Magufuli : 'Hatuchukii wanaotupa changamoto na kutukosoa kwa staha'

Rais wa Tanzania John Magufuli amesema ''yako mambo ya ajabu yanatokea kwenye baadhi ya mataifa na kamwe huwezi kuyaona kwenye vyombo vya habari''.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena kesho

  2. Vikosi vya usalam Uganda vyaizingira nyumba ya Bobi Wine

    Bobi Wine

    Vikosi vya usalama vya jeshi la UPDF na polisi wamezingira nyumba ya aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais kupitia chama cha NUP Robert Kyagulanyi maarufu Bobi wine nyumbani kwake Magere wilayani Wakiso yapata kilomita 10 kutoka mjini Kampala.

    Taarifa zinasema maafisa wa Mamlaka ya mapato URA nchini Uganda wanataka kuchukua gari lake lisilopitwa risasi yaani Bullet Proof Toyota Land Crusel rangi nyeusi, ambalo tayari lina namba ya usajiri ya Uganda.

    Maafisa hao wanajiuliza jinsi lilivyoingia na kupewa nambari hiyo bila kuidhinishwa na mamlaka za ulinzi.

    Siku ya Jumatatu Bobi Wine alilionesha gari hilo kwa umma katika mkutano wa wandishi habari akisema kuwa alinunuliwa na wafuasi wake walioko Ughaibuni katika mkutano uliofanyika ofisi za chama cha NUP Kamokya kitongoji cha jii la Kampala.

    Pia kuna taarifa za kusimamishwa kwa baaadhi ya maafisa wa URA waliosajili gari la Bobi Wine akiwemo Kamishnina msaidizi Jane Akello ambaye amepewa likizo ili kuruhusu uchunguzi zaidi ufanyike.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Msemaji wa URA Ian Rumanyika amevifahamisha vyombo vya habari kwamba hakuna afisa aliyesimamishwa ila uchunguzi unaendelea kuhusiana na gari hilo la Robert Kyagulanyi na hawezi kutoa maelezo zaidi ya hayo hadi watakapokamilisha uchunguzi wao.

    Hii sio mara ya kwanza vikosi vya usalama kuzingira makazi yaBobi Wine.

    Mwezi uliopita baada yaBobi Wine kupiga kura katika uchaguzi wa mkuu wa tarehe 14 Januari, vikosi vya usalama vilizunguka nyumbani kwake na kumzia kutoka nyumbani yeye na mkewe karibu majuma mawili, hadi mawakili wake walipopeleka ombi katika mahakama kuu kuondoa vikosi hivyo kwa Bw Kyagulanyi.

    Mahakamu aliviagiza vikosi vya jeshi la UPDF na polisi kuondoka kwake na kumuachilia huru ndipo vilipoondoka.

    Tukio hili limetokea baada ya Kyagulanyi jana kupeleka ombi katika mahakama ya juu akitaka iondoe kesi ambapo alikuwa ameishitaki kupinga ushindi wa Rais Museveni katika uchaguzi mkuu wa mwezi uliopita.

    Kyagulanyi anadai hana Imani na majaji 3 kati ya majaji tisa wanaoongoza kesi yake akiwemo Jaji mkuu Alfonse Owiny Dollo.

  3. 'Hatuchukii wanaotupa changamoto na kutukosoa kwa staha',

    Rais John Magufuli

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Rais wa Tanzania John Magufuli

    Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, amesema serikali yake haiogopi kupewa changamoto wala kukosolewa kama kukoselewa kwa staha.

    Akizindua studio za vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Magufuli amesema katika kipindi cha miaka mitano serikali yake imeruhusu vyombo vingi zaidi vya habari kuliko wakati mwingine wowote tangu taifa hilo lipate uhuru.

    Amesema mwaka 2015, Tanzania ilikuwa na vituo vya radio 106 na televisheni 25 lakini hadi kufikia mwezi februari 2021 kuna jumla ya vituo vya redio 193, televisheni 46, magazeti 247,televisheni za mtandao 443 na redio za mtandao 23.

    Licha ongezeko hilo Rais Magufuli, amewataka waandishi wa habari kuweka mbele uzalendo na maslahi ya taifa kwanza na kufanya kazi kwa kuzingatia haki hasa kwa yule ambaye habari inamhusu.

    Pia ameongeza kumekuwa na habari nyingi za uzushi nyingine zikizushia watu vifo wakiwemo viongozi na watu mashuhuri.

    ''Yako mambo ya ajabu yanatokea kwenye baadhi ya mataifa na kamwe huwezi kuyaona kwenye vyombo vya habari. Sasa sisi tumekuwa wepesi kwa sababu ya uhuru huu kila kitu hata kile ambacho hakifai kina andikwa'' alisema Bw. Magufuli.

    Aidha Rais Magufuli amewataka watendaji wa serikali kuwa wepesi kwenye kutoa taarifa kwasababu ziko baadhi ya Wizara na Taasisi za umma ambako waandishi wakienda kufuata taarifa habari zinafichwa bila sababu ya msingi.

    Rais Magufuli amekuwa akilaumiwa kwa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari.

    Pia unaweza kusoma:

    • Rais Magufuli asema 'Hatujazuia matumizi ya barakoa'
    • Ubalozi wa Marekani wawaonya watu wanaotaka kusafiri nchini Tanzania
    • Je ni akina nani wamefariki Tanzania mfululizo kwa kipindi kifupi na kwa sababu zipi?
  4. Marekani haina haki ya 'kuisomea' Uganda kuhusu uchaguzi

    President Yoweri Museveni took power in 1986

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Rais Yoweri Museveni aliingia madarakani mwaka 1986

    Marekani inastahili "kuangazia uchaguzi wake" badala ya "kuisomea" Uganda kuhusu uchaguzi wake, msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo amenukuliwa na gazeti la New Vision linalohusishwa na serikali.

    Tamko lake linakuja baada ya Marekani kusema inatafakari "kuchukua hatua" baada ya uchaguzi wa Uganda kukumbwa na "ghasia" na "unyanyasaji" uliofanywa na vikosi vya usalama.

    Akijibu hilo, Bw. Opondo alisema Uganda itasubiri mawasiliano rasmi kutoka kwa serikali ya Marekani.

    "Kwa sasa, nadhani serikali ya Marekani inastahili kushughulikia uchaguzi wake, ambao kulingana na Rais Donald Trump, hata wapigakura waliokufa walishiriki uchaguzi wakati Joe Biden yuko madarakani kupitia njia ya udanganyifu.

    Kwa hivyo wao wanastahili kuwa wa mwisho kutupatia somo,” Bw Ofwono alinukuliwa kusema.

    Soma zaidi:

    • Jinsi Museveni alivyoitawala Uganda miaka 35
    • Bobi Wine: Mbunge wa Uganda anayemkaidi Museveni
    Bobi Wine

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Uganda Yoweri Museveni - ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986 - alitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa mwezi Januari.

    Mpinzani wake mkuu Bobi Wine alisema uchaguzi ulikumbwana udanganyifu na kuwasilisha kesi ya kupinga matokeo uchaguzi huo mahakamani kabla ya kuoindoa.

    Matokeo rasmi yanaonesha Bw. Museveni alipata silimia 59 ya kuru ikilinganishwa na asilimia 35 ya Bobi Wine.

  5. Balozi wa Italia aliyeuawa DRC azikwa

    Luca Attanasio was shot dead apparently in a botched kidnapping attempt

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Luca Attanasio alipigwa risasi na kuuawa katika jaribio lau utekaji nyara uliotibuka

    Mazishi ya kitaifa ya balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamefanyika mjini Rome.

    Luca Attanasio, mlinzi wake polisi wa Italia, Vittorio Iacovacci na derva raia wa DR Congo, Mustapha Milambo, waliuawa Jumatatu baada ya msafara wa magari ya Umoja wa Mataifa uliokuwa ukisafiri Mashariki mwa nchi hiyo DRC.

    Waziri Mkuu Italia, Mario Draghi, alikuwa miongoni mwa waombolezaji waliohudhuria ibada ya mazishi iliyofanyika katika kanisa la Santa Maria Degli Angeli.

    Serikali ya Congo imelaumu kundi la waasi wa Rwanda, FDLR. Waasi hao wamepinga madai hayo.

    Maelezo zaidi:

    • Balozi wa Italia auawa DRC
  6. Bobi Wine atakiwa kuelezea jinsi alivyopata gari lake la kifahari

    Gari la Bobi Wine

    Chanzo cha picha, New Vision

    Mamlaka nchini Uganda zinamtaka kiongozi wa chama cha National Unity Platform (NUP), Robert Kyagulanyi Sentamu kuweka wazi jinsi alivyopata gari lake jipya la kifahari kufikia Machi 31.

    Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Kampala, Mkaguzi Mkuu wa Serikali alitangaza kuwa viongozi wote nchini humo wataanza kutangaza mali zao, vyanzo vyake na madeni waliyonayo kwanzia Machi 1.

    Akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari, mkurugenzi wa kanuni ya maadili katika ofisi ya mkaguzi wa mkuu wa serikali, Annet Twine, alithibitisha kwamba viongozi watahitajika kutangaza mali zao ikiwa ni pamoja na zawadi na misaada waliopokea katika juhudi za kukabiliana na ufisadi.

    Gari la Bobi Wine

    Chanzo cha picha, Bobi Wine

    Huku hayo yakijiri Waziri wa Maadili na Uadilifu Fr Simon Lokodo amekariri kujitolea kwa serikali kupambana na ufisadi.

    Wiki iliyopita Bw. Kyagulanyi, mgombea wa urais wa zamani, alizindua gari lake jimpya aina ya SUV na Cruiser V8 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja za Uganda, ambalo alidai haliingii risasi .

  7. Muigizaji aibua gumzo Kenya baada kukutana na Rais Kenyatta

    Rais Kenyatta

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

    Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Kenya wamekuwa wakitoa maoni mseto kuhusiana na kanda ya video inayomuonesha muigizaji Pascal Tokodi alivyokutana na Rais Uhuru Kenyatta bila kutarajia.

    Katika video hiyo iliyowekwa mtandaoni ni muigizaji huyo, anaonekana akipunguza mwendo wa gari na kumsalimia Rais Kenyatta - ambeye alikuwa akitembea karibu na makazi yake rasmi katika jiji kuu, Nairobi

    Inamuonesha rais akiwa bila walinzi.

    Muigizaji huyo "alitumia muda huo" kumuomba rais atazame kipindi maarufu cha televisheni, Selina, ambacho yeye ni mmoja wa waigizaji wake. Rais alimjibu ''Nimeona''.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wamemkosoa muigizaji huyo, wakisema angelitumia muda huo vizuri.

    "Unakutana na RAIS akitembea peke yake na kile unachotaka akufanyie ni kutazama Selina kwenye Maisha Magic East? Vijana wa Kenya hawana sera na wanataka RAIS kuwapa nyadhifa serikalini wakati anafahamu fika hawawezi kujitetea kwa sekunde 10,"Abraham Mutai aliandika kwenye Twitter.

    Wengine walisema muigizaji huyo hakufany amakosa kunadi kipindi chake.

    "Pascal tokodi ni muigizaji mkuu wa kipindi cha selina, kipindi hicho kinamkimu kimaisha, alikutana na rais kwa chini ya sekunde 10....akamuomba atazame selina n akuungamkono kazi yake, kwa kweli hakufanya kosa lolote,"Chege Githinji aliandika.

  8. Wizara ya Afya Tanzania yahimiza matumizi ya barakoa,

    Muigizaji wa Tanzania

    Chanzo cha picha, AFP

    Waziri wa Afya wa Tanzania Dokta Dorothy Gwajima, amehimiza uvaaji wa barakoa na matumizi ya vitakasa mikono ili kujikinga na maradhi ya Covid 19.

    Dokta Gwajima amehimiza matumizi ya barakoa safi za kujitengenezea wenyewe au kutoka kwa taasisi za serikali au binafis zilizo idhinishwa na Wizara ya Afya.

    ''Vaa barakoa safi na salama ambayo umetengeneza mwenyewe au umenunua kwa watengenezaji wa ndani yan chi waliothibitishwa na wizara ya afya” alisema Dokta Gwajima..

    Waziri amesema ni vyema watu wakazingatia uvaaji wa barakoa kwa usahihi kwenye misongamano ya watu na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima mfano misongamano kwenye usafiri wa umma.

    Wananchi pia wameombwa kuzingatia lishe bora na matumizi ya tiba asili iliyothibitishwa na Baraza la Tiba Asili la Taifa.
    Maelezo ya picha, Wananchi pia wameombwa kuzingatia lishe bora na matumizi ya tiba asili iliyothibitishwa na Baraza la Tiba Asili la Taifa.

    Sambamba na uvaaji wa barakoa na matumizi ya vitakasa mikono,Waziri Gwajima pia amewataka wananchi kufanya mazoezi walao dakika 30 kila siku na kuzingatia lishe bora na matumizi ya tiba asili iliyothibitishwa na Baraza la Tiba Asili la Taifa.

    Waziri amesema ni wajibu wa kila mmoja kuchukua hatua stahiki kwani elimu inatolewa na itaendelea kutolewa hivyo mara mtu anapo dalili za maradhi awahi kituo cha afya kwa huduma.

    Maafisa wa afya walioko mipakani pia wameombwa kuwa makini na kudhibiti kusambaa zaidi kwa magonjwa hususan kipindi hiki cha majira ya mwaka ambapo kunaongezeko la maradhi ya mfumo wa upumuaji.

    Pia unaweza kusoma:

    • Rais Magufuli asema 'Hatujazuia matumizi ya barakoa'
    • Ubalozi wa Marekani wawaonya watu wanaotaka kusafiri nchini Tanzania
    • Je ni akina nani wamefariki Tanzania mfululizo kwa kipindi kifupi na kwa sababu zipi?
  9. Kituo cha wapenzi wa jinsia moja chafungwa Accra Ghana

    Ghana still criminalises same-sex relations

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Ghana haijahalalisha uhusiano wa wapenzi wa jinsia moja

    Polisi nchini Ghana wamefunga kituo cha kuwahudumia wapenzi wa jinsia moja ambacho kilifunguliwa hivi karibuni katika mji mkuu wa Accra, kufuatia malalamishi ya umma.

    "Hatuwezi tena kufikia eneo letu salama na usalama wetu unatishiwa. tunomba mashirika ya kutetea haki za binadamu, na washirika wao kuangazia shambulio hili na uhalifu wa chuki tunaotendewa," Wanaharakati wa kutete haki za wapenzi wa jinsia moja nchini Ghana walisema kwenye mtandao wa Twitter.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Makundi ya kutetea haki, ikiwemo Muungano wa Haki sahihi za Kijinsia, Binadamu na Maadili ya Familia pamoja na Kongamano la Maaskofu wa katoliki Ghana (GCBC), yamekuwa yakishinikiza serikali kufunga kituo hicho.

    Kilifunguliwa kupitia hafla ya mchango wa fedha uliohudhuriwa na wanadiplomasia kadhaa wa Muungano wa Ulaya (EU) na wakigeni.

    Picha za kufunguliwa kwa kituo hicho zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zimezua hisia mseto.

    Soma zaidi:

    • Fahamu mataifa yaliohalilisha na kupinga mapenzi ya jinisia moja Afrika
  10. Makamu wa rais wa Zimbabwe apinga kashfa ya ngono dhidi yake

    Makamu wa Rais wa Zimbabwe Kembo Mohadi amejitetea kuhusu madai ya kashfa ya kingono inayomkabili kupitia vyombo vya habari.

    Amesema yeye ni mwathiriwa wa udukuzi na saiti iliyofanyiwa marekebisho baada ya gazeti moja la mtandaoni kuchapisha rekodi ya mawasiliano yake ya simu na wanawake tofauti wanaodaiwa kumfanyia kazi.

    Akiwa amevalia barakoa na sauti yake kutosikika vizuri, kiongozi huo mwenye umri wa miaka 71 aliwaambia waandishi wa habari kwa rekodi hiyo ilifanyiwa ukarabati akisisitiza hakuhusika na madai hayo.

    “Mimi sina hatia, ni mwathiriwa wa hila za kisiasa zinazoendeshwa kitapeli."

    Aliongeza kuwa madai hayo ni ya uongo na yanalenga kumharibia sifa kama kiongozi wa kitaifa.

    Msemaji wa serikali ameweka mtandaoni video ya Bw. Mohadi akitoa taarifa kwa waandishi wa habari.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  11. Kenya yawazuia wanariadha wake kushiriki Kimanjaro Marathon

    Wanariadha wa Kenya wamekuwa wakitawala mbio hizo katika makala yaliopita.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Wanariadha wa Kenya wamekuwa wakitawala mbio hizo katika makala yaliopita.

    Kenya imekataa kuwaidhinisha wanariadha wake kushiriki mbio za masafa marefu za Kilimanjaro Marathon nchini Tanzania kwa kuhofia janga la corona.

    Mashindano hayo yanayotambuliwa na Shirikisho la Riadha Duniani IAAF- yataandaliwa Jumapili hii chini ya mlima Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika.

    Wanariadha wa Kenya wamekuwa wakitawala mbio hizo katika makala yaliopita.

    Katika taarifa, Shirikisho la Riadha la Kenya limetoa wito kwa "wanariadha wote kutosafiri Tanzania kushiriki mashindano hayo".

    Tanzania haijakuwa ikitoa data ya hali ya corona nchini humo tangu kati kati ya mwaka jana.

    Mapema wiki hii Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitoa wito kwa Tanzania kuanza kutoa data ya watu walioambukizwa virusi vya corona.

    Maelezo zaidi:

    • WHO yaomba Tanzania kutoa takwimu ya walioambukizwa corona
    • Rais Magufuli asema 'Hatujazuia matumizi ya barakoa'
  12. Karibu katika matangazo mubashara leo Alhamisi 25.02.2021