafu kutoka jeshi la Uganda UPDF mwezi Julai

    Jenerali David Sejusa
    Maelezo ya picha, Jenerali David Sejusa, ni miongoni mwa maafisa wa ngazi ya juu wa zamani wa jeshi la Uganda wanaotarajiwa kujiuzulu mwezi Julai

    Takriban majenerali 34 wanatarajiwa kutaafu kutoka jeshi la Uganda (UPDF) mwezi Julai. Kulingana na orodha iliyochapishwa na gazeti la kibinafsi nchini humo la daily Monitor, wawili wana cheo cha Jenerali, watatu wana cheo cha Luteni Jenerali,10 wakiwa na cheo cha Meja Jenerali na 11 ni Mabrigadia.

    Miongoni mwa maafisa wa ngazi ya juu wa jeshi wanaotarajiwa kustaafu ni pamoja na mratibu wa zamani mashirika ya ujasusi, Jenerali David Sejusa, ambaye awali aliomba kuondoka jeshini katika mwaka 1996, na waziri wa zamani wa usalama Jenerali Elly Tumwine.

  9. Habari za hivi punde, Wanajeshi wa Ukraine wanaoilinda Kharkiv wafika mpaka wa Urusi

    Wanajeshi wa Ukraine

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Ukraine

    Wanajeshi wa Ukraine wanaolinda mji wa kaskazini wa Kharkiv wamefika kwenye mpaka wa serikali na Urusi, gavana wa eneo hilo alisema Jumatatu.

    Gavana Oleh Sinegubov alitoa madai hayo kwenye huduma ya ujumbe ya Telegram.

    Bado haijawezekana kuthibitisha madai hayo na haijafahamika mara moja ni wanajeshi wangapi walikuwa wamefika kwenye mpaka wa Urusi na ni wapi.

    Wizara ya ulinzi ya Ukraine imechapisha video inayodaiwa kuwaonyesha wanajeshi kadhaa kutoka kikosi cha ulinzi wa eneo katika eneo lisilojulikana kwenye mpaka.

    "Tumefika, tuko hapa," mmoja wa askari anasema.

    Ukraine imekuwa ikiwafukuza wanajeshi wa Urusi kutoka Kharkiv, mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine.

  10. Vita vya Ukraine: Sweden itajiunga na Nato, licha ya onyo la Urusi

    Sweden joining Nato is supported by most of the country's political parties

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Kujiunga kwa Sweden jkatika Nato kunaungwa mkono na vyama vingi vya kisiasa nchini humo

    Sweden imethibitisha kuwa itawasilisha maombi ya kuwa mwanachama wa Nato katika mabadiliko makubwa ya kihistoria kutokana na uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

    Jumatatu, Waziri mkuu wa Sweden Magdalena Andersson anatarajiwa kwenda bungeni kupata uungaji mkono kwa ajili ya maombi hayo, na pia ataongoza kikao maalum cha baraza la mawaziri kuzungumzia suala hilo.

    Hatua hii inakuja baada ya chama chake cha Social Democratic party – kuacha upinzani wake wa muda mrefu wa kujiunga na muungano wa Nato.

    Jumapili Andersson alisema kutofungamana na upande wowote kwa jeshi kuliisaidia pia Sweden miaka iliyopita, lakini huenda isifanye hivyo siku zijazo.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mzozo wa Ukraine: "Siioni Urusi kama adui": Waukraine wanaounga mkono uvamizi wa Urusi katika eneo la mzozo la Donbas
    • Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
    • Urusi na Ukraine: Usaidizi wa kijeshi ambao nchi za Magharibi zitatuma kwa serikali ya Ukraine (na mabadiliko ya msimamo wa Ujerumani)
  11. Habari za hivi punde, Belarus kutuma vikosi katika mpaka wa Ukraine - Uingereza

    Belarus imetangaza kupeleka vikosi maalum vya operesheni kwenye mpaka wa Ukraine, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema katika taarifa zake za kijasusi.

    Pia imetuma vitengo vya ulinzi wa angani, silaha na makombora kwa mazoezi ya kijeshi magharibi mwa nchi hiyo, taarifa hizo zimeongezea.

    "Uwepo wa vikosi vya Belarus karibu na mpaka wa Ukraine kunaweza kuwazuia wanajeshi wa Ukraine ili kutoweza kupeleka wanakjeshi zaidi kusaidia katika operesheni za jimbo la Donbas lakini inaongezea kwamba kufikia sasa vikosi vya Belarusi havijahusika moja kwa moja katika mzozo huo".

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Unaweza pia kusoma:

    • Mzozo wa Ukraine: "Siioni Urusi kama adui": Waukraine wanaounga mkono uvamizi wa Urusi katika eneo la mzozo la Donbas
    • Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
    • Urusi na Ukraine: Usaidizi wa kijeshi ambao nchi za Magharibi zitatuma kwa serikali ya Ukraine (na mabadiliko ya msimamo wa Ujerumani)
  12. Ufyatuaji wa risasi Buffalo: Mfyatuaji aliwalenga waathiriwa weusi - meya

    Wanawake

    Mwanaume anayeshukiwa kuwafyatulia risasi na kuwauwa watu 10 katika duka la jumla katika mji wa Buffalo, New York, alitafuta kwa makusudi eneo walipokuwa watu weusi maafisa wanasema.

    Mshukiwa, Payton Gendron, mwenye umri wa miaka 18, alisafiri kwa zaidi ya kilomita 320 (maili 200) kufanya shambulio, polisi ilisema.

    Rais wa Marekani Joe Biden amezungumzia juu ya mauaji hayo yaliyochochewa ubaguzi wa rangi katika Buffalo.

    Bw Biden aliuambia umati wa watu kuwa yeye na mke wake, Dr Jill, wanawaombea waathiriwa, na kwamba ''chuki imeendelea kuwa doa kwenye roho ya Marekani ".

    Shambulio hilo linachunguzwa kama kitendo cha uchochezi wa ghasia za ubaguzi wa rangi.

    Meya wa Buffalo Byron Brown alisema mshukiwa aliwasili akilenga kuchukua ’’maisha ya watu weusi wengi iwezekanavyo ".

    Maswali yanaulizwa kuhusu jinsi alivyofanya shambulio wakati alikuwa tayari anachunguzwa na mamlaka.

    Bw Gendron awali alitrishia kufanya shambulio la risasi katika shule yake ya sekondari mwezi Juni mwaka uliopita, afisa wa usalama aliliambia shirika la habari la Associated Press. Alifanyiwa uchunguzi wa afya ya akili baadaye.

    Sawa na mashambulio mengine ya risasi nchini Marekani , mshukiwa aliacha maelezo marefu mtandaoni.

    Chanzo cha picha, ERIE CO DA

    Maelezo ya picha, Sawa na mashambulio mengine ya risasi nchini Marekani , mshukiwa aliacha maelezo marefu mtandaoni.

    Christchurch, El Paso, Pittsburgh na sasa Buffalo – maeneo mengine ambako mashambulio yaliyochochewa na ubaguzi wa rangi, wenye itikadi kali za mtandaoni, wamemefanya itikadi zao kuwa kali na za hatari kiasi cha kuua.

    Mshambuliaji katika Buffalo, sawa na washambuliaji wa awali alipeperusha moja kwa moja mtandaoni tukio hilo la ghasia na kuacha kile kinachoitwa "manifesto" mtandaoni . Ilielezea kwa kina imani zake za itikadi kali na ilijaa takwimu bandia, thana potofu na utani wa mtandaoni kwa njia ya michoro.

  13. Vita vya Urusi: Jeshi la Nato kuanza kufanya mazoezi kihistoria

    NATO

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mazoezi makubwa zaidi katika historia ya ya Baltics ya Muungano wa kijeshi wa Nato yanaanza baadaye hii leo. Mazungumzo hayo yamepewa jina la siri la Hedgehog.

    Mzoezi hayo yatafanyika katika taifa la Estonia kwa kipindi cha wiki mbili zijazo na yatawahusisha wanajeshi 15,000 kutoka nchi kumi, zikiwemo Uingereza, Marekani na wajumbe wa hivi karibuni kabisa wa Muungano wa Nato - Finland na Sweden.

    Licha ya kwamba mazoezi hayo yalikuwa yamepangwa hata kabla ya Urusi kuanza uvamizi wake nchini Ukraine, mazoezi haya sasa yameibua kwa kiasi kikubwa wasi wasi baina ya Nato na Urusi.

    Katika dhana ya uvamizi wa Warusi, mazoezi haya ni muhimu sana kwa mataifa ya Baltic, kwani lengo lake ni kufanya majaribio ya uwezo wao katika kujibu uvamizi sawa wa maadui.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mzozo wa Ukraine: "Siioni Urusi kama adui": Waukraine wanaounga mkono uvamizi wa Urusi katika eneo la mzozo la Donbas
    • Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
    • Urusi na Ukraine: Usaidizi wa kijeshi ambao nchi za Magharibi zitatuma kwa serikali ya Ukraine (na mabadiliko ya msimamo wa Ujerumani)
  14. Mazungumzo yaanza kwa ajili ya kuwaondosha wanajeshi wa Ukraine waliojeruhiwa Mariupol

    Vikosi vya Urusi viliuvamia mji wa Mauripol vilipokuwa vikitaka udhibiti wa jimbo.

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Vikosi vya Urusi viliuvamia mji wa Mauripol vilipokuwa vikitaka udhibiti wa jimbo.

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa wanafanya juhudi kubwa kuhakikisha wanawaondosha wanajeshi wao waliojeruhiwa katika jimbo laMariupol.

    Zelensky alitoa kauli hiyo katika matangazo ya kila wiki ambayo amekuwa akiyatoa tangu uanze uvamizi wa Urusi dhidi yan chi yake.

    Itakumbukwa kwamba Urusi inataka sana kuchukua udhibiti wa mji wa Mariupol, ambao wamekuwa wakiupiga kwa makombora kwa miezi.

    Wakati huo huo, vikosi vya Ukraine vilivyopo karibu na Mariupol vilijificha katika kiwanda cha chumawakati vikosi vya Urusi vilipowashambulia.

    Jeshi limetoa wito wa msaada baada ya wanajeshi wengi kujeruhiwa.

    Hapakuwa na njia ambayo wangeweza kuitumia kutoiroka kwasbabu jeshi la Urusi lilikuwa limezingira eneo lao.

    Katika hotuba hiyo, Rais Zelensky alisema kuwa wameanza mazungumzo ya kuangalia iwapo vikosi vya Urusi vitaruhusu kuwaondoa majeruhi.

    Lakini Zelensky pia alisema yalikuwa ni mazungumzo magumu mno.

    Hakuwataja wawakilishi wa Ukraine katika mazungumzo hayo, lakini alisema ni wao waliotaka yaanzishwe.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mzozo wa Ukraine: "Siioni Urusi kama adui": Waukraine wanaounga mkono uvamizi wa Urusi katika eneo la mzozo la Donbas
    • Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
    • Urusi na Ukraine: Usaidizi wa kijeshi ambao nchi za Magharibi zitatuma kwa serikali ya Ukraine (na mabadiliko ya msimamo wa Ujerumani)
  15. Vita vya Ukraine: Uvamizi wa Urusi haufanyiki kama ulivyopangwa, Nato yasema

    mwanajeshi

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Vikosi vya Urusi havikuwa vimejiandaa kwa upinzani unaofanywa na Ukraine

    Katibu mkuu wa Muungano wa Nato anasema vita vya Urusi nchini Ukraine havifanyiki kama vilivyopangwa na kwamba jaribio lake la kuliteka jimbo la mashariki la Donbas "limekwama".

    Jens Stoltenberg pia amesema kuwa Ukraine inaweza kushinda katika mzozo huo.

    Waziri wa ulinzi wa Uingereza (MoD) anakadiria kuwa Urusi imepoteza karibu theluthi ya vikosi vyake vya mapigano tangu vita vilipoanza mwezi Februari.

    Uvamizi wa Urusi umekuwa ukiathiriwa na upinzani mkali wa Waukraine na matatizo ya vifaa.

    Lengo lake la awali lilionekana kuwa ni kuyateka maeneo yote yan chi na kuupindua serikali ya Ukraine.

    Kinyume chake, Urusi ilijiondoka kutoka katika maeneo yanayozingira mji mkuu, Kyiv baada ya kushindwa kuuteka na tangu katikati mwa mwezi Aprili imekuwa ikiimarisha juhudi zake katika majimbo mawili ya mashariki.

    Katika mji mkubwa wa pili wa Ukraine Kharkiv, maafisa wanasema vikosi vya Urusi vimejiondoa kutoka kwenye mpaka na kwamba wakakazi wanarejea katika mji huo.

    "Vita vya Urusi haviendi kama Moscow ilivyokuwa imepanga," alisema Stoltenberg.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mzozo wa Ukraine: "Siioni Urusi kama adui": Waukraine wanaounga mkono uvamizi wa Urusi katika eneo la mzozo la Donbas
    • Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
    • Urusi na Ukraine: Usaidizi wa kijeshi ambao nchi za Magharibi zitatuma kwa serikali ya Ukraine (na mabadiliko ya msimamo wa Ujerumani)
  16. Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu mubashara leo, ikiw ani tarehe 16.05.2022