Chadema wamchagua mgombea wao wa urais
Mpeperusha bendera wa Chadema kupitishwa rasmi kesho Jumanne.
Moja kwa moja
Habari za hivi punde, Tundu Lissu ashinda tiketi ya urais Chadema
Baraza Kuu la chama cha upinzani Chadema limemchagua Tundu Lissu kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi wa Tanzania Oktoba 28.
Lissu amejinyakulia kura 405 sawa na asilimia 91 akifuatiwa kwa mbali na Lazrao Nyalandualiyepata kura 36 sawa na asilimia 8 na Maryrose Majige aliyepata kura 1 sawa na asilimia 0.23.
Matokeo Chadema hivi punde

Zoezi la kuhesabu kura za wagombea wa tiketi ya urais kwa chama kikuu cha upinzani Tanzania Chadema limekamilika, na matokeo yanatarajiwa kutangazwa hivi punde.
Waliopigiwa kura katika kinyang'anyiro cha urais ni Tundu Lissu, Lazaro Nyalandu na Maryrose Majige.

Said Issa Mohammed amepitishwa na Baraza Kuu la chama hicho kuwa mgombea wa urais wa chama hicho kwa upande wa Zanzibar.
Baraza Kuu la Chadema pia limempitisha Salum Mwalimu kuwa Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho.
Waliopigiwa kura katika kinyang'anyiro cha urais ni Tundu Lissu, Lazaro Nyalandu na Maryrose Majige.

Dira ya Dunia mubashara
Sikiliza matangazo mubashara ya Dira ya Dunia kutoka idhaa ya Kiswahili ya BBC:
Kura kwa picha
Jinsi kura zinavyopigwa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa urais Chadema kati ya wagombea Tundu Lissu, Lazaro Nyalandu na Maryrose Majige.




Chadema wamchagua mgombea wao wa urais

Maelezo ya picha, Wajumbe wa Baraza Kuu la Chadema kuchagua mgombea wa Chadema Wajumbe wa Baraza Kuu la chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema, wameanza zoezi la kupiga kura ili kupendekeza jina la atakayekuwa mgombea wao wa urais.
Wanachama watatu wa chama hicho, Dkt Maryrose Majige, Lazaro Nyalandu na Tundu Lissu ndio wanaopigiwa kura.
Uchaguzi huo wa ndani unafanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City.
Mshindi atakeyepatikana leo atapelekwa katika kikao cha Mkutano Mkuu wa chama hicho kupitishwa rasmi.

Maelezo ya picha, Dkt Maryrose Majige ndiye mgombea pekee mwanamke akichuana na Tundu Lissu na Lazaro Nyalandu. Ramaphosa awaonya 'fisi' wanaoiba pesa za Covid-19

Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa Afria Kusini Cyril Ramaphosa ameonya kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watu aliowaita ya "fisi " ambao wananufaika kutokana na pesa za umma ambazo zilipangiwa kutumiwa katika mapambano dhidi ya janga la virusi vya corona.
Kauli zake kali ambazo ziliandikwa katika waraka wake wa kila wiki, zinawalenga maafisa wa taifa hilo ambao wanashutumiwa kuchukua zabuni za serikali, wafanyabiashara ambao wanapandisha bei za usambazaji wa vifaa vya kinga (PPE), na maafisa utawala wa kimaeneo wanaojilimbikizia msaada wa chakula.
"Kujaribu kupata faida kutokana na janga ambalo linagarimu maisha ya watu wetu kila siku ni kitendo cha unyama. Nikama kundi la fisi waliozingira mzoga," alisema Ramaphosa.
Msemaji wake mwenyewe alichukua likizo wiki iliyopita baada mume wake kutajwa kuhusiana na zabuni katika idara ya afya ya jimbo la Gauteng. Yeye na mke wake walikanana kufanya kosa lolote.
Rais aliapa kuchukua hatua kali dhidi ya wale watakaobainika kuhusika na matumizi mabaya ya fedha za Covid-19.
"Wale watakaopatikana na hatia ya kuvunja sharia kujitajirisha kupitia mzozo wataona cha mtemakuni , bila kujali ni akina nani au wana uhusiano na nani," alisema.
Afrika Kusini ndio nchi iliyoathiriwa vibaya zaidi na mlipuko wa corona na idadi ya watu waliopatikana na virusi wamepita zaidi ya nusu milioni mwishoni mwa juma.
Makonda: Mwendo nimeumaliza

Chanzo cha picha, Paul Makonda
Maelezo ya picha, Paul Makonda Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekabidhi rasmi leo ofisi ya jiji hilo kwa Mkuu mpya wa mkoa wa mkoa Aboubakar Kunenge.
Bwana Makonda aliondolewa katika nafasi hiyo mwezi jana baada ya kugombea kiti cha ubunge wa jimbo la Kigamboni. Hata hivyo alishindwa katika kinyang'anyiro cha kura za maoni.
"Yote tuliyoyafanya unayajua na nina imani uwezo wa kuyasimamia unao kwa sababu tulifanya kazi pamoja. Ninamshukuru mheshimiwa rais (John Magufuli) kwa kukuchagua kuliongoza jiji hili", amesema Bwana Makonda ambaye anasema jambo ambalo anasikitika kuwa hakulitimiza alipokuwa madarakani ni kutoweza kufanikiwa kuanzisha upimaji wa tezi dume kwa kaya.
Bwana Makonda amewaambia Watanzania wasiwe na wawiwasi na maisha yake baada ya kuondoka katika kiti cha ukuu wa mkoa:
"Mwendo nimeumaliza...Ninashukuru kwa kupata nafasi ya kutunza familia kama baba wa familia’’, amesema Makonda.
Akiwa madarakani, Makonda amevuta wafuasi na 'maadui' pia. Amekuwa akisifiwa kwa kuja na mipango kadhaa ya kusaidia jamii katika sekta za elimu, afya na ustawi wa jamii.
Hata hivyo mipango hiyo pia imekuwa ikikosolewa kwa kutofuata taratibu rasmi na mwisho wa kueleweka.
Makonda pia alikosolewa kitaifa na kimataifa kwa kuvamia kituo binafsi cha habari Clouds Media Group na kutangaza vita dhidi ya wapenzi wa jinsia moja akiwa madarakani .
Drogba 'atia nia' kuongoza soka Ivory Coast
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba ametuma rasmi maombi ya kukiongoza chama cha soka cha nchi yake Ivory Coast Football Federation (FIF).
Drogba alirejesha fomu za maombi yake jana Jumapili na kulakiwa na maelfu ya mashabiki wake.
Uchaguzi wa FIF unatarajiwa kufanyika baadae mwezi ujao na Drogba ni miongoni mwa wagombea wanne waliojitokeza katika kinyang'anyiro hicho.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Makabidhiano ya Laizer na Serikali

Maelezo ya picha, Mchimbaji Saniniu Laizer akikabidhi jiwe la kilo 6.3 kwa serikali ya Tanzania. 
Maelezo ya picha, Saniniu Laizer akikabidhiwa mfano wa hundi ya Shilingi za Tanzania bilioni 4.8 baada ya kuuza jiwe lake la kilo 6.3. Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Laizer auza jiwe la Tanzanite kwa bilioni 4.8

Serikali ya Tanzania imenunua jiwe la kilo 6.3 la madini ya Tanzanite kutoka kwa mchimbaji Saniniu Laizer kwa shilingi za Tanzania bilioni 4.8.
Kwa mujibu wa Wizara ya Madini ya Tanzania, jiwe hilo lilichimbwa pamoja na mengine makubwa mawili ambayo yalinunuliwa na serikali mwishoni mwa mwezi Juni.
"Jiwe hili jipya alilipata wakati wakiondoa miamba kwenye eneo ambalo walipata mawe mengine...walikuwa wakisafisha eneo kabla ya kuanza kuchimba upya," ameeleza Dotto Biteko, Waziri wa Madini Tanzania.
Kwa upande wake mchimbaji Laizer amewataka wachimbaji wengine kuwa wazalendo na kuiamini serikali katika kufanya biashara hiyo.
Muuguzi wa Kenya afariki kwa corona baada ya kujifungua
Makali ya ugonjwa wa virusi vya corona yanaendelea kuripotiwa nchini Kenya, na sasa watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini humo wanaomboleza kifo cha muuguzi kilichotokana na virusi hivyo baada ya kujifungua.
Ruka X ujumbe, 1Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Ruka X ujumbe, 2Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Mamia wajitokeza kushuhudia mnada wa Tanzanite
Mamia ya Watanzania wamejitokeza katika migodi ya mirerani iliyopo mkoani Manyara nchini Tanzania kushuhudia mnada wa madini ya Tanzanite, ambapo mchimbaji maarufu Saniniu Laizer anatarajiwa kuuza jiwe la kilo 6.3.
Hii ni mara ya pili katika kipindi kisichozidi miezi miwili ambapo mchimba madini huyo kugundua mawe makubwa zaidi ya madini hayo yanayopatikana kaskazini mwa Tanzania tu.



Chanzo cha picha, 3

Laizer 'kuzoa' tena mabilioni ya Tanzanite

Chanzo cha picha, Wizara ya Madini, Tanzania
Mchimbaji wa madini nchini Tanzania, Saniniu Laizer hii leo anatarajiwa kuongeza utajiri wake kwa kuiuzia serikali jiwe la Tanzanite enye uzito wa kilo 6.3.
Laizer alipata umaarufu hivi karibuni, baada ya kugundua mamwe mawili ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 9.2 na kilo 5.8 na kuyauza kwa serikali kwa shilingi za Tanzania bilioni 7.8 (sawa na dola milioni 3.4) mwishoni mwa mwezi Juni.
Mwishoni mwa mwezi ulopita, Laizer pia aligundua jiwe jipya lenye kilo 6.3 ambalo litauzwa kwa mnada asubuhi ya leo.
Thamani ya jiwe hilo pia inatarajiwa kuwa ya juu. inatarajiwa kutangazwa na kumuongezea utajiri Bwana Laizer.
Inaaminiwa kuwa jiwe hili jipya la Tanzanite ni la pili kwa ukubwa kuwahi kuchimbwa. Jiwe la kwanza kwa ukubwa, lenye kilo 9.2, pia liligunduliwa na Laizer.
Kabla ya hapo jiwe ambalo liliaminika kuwa kubwa zaidi lilikuwa na kilo 3.3.
Karibu katika matangazo mubashara ya BBC Swahili leo Jumatatu ya Agosti Mosi.
