Rais Samia kukutana na viongozi wa kisiasa Tanzania
Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan analihutubia Bunge kwa mara ya kwanza toka alipoingia madarakani mwezi mmoja uliopita.
Moja kwa moja
Rais Samia: Tukosoeni vikali
Rais Samia ametumia hotuba yake bungeni hii leo kuwaalika wabunge kuikosoa serikali yake, na hata ikibidi wafanye hivyo kwa ukali alimradi watumie "lugha za kibunge."
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Rais Samia awaonya 'wezi na wachonganishi wa mtandaoni'
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametumia hotuba yake ya bunge kutuma kile alichokiita ni onyo kwa watu wanaofanya umadhirifu wa mali za umma na "kufanya uchonganishi kupitia mitandao ya kijamii".
Kwa mujibu wa Rais Samia, mara baada ya kifo cha rais Magufuli mwezi mmoja uliopita. Tayari kuna viongozi wa umma pamoja na mashirika ambayo yameanza kulegalega.
"Niwaonye wale wote wanaosimamia mali za umma, ukwepaji kodi, ubadhirifu, kukemea uzembe na uvivu kuwa yameondoka kutokana na kuondoka kwa Hayati Magufuli, amekwenda peke yake, lakini maoni na mikakati tunaifanyia kazi."
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Rais Samia pia ameonya juu ya uchochezi aliosema kuwa unafanyika mtandaoni juu ya kifo cha hayati Magufuli. Akisema kama kuna mtu yeyote mwenye taarifa kinyume cha ripoti ya madaktari basi azipeleke kwenye mamlaka husika na si kuchochea uhasama mtandaoni.
"Taarifa tuliyopewa juu ya kifo cha mpendwa wetu ni udhaifu wa moyo ambao ameishi nayo kwa zaidi ya miaka kumi. Kuna watu huko mitandaoni wanasema, fulani na fulani wamempa sumu. Kama wana taarifa waje tuwasikilize na taarifa zao," ameeleza rais Samia.
Rais Samia: Nakusudia kukutana na viongozi wa kisiasa
Rais Samia ameliambia Bunge kuwa anapanga kukutana na viongozi wa kisiasa "ili kwa pamoja tuweke msimamo wa kuendesha shughuli za kisiasa."
Kiongozi huyo amesema hayo wakati akitaja namna anavyopanga kuboresha mazingira ya uhuru na demokrasia nchini Tanzania.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Rais Samia: Tutaendelea kuilea ATCL kimkakati

Chanzo cha picha, IKULU, TANZANIA
Rais Samia amesema kuwa serikali yake itaendelea kulilea shirika la nchi hiyo kimkakati ikiwemu kulitua mzigo wa madeni
Kiongozi huyo amesema ATCL limerithi madeni na hivyo kwa sasa linaonekana kuwa halina thamani na kutengeneza hasara.
"Hatutakubali liendelee kutengeneza hasara baada ya uwekezaji mkubwa uliofanyika...Tunaenda kulifanyia uchambuzi yakinifu na tutawaweka watua ambao wataliongoza ili kutengeneza faida."
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Rais Samia pia amesisitiza kuwa serikali inatambua kuwa biashara ya usafiri wa ndege ni ngumu na inajitahidi kuepuka yote ambayo yhayana tija kwa shirika.
Rais Samia: Tumelalamikiwa sana kuhusu mazingira ya uwekezaji
Rais Samia ameliambia bunge kuwa serikali yake itafanya mabadiliko ya kisera na sheria ili kuwavutia wawekezaji zaidi nchini humo.
Amesema kwa kuwa kumekuwa na malalamiko juu ya urasimu, na kutokutabirika kwa sera za uwekezaji, eneo hilo litawekewa kipaumbele ili kutoa tija kwa uchumi wa taifa hilo.
Kwa mujibu wa Rais Samia, athari za mlipuko wa virusi vya corona umefanya ukuaji wa uchumi wa taifa hilo kuanguka kutoka wastani wa asilimia 6.9 mwaka jana mpaka asilimia 4.7 mwaka huu.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
“Ningependa kuona wafanya biashara wawekezaji na wananchi wanalipa kodi bila shuruti wala matumizi ya nguvu.”
Rais Samia: Mimi na hayati Magufuli tulikuwa kitu kimoja
Rais Samia amesema kuwa lengo kuu la serikali yake ni kuendeleza na kuboresha mambo yote mazuri yaliyofanyika na watangulizi wake.
Kiongozi huyo pia ameliambia Bunge kuwa mabadiliko yatafanyika katika baadhi ya maeneo ili kuongeza ufanisi wa kiutendaji.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
"Ndio maana kauli mbiu yetu ni 'Kazi Iendelee'."
Rais Samia amesisitiza kuwa serikali yake itaendeleza mipango na dira ya maendeleo ambayo iliandaliwa na utawala uliopita kwa kuzingatia ilani ya ya uchaguzi ya chama tawala CCM.
"Nilishiriki kikamilifu katika mipango hiyo, ndio maana nikasema mimi na hayati Magufuli tulikuwa kitu kimoja."
Wabunge wamuomboleza Magufuli kwa dakika moja
Rais Samia ameongoza wabunge na wageni mbalimbali kumkumbuka rais wa Tanzania aliyefariki mwezi uliopita kwa kusimama kwa dakika moja.
Mama Samia ameeleza kuwa kufariki kwa Rais Magufuli kulikuwa ni kipindi kigumu zaidi katika historia ya uongozi wa Tanzania.
"...Tunathamini mchango wake kwa Tanzania. Mapenzi ya wananchi kwa Magufuli tuliyaona wakati wa mazishi...alikuwa kiongozi bora na shupavu..."
'Nasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania'
Rais Samia ameanza hotuba yake kwa salamu yake ya kipekee: "Nasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."
Salamu hiyo aliitoa kwa mara ya kwanza katika hotuba zake za awali mwezi uliopita.
Viongozi mbali mbali wapo bungeni kumsikiliza Rais Samia
Viongozi mbalimbali wa serikali na wastaafu nchin Tanzania wapo katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kusikiliza hotuba ya kwanza ya Rais Samia Suluhu Hassan jioni hii.
Awali bunge lilibali kanuni zake ili kuruhusu viongozi hao kuingia ukumbini humo. Viongozi waliohudhuria ni pamoja na Makamu wa Rais Philip Mpango, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji Mkuu wa Zanzibar pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
Viongozi wastaafu waliopo bungeni ni Rais wa pili wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, Rais wa nne Jakaya Kikwete na Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume.
Rais Samia awasili viwanja vya Bunge

Chanzo cha picha, MKURUGENZI WA MAWASILIANO AFISI YA RAIS TANZANIA
Maelezo ya picha, Itakua ni mara yake ya kwanza kwa Rais Suluhu kulihutubia Bunge toka alipochukua hatamu ya uongozi wa nchi Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan amewasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma tayari kwa kuuhutubia mhimili huo.
Hii itakuwa ni mara yake ya kwanza kwa kiongozi huyo kulihutubia Bunge toka alipochukua hatamu ya uongozi wa nchi hiyo mwezi uliopita kufuatia kifo cha mtangulizi wake Rais John Magufuli mwezi mmoja uliopita.
Mara baada ya kuwasili, Rais Samia alipokelewa kwa heshima za kijeshi na kukagua gwaride maalumu la polisi liloandaliwa kwa ajili yake.
Hotuba yake leo inatarajiwa kuainisha vipaumbele vyake na mwelekeo wa Tanzania katika kipindi cha uongozi wake wa awamu ya sita mpaka mwaka 2025.
Unaweza pia kusoma :
Corona Kenya: Maeneo ya kuchoma miili ya wafu ‘yaishiwa na kuni’ Kenya

Maeneo ya kuhifadhi miili ya watu waliokufa kwa njia ya kuichoma katika jiji kuu la Kenya Nairobi yanakabiliwa na upungufu wa kuni kwasababu ya wingi wa vifo vinavyotokana na Covid-19, limeripotui gazeti la The Star.
Kituo cha kuchoma miili cha Kariokor jijini Nairobi ambacho huchoma miili ya wafu wenye asili ya Asia kinaomba msaada wa haraka wa kuni zilizokauka ili kuwachoma wafu, limeripoti gazeti hilo.
"Wiki iliyopita, tuliwaombawatu wote wa jamiii ya Asia la kutoa msaada wa wa kuni kwasababu kituo chetu cha kuchoma miili ya wafu kimeishiwa na kuni ," mmoja wa watu wa jamii hiyo alinukuliwa akisema.

Wahudumu wa maiti katika kituo hicho waliliambia gazeti hilo kwamba uhaba wa maeneo ya kuchoma miili umekuwepo kwa wiki mbili hadi tatu.
Katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita Kenya imeshuhudia ongezerko la juu la vifo, huku ikikabiliwa na wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona.
Nchi hiyo kwa sasa imethibitisha maambukizi ya watu53,000 na vifo 2,540 tangu mlipuko wa Covid-19 ulipoanza.
Unaweza pia kusoma:
- Umefika wakati mwili wa binadamu uteketezwe badala ya kuzikwa kaburini?
Majambazi waliokuwa kwenye pikipiki wawauwa watu zaidi ya 50 Nigeria

Chanzo cha picha, AFC
Taarifa kutoka kaskazini magharibi mwa Nigeria zinasema kuwa majambazi waliokuwa wakiendesha pikipiki wamewauwa zaidi ya watu hamsini katika msururu wa uvamizi uliodumu kwa saa kadhaa katika vijiji vya mbali.
Wakazi wa Magami waliiambia BBC kwamba watu wenye silaha kwanza walishambulia kijiji cha ‘Yar-Doka Jumatano wakati walinzi wa kijiji kutoka vijiji jirani walipoingilia kati kusaidia, washambuliaji walizidisha mashambuliokatika maeneo mengine ya vijiji.
Baadhi ya wakazi wanasema walihesabu miili ya watu walau 51 na watu wengine zaidi hawajulikani walipo.
Majeruhi wanatibiwa katika hospitali iliyopo katika Magami uliopo karibu. Msemaji wa polisi katika jimbo la Zamfara, Muhammad Shehu amethibitisha mashambulio hayo katika mazungumzo na BBC lakini hakuweza kutoa idadiyoyote ya majeruhi.
Alisema kikosi cha usalama na maafisa wa serikali walikuwa njiani kuelekea katika eneo la tukio kutathmini hali.
Baadhi ya waathiriwa wanasemekana kuwa watu ambao walikuwa wamesambaratishwa na mashambulio ya awali ambao sasa walikuwa wanarejea nyumbani – wakitumai kuandaa mashamba yao kwa ajili ya msimu wa mvua unaoanza.
Jimbo hilo limekuwa likihangaika na harakati za magenge ambayo yamekua yakiendesha mashambulio hivi karibuni- na kufanya uvamizi mbaya na utekaji nyara kwa ajili ya kikombozi.
Mauaji katika jimbo la Zamfara yalitolewa chini ya saa 24 baada ya kikundi kingine kuvamia chuo kiku katika jimbo jirani la kaduna na kumpiga risasi hadi kumuua mfanyakazi na kuwateka nyara watu wanafunzi.
Mfanyakazi wa hospitali ya Italia anayeshtumiwa kutoripoti kazini kwa miaka 15

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mwanaume huyo alikuwa ameajiriwa kama mfanyakazi wa umma katika hospitali mjini ya Calabria, Italia Mfanyakazi wa hospitali nchini Italia ameshutumiwa kwa kuacha kazi ingawaje ameendelea kupokea malipo kamili kwa miaka 15, ripoti vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.
Mwanamume huyo anadaiwa kuacha kuripoti kazi katika hospitali ya Ciaccio kusini mwa jiji la Catanzaro mnamo 2005.
Sasa anachunguzwa kwa ulaghai, wizi na utumizi mbaya wa ofisi, shirika la habari la habari la Italia Ansa limeripoti.
Inasemekana alilipwa € 538,000 (Pauni 464,000) kwa jumla kwa miaka ambayo hakuwa akifanya kazi.
Mameneja sita katika hospitali hiyo pia wanachunguzwa kuhusiana na tukio hilo.
Kukamatwa kwake ni matokeo ya uchunguzi wa muda mrefu wa polisi juu kuhusu tabia ya watu kukwepa kufanya kazi na udanganyifu katika sekta ya umma ya Italia.
Mfanyakazi huyo alikuwa mtumishi wa serikali, na alipewa kazi katika hospitali mnamo 2005.
Ilikuwani wakati huo ambapo aliacha kwenda kazini, polisi walisema. Polisi pia wamemtuhumu kwa kumtishia meneja wake kumzuia kumchukulia hatua za kinidhamu Meneja huyo baadaye alistaafu,
polisi iliongeza, na kutokuwepo kwake hakukugunduliwa kamwe na aliyechukua nafasi yake au idara ya kusimamia wafanyikazi
Mawakili wa Zuma wajiondoa katika uwakilishi wake kabla ya kesi ya ufisadi kuanza

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Bwana Zuma anakana mashiotaka yote dhidi yake Mawakili wa rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma wamewasilisha waraka wa kujiondoa katika uwakilishi wake.
Mawakili hao hawakutoa sababu ya kufanya hivyo.
Waraka huo uliwasilishwa Jumatano kufuatia hukumu ya wiki iliyopita ambapo rais huyo wa zamani alishindwa katika kesi ya rufaa dhidi ya azma ya taifa ya kutaka kupata pesa ambazo lilimgarimia kisheria Bw Zuma.
Hii inakuja kabla ya kuanza kwa kesi ya ufisadi inayotarajiwa kuanza tarehe 17 Mei.
Bw Zuma anakabiliwa na mashitaka 16 juu ya dola bilioni $2 (£1.4bn) za mkataba wa taifa wa silaha, ikiwa ni pamoja na wizi, utakatishaji wa pesa - mashitaka ambayo anayakana.
Majeshi ya Kenya kujiunga na kikosi cha Monusco nchini DRC

Chanzo cha picha, State House Kenya/Twitter
Wanajeshi wa Kenya watajiunga na Kikosi cha FIB(Force Intervention Brigade) Mashariki mwa DRC ili kulisadia jeshi la nchi hiyo kukabiliana na makundi ya waasi mashariki mwa nchi hiyo.
Hilo limetangazwa na rais wa DRC Felix Tshisekedi katika makubaliano ya ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili . Rais Uhuru Kenyatta yupo nchini DRC kwa ziara ya siku tatu ambayo imefanikisha mikataba katika sekta za kibiashara ,usalama na miundo mbinu .
Sekta za uchumi zinazolengwa na mfumo mpana ni kilimo, elimu, afya, michezo na utalii. Nyingine ni mazingira, biashara za ndogo na za kadri, makazi, nishati na maendeleo ya miundombinu.
Imetiwa saini pia mikataba miwili baina ya nchi hizo juu ya usalama na ulinzi ambayo hutoa mifumo ya ushirikiano kati ya Kenya na DR Congo katika maeneo kama vile ugaidi, uhamiaji, usalama wa mtandao, na forodha na udhibiti wa mipaka.
Makubaliano yaliyofufuliwa juu ya usafirishaji wa baharini yanalenga kuiweka tena bandari ya Mombasa kama lango kuu la kuingia DR Congo kwa kurahisisha usafirishaji wa bidhaa hadi nchini humo .
Baraza la Muungano wa Afrika kuhusu usalama kukutana kujadili mizozo ya Chad na Somalia

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Kuna hofu kwamba kifo cha rais wa Chad Idriss Déby kinaweza kuyumbisha uthabiti wa kisiasa katika kanda hiyo Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika linakutana Alhamisi kujadili mizozo ya kisiasa nchini Chad na Somalia.
Katika taarifa fupi, msemaji wa mwenyekiti wa AU Ebba Kalondo alisema mkutano huo unaambatana na agizo la baraza hilo kama chombo kinachosimamia maamuzi kwa kuzuia, usimamizi na utatuzi wa mizozo na hali za mgogoro barani.
Hii inakuja siku moja tu baada ya wanasiasa wa upinzani nchini Chad kukataa uteuzi wa jeshi la nchi hiyo wa mtoto wa Rais Idriss Déby kuchukua wadhifa wa urais baada ya kifo chake.
Bwana Déby, 68 - ambaye alikuwa mamlakani kwa miongo mitatu - alifariki baada ya kupigwa risasi wakati akipambana na waasi kwenye mstari wa mbele vitani .
Chad ni nchi muhimu kwa juhudi za kimataifa za kupambana na wanamgambo wa Kiislamu barani Afrika.
Wakati huo huo, Somalia pia inakabiliwa na mgogoro wa kikatiba baada ya uchaguzi kukosa kufanyika na bunge kumpa muda wa miaka miwili zaidi rais Mohamed Abdullahi Farmajo.
Unaweza pia kusoma:
- Idriss Deby: Upinzani walaani mapinduzi ya ‘kifamilia’ Chad
- Idriss Deby: Mfahamu Jenerali Mahamat Kaka mtoto wa Déby aliyerithi madaraka ya Chad
- LiIdriss Déby: Mwisho wa Rais na jenerali mpambanaji wa Chad
Wakazi wa maeneo ya mwa mwambao wa Tanzania watahadharishwa kufuatia Kimbunga jobo

Kimbunga hafifu kimefika karibu namaeneo ya mwambao wa bahari ya Hindi nchini Tanzania jana kufuatia kujitokeza kwa mgandamizo wa hewa katika maeneo hayo.
Kulingana na mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania Kimbunga hicho kinatarajiwa kusababisha ongezeko la upepo hususan katika maeneo ya mwambao wa pwani ya kusini, maeneo ya Lindi na Mtwara .
Samwel Mbuya Meneja wa Kituo kikuu cha utabiri Mamlaka kuu ya hali ya hewa Tanzania amesema kimbunga hicho kipo umbali wa takriban kilomita 930 kutoka pwani ya Lindi na takriban kilomita 1030 pwani ya Mtwara.
Mamlaka ya hali ya hewa nchini imewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kuzingatia mwelekeo wa upepo na mawimbi ya bahari katika maeneo husika. Kimbunga hicho pia kilisafiri kwa kasi ya mwendo wa Kilomita 1,022 kaskazini mwa mji mkuu wa Madagascar Antananarivo.
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo tarehe 22.04.2021
