Mkenya aliyekuwa akitafutwa na ICC ajisalimisha

Wakili nchini Kenya aliyekuwa akitafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai (ICC) amejisalimisha baada ya miaka mitano tangu mahakama hiyo ilipotoa kibali cha kukamatwa kwake

Moja kwa moja

Asha Juma

  1. Na hadi kufikia hapo ndio nakamilisha matangazo yetu ya moja kwa moja kwa hii leo. Asante kwa kuwa nasi na kwaheri.

  2. Mkenya aliyekuwa akitafutwa na ICC ajisalimisha

    Wakili nchini Kenya aliyekuwa akitafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai (ICC) amejisalimisha baada ya miaka mitano tangu mahakama hiyo ilipotoa kibali cha kukamatwa kwake, kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya.

    Mahakama hiyo ilimshtaki Paul Gicheru na wengine wawili kwa kuingilia mfumo wa sheria na kuwashtumu kwa kuingilia mashahidi wa waendesha mashtaka katika kesi dhidi ya wanaodiwa kuwa waandaaji na wafadhili wa ghasia za mwaka 2007.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Zaidi ya watu 1,000 waliuawa, visa 900 vya ubakaji na unyanyasaji wa king’ono vikarekodiwa huku watu 350,000 wakilazimika kuhama makazi yao kulingana na tovuti ya taarifa za habari Kenya ya The Star.

    Mahakama ya ICC inamshutumu Bwana Gicheru na wengine na kufanya njama ya kuwasiliana na mashahidi, kuwadanganya na kutumia njia za ufisadi kulikowachochea kujiondoa kwenye kesi hiyo.

    Hivi sasa Bwana Gicheru hajasema lolote.

    Rais Uhuru Kenyatta na makamu wake William Ruto walikuwa miongoni mwa watu sita walioshtakiwa na mahakama ya ICC kwa jukumu walilotekeleza kwenye ghasia za baada ya uchaguzi.

    Baada ya miaka kadhaa, mwendesha mashtaka wa ICC alitupilia mbali kesi dhidi ya Kenyatta mwaka 2015, huku ya Ruto nayo ikifuata mkondo huo mwaka mmoja baadae akilaumu kuingiliwa kwa mashahidi.

  3. Shule zafunguliwa rasmi Rwanda baada ya miezi nane,

    wanafunzi

    Shule zimefunguliwa rasmi leo nchini Rwanda baada ya kufungwa kwa miezi nane kufuatia mikakati ya nchi hiyo kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona.

    Wizara ya elimu nchini humo imesema shule zitafunguliwa kwa awamu tofauti na kila shule lazima kuzingatia masharti ya kujilinda na Covid19.

    Baadhi ya wazazi wanasema hali ya kiuchumi iliyosababishwa na covid19 inawatatiza kuwarudisha watoto wao shuleni.

    n

    Katika Shule nyingi mjini Kigali kumewekwa sehemu ya wanafunzi kuosha mikono.Kabla ya kuingia shuleni kila mmoja anapimwa joto na lazima kuvaa barakoa kwa wanafunzi na waalimu.

    nnn

    Wizara ya elimu imesema kwamba muda wa vipindi vya masomo utapungua katika shule nyingi za serikali kutokana na kwamba wanafunzi watalazimika kusoma kwa kupishana kwa zamu ili kuheshimu masharti ya kujilinda yakiwemo kuacha mwanya baina ya wanafunzi.

    Na kwa wanafunzi wa sekondari wanaoishi shuleni watalazimika kuendelea kukaa shuleni hadi mwezi wa tano mwakani pasipo kutembelewa na wazazi.

    mmm

    Darasa moja limetakiwa kubeba wanafunzi 23 ili kuweka mwanya wa mita moja baina ya wanafunzi.

  4. Baadhi ya maeneo yaliyotarajiwa kuwa na maandamano Dar es Salaam

    Dar

    Baadhi ya maeneo ambayo vyama vya upinzani Tanzania vilitaja kuwa na maandamano leo hii.

    Watu wameonekana kuendelea na shughuli zao kama kawaida na hakuna maandamano yoyote yanayoendelea.

    bb
    n
    nn
  5. Kenya huenda ikafungwa tena kwa wimbi la pili la maambukizi

    corona

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kenya huenda ikakabiliwa tena na hatua za kufunga shughuli za kiuchumi kama njia moja ya kukabiliana wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya corona.

    Raisi Uhuru Kenyatta hapo jana katika maaadhimisho ya miaka hamsi ya Kanisa la All Saints Cathedral alionesha changamoto zilizopo na uwezekano wa kufikiria kuchukua tena hatua za kuwezesha kupunguza kwa maambukizi.

    Siku za hivi karibuni, Kenya imekuwa ikishuhudia ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona, huku rais akiashiria kukumbwa na kipindi kigumu cha maamuzi. ‘’Tunapitia kipindi kigumu cha kusema sasa, tutafanya nini tena? Je tufunge? Tutazungumzia hilo, sio leo lakini karibuni,’’ alisema rais Kenyatta.

    Raia wamekuwa wakionekana kama wasiofuatilia kanuni za afya za kupamba na virusi vya corona zilizowekwa tofauti na kipindi cha nyuma.

    Bwana Kenyatta aliongeza kuwa ugonjwa wa Covid-19 ni tatizo na ana wasiwasi kuwa idadi ya waliopata maambukizi imekuwa ikiongezeka wiki kadhaa zilizopita.

    ‘’Hatungekuwa na haja ya kufanya hivyo ikiwa tu watu wangefuatilia hatua za kiafya zilizowekwa na kujali wengine.’’

    Rais anatarajiwa kuitisha mkutano wa dharura na viongozi wa kaunti kujadiliana suala la kuongezeka kwa maambukizi mapya na athari zake.

  6. Museveni ateuliwa kuwania nafasi ya urais kwa mara nyingine tena,

    Wafuasi wa NRM wakimusubiri Mseveni kupata mafuta ya bure
    Maelezo ya picha, Wafuasi wa NRM wakimusubiri Mseveni kupata mafuta ya bure

    Rais Yoweri Museveni amekuwa wa kwanza kuteuliwa na tume ya uchaguzi kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2021.

    Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Simon Byabakama na jopo lake wamemuhidhinisha rais Museveni baada ya kuhakiki nyaraka zake zote vikiwemo vyeti vyake vya elimu, risiti ya benki ya kuhakikisha kama amelipa milioni 20 za usajili na cheti cha wanaomuunga mkono kutoka katika wilaya 98.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Wengine wanaoteuliwa leo ni Jenerali Tumukunde Henery ambaye ni mgombea wa kujitegemea asiyekuwa na chama. Mgombea mwingine ni Katumba John wa kujitegemea, kiongozi wa chama cha ANT Jenerali Mugisha Muntu na mgombea wa mwisho kuteuliwa ni mwanamke pekee katika uchaguzi huu Kalembe Nancy Linda.

    n

    Zoezi hilo litaendelea hapo kesho na kiongozi wa chama cha NUP Msanii Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine ndiye atakuwa wa kwanza kuteuliwa , wengine ni Mayambala Willy, Amuria Oboi Patrick wa chama cha FDC, Mwesigye Fred wa kujitegemea na mwandishi habari ambaye ni mgombea wa kujitegemea Josephy Kabuleta.

  7. CUF 'Hatutashiriki tena Uchaguzi bila Tume huru'

    cuf

    Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha CUF, nchini Tanzania kimesema chama chake hakitashiriki tena uchaguzi nchini humo mpaka Tume huru ya uchaguzi iundwe.

    Profesa Ibrahimu Lipumba amesema hakubaliani na matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 28, kwa kuwa umegubikwa na mapungufu.

    "Zoezi la kuwaapisha mawakala liliendeshwa kinyume Cha taratibu,Uchaguzi wa Mwaka huu haukuwa na siri. kwa sababu kwenye karatasi za kupiga kura ziko namba za vitambulisho vya wapiga kura."

    CUF

    CUF imefikia maazimio ya kuhamasisha wananchi na wadau wengine kudai katiba mpya yenye misingi ya demokrasia na utawala bora.

    Na chama hicho kinaomba wanachama na watanzania kwa ujumla kufunga kula chakula cha mchana siku ya Alhamis na kufanya Dua kila mmoja na imani yake kumuomba Mungu hukumu ya haki kwa kilichotokea katika uchaguzi mkuuwa mwaka huu.

    Aliongeza kusema CUF itaaanzisha mazungumzo na Jumuiya ya Kimataifa kuhusiana na suala hili.

  8. Dkt.Hussein Mwinyi ala kiapo cha urais Zanzibar

    Ni rasmi sasa Dkt.Hussein Mwinyi ndio rais wa Zanzibar baada ya kula kiapo muda mfupi uliopita, Hivi ndivyo alivyokula kiapo:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  9. Mgogoro wa ukubwa wa kaburi wachelewesha mazishi

    kaburi

    Mazishi yalicheleweshwa kwa muda wa saa mbili baada ya mgogoro wa ukubwa wa kaburi kuibuka katika mazishi ya mzee mwenye miaka 98.

    Mtoto wa marehemu,Peter Worby alisema baba yake William alitakiwa kuzikwa lakini Padre kutoka kanisa la Old Hall Green huko Hertfordshire alisema kina cha kaburi hilo ni kifupi kuliko inavyostahili hivyo hawezi kuendesha ibada ya maziko hayo.

    Baada ya kufikiwa kwa makubaliano, kasisi huyo aliruhusu mazishi ya mzee huyo kuendelea, lakini Bwana Worby alisema familia yake ilinyimwa "muda wa kuomboleza".

    Aidha askofu wa Kanisa Katoliki aliomba msamaha kwa kuwaongezea msongo wa mawazo.

    Kwa mujibu wa chama kinachoshughulikia masuala ya waliokufa kilisema, hakuna kina maalum ambacho kimepitishwa kisheria lakini Wizara ya Sheria inapendekeza angalau kaburi liwe na kina cha sentimita 61 kuanzia kwenye mchanga wa jeneza linapoishia hadi eneo la juu ya ardhi.

  10. Upinzani Ivory coast waonywa dhidi ya vurugu baada ya matokeo ya uchaguzi

    Ivory

    Chanzo cha picha, EPA

    Chama tawala nchini Ivory Coast kimewaonya viongozi wa upinzani dhidi ya jaribio lolote la kusababisha vurugu nchini humo baada ya kukataa matokeo ya uchaguzi wa Jumamosi ambapo rais aliye madarakani Alassane Ouattara aliwania kuchaguliwa tena kwa muhula wa tatu.

    Upinzani ambao ulisusia uchaguzi huo umeitisha maandamano kuzuia kile wanachokielezea kama uchaguzi wa kulazimisha madaraka.

    Bwana Ouattara ameanza kuchukua uongozi wa mapema kwa kupata asilimia 99 ya kura katika baadhi ya maeneo ambayo ni ngome ya chama tawala.

    Zaidi ya watu 30 wameuawa katika ghasia za Bwana Ouattara alitangaza kwamba anagombea tena baada ya aliyekuwa amechaguliwa na chama chake kumrithi kufariki dunia ghafla mwezi Julai.

  11. Mkuu wa WHO yuko karantini

    who

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameanza kujitenga baada ya kukutana na mtu aliyebainika kupata maambukizi ya virusi vya corona.

    Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema yeye binafsi hakuwa na dalili za corona.

    "Mtu niliyekutana naye hivi karibuni amebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona. Niko sawa kuwa sina dalili zozote lakini nitajitenga kwa siku kadhaa zijazo, kama ilivyo katika muongozo wa WHO, na kufanya kazi nyumbani," ameandika kwenye ujumbe wa Twitter.

    "Wafanyakazi wenzangu wa WHO na mimi tutaendelea kushirikiana na wengine kuokoa maisha na kulinda maisha ya walio hatarini," aliongeza.

    Dkt.Tedros mwenye miaka 55, alikuwa waziri wa afya nchini Ethiopian alisema "ni muhimu sana kufuata muongozo wa wizara ya afya". "Kwa njia hii, ndio tutafanikiwa kukabiliana na usambaaji wa ugonjwa wa Covid-19 kukabiliana na kirusi hichi, na kulinda mifumo ya afya."

    Dkt Tedros, kama anavyopenda kufahamika, ni kiongozi wa kwanza wa Afrika katika shirika la WHO.

  12. Karibuni katika matangazo yetu ya moja kwa moja hii leo ikiwa ni tarehe 02.11.2020.