Katiba mpya: CHADEMA kimesema hakitaendelea kumpigia magoti Rais-Mbowe

Chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania, CHADEMA kimesema hakitaendelea kumpigia magoti Rais wa nchi hiyo, Samia Hassan Suluhu kuhusu mustakabali wa taifa hilo.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Na kufikia hapo tumefika mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja .Hadi hapo kesho majaaliwa

  2. Virusi vya nyani - Monkey B vyasababisha kifo cha mtu mmoja China

    virusi

    Chanzo cha picha, BARCROFT MEDIA/GETTY

    Mtu mmoja amepoteza maisha baada ya kuambukizwa virusi vya Nyani jijini Beijing China.

    Gazeti la Global Times limethibitisha taarifa za kifo chake.

    Kwa mujibu wa Global Times, mtu huyo amekufa baada ya kupata maambukizi ya virusi vya nyani, na wale wote waliokuwa karibu na mtu huyo wako salama.

    Mtu huyo, daktari mwenye miaka 53 alikuwa akifanyianyani utafiti

    Mwezi Machi walifanya utafiti kwa nyani wawili waliokuwa wamekufa, na mwezi mmoja baadayewalianza kupata kichefuchefu na kutapika.

    Hii iliripotiwa na jarida la wiki la China CDC Jumamosi iliyopita.

    Madaktari walitibiwa katika hospitali kadhaa, lakini walipoteza maisha tarehe 27 mwezi Mei.

    Hakuna maambukizi mengine yaliyohusishwa na virusi hivyo hapo kabla. Ni mara ya kwanza kumeripotiwa maambukizi ya virusi vya monkey B na vifo.

    Watafiti walichukua sampuli za neva mwezi Aprili na kubaini kuwepo kwa virusi vya nyanindani yake.

    Lakini habari njema ni kuwa hakuna aliyeambukizwa wala kuonesha dalili za maambukizi.

    Virusi vya nyani vilijitokeza duniani mwaka 1932. Kirusi husambaa kupitia kugusana na nyani . Uwezekano wa vifo kutokana na virusi vya monkey B ni asilimia 70 mpaka 80.

    Hivyo, virusi hivyo vinaweza kuwa hatari na tahadhari ya hali ya juu inapaswa kuchukuliwa.

    Virusi vya Monkey B ni nini ?

    Virusi vya monkey B au virusi vya herpes huambukizwa kutoka kwa nyani wakubwa (nyani wenye mikia).

    Virusi hivi huwa ni nadra kuwepo kwa binadamu. Lakini mtu akiambukizwa, anaweza kupata maradhi ya mahusiano na neva, pia kuvimba kichwa na uti wa mgongo.

    Virusi vinasambaa vipi?

    Ikiwa nyani aina ya macaque ataiuma ngozi au kuikwaruza, virusi vinaweza kusambaa kwa binadamu pia kutoka kwenye mate na kinyesi cha nyani walioathirika.

    Mbali na hili, vinaweza kufikia miili ya binadamu katakana na sindano zenye maambukizi.

    Virusi vinaweza kuishi kwa saa nyingi kwenye vitu.

    Kwa mujibu wa Tume ya afya ya Boston, watu wanaofanya kazi kwenye maabara , waganga wa mifugo au wanaowatibu nyani wako hatarini kuathiriwa na virusi.

    Dalili za virusi

    Virusi vinapoingia kwenye mwili wa mtu , dalili zake hujitokeza ndani ya mwezi mmoja.

    Mara nyingi dalili hizi zinaweza kujitokeza kuanzia siku tatu mpaka saba. Kwa namna gani dalili hizi husambaa hutegemea chembechembe za maambukizi.

    Hatahivyo dalili si lazima zifanane katika kila maambukizi.

    Dalili zinazojitokeza

    Kutoboka sehemu yenye maambukizi

    Kuwashwa au maumivu ya kuwaka moto karibu na kidonda

    Kupata kama mafua

    Kuhisi homa au baridi

    Maumivu ya kichwa kwa zaidi ya saa 24

    Uchovu

    Maumivu ya misuli

    Changamoto ya kupumua

    Kukosa pumzi kunaweza kutokea kutoka siku ya tatu mpaka majuma matatu na hali ikiendelea hivi husababisha kifo.

    Tiba

    Tume ya Afya ya Boston imeripoti kuwaikiwa mtu aliyeathirika na virusi hatatibiwa, mtu huyo anaweza kufa kwa asilimia 70 ya maambukizi. Ikiwa utang’atwa na nyani, unaweza kupata maambukizi.

    Ikiwa hali hii itajitokeza huduma ya kwanza inahitajika kuanza haraka sana

    Ni muhimu kusafisha jeraha vizuri kwa sabuni na maji .

    kwa mujibu wa ripoti ya tume hiyo, dawa za kupambana na virusi zinapatikana kwa ajili ya kupambana na virusi vya monkey B, lakini hakuna chanjo yoyote inayopatikana.

  3. Maelfu ya farasi wa mashindano wachinjwa Uingereza na Ireland-Lakini kwanini?

    FARASI

    Chanzo cha picha, ANIMALAID

    Maelfu ya farasi wa kukimbia wanapelekwa kwenye vichinjio huko Uingereza na Ireland, uchunguzi wa BBC Panorama umegundua

    Baadhi ya wanyama waliochinjwa walikuwa wanamilikiwa na kufundishwa na watu wenye majina tajika katika fani ya mashiondano ya farasi .

    Picha za video zilizorekodiwa kisiri pia zilionyesha jinsi sheria zilizoundwa kulinda farasi kutokana na vifo vya kikatili zinaonekana kupuuzwa mara kwa mara kwenye moja ya vichinjio vikubwa nchini Uingereza.

    Vichinjio hivyo vimeiambia BBC kuwa havikubali aina yoyote ya unyanyasaji wa wanyama.

    Mtaalam mmoja alielezea picha ya siri, kutoka kwa kamera zilizowekwa na kikundi cha kampeni ya haki za wanyama Animal Aid ,kama ushahidi wa ukiukaji wa wazi wa kanuni.

    Mnamo Februari iliyopita, picha ya mkufunzi wa hali ya juu wa farasi wa mashindano Gordon Elliott akiwa amekaa juu ya farasi aliyekufa ilizua mihemko na mawimbi ya lalama kotekatika ulimwengu wa mbio za farasi .

    Elliott, ambaye amewafundisha washindi watatu wa Grand National, alishtumiwa vikali, na kusimamishwa kucheza hadi 9 Septemba mwaka huu.

    Tukio hilo lilisababisha lalama, lakini pia lilionyesha hatima ya farasi wengi kwenye fani hiyo ambao hufa mashindanoni, kwenye mazoezi au kwenye vichinjio.

    Uhuru wa maombi ya habari ulifichua kwamba farasi wa zamani wa mbio 4,000 walichinjwa huko Uingereza na Ireland tangu mwanzo wa 2019. Wengi, lakini sio wote, walifundishwa nchini Ireland.

    Animal Aid , ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikifanya kampeni ya kumaliza mbio za farasi, iliweka kamera za kufichwa huko Drury and sons kichinjio huko Uingereza ambacho kina leseni ya kuua farasi.

    "Tulipotazama video tulishangazwa sana na idadi kubwa ya farasi wachanga wanaouliwa," alisema msemaji wa Animal Aid Dene Stansall.

    Video hiyo ilirekodiwa kwa zaidi ya siku nne mwishoni mwa 2019 na mwanzo wa 2020.

    Ilinasa farasi kadhaa wa zamani wa mbio wakichinjwa, wengi wao kutoka Ireland na wachanga

    FARASI

    Farasi wengine waliopigwa risasi kwenye vichinjio walikuwa na taaluma nzuri za mbio, wakishinda maelfu ya pauni.

    Watatu kati yao walikuwa wamefundishwa na Gordon Elliott katika zizi lake la kisasa huko County Meath, Ireland.

    Aliiambia Panorama hakuna mnyama hata mmoja kati ya wale watatu aliyetumwa vichinjio naye.

    Farasi walikuwa wamestaafu mbio kutokana na majeraha, alisema, na hawakuwa chini ya uangalizi wake wakati walipouawa.

    Elliott alisema farasi wawili walitumwa kwa muuzaji wa farasi "apewe jina jipya ikiwezekana, na ikiwa sivyo, auawe kwa njia ya kiutu " kulingana na kanuni.

    Alisema alimpa farasi mwingine wa tatu kwa mtu kama alivyoomba mmiliki wake.

    Na akasema mara ya kwanza kujua hatima yao ni wakati Panorama ilipowasiliana naye.

    Elliott alisema amehakikisha njia sahihi na na zifaazo za wanyama ambao amekuwa akiwamiliki na amewapa hifadhi wengi wa farasi hao

  4. Katiba mpya: 'tuko tayari wote kuwekwa ndani, asema Kiongozi wa Upinzani Tanzania Mbowe

    The Citizen

    Chanzo cha picha, The Citizen

    Chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania, CHADEMA kimesema hakitaendelea kumpigia magoti Rais wa nchi hiyo, Samia Hassan Suluhu kuhusu mustakabali wa taifa hilo.

    Mwenyekititi wa CHADEMA, Freeman Mbowe amewaambia waandishi wa habari hayo leo, kufuatia Jeshi la Polisi la nchi hiyo kuwakamata viongozi, wanachama wa chama hicho pamoja na viongozi wa dini 38 waliokuwa wahudhurie mkutano wa chama hicho kupitia baraza lake la vijana (BAVICHA) wenye lengo la kuhamasisha kupatikana kwa katiba mpya ya nchi hiyo.

    Mara baada ya kuingia madarakani mwezi Machi mwaka huu, Rais Samia alitangazia umma dhamira yake ya kukutana na wapinzani ili kuzungumzia maswala mbalimbali ikiwemo ya kisiasa na namna gani ya kuendesha shughuli za siasa. Licha ya kukutana na makundi mengine kama vijana, wazee na wanawake mpaka sasa Rais Samia hajakutaa na wapinzani.

    ‘‘Hatuwezi kuendelea na ule utaratibu wa zamani, tuna haki ya kukutana tunakamatwa, tunapigwa, tunashitakiwa, tunasoteshwa mahakamani miaka miwili miaka mitatu, kisha tunaachiwa huru, ama tunahukumiwa vifungo batili tukikata rufaa sote tunashinda’, alisema Mbowe

    Pamoja Polisi kuzuia mkutano huo uliokua ufanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Boma wiki hii na kukamata watu hao 38, Kiongozi huyo wa Upinzani amesema, mkutano upo pale pale na utafanyika wiki hii na kama kukamatwa wako tayari kukamatwa wote.

    ‘Kama wanataka kuwaweka ndani wanachadema kwenye hoja hii ya katiba, wapanue kwanza na magereza, kwa sababu tuko tayari wote tuwekwe ndani , na wala hatutaomba dhamana’ alisema Mbowe kabla ya kulaani kitendo cha Jeshi la Polisi Mwanza, kuwakamata viongozi wa dini na wafuasi wa chama hicho

    Kwa zaidi ya miaka mitano sasa tangu utawala wa Rais John Magufuli na sasa utawala wa Rais Samia mikutano ya kisiasa imezuiliwa kufanyika nchini humo, hatua inayopingwa vikali na upinzani wanaosema, katiba inaruhusu mikusanyiko na sheria za nchi zinaruhusu mikutano hiyo ya kisiasa kufanyika.

    Mbowe amesema kama Chama na wananchi wa Tanzania wana haki ya kukutana kwa mujibu wa sheria, hivyo chama chake kitafanya mkutano wa juu wa Baraza kuu la chama Julai 31 mwaka huu ili kutoa baraka ya kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima.

    ‘Ni haki yetu kukutana, tutahama kutoka mikutano ya hadhara na sasa tutaingia kuandamana. Tunamwambia mama Samia Suluhu, akizidi kuchelewesha jambo hili, anazidi kuleta mpasuko katika nchi hii, anavyolichelewesha anachelewesha kuwaunganisha Watanzaia, tujenge taifa moja la watu wanaopenda na kuheshimiana’, alisema Mbowe

    Alipozungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, kuhusu masuala ya katiba mpya na na mikutano ya hadhara Rais Samia alisema kwanza apewe muda wa kujenga uchumi na kufungua nchi kabla ya kuruhusu mikutano hiyo na masuala mengine ya kisiasa.

    Unaweza pia kusoma:

    • Siku 100 za Rais Samia Suluhu: Zama zinarejea lakini Katiba Mpya ni mfupa mgumu kwa Samia
    • Katiba Mpya Tanzania: Ni mtego kwa Rais Samia?
    • Tundu Lissu amtaka Rais Samia kuanzisha mchakato wa katiba mpya Tanzania
  5. Hija 2021: Tazama jinsi mahujaji wanavyoondoka kutoka msikiti wa Namirah

    Mahujaji wameondoka kwenye msikiti baada ya kumaliza sala ya saa sita na ya mchana kwa pamoja

    Maelezo ya video, Video kutoka Haramain Sharifain
  6. Caroline Kagongo: ‘Binti yangu alijiua ,hakuuawa’ asema babake polisi aliyekuwa akisakwa Kenya

    KAGONGO

    Chanzo cha picha, DCI/TWITTER

    Baba wa afisa wa polisi aliyekuwa akisakwa nchini Kenya Caroline Jemutai Kangogo - aliyekufa kwa kushukiwa kujiua Ijumaa - amepinga ripoti kwamba binti yake aliuawa, akisisitiza kwamba alijiua katika mahojiano na gaeti la Daily Nation nchini humo .

    Mzee Barnabas Korir, ambaye mwenyewe aliwahi kuwa afisa wa cheo cha Inspekta katika idara ya polisi, kutoa maelezo zaidi juu ya nyakati za mwisho za Kangogo na jinsi alivyoingia kwenye boma la familia yao kwenye boda boda mwendo wa saa 10 usiku lakini hakuonekana na mtu yeyote wa familia hadi mwili wake ulipogunduliwa na mama yake Leah wakati akifanya usafi

    Mzee Kibor sasa anasema kuwa kutokana na tathmini yake mwenyewe ya eneo hilo, hakuna daalili ya njama ya mauaji ya binti yake .

    "Sipendi wakati watu wanaendelea na maneno haya kwamba huenda aliuawa. Ikiwa unajua hakika aliuawa, basi njoo na usema hivyo. Lakini kwa ninavyoona, msichana huyu, binti yangu, alijiua mwenyewe kulingana na jinsi tulivyompata, ” Mzee Kibor amenukuliwa na gazeti hilo .

    Tathmini yake amesema inatokana na ukweli kwamba bafu ambako mwili wa binti yake ulipatikana, mita 40 kutoka nyumba kuu, ilikuwa imefungwa kutoka ndani.

    “Hakuna njia ambayo mtu angeweza kuuleta mwili na kuutupa bafuni humo, akiwa ameufunga mlango kutoka ndani ambapo tulipata mwili wake. Alijifungia ndani’ amenukuliwa akisema na Daily Nation .

    Kulingana na polisi afisa huyo alimpiga risasi mwenzake John Ogweno Jumatatu tarehe 5 Julai na kisha kutorokea eneo la Juja viungani mwa mji wa Nairobi alipomuua mwanamme mwingine aliyetambuliwa kama Peter Ndwiga kwa kumpiga risasi katika chumba cha malazi hotelini.

  7. Hija Kwa Picha: Baadhi ya mahujaji katika uwanja wa Arafa wakisikiliza mawaidha

    Moja ya jambo kuu lililojitokeza katika Hija ya mwaka huu ni uamuzi wa Saudi Arabia wa kuweka ukomo wa idadi ya Waislamu watakaohudhuria sala ya Hija hadi watu 60,000.

    Maafisa wa nchi hiyo walisema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kwasababu ya ongezeko la kuenea kwa virusi vya Corona.

    Kabla ya mlipuko wa Covid 10 mwaka jana,mamilioni ya watu walishiriki Hija kila mwaka.

    Zifuatazo ni picha za baadhi ya mahujaji wa Kiislamu waliohudhuria hija ya mwaka huu wakisikiliza mawaidha katika uwanja wa Arafa.

    Haramain Sharifain/BBC Hausa

    Chanzo cha picha, Haramain Sharifain/BBC Hausa

    Haramain Sharifain/BBC Hausa

    Chanzo cha picha, Haramain Sharifain/BBC Hausa

    Haramain Sharifain/BBC Hausa

    Chanzo cha picha, Haramain Sharifain/BBC Hausa

    Haramain Sharifain/BBC Hausa

    Chanzo cha picha, Haramain Sharifain/BBC Hausa

  8. Mzozo wa Jimbo la Ethiopia Tigray unasambaa kwenye majimbo mengine

    Vikosi vya Serikali na vya jimbo la Tigray vimekuwa vikipigana kwa miezi minane

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Vikosi vya Serikali na vya jimbo la Tigray vimekuwa vikipigana kwa miezi minane

    Mzozo wa Tigray nchini Ethiopia unaonesha dalili za kupanuka zaidi kwenye maeneo mengine huku mapigano yakiripotiwa sasa katika jimbo la Afar.

    Serikali inawashutumu waasi wa Tigray Liberation Front (TPLF) ikisema wanawalenga wanamgambo wanaounga mkono serikali katika jimbo hilo.

    TPLF walisema kuwa mashambulio yao karibu na mpaka wa Afra wikendi yalikuwa "machache", ingawa serikali inashutumiwawaasi hao kwa kutumia silaha nzito.

    Kikundi hicho cha waasi kimeliambia shirika la habari la AFP kwamba kilikuwa kikiwalenga wapiganaji kutoka Oromi ambao waliletwa ndani ya eneo hilo.

    Ni vigumu kuthibitisha maelezo kuhusu mapigano au kubaini idadi ya waathiriwa.

    Mapigano mapya karibu na mpakakati yaAfar na Tigray yanaweza kuzuia juhudi za kutoa msaada wa kibinadamu – na kufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa raia wanaoishi katika jimbo lililoathiriwa mzozo la Tigray.

    Jimbo la Afar liko masharikii mwa Tigray – kaskazini mashariki mwa Ethiopia.

    Barabara za kuingia Tigray zimefungwa kutokana na mapigano na wakati jimbo la Afar limekuwa ni eneo muhimu la kupitisha misaada inayoelekea Tigray.

    Jumapili Waziri mkuu wa Ethiopia alisema kuwa jeshi na vikosi kutoka katika majimbo hayo “vinajipanga” kuwamaliza wapiganaji wa TPLF.

    Majimbo zaidi-likiwemo jimbo la Somali, Gambella, Harari – kwa sasa yanakusanya vikosi vyake ili vijiunge na mapigano na mzozo huo wa miezi minane unaonekana unaendelea kupanuka.

  9. Ujerumani yakubali kurudisha kazi za sanaa zilizoibwa Nigeria

    Vinyago

    Chanzo cha picha, ©CHRISTIE’S IMAGES LTD, 2020

    Serikali za Nigeria na Ujerumani zimekubaliana muda wa mwisho wa kurejesha vinyago vya kuchingwa vilivyoibiwa kutoka nchini Nigeria.

    Waziri wa habari na utamaduni wa Nigeria ameyasema hayo katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Lagos, uliolenga kuwafahamisha Wanigeria ni wapi zipofikia juhudi za kuhakikisha vinyago vya nchi hiyo vilivyoibiwa na kupelekwa katika maeneo mbali mbali duniani vinarudhishwa.

    Amesema pia kwamba jukumu la serikali kisheria kuchukua vinyago vya Nigeria vilivyoporwa Ujerumani nanchi nyingine kwasababu ni jambo la kisheria.

    Vinyago

    Chanzo cha picha, BRITISH MUSEUM

    Waziri huyo ameyasema hayo baada ya kuwepo kwa taarifa potofu baada ya baadhi ya ujumbe wa Nigeria kufanya ziara Ujerumani kujadili ni jinsi gani watakavyorudisha vinjyago vilivyotengenezwa kwa shaba ya Benin vipatavyo 1, 130 nchini Nigeria.

    Bw Lai serikali ya Nigeria na serikai ya Ujerumani zimekubaliana juu ya muda wa kurudisha vinyago kwasababu Nigeria tayari imeweka muda wa kurudishwa kwake.

    Amesemawalisaini makubaliano juu ya kurejeshwa kwa vinyago hivyomwezi Disemba 2021 na kuhakikisha shughuli hiyo inakamilika mwezi Agosti 2022 bila masharti.

  10. Serikali ya Tanzania kupitia upya tozo za miamala ya simu

    Mwanamke

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Serikali ya Tanzania imetangaza hii leo kuwa ipo katika mchakato wa kupitia upya tozo mpya ambazo watumiaji wa simu wanalipishwa katika miamala ya simu wanayoifanya.

    Katika taarifa iliyotolewa leo asubuhi na Waziri wa Fedha wa Tanzania Mwigulu Nchemba, serikali ya Tanzania imesema kuwa imekuwa ikipokea malalamiko juu ya utozwaji wa tozo hizo mpya.

    Tozo hizo zilizofungamanishwa na dhana ya uzalendo zilianza kutozwa Alhamisi ya wiki iliyopita na toka hapo kumekuwa na sintofahamu kubwa nchini Tanzania.

    "Rais (Mama Samia) ameshaguswa na malalamiko ya tozo za miamala ya simu, yameshatolewa maelekezo tufanyie kazi...nitoe rai kwa wananchi kuwa watulivu kwenye jambo hili," ameeleza Nchemba ambaye alikuwa ameambatana na waziri wa Mawasiliano Faustine Ndugulile.

    Kwa mujibu wa Nchemba, kikao cha ngazi ya juu cha kupitia upya jambo hilo kitafanyika kesho na kitakuwa chini ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

    • Athari tano za kiuchumi zinazoweza kutokea baada ya kuongezeka kwa tozo za miamala ya simu Tanzania

    Waziri Nchemba amesema watapitia sheria ya mfumo wa malipo serikalini inayosimamia tozo hizo pamoja na kanuni nyengine. Tangazo hilo lilorushwa mbashara kupitia runinga kadhaa ikiwemo ya taifa TBC1.

  11. Ni lini madaktari watalitibu bega la Rashford?

    Rashford

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Meneja Ole Gunnar Solskjaer, anasema hajui ni lini Rashford atafanyiwa upasuaji wa bega

    Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema haijulikani iwapo madaktari watatibu jeraha la Marcus Rashford baadaye mwezi huu.

    Wiki iliyopita Rashford alimuona daktari, ambaye alipendekeza bega lake lifanyiwe upasuaji, ili kupunguza maumivu ambayo amekuwa nayo kwa miezi kadhaa.

    Lakini meneja wa Manchester United Solskjaer na wafanyakazi wake wanasema hastahili kupewa kazi.

    Akizungumza baada ya ushindi wa 2-1 wa United katika mchezo wa kirafiki, Solskjaer alisema hakuna makubaliano yaliyofikiwa .

    "Tutaamua siku za usoni iwapo tutamtumia, na bila shaka tutazungumza na wataalam kutathmini zaidikiwango cha jeraha.

    Manchester United ilikuwa ya pili katika michuano ya Primia Ligi na ilifika katika fainali za Lihgi ya Ulaya , Villareal ilichukua kombe hilo.

  12. Je Zimbabwe inaweza kuzuia uvaaji wa sketi fupi?

    Wanawake

    Chanzo cha picha, AFP

    Chama tawala nchini Zimbabwe kimekanusha ripotikwamba kimepanga kuwazuia wanawake uvaaji wa sketi fupi (vimini) kwa wanawake na wasichana pamoja na suruali katka maeneo ya umma.

    Msemaji wa taifa wa Zanu-PF Simon Khaya Moyo katika taarifa yake alielezea ripoti hizo kama taarifa gushi.

    Hii inafuatia ripoti kuwa chama hicho kilikuwa kinapanga kuanzisha sheria ambayo itazuia wanawake wa miaka 16 na zaidi kuvaa suruali na sketi fupi.

    "Zanu-PF imekataa taarifa hizo na zilizoenea mitandaoni, ikisema kuwa chama hicho kinapania kuzuia uvaaji wa sketi fupi na suruali ," ilisema taarifa

    Chama hicho kinalishutumu shirika lisilo la kiserikali lenye ushirika la chama cha upinzani cha MDC kwa kueneza tetesi hizo.

    Bw Moyo amesema kwamba mapambano ya ukombozi wa Zimbabwe yalifanywa na wote wanaume na wanawake na chama kifikia "hatua kubwa " kuendeleza haki za wamawake kwa njianjingi.

    " Kwa hiyo ni ujinga sana kwamba chama kikubwa ambacho kilijengwa kupitia muungano wa wanawake kinaweza kutoa muongozo wa aina hiyo wa mavazi ," ilisema ytaarifa hiyo.

  13. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Jumatatu tarehe 19.07.2021