Magufuli awaomba Watanzania kushirikiana na Wakenya katika maombi dhidi ya corona

Rais John Magufuli amewaomba Watanzania kushirikiana na Wakenya katika maombi dhidi ya corona kwa muda wa siku tatu.

Moja kwa moja

Asha Juma

  1. Na hadi kufikia hapo ndio nakamilisha matangazo yetu ya moja kwa moja. Kuwa na wikendi njema.

  2. Mbunge wa Burundi ashtakiwa na makosa ya uchochezi dhidi ya rais

    Fabien Banciryanino

    Chanzo cha picha, BUNGE LA BURUNDI

    Maelezo ya picha, Aliyekuwa mbunge wa Burundi Fabien Banciryanino ameshtakiwa

    Aliyekuwa mbunge wa Burundi Fabien Banciryanino ameshtakiwa kwa makosa ya uasi na kutoa matamshi ya uchochezi dhidi ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza.

    Mapema mwaka huu, Bwana Banciryanino alisema bungeni kwamba rais Nkurunziza "anastahili kushtakiwa kwa makosa ya ukiukaji wa haki za kibinadamu na mauaji yaliyotokea akiwa madarakani".

    Baadae alipoteza kiti chake wakati wa uchaguzi uliofanyika Mei.

    Wakili wake Christophe Nkeringanji ameiambia BBC kwamba wabunge hawastahili kushtakiwa kwa maneno yaliosemwa bungeni.

    Kushtakiwa kwake kumesababisha hisia mseto nchini Burundi huku baadhi ya watu wakisema alikuwa akizungumza kwa niaba ya wengi, na wengine wakihisi kwamba alimkosea heshima rais.

  3. Wanawake waandamana kupinga ubakaji na mauaji ya msichana mdogo

    Chaïma

    Chanzo cha picha, CHAIMA

    Maelezo ya picha, Mwili wa Chaïma ulipatikana ukiwa umechomwa

    Maandamano yamefanyika katika miji kadhaa ya Algeria yakitaka hatua kuchukuliwa kusitisha unyanyasaji dhidi ya wanawake baada ya msichana kijana kubakwa na kuuawa.

    Mwili ulichomwa moto wa Chaïma, 19, ulipatikana katika kituo cha petroli kilichojitenga huko Thenia, kilomita 80 mashariki mwa mji mkuu wa Algiers mwezi huu.

    Aliyemuua amekiri kutekeleza uhalifu huo na amekamatwa, kulinga na vyombo vya habari vya eneo.

    Pia kuna taarifa kwamba mwili wa mwanamke mwingine umepatikana msituni ukiwa umechomwa usiku wa manane.

    Maandamano Algiers

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Waandamanaji wanasema polisi wengi wamepelekwa kwenye maeneo ya maandamano

    Wanawake wamefanya maandamano katika miji ya Algiers na Oran, wakitaja jina 'Chaïma' la msichana aliyeuawa na kutoa wito wa kukomeshwa kwa unyanyasaji wa kijinsia.

    Wanaharakati wanasema polisi wengi wamepelekwa kwenye maeneo ya maandamano.

    "Serikali hii haitoi ulinzi wowote au mikakati ya kulinda waathirika dhidi ya wanao dhulumiwa, serikali hii inasema kwamba ina sheria lakini ukweli ni kwamba wanawake hutakiwa kusamehe wanao washambulia, ama wawe kaka zao, baba zao au yeyote yule," mmoja wa waandamanji amesema.

    Mama ya Chaïma alisema mshukiwa alijaribu kumbaka binti yake 2016, akiwa na umri wa miaka 15 lakini kesi hiyo ikatupiliwa mbali.

  4. Magufuli awaomba Watanzania kushirikiana na Wakenya katika maombi dhidi ya corona

    Rais John Pombe Magufuli
    Maelezo ya picha, Rais John Pombe Magufuli

    Hii leo katika mkutano wa kampeni ya urais ya chama cha Mapinduzi (CCM) jijini Dar es Salaam, Rais John Magufuli amewaomba Watanzania kushirikiana na Wakenya katika maombi dhidi ya corona.

    Magufuli amesema Kenya watafanya maombi ya kitaifa kuanzia leo, kesho Oktoba 10 na Jumapili Oktoba 11.

    Aliongeza kusema pia "inabidi kuwaombea ili corona iondoke kwao kama Mungu alivyoindoa hapa Tanzania".

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Mapema wiki hii rais Uhuru Kenyatta alitangaza kuongoza taifa katika ibada maalumu ya kitaifa ili kuiombea nchi kukabiliana na janga la corona.

    Katika ibada hiyo masuala mengine ambayo ni changamoto nchini humo yatajumuishwa katika maombi.

    Ibada ya siku ya Jumamosi inatarajiwa kufanyika Ikulu ya Nairobi kuanzia saa nne asubuhi.

    Vilevile matangazo ya televisheni na redio yatarushwa moja kwa moja katika nchi nzima pamoja na mitandao ya kijamii.

  5. Wanawake waandamana dhidi ya serikali ya rais Chakwera Malawi - kunani?

    Vuguvugu la wanawake nchini Malawi limeanza maandamano yanayopinga ukosefu wa usawa wa kijinsia katika uteuzi wa nyadhifa za umma huku kukiwa na jeshi kubwa la polisi eneo hilo.

    Wanawake wanamshutumu rais Lazarus Chakwera kwa kushindwa kuafikia hitaji la uwiano wa usawa wa kijinsia la 60:40 katika uteuzi wake.

    Rais alisema alihitaji muda zaidi kuafikia usawa huo wa kijinsia.

    Gazeti la Nation nchini Malawi limeweka picha kwenye mtandao wa Twitter zinazoonesha polisi waliopelekwa katika maeneo hayo kukabiliana na waandamanaji.

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Ruka X ujumbe, 2

    Mwisho wa X ujumbe, 2

    Kundi la haki za wanawake limeweka picha za maandamano hayo kwenye mtandao wa Twitter

    Ruka X ujumbe, 3
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 3

  6. Chama tawala Sudan chashtakiwa kwa kunyima wanawake nafasi za uongozi

    Rais Salva Kiir (katikati)

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wanaharakati wanataka Rais Salva Kiir (katikati) kubalisha magavana wawili aliowachagua na wanawake

    Kundi la wanaharakati nchini Sudan Kusini limeshitaki chama tawala cha Sudan People’s Liberation Movement (SPLM), katika mahakama ya juu kabisa kwa kile wanachosema ni ukiukaji wa haki za wanawake kulingana na katiba.

    Walishtumu chama hicho kwa kutoheshimu katiba na ukiukaji wa Makubaliano ya Amani ya 2018 ambayo yanahakikisha wanawake asilimia 35 ya nafasi za uongozi katika ngazi zote za serikali.

    Ombi hilo lilipokelewa na naibu jaji mkuu, John Gatwich Lul, aliyeahidi kuliwasilisha kwa Jaji Mkuu, Chan Reec Madut, ili kuzingatiwa.

    Juni, Rais Salva Kiir aliteuwa magavana 9 katika majimbo 10 nchini humo. Mmoja pekee ndio mwanamke, Sarah Cleto Rial, aliyechaguliwa na chama cha naibu rais wa kwanza Riek Machar.

    Chama cha rais hakikumteua mwanamke yeyote katika nafasi zake sita za ugavana.

    “Tunasihi mahakama ya juu zaidi kutoa agizo kwa chama cha SPLM na kuwalazimisha kuondoa magavana wawili wanaume na nafasi hizo zipewe wanawake,” Wani Michael, mlalamishi amezungumza na BBC katika mji mkuu wa Juba, Alhamisi.

    Bwana Wani amesema ikiwa mahakama itashindwa kuchukua hatua ya kuzingatia ombi lao, kuna uwezekano wa kulipeleka katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki mjini Arusha nchini Tanzania.

    Sudan Kusini ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini bado haijathibitishwa kuwa mwanachama kamili.

  7. Kenya yamuunga mkono mgombea wa Nigeria kuwania uongozi wa WTO

    Ngozi Okonji-Iweala

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Ngozi Okonji-Iweala ameingia kwenye fainali ya kuwania uongozi wa WTO

    Kenya yamuunga mkono mgombea wa Nigeria, Ngozi Okonji-Iweala anayewania nafasi ya WTO baada ya Waziri wa michezo wa Kenya Amina Mohamed kushindwa kuingia kwenye fainali.

    Katika taarifa yake iliyoitoa Alhamisi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya, ilisema ingawa Mohamed "alikuwa mgombea aliyefaa zaidi kushikilia wadhifa wa WTO, tunakubali kwamba mchakato huo umesonga mbele bila ya yeye."

    "Hivyobasi, Kenya inamuunga mkono moja kwa moja Ngozi Iweala wa Nigeria, inamtakia kila kheri na inatarajia jumuiya ya kimataifa kutimiza ahadi hii muhimu, wakati wagombea wawili wanasonga mbele katika awamu ya mwisho.

    Iweala, ambaye atakabiliana na Waziri wa Biashara wa Korea Kusini Yoo Myung-hee katika duru ya mwisho, amehudumu kama waziri wa fedha wa Nigeria na waziri wa mambo ya nje.

    Ikiwa itafanikiwa, Nigeria itakuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuwa Mkurugenzi Mkuu wa WTO.

  8. Wabunge Kenya kuchukua likizo fupi kurekodi video ya wimbo 'Jerusalema'

    Wabunge nchini Kenya wiki ijayo watachukuwa mapumziko mafupi kwenda kurekodi video ya densi ya Jerusalema maarufu kama #JerusalemaDanceChallenge ambayo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

    Wimbo wa Jerusalema uliombwa na mwanamuzi wa Afrika Kusini Master KG umechochea kutengenezwa kwa video nyingi kote duniani.

    Kiongozi wa walio wengi wa bunge la Kenya, Amos Kimunya, amenukuliwa akisema Spika na wakuu wote wa kamati za idara mbalimbali wataongoza wabunge wengine katika densi hiyo.

    Alisema video hiyo itaangazia kazi za bunge na kuonesha umoja na waathirika wa janga la virusi vya corona.

    Jennifer Shamalla, mbunge aliyeteuliwa, ametuma video kwenye mtandao wa Twitter inayoonesha wabunge wenzake wakifanya mazoezi.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  9. Zitto Kabwe afanyiwa upasuaji baada ya ajali

    Zitto Zuberi Kabwe
    Maelezo ya picha, Zitto Zuberi Kabwe

    Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe anaendelea kupata nafuy baada ya kufanyiwa upasuaji. Hayo yamethibitishwa na mke wake aliyetuma ujumbe kwa njia ya Twitter.

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Bwana Zitto anapokea matibabu katika hospitali ya Aga Khan ambako amelazwa kulingana na mgombea rais wa chama hicho Bernard Membe aliyemtembelea hospitali.

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

    Zitto na wanachama wengine walipata ajali ya barabarani Jumatatu huko jimboni Kigoma Kusini, wilaya ya Uvinza, mjini Kigoma, Magharibi mwa Tanzania.

    Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa Tanzania bara, Joran Bashange, ajali hiyo ilitokea akiwa kwenye shughuli za kampeni, akitoka katika eneo la kata ya Kalya kuelekea Lukoma.

    ''Gari lake liligongwa nyuma kisha likapoteza muelekeo na kupinduka zaidi ya mara mbili.''

    Miongoni mwa waliompa pole Mheshimiwa Zitto, ni pamoja na Rais Magufuli kulingana na ujumbe uliochapishwa na na mkurugenzi wa mawasiliano ya rais Gerson Msigwa.

    Ruka X ujumbe, 3
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 3

  10. Chakwera akatiza ziara yake nchini Tanzania

    John Pombe Magufuli na Lazarus Chakwera

    Chanzo cha picha, IKULU YA TANZANIA

    Maelezo ya picha, Rais John Pombe Magufuli (kushoto) na rais Lazarus Chakwera wa Malawi (kulia)

    Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amekatiza safari yake nchini Tanzania alikokuwa kwa ziara rasmi, baada ya kufanya mazungumzo na Rais John Pombe Magufuli.

    Kwa mujibu wa afisa wa mawasiliano wa rais nchini Malawi Brian Banda aliyenukuliwa na gazeti la Nyasa Times, Chakwera alitarajiwa kuwasili nyumbani Alhamisi mchana katika uwanja wa kimataifa wa Kamuzu.

    “Ndio, rais anakuja saa kumi na nusu mchana. Awali, ilitakiwa kuwa ziara ya siku tatu lakini Rais ana majukumu mengine nyumbani,” Banda amesema.

    Ikulu ya Malawi imethibitisha kwamba Chakwera alirejea nyumbani siku moja kabla ili kushughulikia mambo ya msingi ndani ya nchi.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Rais Chakwera aliwasili Tanzania Jumatano kwa ziara rasmi ya wa siku tatu na alitarajiwa kuondoka nchini humo leo Ijumaa.

    Aidha, Ziara ya Chakwera nchini Tanzania ilitanguliwa na ziara yake ya Msumbiji Jumanne.

  11. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja