Rais Samia: Nimekuja Kenya kunyoosha palipopinda

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania ameliambia Bunge la Kenya kuwa ziara yake nchini Kenya imelenga kukazia maeneo ambayo yalilegalega katika uhusiano wa nchi hizo mbili.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya moja kwa moja. Kwaheri.

  2. Marufuku dhidi ya Trump kutotumia Facebook yaendelezwa

    Donald Trump

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Bodi ya usimamizi ya mtandao wa Faceboook imeendeleza marufuku aliyowekewa aliyekuwa Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya kutumia mtandao wa Facebook na Instagram.

    Lakini ilikosoa marufuku hiyo iliyowekwa kuwa ya kudumu na kusema kwamba ilizidi adhabu za kawaida zinazotolewa na mtandao huo.

    Hivyobasi, imeagiza uamuzi huo kupitiwa tena na "kuchukua hatua stahiki" ambayo inatumika kwa kila mmoja ikiwemo watu wa kawaida.

    Donald Trump alipigwa marufuku na kutumia mitandao ya Facebook na Instagram mnamo mwezi Januari baada ya bunge la Marekani kuvamiwa.

    Bodi ya mtandao huo imesema uamuzi wa awali wa kumpiga Bwana Trump marufuku ya kutotumia mtandao huo kabisa "haukuwa na kipimo", na kwamba uamuzi stahiki unastahili kuwa "wenye kwendana na sheria ambazo zinatumika kwa kila mtumiaji wa jukwa hilo la mawasiliano".

    Aidha, bodi hiyo imetaka mtandao wa Facebook kuchukua hatua kwa kuzingatia ushauri wake ndani ya miezi sita.

  3. Mfahamu Melinda Gates ni nani?

    Maelezo ya video, Mfahamu Melinda Gates mtalaka wa Bill Gates ni nani
  4. Rais Samia: Nimekuja Kenya kunyoosha palipopinda

    Rais Samia

    Chanzo cha picha, IKULU KENYA

    Maelezo ya picha, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

    Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania ameliambia Bunge la Kenya kuwa ziara yake nchini Kenya imelenga kukazia maeneo ambayo yalilegalega katika uhusiano wa nchi hizo mbili.

    Bi Samia ameuambia mkutano maalumu wa pamoja wa bunge la seneti na bunge la kitaifa nchini Kenya ustawi wa mataifa hayo mawili unaathiri ustawi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa pamoja.

    "Kila mara panapotokea kutoelewana kati yetu tunadhoofisha uhusiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, bila kukusudia pia tunaathiri utangamano wa Afrika Mashariki, hivyo hatuna budi kuendelea kuelewana."

    Rais Samia amesema kuwa kuna kipindi jumuiya hiyo ilijaribiwa kufuatia, maneno na vitendo ambavyo vilipima uimara wa dhamira za nchi wananchama wa jumuiya hiyo kuendelea na safari ya utangamano.

    "Niwahakikishie, mimi na wenzangu nchini Tanzania tutahakikisha kuwa uhusiano wetu unang'ara na kwa kufanya hivyo tung'arishe uhusiano wa Afrika Mashariki. Tanzania itaendelea kuwa jirani na mbia mwaminifu wa Kenya na mwanachama muadilifu wa Afrika Mashariki," amesisitiza Rais Samia.

    • Ziara ya rais Samia Suluhu: 'Tanzania Iko tayari kwa wawekezaji kutoka Kenya '
    • Samia Suluhu Hassan: Rais mpya anayekabiliana na dhana ya kutokuwepo kwa corona Tanzania
  5. 'Lazima tushirikiane na Kenya kwenye vita dhidi ya corona'

    Rais Samia

    Chanzo cha picha, IKULU Kenya

    Rais Samia Suluhu Hassan ameliambia Bunge la Kenya kuwa Tanzania itashirikiana na nchi jirani ikiwemo Kenya katika mapambano dhidi ya mlipuko wa corona.

    Rais Samia amewaambia wabunge na maseneta wa Kenya kuwa tayari Tanzania imeshaanza kuchukua hatua tahadhari juu ya corona ikiwemo kusitisha safari za moja kwa moja na nchi zenye kasi ya maambukizo ya corona.

    Akihutubia mkutano maalumu ulioandaliwa kwa ajili yake, amesisitiza kuwa Tanzania si kisiwa katika mapambano dhidi ya corona, na wakati ikisubiriwa mapendekezo kutoka kamati maalumu aliyoiunda, kitu ambacho ana hakika nacho ni lazima kushirikiano na majirani.

    "Lazima tushirikiane na majirani katika vita dhidi ya corona, lazima tushirikiane na kenya katika hili," amesema Rais Samia.

    • Ziara ya rais Samia Suluhu: 'Tanzania Iko tayari kwa wawekezaji kutoka Kenya '
    • Samia Suluhu Hassan: Rais mpya anayekabiliana na dhana ya kutokuwepo kwa corona Tanzania
  6. Rais Samia alihutubia Bunge la Kenya

    Rais Samia Bungeni

    Chanzo cha picha, IKULU Kenya

    Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amehutubia kikao cha pamoja cha Bunge la taifa na Bunge la Seneti nchini Kenya.

    Rais Samia amekuwa nchini Kenya kwa ziara ya siku mbili ya kikazi.

    Ziara yake ni muendelezo wa jitihada za nchi hizo mbili kuboresha na kuendeleza uhusiano wa muda mrefu.

    Bunge la Kenya

    Chanzo cha picha, IKULU KENYA

    Soma zaidi:

    • Ziara ya rais Samia Suluhu: 'Tanzania Iko tayari kwa wawekezaji kutoka Kenya '
    • Samia Suluhu Hassan: Rais mpya anayekabiliana na dhana ya kutokuwepo kwa corona Tanzania
  7. Kenyatta: Mahindi yaliyokwama mpakani yaruhusiwa kuingia nchini

    Rais Kenyatta

    Chanzo cha picha, Ikulu ya Rais Kenya

    Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amemuagiza waziri wake biashara kuondoa msongamano wa bidhaa katika mpaka ya Kenya na Tanzania.

    Bw. Kenyatta ametoa muda wa wiki mbili mahindi yote yaliyokwama mpakani kuruhusiwa kuingia nchini.

    ''Hiyo mahindi imelala hapo mpakani,Waziri mimi nakupatia wiki mbili…yote ifunguliwe na hiyo maneno iishe'' alisema.

    Kenyata ametoa tamko hilo leo mbele ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakati wa kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya linaloendelea jijini Nairobi.

    Mlolongo mrefu wa malori ya kubeba mizigo

    Chanzo cha picha, NTV

    Maelezo ya picha, Mlolongo mrefu wa malori ya kubeba mizigo

    Mapema mwezi Machi Kenya ilipiga marufuku ununuzi wa mahindi kutoka mataifa jirani ya Tanzania na Uganda.

    Uamuzi huo ulifikiwa baada ya uchunguzi kubaini kwamba mahindi kutoka mataifa hayo mawili sio salama kwa matumizi ya chakula cha binadamu.

    • Kenya yapiga marufuku ununuzi wa mahindi kutoka Tanzania na Uganda
    • Tanzania yatoa ufafanuzi kuhusu mahindi yake kupigwa marufuku Kenya
  8. Ujumbe wa India katika mkutano wa G7 London wapatikana na Corona

    India's foreign minister, right, met with the US delegation and the UK home secretary on Tuesday

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Waziri wa mambo ya nje India,kulia alikutana ujumbe wa Marekani na Waziri wa Mambo ya ndani wa Uingereza Jumanne

    Ujumbe wa India unaohudhuria mkutano wa G7 jijini London wamepatikana na virusi ya Corona.

    Waziri wa Mambo ya nje wa India Subramanyan Jaishankar Katika mtandao wa twitter amethibitisha kwamba Wajumbe hao sasa wamejitenga na watahudhuria mkutano huo kupitia mtandao.

    Afisa wa serikali ya Uingereza alisema washiriki wawili walipimwa na kupatikana na Corona baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kila siku katika mkutano huo.

    Mkutano huo wa mataifa ya G-7 unaingia siku yake ya mwisho huku mawaziri wa Mambo ya nje wa mataifa hayo wakijadili usambazaji wa chanjo ya corona ulimwenguni.

    Shirika la Afya Duniani WHO lilikuwa limehimiza mataifa yalioendelea kusaidia nchi masikini kupata chanjo hizo.

  9. Uwanja wa ndege wa Indonesia warejelea matumizi ya vijiti vya kupima corona

    Raia wa Indonesia

    Chanzo cha picha, EPA

    Kampuni ya dawa ya serikali nchini Indonesia imeshtakiwa kwa kuosha vijiti vya pamba vya kupima Corona puani.

    Takriban abiria 9,000 katika uwanja wa ndege wa Kualanamu nchini Indonesia huenda wamepimwa Corona na vijiti vya pamba vilivyotumiwa kwa abiria wengine.

    Polisi wamewakamata wafanyakazi wa kampuni ya dawa inayoshtakiwa kwa kuosha vifaa hivyo vya kupima Covid.

    Kampuni hiyo inayomilikiwa na serikali Kimia Farma sasa inakabiliwa na kesi itakayofunguliwa kwa niaba ya wasafiri.

    Mwenendo wa kupima biria puani umekuwa kama kawaida katika nchi nyingi zilizoathiriwa na janga la Corona.

    Polisi wanaamini ulaghai huo ulianza tangu ,mwezi Disemba 2020 katika uwanja wa ndege wa Kualanamu huko Medan, Sumatra Kaskazini.

    Abiria wanahitajika kupimwa kabla kusafiri. Mamlaka ya uwanja wa ndege zimekuwa zikitumia vifaa vya vipimo vya Covid-19 vilivyosambazwa na kampuni ya serikali ya Kimia Farma.

  10. Kenya yachunguza kisa cha 'mtoto aliyefariki' polisi wakitekeleza amri ya kutotoka nje

    Police have put up roadblocks nationwide to enforce a curfew introduced to reduce coronavirus infections

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Polisi wameweka vizuizi barabarani kote nchini kutekeleza amri ya kutotoka nje

    Mamlaka ya kutathmini utendakazi wa polisi nchini Kenya (IPOA), imeanza kuchunguza ripoti kwamba mtoto alifariki baada ya maafisa waliokuwa wakitekeleza amri ya kutotoka nje nyakati za usiku kama hatua ya kuzuia kuenezwa kwa virusi vya corona kukataa kufungulia gari lililokuwa likimpeleka hospitali.

    Mtoto huyo wa miezi minne aliyekuwa na tatizo la kupumua alikuwa akikimbizwa hospitali jumamosi iliyopita, babu yake aliambia gazeti la Nation.

    Madaktari walisema mtoto huyo alihitaji kupelekwa katika hospitali ya rufaa iliyokuwa umbali wa kilomita 25.

    Lakini maafisa waliokuwa katika kizuizi cha barabarani wanadaiwa kukataa kuwafungulia njia kwa sababu ya utekelezaji amri ya kutotoka nje iliyowekwa kuzuia maambukizi ya Covid 19.

    "Isingekuwa kizuizi hicho cha barabarani, maisha ya mjukuu wangu yangeweza kuokolewa," babu ya mtoto huyo, alisema kwenye video iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Nation.

    Kenya imeweka amri ya kutotoka nje kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri ili kuzuia kuongezeka kwa maambukizo ya virusi vya corona.

    Polisi haijajibu ombi la BBC la kupata kauli yao kuhusiana na suala hiyo.

    Mwezi uliopita, maelfu ya waendeshaji magari na abiria walikwama kwa masaa kadhaa katika trafiki katika mji mkuu, Nairobi, baada ya polisi kufunga barabara kuu jijini.

    Mamlaka zikosolewa sana lakini wanasisitiza kwamba utekelezaji mkali wa amri ya kutotoka nje ni muhimu kushughulikia kuongezeka kwa maambukizo.

  11. Muigizaji Will Smith akiri kuwa na 'muonekano mbaya zaidi'

    Will Smith

    Chanzo cha picha, AFP/GETTY

    Mwigizaji wa Marekani Will Smith amekiri kuwa na "muonekano mbaya zaidi" katika maisha yake baada ya kuweka picha yake akiwa bila shati katika mtandao wa Instagram.

    Will Smith, 52, anaonekana katika picha hiyo akiwa ameinua mikono kuashiria hajaridhishwa na jinsi alivyoongeza uzani wa mwili.

    Katika ujumbe alioandikia mashabiki wake milioni 53, Will alisema: "Naomba niwe muwazi kwenu nyote – muonekano wangu wa sasa ni mbaya zaidi katika maisha yangu."

    Ruka Instagram ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa Instagram ujumbe

    Baadhi yaa mashabiki wake walimpongeza kwa kuwa mjasiri kwani ni hatua moja ya kujikubali na kushughulikia changamoto inayomkabili.

    Muigizaji huyo aliyewahi kupunguza na kuongeza uzani wake wa mwili ili kuigiza katika vipindi tofauti ikiweo ile ya ‘Will Smith’-The Fresh Prince of Bel-Air iliyopata umaarufu mkubwa miaka ya 1990.

  12. Mwanamke ajifungua watoto tisa Mali

    Watoto

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mwanamke mmoja nchini Mali amejifungua watoto tisa katika hali ambayo sio ya kawaida.

    Halima Cisse, 25, alijifungua watoto wa kike watano na wavulana wanne katika hospitali ya Morocco siku ya Jumanne ambako alikuwa amelazwa, Waziri wa Mali Fanta Siby alisema katika taarifa. Alijifungua kupitia njia ya upasuaji.

    Bi Cisse amekuwa akitarajia kijifungua watoto saba kulingana na uchunguzi wa skani ya tumbo aliyofanyiwa nchini Mali na Morocco lakini skani hiyo haikugundua amebeba watoto wengine wawili.

    Siku ya Jumanne, Dkt Siby alisema watoto hao na mama yao “wanaendelea vyema”. Wanatarajiwa kurejea nyumbani wiki chache zijazo.

    Aliwapongeza madaktari waliomhudumia Mali na Morocco, “ambao ujuzi wao ni chanzo cha matokeo mema ya ujauzito huu".

    Mimba ya Bi Cisse imeshangaza taifa hilo la Afrika Magharibi na imewavutia baadhi ya wakuu wa nchi hiyo – huku baadhi yao wakisafiri had Morocco alipohitaji utunzi wa kitaalamu, shirika la habari la Reuters liliripoti.

    Msemaji wa wizara ya afya ya Morocco, Rachid Koudhari, ameliambia shirika la habari ya AFP kwamba hakujua uzazi wa aina hiyo hutokea nchini humo.

  13. Hujambo na karibu katika matangazo mubashara leo Jumatano 05.05.2021.