Seneta wa Nigeria atozwa faini kwa kumdhalilisha mwanamke
Seneta mmoja nchini Nigeria ametozwa faini ya dola 130,000 na kuagizwa amuombe mwanamke aliyemtukana katika duka la kuuza vifaa vya kujifurahisha wakati wa ngono mwaka jana.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi
Seneta wa Nigeria atozwa faini kwa kumdhalilisha mwanamke

Chanzo cha picha, SENATOR ELISHA
Seneta mmoja nchini Nigeria ametozwa faini ya dola 130,000 na kuagizwa amuombe msamaha mwanamke aliyemtukana katika duka la kuuza vifaa vya kujifurahisha wakati wa tendo la ndoa mwaka jana.
Mahakama Kuu mjini Abuja, iliamua kuwa kitendo kilichofanywa na Seneta Elisha Abbo ‘’kilimdhalilisha " na kukiuka haki ya muathiriwa, Osimibibra Warmate.
Tukio hilo ambalo lilinaswa katika kanda ya video na kusambazwa katika mitandao ya kijamii ilimuonesha Bw. Abbo akimzaba kofi Bi Warmate.
Baada ya kitendo hicho kulaaniwa vikali na kusababisha maandamano, Seneta huyo aliomba radhi lakini Bi Warmate alikuwa tayari amewasilisha kesi mahakamani.
Kando na fedha taslimu ambazo anatarjiwa kumlipa Bi Warmate mahakama imemuagiza Bw. Abbo kumuomba radhi kupitia gazeti la kila siku la kitaifa.
Hatua hiyo imeungwa mkono na wanaharakati wa kutetea haki za wanawake.
Covid-19: Congo yaondoa kafyu
Jamhuri ya Congo imeondoa kafyu ya kitaifa iliyokuwa imeweka katika maeneo 10 ma kulegeza masharti ya kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona katika miji miwili mikubwa.
Muda wa kafyu sasa utakuwa kati ya saa tano usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi (majira ya Afrka ya kati) katika mji wa Pointe Noire na mji kuu wa Brazzaville.
Tangu mwezi Machi tarehe 14,nchi hiyo imethibitisha kuwa na watu karibu 5,000 wanaougua Covid-19.
Makundi kadhaa ya kutetea haki hivi karibuni yaliomba serikali kuondoa kafyuyakisema kuwa hali hiyo imechangia ukosefu wa.
Afrika yapoteza mabilioni ya madola kupitia uhamishaji haramu wa fedha

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Uhamishaji haramu wa fedha unahusishwa na usafirishaji nje wa bidhaa za thamani kama vile dhahabu Afrika imepoteza dola bilioni 836 sawa na (£650bn) kupitia uhamishaji haramu wa fedha kutoka barani humo kwa miaka 15 hadi mwaka 2015, ripoti mpya ya Shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa inakadiria.
Uhamishaji huo haramu wa fedha unahusishwa na usafirishaji nje wa bidha za thamani kama vile dhahabu, almasi na platini. Fedha zinazopatikana kwa njia ya ufisadi, wizi na kukwepa kulipa kodi.
“Uhamishaji haramu wa fedha unainyang’anya Afrika na watu wake mali hali inayotokana na uhujumu wa uchumi ambayo inafanya taasisi zake kutoaminika,” alisema Katibu Mkuu wa UNCTAD Mukhisa Kituyi.
Ripoti hiyo inaonya kwamba ingawa kiasi cha mtiririko huo wa fedha haramu ni mkubwa, takwimu zinaweza kupuuza changamoto na athari.
''Uhamishaji haramu wa fedha pamoja na ufisadi ni hali ambayo inazuia maendeleo katika nchi za Afrika kuwa kumaliza pesa za kigeni, kupunguza raslimali nza ndani, kukwamishabiashara za kuimarisha uchumi na kuzidisha umasikini na ukosefu wa usawa.'', aliongeza kusema Bw. Kituyi.
Togo yamteua Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke
Rais wa Togo Faure Gnassigbe amemteua mwanamke wa kwanza kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa nchi hiyo.
Victoire Tomegah Dogbe ambaye amesomea shahada ya uchumi na uuzaji aliwahi kushikilia nafasi ya ngazi ya juu katika afisi ya rais.
Kabla ya uteuzi huo alikuwa waziri wa maendeleo na vijana vijijini kwa miongo kadhaa.
Aliwahi pia kufanya kazi na mradi wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa.
Urusi, China na Iran zinamtaka nani kushinda uchaguzi wa Marekani?

Chanzo cha picha, Getty Images
Shirika la ujasusi la Marekani limesema nchi hizo tatu hao zinajaribu kuingilia uchaguzi wa Novemba lakini malengo yao yanatofautiana.
Covid-19: Guterres aomba ulimwengu kujifunza kutokana na makosa

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, ametoa wito kwa kila mmoja duniani kujifunza kutokana na makosa ya kushughulikia janga la corona, idadi ya watu waliofariki kutokana na virusi vya corona ikipita milioni moja.
Bw Guterres amesema idadi hiyo inatia hofu; huku akiomba watu kuheshimu sayansi wanapokabiliana na janga hilo, akionya kuwa taarifa za upotfu zimesababisha vifo vya watu.
Marekani, Brazil na India zinachangia karibu nusu milioni ya walioathirika.
Baadhi ya wataalamu wanaamini kuwa idadi halisi ya waliofariki huenda ikawa juu, kwasababu viwango vya upimaji wa virusi hivyo katika baadhi ya nchi viko chini, kumaanisha vifo vinavyohusishwa na Covid-19 havinakiliwi kikamilifu.
Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani kinasema karibu watu milioni 23 wamepona kutokana na virusi hivyo.
Uganda 'kufanyia binadamu majaribio' ya chanjo ya Covid-19

Chanzo cha picha, Getty Images
Uganda inatarajiwa kuanza kufanyia binadamu majaribio ya chanjo ya Covid-19 mwezi Novemba, Ripoti ya gazeti la Daily Monitor imewanukuu maafisa wa Wizara ya Afya.
Chanjo hiyo imeandaliwa kupitia ushirikiano kati ya Taasisi ya utafiti ya Uganda na Chuo Kikuu cha Uingereza.
Mkuu wa Jopokazi linalohusika na majanga Monica Musenero, amenukuliwa akisema awamu ya kwanza ya majaribio ya chanjo hiyo itahusisha Waganda 10.
Awamu ya kwanza ikifanikiwa, awamu ya pili itajumuisha watu kati ya 100 hadi 200 ikifuatiwa na awamu ya mwisho itakayojumuisha watu kati ya 1,000 na 3,000,alisema.
Sehemu kubwa ya mradi huo umegharamiwa na Chuo Kikuu cha Uingereza .
Taifa hilo la Afrika Mashariki kufikia sasa imethibitisha kuwa watuzaidi ya 7,000 walioambukizwa virusi vya corona huku 75 wakifariki.
Waziri wa Zimbabwe adai upinzani una njama ya kuingiza silaha nchini

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa Waziri wa usalama wa kitaifa wa Zimbabwe, Owen Ncube, anadai kuwa upinzani unafanya kazi na nchi za magharibi kuingiza silaha kimagendo nchini humo kwa lengo la kumuondoa madarakani Emmerson Mnangagwa.
Maafisa kutoka chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change hata hivyo wamepuuza madai hayo wakisema kuwa hayana msingi wowote.
Bila kutoa ushahidi, Bw. Ncube amesema nchi za Magharibi ambazo hakuzitaja zimekuja na mkakati wa kuvuruga utawala wa Zimbabwe ili wathibitishe haja mataifa ya kigeni kuingilia kati kutatua mzozo.
Makundi ya kutetea haki yanasema serikali ya Rais Mnangagwa imekuwa ikikosolewa vikali hasa wakati huu ambapo mzozo wa kiuchumi wa nchi hiyo unaendelea kufukuta.
Wamelaani hatua ya hivi karibuni ya kufungwa kwa wanasiasa na wanaharakati kwa kile walichodai kuwa mashitaka ya uongo.
Wagonjwa waathirika na mgomo wa wahudumu wa afya KNH

Mtu mmoja amefariki katika eneo la kuegesha magari siku ya Jumatatu akisubiri kupewa matibabu katika Hospitali Kuu ya Rufaa ya Kenyatta nchini Kenya baada ya wahudumu wa afya katika hospitali hiyo kususia kazi wakishinikiza mazingira bora ya kazi na nyongeza ya mishahara na marupurupu.
Mamlaka ya usimamizi wa Hospitali ya Kenyatta zinasema mtu huyo ambaye alikuwa mwendesha pikipiki aliwasili katika hospitali hiyo akiwa hali mahututi na kuongeza kuwa hakuna kitu kingefanywa kuokoa maisha yake.
Stanley Kamau,mwanachama wa bodi ya hospitali hiyo amesema, wafanyakazi hawawezi kulaumiwa kutokana na tukio hilo kwa sababu walitoa notisi ya mgomo.
Wafanyakazi wanataka makubaliano yaliyopitishwa kati yao kamati kuu ya ushauri yatekelezwe, uamuzi ulipitishwa mwaka 2012.
Ngozi ya wanyama wa Afrika Kusini yanaswa Sudan Kusini

Chanzo cha picha, Philip Buda Ladu
Maelezo ya picha, Ngozi ya wanyama hutumiwa kutengeneza nguo, viatu na mikoba ya wanawake Maafisa wa usalama nchini Sudan Kusini wamenasa zaidi ya kilo 320 ya ngozi ya wanyamapori iliyoingizwa kimagendo nchini humo kutoka Afrika Kusini, afisa wa wanyamapori ameiambia BBC.
Ngozi hizo zilikamatwa katika uwanja wa kimataifa wa ndege mjini Juba, baada ya kusafirishwa nchini humo kupitia ndege ya shirika la ndege la Ethiopia, alisema Mkurugenzi Mkuu wa huduma za wanyamapori nchini Sudan Kusini, Aldo Geake.
Mtu anayeshukiwa kuongoza mtandao wa watu wanaofanya biashara haramu ya bidhaa za wanyamapori amekamatwa.
Inashukiwa ngozi hizo zilikuwa zisafirishwe kimagendo hadi Ulaya, Waziri wa Uhifadhi wa wanyamapori wa Sudan Kusini Rizik Zachariah Hassan, amenukuliwa na kituo kimoja cha Redio nchini.
Hatahivyo, Jenerali Geake ameiambia BBC kwamba hakuna mtu aliyekamatwa na kwamba kuna hali ya utata kuhusu mahali ambako ngozi hizo zilikuwa zisafirishwe.
Ngozi ya wanyama inatumiwa kutengeneza bidhaa tofauti ikiwa ni pamoja na nguo, viatu na mikoba ya wanawake.
Karibu katika matangazo mubashara Jumanne 29.09.2020
