Hali ilivyokuwa Kenyatta alipotangazwa mshindi wa uchaguzi wa marudio Kenya

Bw Uhuru Kenyatta ametangazwa mshindi wa urais Kenya akiwa na kura 7,483,895 sawa na 98% na tume ya uchaguzi IEBC.

Moja kwa moja

  1. Kwaheri

    Hapo ndipo tunapohitimishia taarifa za moja kwa moja kuhusu matokeo ya uchaguzi wa marudio Kenya. Twakushukuru sana kwa kuwa nasi.

  2. Museveni ampongeza Kenya kwa ushindi wake

    Rais wa Uganda Yoweri Museveni amempongeza Rais Kenyatta baada yake kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa marudio wa urais.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  3. Odinga kutoa mwelekeo kwa wafuasi wake kesho

    Kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga, ambaye alisusia uchaguzi wa marudio wa Alhamisi wiki iliyopita, alikuwa ametarajiwa kutangaza mwelekeo kwa wafuasi wake baada ya tangazo la matokeo kufanywa na Bw Chebukati.

    Taarifa zinasema ameamua kufanya hivyo hapo kesho.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  4. Ruto: Tulipata zaidi ya tulivyoomba

    Naibu Rais William Ruto, akizungumzia ushindi wao uchaguzi wamarudio uliosusiwa na upinzani, amesema walipata zadi ya walivyokuwa wameomba kwa Mungu.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  5. Kenyatta: Tunaweza kuzungumza na upinzani baadaye

    Rais Kenyatta amesema atasubiri taratibu zote zikamilike, ikiwa ni pamoja na mahakama, kabla ya kushirikisha upinzani katika mustakabali wa nchi hiyo.

    Amesema ni haki yao kwenda mahakamani.

  6. Kenyatta: Wakenya wengi walitekeleza haki yao

    Bw Kenyatta amesema mpinzani wake Raila Odinga aliamua kutofuata uamuzi wa Mahakama ya Juu kwamba uchaguzi mpya wa urais ufanyike katika siku 60.

    Ameshutumu wanaosema kwamba idadi ya waliojitokeza walikuwa wachache uchaguzi wa sasa walikuwa wachache.

    Amesema takwimu zinaonesha vingine, asilimia 98 ya waliojitokeza walinipigia kura.

    Amesema ataendelea kufuata na kuiheshimu katiba na sheria.

  7. Kenyatta: Nilisikia kilio cha Wakenya na sikuidhinisha marekebisho ya sheria

    Bw Kenyatta kwa mara ya kwanza amekiri hadharani kwamba hakutia saini mswada wa marekebisho ya sheria za uchaguzi kuangazia baadhi ya mambo yaliyosababisha Mahakama ya Juu kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais wa Agosti.

    Amesema alisikia maoni ya waliopinga marekebisho hayo na waliokuwa wanayatazama kama juhudi za kujifaa binafsi.

    Bw Kenyatta alikuwa awali amesetangaza hadharani kwamba akipokea mswada huo wa marekebisho angeutia saini.

  8. Habari za hivi punde, Kenyatta: Nashukuru sana, Wakenya hawatachoka

    Rais Kenyatta, akihutubu baada ya kutangazwa mshindi, amewashukuru waliompigia kura.

    Amesema uchaguzi uliomalizika ni ishara ya uthabiti wa demokrasia na uthabiti wa taasisi za Kenya pamoja na Wakenya wenyewe.

    "Agosti 8, na sitachoka, Wakenya walirauka kupiga kura. Na siku hiyo walinichagua bila shaka. Ushindi wangu ulipopingwa Mahakama ya Juu, kwenye hukumu, mahakama haikupinga ushindi wangu wa 54%. Takwimu hazikupingwa. Kilichokosolewa ni utaratibu uliopelekea ushindi wangu," amesema.

  9. Habari za hivi punde, Chebukati: Kenyatta ndiye mshindi wa urais Kenya

    Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Wafula Chebukati amemtangaza rasmi Rais Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi wa marudio wa urais.

    Amesema ametimiza matakwa yote yanayohitajika kutimizwa na mgombea kabla ya kutangazwa mshindi.

    "Namtangaza Bw Uhuru Muigai Kenyatta na William Samoei Ruto kuwa rais mteule na naibu rais mteule mtawalia," amesema Bw Chebukati.

  10. Habari za hivi punde, Uhuru Kenyatta alipata kura 7,483,995

    Uhuru Kenyatta alipata kura 7,483,995, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Kenya Wafula Chebukati ametangaza.

    Matokeo kamili ya wagombea wote:

    • Uhuru Kenyatta Jubilee 7,483,895 (98.28%)
    • Raila Odinga (Alisusia) ODM 73,228 (0.96%)
    • Mohamed Abduba Dida ARK 14,107 (0.19%)
    • Japheth Kavinga Kaluyu Mgombea wa kujitegemea 8,261 (0.11%)
    • Michael Wainaina Mwaura Mgombea wa kujitegemea 6,007 (0.08%)
    • Joseph Nthiga Nyagah Mgombea wa kujitegemea 5,554 (0.07%)
    • John Ekuru Aukot Thirdway Alliance 21,333 (0.28%)
    • Cyrus Jirongo UDP 3,832 (0.05 %)
  11. Chebukati: Homa Bay hakuna matokeo yoyote

    Mwenyekiti wa IEBC anaendelea kusoma matokeo ya urais ya kila kaunti. Katika kaunti nne ambazo uchaguzi ulikuwa umeahirishwa baadhi ya maeneo, kuna kura zilizopatikana Migori na Kisumu.

    Lakini Homa Bay amesema hakuna matokeo yoyote.

    Kaunti
  12. Chebukati aanza kusoma matokeo

    Baada ya kupumua kwa muda, Bw Chebukati ameanza kusoma matokeo ya wagombea katika kila jimbo kati ya majimbo 47 pamoja na watu wanaoishi nje ya nchi.

    Ameanza na kura za jimbo la Mombasa.

  13. Chebukati: Siasa zikitatuliwa uchumi utaimarika

    Bw Chebukati amesema matatizo ya kisiasa yakitatuliwa Kenya, uchumi wake na wa wananchi utaimarika.

  14. 'Uchaguzi huu uwe wa mwisho kukumbwa na changamoto'

    Chebukati amesema inasikitisha kwamba kila wakati wa uchaguzi, shida zile zile hujirudia.

    Amesema kuna maswali ambayo atauliza na yakijibiwa shida hizo zitazuiwa.

    Kwanza ni kwa nini uchaguzi wa urais huwagawanya watu? Mbona kila wakati tume ya uchaguzi hulaumiwa?

    Tume za uchaguzi kwingine husifiwa na wanasiasa, mashirika ya kijamii na waangalizi.

  15. Chebukati: Waliotafuta gunia la kupiga, walilipata kwangu

    Bw Chebukati anasema alishangaa kwamba watu waliotafuta wa kushambulia walimwendea yeye.

    Hata hivyo, anasema ndani ya tume nao walimwogopa.

    "Hatutaweza kufurahisa kila mtu. Nimedumisha na kuheshimu sheria, kama mwanasheria ziwezi kuvunja sheria niliyojitolea kuilinda," amesema.

    Amewatakia watahiniwa wa mtihani wa darasa la nane ufanisi katika mtihani huo.

    Baadhi ya shule zilitumiwa kama vituo vya kupigia kura.

  16. Chebukati: Katika baadhi ya maeneo ilikuwa vigumu kuandaa uchaguzi

    Amesema katika baadhi ya maeneo, maeneo bunge 25, hali ya kiusalama ilizuia maafisa wa tume kuandaa uchaguzi.

    Kwingine, uchaguzi ulitatizwa na hali ya hewa, sana mafuriko.

  17. Chebukati: Nimeridhishwa mambo niliyotaka yalitimizwa

    Mwenyekiti wa IEBC amesema mambo aliyosema yalihitajika kufanyika kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki yalitimizwa.

    Amesema walitaka kuhakikisha kila kitu kilikuwa sawa.

    "Hata tulibadilisha tarehe kutoka 17 hadi 26 Oktoba kuhakikisha tuna muda wa kutosha," amesema.

    Kadhalika, amesema alikuwa na kundi la kusimamia mradi wa uchaguzi wa urais kuondoa majukumu kutoka kwa makamishna ambao walituhumiwa na baadhi ya wadau.

    "Naweza kusema kwa uhakika, kwamba 26 Oktoba kabla ya uchaguzi kuanza, nilikuwa nimeridhika kwamba tulikuwa tumefanya kila kitu kuhakikisha kila Mkenya angetekeleza haki yake kikatiba," amesema.

    "Na haki hii mtu anafaa kuitekeleza bila kutishiwa au kuzuiwa."

  18. Chebukati: Inasikitisha kwamba watu wameuawa

    Bw Chebukati amesema anasikitika sana kwa sababu kuna watu walifariki kutokana na mashindano ya kisiasa. Amewataka waliopo ukumbini kukaa kimya kwa muda kwa heshima ya waliouawa.

  19. Chebukati aanza kutoa taarifa yake ya matokeo

    Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amenza kutoa taarifa yake ya matokeo.

    Bomas
  20. Shughuli ya kutangazwa kwa matokeo yaanza

    Naibu mwenyekiti wa IEBC Consolata Nkatha amekaribisha rasmi wageni kwa kikao cha kutangazwa kwa mshindi wa urais wa uchaguzi uliofanyika tarehe 26 Oktoba.

    Shughuli inaanza kwa wimbo wa taifa.