Rais wa Mali anusurika baada ya jaribio la kumdunga kisu Msikitini

Wanaume wawili wamejaribu kumdunga kisu rais wa mpito wa Mali Assimi Goïta katika msikiti uliopo katika mji mkuu, Bamako

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Sala ya Eid al-Adha yaendelea wakati makombora yakipigwa Afghanistan

    Huu ni wakati ambao makombora yalikuwa yanapigwa katika mji wa Kabul nchini Afghanstan, karibu na Ikulu ya rais wakati wa sala za sherehe za Eid al-Adha:

    Maelezo ya video, Eid al-Adha prayers continue as rockets fired in Afghanistan
  2. Rais wa Mali ni 'salama' baada ya shambulio la kisu Msikitini

    Rais Assimi Goïta (aliyeva kanzu ya blu) kabla ya shambulio

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Rais Assimi Goïta (aliyeva kanzu ya blu) kabla ya shambulio

    Rais wa Mali Assimi Goïta ni ‘’salama " baada ya mshambuliaji aliyekuwa amejihami kwa kisu kumshambulia katika msikiti uliopo katika mji mkuu , Bamako, imesema ofisi yake.

    Mwandishi wa habari wa AFP aliyekuwa katika msikiti wa Bamako-Grande Mosque ambako Kanali Goïta alikuwa amejiunga na waumini kwa ajili ya ibada ya Idd ul-Adha amesema kuwa alishmbuliwa na wanaume wawili, lakini ni mmoja aliyekuwa amejihami kwa kisu.

    Taarifa ya ofisi ya rais imesema kuwa mshambuliaji alikamatwa mara moja na rais aliondoshwa msikitini kwa gari mara moja hadi katika kambi za jeshi zilizopo nje ya jiji .

    AFP imesambaza picha ya kanali Goita akipunga mkono baada ya tukio:

    Goita

    Chanzo cha picha, AFP

    Waziri amelielezea shambulio hilo kama jaribio dhidi ya maisha ya rais.

    Umati mkubwa ulikuwa umekusanyika katia msikiti kwa ajili ya sala, ya Idd ya kuchinja kafala.

    Goita

    Chanzo cha picha, AFP

    Wengi walisali kwenye viwanja vya msikiti

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Wengi waliisali kwenye viwanja vya msikiti
    Kondoo

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Kondoo alitolewa kafara na Imam mwisho wa sala

    Shambuliolinalia hofu kwa nchi inayokabiliwa na changamoto za kiusalama, ikiwa ni pamoja na uasi wa makundi ya jihad yanayofanya mashambulio ya mara kwa mara ya makundi yenye uhusiano naal-Qaeda na Islamic State

    Kanali Goïta ni mtu mwenye utata – kwa kufanya mapinduzi mawili ya kijeshi chini ya mwaka mmoja .

    Alijitangaza kama rais mwezi Mei baada ya kuiondoa mamlakani serikali iliyokuwa imewekwa baada ya kuongoza mapinduzi dhidi ya rais wa zamani Ibrahim Boubacar Keïta mwezi Agosti mwaka jana.

    Aliahidi kuirejesha nchi katika utawala kamili wa kiraia mapema mwaka ujao.

  3. Maelfu wajitokeza kuuaga mwili wa Kardinali DRC

    Umati

    Maelfu ya watu katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo wanatoa heshima zao kwaKardinali Laurent Monsengwo – Askofu mkuu wa zamani wa Kanisa Katoliki aliyeheshimiwa na watu wengi kwa kuongoza juhudi za kutetea haki za binadamu

    Rais Félix Tshisekedi na mwenzake wakutoka nchi jirani ya Kongo –Brazaville, Denis Sassou-Nguesso wanahudhuria ibada maalum ya wafu inayofanyika katika mji mkuu Kinshasa.

    Kardinali Monsengwo alizungumzia na kulaani unyanyasaji uliofanya na jeshi na alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali za kurithishana.

    Umati

    Pia alihusika katika utekelezaji wa jukumu muhimu kama mpatanishi wakati mzozo DRC ilipokumbwa na mizozomikubwa wa kisiasa, kwanza katika miaka ya 1990 wakati wa utawala wa Mobutu Sese Seko na ule uliotokea wakati wa utawala wa Joseph Kabila.

    Umati
  4. Wajaribu kumdunga kisu kiongozi wa mpito wa Mali Msikitini

    Kanali Goïta

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Haijawa wazi iwapo Kanali Goïta, aliyengoza jeshi kutwaa mamlaka mwezi Agosti, amejeruhiwa

    Wanaume wawili wamejaribu kumdunga kisu rais wa mpito wa Mali Assimi Goïta katika msikiti uliopo katika mji mkuu, Bamako.

    KanaliGoïta allikuwa akihudhuria ibada ya siku ya Eid ul-Adha katika msikiti wa Grand Mosque.

    Mafisa wanasema washambuliaji, ambao kwa mujibu wa Shirika la habari la AFP walikuwa ni wawili, wamekamatwa na rais ameondolewa kwenye msikiti huo kwa usalama wake.

    Haijafahamika iwapo Kanali Goïta, ambaye aliongozajeshi kuchukua mamlaka mwezi Agosti, alijeruhiwa.

    Waziri wa masuala ya kidini Mamadou Kone aliliambia shirika la AFP kwamba mwanaume ali "jaribu kumuua rais wa kisu".

    Mkurugenzi wa msikiti aliliambia shirika la habari kwamba mtu alimlenga waziri lakini alimjeruhi mtu mwingine.

    Kabla ya mapinduzi ya mwezi Agosti nchi hiyo ilikuwa inakabiliwa na maadamano juu ya ufisadi na waasi wa Kiislam walikuwa wameyateka maeneo mengi ya nchi.

    Kanali Goïta aliingilia kati tena mwezi Mei, akachukua nafasi ya serikali ya mpito na kuchukua mamlaka kama rais- aliahidi kukabidhi utawala wa kiraia mamlaka kama ilivyopangwa mwaka ujao.

  5. Mtu tajiri zaidi duniani kupaa anga za mbali leo

    Safari za New Shepard zinaendeshwa kutoka eneo la jangwa katika West Texas

    Chanzo cha picha, BLUE ORIGIN

    Maelezo ya picha, Safari za New Shepard zinaendeshwa kutoka eneo la jangwa katika West Texas

    Bilionea Jeff Bezos ataingia katika anga za mbali Jumanne katika chombo chake cha kwanza chenye wahudumu cha roketi yake inayofahamika kama New Shepard.

    Atakuwa ameambatana na Mark Bezos, kaka yake, Wally Funk,na mwanzilishi wa mbio za anga za mbali mwenye umri wa miaka 82, pamoja na mwanafunzi mwenye umri wa miaka 18.

    Watasafiri katika chombo chenye madirisha makubwa zaidi, yatakayowawezesha kutazama mandhari nzuri za kushangaza za dunia.

    Kutoka kushoto: Mark Bezos, Jeff Bezos, Oliver Daemen, Wally Funk

    Chanzo cha picha, IMAGE COPYRIGHTBLUE ORIGIN

    Maelezo ya picha, Kutoka kushoto: Mark Bezos, Jeff Bezos, Oliver Daemen, Wally Funk

    Chombo hicho cha anga za mbali New Shepard, kilichotengenezwa na kampuni ya Bezos Blue Origin, kimeundwa kwa kwa ajili ya kuhuduma za sokko la utalii wa anga za mbali.

    "Nimefuhrahi. Watu wanaendelea kuniuliza kama . Sina hofu kusema kweli, nina udadisi. Ninataka kujua nini tunaenda kujifunza ," Bezos alisema katika mahojiano na kituo cha habari cha CBS News.

    "Tumekuwa tukifanya mafunzo. Gari hili liko tayari, wasafiri hawa wako tayari, timu hii ni nzuri. Kusema kweli tunahisi vizuri juu ya safari hii."

  6. Kiongozi anayeshutumiwa kufanya kampeni ya kujitenga jimbo la Nigeria akamatwa

    Sunday Igboho amekuwa akifanya kampeni kwa ajili ya kuundwa kwa jimbo huru la Yoruba

    Chanzo cha picha, SAIF

    Maelezo ya picha, Sunday Igboho amekuwa akifanya kampeni kwa ajili ya kuundwa kwa jimbo huru la Yoruba

    Kiongozi wa anayepigania kujitenga kwa kabila la Yoruba Sunday Adeyemo, al maarufu kama Sunday Igboho, amekamatwa katika nchi jirani yaBenin, wiki kadhaa baada ya kutangazwa kuwa anasakwa kwa madai ya kukusanya silaha.

    Bw Igboho alikamatwa na vikosi vya uslama katika uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Benin -Cotonou, Jumatatu usiku.

    Vyanzo vya habari vimeviambia vyombo vya habari kwamba alikuwa anaelekea nchini Ujerumani na sasa atarudishwa nchini Nigeria Jumanne.

    Idara ya huduma za kitaifa nchini Nigeria awali ilisema kuwa inamtafuta Bw Igboho baada ya kukwepa uvamizi uliofanywa kwenye makazi yake kusini-mashariki mwa jimbo la Oyo.

    Vikosi vya usalama nchini Nigeria bado havijatoa kauli yoyote juu ya kukamatwa kwake.

    Vikosi vya usalama vilifanya uvamizi tarehe 1Julai katika makazi ya Bw Igboho, siku mbili baada ya mwanaharakatihuyo kuitisha maandamano dhidi ya serikali. Shirika hilo lilisema kuwa liligundua rundo la silaha kutoka kwenye nyumba ya Bw Igboho.

    Bw Igboho amekuwa akifanya kampeni kwa ajili ya kuunda jimbo huru la Yoruba lililopo kusini-magharibi mwa Nigeria.

    Kiongozi huyo anayetaka kujitenga amekuwa akishutumiwa kwa kuchochea ghasia dhidi ya wafugaji wa jamii ya Fulani katika majimbo ya kusini, madai ambayo anayakana.

  7. Mwanamfalme wa Saudia awapatia vijana mamilioni ya pesa za kuoa

    Mwanamfalme

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mwanamfalme wa Saudia Muhammad Bin Salman ameidhinisha kutolewa kwa pesa milioni 3.74 za riyali, sawa na dola milioni 1 za kimarekani, ili zigawiwe kwa vijana 200 kama ruzuku ya kuoa.

    Gazeti la serikali la Saudi Arabia limeripoti kwamba tangazo hilo lilitolewa na Shirika la habari la Saudia siku ya Jumapili.

    Taarifa hiyo ilisema kuwa fedha hizo zitagawanywa kwa vijana wa kiume na wa kike kote nchini humo.

    Limesema agizo la Mwanamfalme huyoni katika juhudi za kuwasaidia yatima wenye ulemavu na watu wenye ulemavu ambao wamekuwa na shida ya kuoa.

    Katika awamu ya kwanza ya mpango huo, riyali milioni 250 za msaafda zilisambazwa, kwa watu zaidi ya 26,000 kutoka maeneo tofauti ya nchi hiyo.

    Licha ya kupewa pesa, vijana watafundishwa jinsi ya kutumia pesa.

    Mpango wa Mwanamfalme Muhammed Bin Salman ulianzishwa kwa lengo la kuimarisha uchumi na jamii ya watu wa nchi hiyo kuboresha maisha ya watu.

  8. Tanzania kupewa chanjo ya corona chini ya mpango wa Uholanzi

    Corona

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Afrika zitakazonufaika na mpango wa chanjo unaosimamiwa na Serikali ya Uholanzi.

    Uholanzi imetenga dozi 750,000 za chanjo aina ya Astrazeneca kwa ajili ya nchi zenye mahitaji ikiwemo Tanzania na Namibia. Dozi hizo zimehifadhiwa tayari kwa ajili ya kusambazwa kwa nchi hizo zilizoonyesha nia ya kusaidiwa.

    Uholanzi kupitia mamlaka zake za afya inachangia chanjo kusaidia nchi masikini kukabiliana na virusi vya Corona, ikifanya hivyo pia kwa kuchangia karibu dozi nusu milioni kwenye mpango wa chanjo kwa nchi masikini (Covax).

    Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu Uholanzi inatarajiwa kuchangia dozi milioni 20 kwenye mpango huo.

    Kwa mujibu wa tovuti ya Uholanzi mbali na Tanzania, Cape Verde na Indonesia ni miongoni mwa nchi zilizonufaika na hatua hiyo ya Uholanzi.

    Mapema mwezi huu, Uholanzi ilitangaza kuipa Indonesia dozi milioni 3 za chanjo hiyo, ingawa haijafahamika wazi, ni kiwango gani cha chanjo zitapelekwa Tanzania na Namibia,

    Serikali ya nchi hiyo imeeleza kuwa wizara yake ya afya itasimamia usambazaji wake kuzifikia nchi hizo.

    Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi chache duniani ambazo hazikuwa zimekubali chanjo ya Corona, hasa kutokana na msimamo wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, John Magufuli, aliyekuwa anazitilia shaka chanjo za corona, akitaka ufanyike utafiti wa kina kabla ya kuzikubali.

    Wakati upande wa pili wa Muungano, Zanzibar ukiendelea kutoa chanjo, Serikali ya Tanzania kupitia Rais Samia Suluhu Hassan iko katika hatua mbalimbali za kuingiza chanjo mbali mbali za corona ambazo zitatolewa kwa uhuru kwa wananchi wake.

    Unaweza pia kusoma:

    • Virusi vya Corona: WHO yasema chanjo ya corona inaweza kufika Tanzania ndani ya wiki mbili
    • Virusi vya corona: Marekani yaunga mkono ruzuku ya hakimiliki ili kuongeza usambazaji wa chanjo
    • Virusi vya Corona Tanzania: Tanzania kuna wagonjwa zaidi ya 100 wa wimbi jipya la corona
  9. Majambazi waidungua ndege ya jeshi ya Nigeria

    Rubani Luteni Abayomi Dairo alipongezwa na Mkuu wa kikosi cha anga , Air Marshal Oladayo Am

    Chanzo cha picha, NAF

    Maelezo ya picha, Rubani Luteni Abayomi Dairo alipongezwa na Mkuu wa kikosi cha anga , Air Marshal Oladayo Amao

    Majambazi nchini Nigeria wameidondosha ndege ya jeshi katika tukio la nadra la kuangushwa kwa ndege ya kijeshi la kuangushwa kwa ndege na genge la uhalifu nchini humo.

    Rubani alikuwa amekamilisha uvamizi dhidi ya watekaji nyara wakati aliposhambuliwa kwa risasi, limesema jeshi la anga.

    Rubaji wa ndege hiyo Luteni Abayomi Dairo alifanikiwa kutokandani kwa kutumia"mbinu za kujiokoa" ili kuepuka kukamatwa na baadaye akatafuta mahala pa kujihifadhi, kabla ya kujiunga tena na wenzake.

    Shambulio hilo lilitokea kwenye mpaka wa kaskazini uliopo baina ya majimbo ya Zamfara na Kaduna.

    Magenge yenye silaha –yanayoelezewa nan a wakazi wa eneo hilo kama ‘’majambazi’’-yamekuwa yakilaumiwa kwa msururu wavitendo vya utekaji nyarakatika eneo hili la kaskazini mwa Nigeria.

    Wanafunzi na watoto wa shule wamekuwa wakilengwa na utekaji huo-huku zaidi ya 1000 wakiripotiwa kutekwa nyara tangu mwezi wa Disemba. Wengi wao wameokolewa, baada ya kulipa kikombozi, lakini baadhi yao wamekuwa wakiuawa.

    Katika siku za hivi karibuni, Rais Muhammadu Buhari aliagizajeshi kufanya liwezekanalo kuwamaliza wahalifu katika majimbo ya Katsina, Zamfara na Kaduna.

    Kikosi cha anga cha Nigeri-The Nigerian Air Force kimesema kuwa kimeanza harakati za usiku na mchana dhidi ya majambazi kwa ushirikiano na kikosi cha ardhini. Ilikuwa ni katika maojawapo ya harakati hizo ambapo moja ya ndege zake aina ya jet ilidondoshwa.

  10. Eid Mubarak!, na karibu tena kwa matangazo yetu mubashara leo Jumanne tarehe 20.07.2021