NEC yakijibu Chadema juu ya zabuni za makaratasi ya kupigia kura
Tume ya uchaguzi nchini Tanzania imelaani taarifa zilizotolewa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na Katibu mkuu wa chama cha upinzani nchini humo Chadema, Bw John Mnyika kuhusu mchakato wa zabuni ya uchapishaji wa makaratasi ya kupigia kura pamoja na jina la mzabuni.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Akamatwa baada ya mteja kupata wembe katika Pizza

Chanzo cha picha, SACO POLICE DEPARTMENT
Maelezo ya picha, Nicholas Mitchell alikua akifanya kazi katika kampuni ya It'll Be Pizza, inayotengeneza mikate Mfanyakazi wa zamani wa kampuni ya kutengeneza pizza amekamatwa nchini Marekani baada ya mteja kupata wembe ndani ya mkate wa pizza alioununua, polisi imesema.
Duka la bidhaa mbalimbali - Saco Hannaford Supermarket, lililopo eneo la Maine liliifahamisha polisi baada ya wembe kupatikana katika mkate wa pizza wenye nembo ya Portland Pie ulionunuliwa katika duka hilo.
Nicholas Mitchell, ambaye ni mfanyakazi wa zamani wa kampuni ya 'It'll Be Pizza', ambayo ilitengeneza pizza hiyo, alikamatwa.
Picha ya video ya CCTV katika duka hilo ilikuwa imeonesha mwanaume akichezea bidhaa.
Haikubainika ni kwa sababu gani aliamua kufanya kitendo hicho.
Mshukiwa alikamatwa katika kituo cha polisi cha New Hampshire baada ya polisi kuweka rufaa.
Mteja aliyenunua mkate huo wa pizza kutoka Portland Pie na mkate wa jibini kutoka kampuni hiyo ya Portland Pie katika duka lolote la Hannaford kati ya Agosti 1 na 11 Oktoba wametakiwa kuirejesha dukani, limesema duka hilo.
"Baada ya kile kinachoaminiwa kuwa tukio la uchezeaji wenye nia mbaya uliohusisha vifaa vya chuma vilivyoingizwa kwenye bidhaa za Portland Pie, Hannaford imeondoa dukani bidhaa zote za Portland Pie na imesitisha kuleta tena bidhaa hizo dukani kwa muda usiojulikana," Hannaford ilisema katika taarifa yake.
Mfahamu msanii anayeweza kupodoa uso wake kufanana na mtu yeyote duniani
Maelezo ya video, Ebube Jane Richard: Msanii anayeweza kubadili uso wake kufanana na mtu yeyote duniani Hospitali ya Benjamin Mkapa yatoa huduma za matibabu bure,

Hospitali ya Benjamin Mkapa nchini Tanzania imeandaa kambi ya wiki moja ya ambapo madaktari bingwa wanatoa huduma mbalimbali bure. Miongoni mwa huduma hizo ni upimaji wa saratani ya matiti pamoja na shingo ya uzazi.
Vilevile kuna upimaji wa magonjwa mengine kama macho. Upimaji huu pia unaenda sambamba na maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo.

Maelezo ya picha, Miongoni mwa huduma zinazotolewa bure ni pamoja na upimaji wa saratani ya matiti na shingo ya uzazi 
Hospitali ya Benjamin Mkapa ni miongoni mwa hospitali kubwa za rufaa nchini Tanzania ambayo inahudumia zaidi watu wa mikoa ya kanda ya kati kama vile Singida, Dodoma na Morogoro.
Mpaka sasa hospitali BMH mbali na kutibu magonjwa mengine lakini imejikita zaidi katika matibabu ya figo na upandikizaji wake.
Video ya wasichana wa shule ‘wakinyunyiziwa’dawa ya kuua virusi' yawakera Wakenya
Video inayoonesha wasichana wa shule wakiwa wamejipanga msururu kwa ajili ya kunyunyiziwa dawa kama sehemu ya hatua za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona imeleta mgawanyiko miongoni mwa Wakenya mtandaoni.
Video fupi ya sekunde 30 iliyopakuliwa kwenye Twitter na gazeti nchini humno inaonesha mwanaume aliyevalia mavazi ya kujikinga akiwanyunyizia kimiminika wasichana kwenye mikono, miguu na sare za shule:
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Shirika la afya duniani halishauri kuwanyunyizia watu dawa ya kuua virusi na linasema inaweza kuleta madhara ‘’kimwili, na kisaikolojia’’
Shule zimefunguliwa Jumatatu nchini Kenya kwa ajili ya wanafunzi wanaohitimu huku miongozo ikitolewa kuhusu utoaji wa vitakasa mikono na mahala pa kunawa mikono na kuzingatiwa kwa sharti la kutosogeleana ili kuzuwia usambaaji wa virusi vya corona.
Wakenya kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter wameelezea maoni yao tofauti kuhusu kunyunyiziwa kwa wanafunzi.
"Vitu kama hivyo na vifaa vya kunyunyiza vilipigwa marufuku na wizara ya afya Kwa vipi watu wazima wanakaa chini na kuamua kwamba kuwanyunyizia watoto kama hivi kutadhibiti #Covid19? Vipi kuhusu maji na sabuni ? " Dkt Mercy korir aliandika kwenye tweeter.
"Halafu kuanzia siku inayofuata tunakua na matatizo ya ngozi, kifua,maradhi ya pumu yote kwa sababu ya kisingizio cha pesa. Wazazi walilazimika kulipakwa ajili ya watoto wao ili wanyunyiziwe dawa kama ng’ombe ,"Phill Kamara aliandika tweeter.
"Sioni tatizo lolote kuhusu shughuli hii.. Ulitarajiwa watatakaswa vipi na maambukizi? .. Baadhi yenu ni waasi tu bila sababu," Denno Duevshi aliandika mtandaoni.
'Lazima serikali ijibu vilio vya Wanigeria', asema Kanye West

Chanzo cha picha, Getty Images
Muimbaji wa muziki wa Rap nchini Marekani Kanye West ameelezea kuunga mkono Wanaigeria wanaoandamana dhidi ya ukatili uliofanywa na kikosi maarufu cha polisi cha kukabiliana na wizi (Sars).
Maandamano yaliyosambaa kote nchini Nigeria yamemlazimisha Rais Muhammadu Buhari kuvunja kikosi hicho. Lakini waandamanaji wanataka maafisa wa kikosi hicho kukabiliana na mkono wa sheria.
Kanye West ametuma tweet kwamba serikali ya Nigeria "lazima ijibu kilio cha watu ":
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Kenya yaitaka Uingereza iwachukulie hatua polisi wake 'waliomtesa Mkenya'

Chanzo cha picha, Mitandao ya kijamii
Maelezo ya picha, Bw. Wycliff Cox ameripotiwa kuwa ana ugonjwa wa akili Kenya imeiandikia Uingereza ikidai haki juu ya ukatili dhidi ya raia wa Kenya unaodaiwa kufanywa na maafisa wa polisi katika eneo la Colchester, Essex nchini humo.
Tukio la ukatili huo lilichukuliwa kwenye picha ya video ambayo ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kuibua hasira na vilevile kuchochea vugu vugu la ‘Black Lives Matter’ dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Katika video hiyo, polisi takriban sita wa Uingereza wanaonekana wakimtesa Mkenya aliyetambuliwa kama Wycliff Cox walipokuwa wakitaka kumkamata kwa madai ya kukiuka sheria za dhamana.
Maafisa hao wanaonekana wakikandamiza kichwa cha Wycliff ardhini huku wakishikia shingo yake, huku watu wa familia yake ikitazama na mama yake akisikika akiomba : “Usimuue kijana wangu.”
Huku uso wake ukionekana kutoka damu, mikono na miguu ikiwa imefungwa, Wycliff, ambaye ameripotiwa kuwana ugonjwa wa akili, anaonekana akichukuliwa na polisi na kuingizwa ndani ya gari la polisi lililokuwa linasubiri.
Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatatu , Ubalozi wa Kenya nchini Uingereza ulitoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya mafisa hao kwa ‘’matumizi ya nguvu zisizo za lazima kwa mtu ambaye hakuwa na silaha.
“Ubalozi wa Kenya nchini Uingereza umepokea video ya kusikitisha inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo polisi katika Colchester, Essex wanaonekana wakimtesa Mkenya , Bw. Wycliff Cox,” alieleza taarifa ya ubalozi wa Kenya nchini Uingereza:
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Yanga SC yamsajili mchezaji wa Burundi aliyeifunga bao Taifa Stars

Chanzo cha picha, Young African SC/TWITTER
Timu ya soka ya Tanzania Young Africans Sports Club imemsajili mchezaji wa Burundi Saidi Ntibazonkiza.
Ntibazonkiza ambaye amekuwa akicheza katika safu ya mashambulizi ya timu ya soka ya Burundi -Vitalo anahamia Yanga SC baada ya kuifunga timu ya taifa ya Tanzania. Taifa Stars – katika mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya lake, Intamba Murugamba mnamo dakika ya 85 siku ya Jumapili.
Yanga imetuma imedhihirisha usajiri huu kwenye ukurasa wake wa twitter:
Ruka X ujumbe, 1Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Mashabiki wa Yanga pia walielezea pia hisia zao juu ya usajiri wa Said Ntibazonkiza:
Ruka X ujumbe, 2Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Ruka X ujumbe, 3Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Ruka X ujumbe, 4Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 4
Ntibazonkiza amewahi kucheza soka katika timu za Ufaransa, Poland na Holand na Kazakistan.
Rwanda yapunguza muda wa amri ya kutotoka nje usiku

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Wanaokiuka miongozo ya kukabiliana na corona Rwanda hulazimishwa kuketi hadi siku inayofuata Baraza la mawaziri nchini Rwanda limepunguza muda wa amri ya kutotembea nje wakati wa usiku kwa saa mbili huku idadi ya watu wapya wanaopata maambukizi ikipungua.
Amri ya kutotembea nje usiku sasa itaanza kutekelezwa kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri kwa saa za Rwanda.
Sasa mabasi ya abiria ya umma yatajaza viti vyote vya abiria huku idadi ya abiria wanaosimama wakiruhusiwa kuwa nusu ya wale waliokuwa wakiruhusiwa kusimama ndani ya basi.
Watu wanaohudhuria mikutano hawatahitajika tena kudhihirisha kuwa hawana Covid-19, lakini waandalizi watatakiwa kuheshimu miongozo ya kukaa mbali kwa kuwa na 50% ya mahudhurio ya washiriki.
Baraza la mawaziri limesema kuwa adhabu ya kutovaa barakoa na kukiuka amri ya kutotoka nje itaendelea kutekelezwa.
Wale wanaopatikana bila kuvaa barakoa katika maeneo ya umma watatozwa faini ya $10. Kiwango hicho cha faini pia kitatozwa kwa wale wasioheshimu miongozo ya kukaa umbali wa mita 2 kati ya mtu na mtu na kupuuza amri ya kutotoka nje nyakatoi za usiku.
Baadhi ya watu wanaokiuka maagizo hayo hulala kwenye viwanja vya michezo au majengo ya shule ambako huketi hadi asubuhi ya siku inayofuata.
Hadi sasa Rwanda imethibitisha kuwa watu 4,905 walipatwa na maambukizi ya virusi vya corona
NEC yakijibu Chadema juu ya zabuni za makaratasi za kupigia kura.

Chanzo cha picha, CHADEMA
Maelezo ya picha, Bwana Mnyika aliitaka NEC kuitaja kampuni ya uchapishaji wa karatasi za kupigia kura Tume ya uchaguzi nchini Tanzania imepinga taarifa zilizotolewa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na Katibu Mkuu wa chama cha upinzani nchini humo Chadema, Bw John Mnyika kuhusu mchakato wa zabuni ya uchapishaji wa makaratasi ya kupigia kura pamoja na jina la mzabuni.
Tume hiyo imezitaja taarifa za Chadema kuwa ni za upotoshaji, na kuongeza kuwa Manunuzi ya jumla ya zabuni 47 ziliorodheshwa ikiwemo zabuni iliyoyohusu uchapishaji wa karatasi za kupigia kura na njia ya kumpata mshindi iliyotangazwa ni ya ushindani wa wazi wa kimataifa.
Taarifa hiyo ya NEC imetolewa baada ya Chama cha Chadema kupitia Katibu wake Mkuu Bw John Mnyika kuitaka NEC kutaja kampuni ya uchapishaji wa karatasi za kupigia kura. Bwana Mnyika amesema hayo katika mazungumzo na waandishi wa habari:
’’Kuna jambo ambalo naamini waandishi wa habari hamlifahamu na umma haulifahamu na kupitia kwenu ni vizuri jambo hili likawa wazi kwa umma... tarehe nane mwezi Oktoba, Tume ya uchaguzi iliitisha kikao cha kwanza cha tume ya taifa cha manunuzi na lojistiki... tafsiri yake ni nini...toka mchakato wa uchaguzi umeanza, tume ya taifa ya uchaguzi imekuwa ikifanya manunuzi na kufanya lojistiki mbali mbali za uchaguzi bila kuhusisha vyama vya siasa mpaka tarehe nane Oktoba, wameita kikao ambacho kimsingi ni kuvieleza tu vyama kwamba tayari tume imekwisihafanya manunuzi ya vifaa vya kiuchaguzi katika masuala ambayo yanapaswa kuwa wazi kwa umma’’, Mnyika amesema.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkutugenzi wa uchaguzi NEC Dkt. Wilson M.Charles imesema licha ya Tume kuvishirikisha vyama vya kisiasa kwenye eneo la upatikanaji wa vifaa vya uchaguzi kikiwemo Chadema vyama hivyo havikuteua wajumbe wa kuunda kamati ya Lojistiki, licha ya vyama hivyo kuandikiwa barua na tume tarehe 30 Juni, 2020.
Tume ya uchaguzi nchini Tanzania ndio yenye mamlaka ya kikatiba ya kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais Wabunge na Madiwani kwa upande wa Tanzania bara.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Weah aiomba Marekani kusaidia uchunguzi wa mauaji ya ajabu

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, George Weah ambaye ni nyota wa zamani wa soka alikuwa rais wa liberia 2018 Rais wa Liberia George Weah ameiomba Marekani kusaidia katika uchunguzi wa mauaji ya ajabu ya maafisa wa ngazi ya juu katika nyadhifa zinazohusiana na masuala ya fedha nchini mwake, limeripoti shirika la habari lenye uhusiano na serikali ya Liberia {LINA}
Vifo vya maafisa hao vimeibua tetesi za kampeni ya mauaji, kulingana na taarifa ya shirika la habari la AFP.
LINA lilimnukuu Bwana Weah akiwataka watu kuacha kubashiri, na kusubiri matokeo ya uchunguzi.
Bwana Weah alikuwa amemuagiza Waziri wa Fedha, Frank Musa Dean kuratibu juhudi zake na washirika wa serikali , ikiwa ni pamoja na LINA limeripoti.
Ilimtaja mmoja wa maafisa aliyeuawa kuwa alikuwa mkuu wa Shirika la ukaguzi wa ndani, Emmanuel Nyeswua.
Wengine walikuwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato nchini Liberia, lakini LINA halikuwataja.
Shirika la AFP limeripoti kuwa ni watu wanne – na sio watatu waliokufa katika kipindi cha wiki moja tu.
Walikuwa ni:
- Bwana Nyeswa, ambaye alipatikana akiwa amekufa katika makazi yake yaliyopo mji mkuu , wa Monrovia, Jumamosi.
- Afisa katika Mamlaka ya Mapato ya Liberia aliyeuawa katika ajali ya gari katika mji mkuu Monrovia tarehe 4 Octoba
- Maafisa wengine wawili zaidi katika mamlaka ya ukusanyaji wa kodi ambao walipatikana wakiwa wamekufa ndani ya gari siku iliyofuatia.
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Jumanne tarehe 13.10.2020

