Odinga na Kenyatta: Mambo yalivyokuwa siku ya Uchaguzi Mkuu Kenya 2017 tarehe 8 Agosti
Muungano wa upinzani nchini Kenya umepinga matokeo ya urais ambayo yamekuwa yakitangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi IEBC.
Moja kwa moja
Matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais kufikia sasa
Imepakiwa mnamo 21:15
Katika matokeo ya awali ya vituo 39620 out of 40883 yaliyopakiwa na IEBC mtandaoni:
Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 8009175 votes (54.31%)
Raila Odinga wa ODM ana kura 6608405 votes (44.81%)
Kura zilizoharibika kufikia sasa ni 393969
IEBC: Mfumo wetu wa matokeo haukudukuliwa
Tume ya uchaguzi nchini Kenya imesema kuwa mfumo wake wa kutoa matokeo haukudukuliwa kama ilivyodaiwa na upinzani.
Mkurugenzi mkuu wa tume hiyo Ezra Chiloba amesema kuwa madaia yaliotolkewa na mgombea wa upinzani Raila Odinga hayana msingi wowote.
Amesema kuwa tume hiyo imefanya uchunguzi kubaini hayo.
Ameongezea kuwa kufikia sasa wamepokea fomu 29,000 34A na kwamba wanatarajia fomu zote 40,000 kufikia kesho alfajiri.
Vilevile ameongezea kuwa upigaji kura umkamilika katika vituo vyote nchini
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mkurugenzi wa IEBC Ezra Chiloba
John Kerry na maafisa wa IEBC
Aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry akimsikiliza afisa mmoja wa uchagui nchini Kenya.
Wengine ni makamishna wa IEBC na wawakilishi wa vyama vya kisiasa.
Maelezo ya picha, John Kerry na maafisa wa IEBC
AU yapongeza IEBC kwa uchaguzi Kenya
Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC inaonekana ilitekeleza majukumu yake kulingana na sheria, mkuu wa kundi la waangalizi wa Umoja wa Afrika ,Thabo Mbeki amesema.
Mbeki ambaye alikuwa rais wa Afrika Kusini aliongezea kuwa mahakama ya Kenya imejiandaa kukabiliana na mgogoro utakaozuka katika uchaguzi huo.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amedai kwamba mfumo wa kidijitali wa tume hiyo ulidukuliwa , na matokeo kuvurugwa ili kumpatia ushindi rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Tume ya IEBC imeahidi kuchunguza madai hayo
Maelezo ya picha, Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki
Uchaguzi Kenya: Hakuna matokeo ya mwisho usiku wa leo
Tume ya uchaguzi nchini Kenya imewashauri raia kupuuzilia mbali madai ya uwongo yanayosambazwa kupitia ujumbe kwamba matokeo ya uchaguzi huo wa urais yatachapishwa usiku wa leo
Chanzo cha picha, Twitter
Maelezo ya picha, Ujumbe wa Twitter
Matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais kufikia sasa
Katika matokeo ya awali ya vituo 39091 kati ya 40883 yaliyopakiwa na IEBC mtandaoni:
Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 7,977,905 (54.32%)
Raila Odinga wa ODM ana kura 6,578,586 (44.79%)
Kura zilizoharibika kufikia sasa ni 387,959.
Mtu mmoja afariki katika maandamano Kenya
Mtu mmoja ameuawa katika makabiliano na maafisa wa polisi katika ngome ya upinzani ya Mathare katika mji mkuu wa Nairobi nchini Kenya, walioshuhudia wameambia BBC.
Risasi zilifyatuliwa wakati wa makabiliano hayo kulingana na walioshuhudia.
Kitengo cha habari cha AFP kilimnukuu afisa mmoja wa polisi aliyesema kuwa watu wawili waliuawa.
''Walikuwa miongoni mwa kundi la waandamanaji katika eneo hilo na maafisa walitumwa kuzima ghasia hizo'', afisa huyo aliambia AFP.
''Tumeambiwa kwamba wengi wao walikuwa wezi ambao walitumia fursa hiyo na hawakuweza hata kuwaheshimu polisi''.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesema kuwa uchaguzi huo umefanyiwa udanganyifu ili kumpokonya ushindi.
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Baadhi ya waandamanaji wanaopinga matokeo ya uchaguzi Kenya
Je fomu 34A na 34B ni zipi?
Kukataliwa kwa matokeo ya uchaguzi katika tovuti ya tume ya uchaguzi nchini Kenya kwa mara nyengine tena kumezua majina ya fomu zinazotumiwa katika kunakili matokeo ya uchaguzi.
Fomu zilizotajwa na mgombea wa upinzani wa Nasa Raila Odinga ni zile za 34A na 34B.
Katika kuyakataa matokeo hayo ya IEBC katika mtandao wake bwana Odinga alisema kuwa fomu 34A na 34B lazima zitolewe.
IEBC imesema kuwa maajenti wa mgombea huyo wa urais wataonyeshwa fomu 34A.
Je hizi ni fomu gani?
Chini ya sheria ya uchaguzi, fomu 34A ndio fomu ya kwanza inayotumika kunakili matokeo ya uchaguzi wa urais.
Fomu hiyo hujazwa na afisa wa tume ye uchaguzi anayesimamia uchaguzi huo kwa jina la Presiding officer baada ya kuhesabiwa kwa kura katika kituo cha kupigia kura.
Fomu hiyo huwa na maelezo kuhusu kura zilizohesabiwa za kila mgombea mbali na kuwa na idadi ya wapiga kura katika kituo hicho, kura zilizoharibika, zile zilizo na utata na kura zilizokubalika.
Mgombea ama ajenti wake baadaye hutakiwa kutia saini ili kuthibitisha kwamba yaliomo ndani ya fomu hiyo ni sahihi.
Kifungu cha 39 cha uchaguzi kinasema kuwa ili kufanyika kwa uchaguzi wa urais tume ya uchaguzi itatoa matokeo hayo kielektroniki baadaye kuyasafirisha kutoka katika kituo cha kupigia kura hadi katika kituo cha kuhesabia kura cha eneo bunge na baadaye katika kituo cha kitaifa cha kuhesabia kura.
Form 34A hupewa afisa anayesimamia uchaguzi katika eneo bunge ambaye hujaza fomu 34B.
Hutumika kuonyesha matokeo ya kura ya urais.
Fomu hiyo huonyesha nambari ya kituo cha kupigia kura, jina la kituo cha kupigia kura, idadi ya watu waliojisajiliwa kupiga kura katika kituo hicho, matokeo ya kila mgombea na idadi ya kura zilizokubalika.
Afisa anayesimamia shughuli ya uchaguzi katika eneo bunge kwa jina Returning officer humpelekea fomu hiyo mwenyekiti wa tume ya auchaguzi IEBC ambaye ndio afisa mkuu wa matokeo ya uchaguzi wa urais.
Katika mkutano na vyombo vya habari makamu wa mwenyekiti wa tume ya IEBC Consolata Maina amesema kuwa fomu hiyo ndio itabaini ni nani mshindi wa kura ya urais.
Sheria inaruhusu kuipata fomu 34B kutoka kwa kila Retuning officer kabla ya kutangaza matokeo.
''Utangazaji wa matokeo unategemea fomu 34B ambayo tutapata kutoka kwa Retuning Officers'', alisema bi Maina.
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati
Matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais kufikia sasa
Katika
matokeo ya awali ya vituo 39091 kati ya 40883 yaliyopakiwa na IEBC mtandaoni:
Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana
kura 7,915,044 (54.35%)
Raila Odinga wa ODM ana kura 6,520,918
(44.78%)
Kura zilizoharibika kufikia sasa
ni 387,959.
Tume ya uchaguzi yaweka wazi fomu za matokeo
Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Kenya imekubali kutoa fomu
za matokeo ya vituo vya kupigia kura maarufu kama Fomu 34A.
Muungano wa upinzani ulikuwa umelalamikia kukosekana kwa
fomu hizo na kusema ilikuwa vigumu kukagua matokeo yaliyokuwa yakipeperushwa
katika mtandao wa tume hiyo.
Mwenyekiti wa tume hiyo Bw Wafula Chebukati amewaambia
wanahabari kwamba meza maalum itatengwa katika kituo kikuu cha kujumlishia
matokeo ukumbi wa Bomas, Nairobi kwa ajili ya maajenti wa vyama ambao
wangependa kukagua fomu hizo
Aidha, ameongeza kwamba fomu hizo zitapakiwa kwenye tovuti
ya tume hiyo. Tayari baadhi zimeshapakiwa.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Polisi wakabiliana na waandamanaji Mathare
Tumepokea picha za polisi wa kupambana na fujo wakijaribu kuzima maandamano katika ngome ya upinzani katika mtaa wa Mathare, Nairobi.
Chanzo cha picha, Reuters
Chanzo cha picha, Reuters
Chanzo cha picha, Reuters
Polisi wamekuwa wakisaidia pia kuzima maandamano mjini Kisumu ambapo baadhi ya wakazi walikuwa wamefunga barabara na kuwasha moto matairi.
Chanzo cha picha, Reuters
Chanzo cha picha, Reuters
Chanzo cha picha, Reuters
Waziri apuuzilia mbali madai ya maandamano na fujo
Kaimu waziri wa usalama Dkt Fred Matiang'i amepuuzilia mbali taarifa ambazo amesema zinaenezwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna maandamano na fujo katika baadhi ya maeneo Kenya.
Amesema taarifa hizo hazina msingi wowote.
"Iwapo kungekuwa na jambo, mkuu wa polisi ndiye huyu hapa angekuwa wa kwanza kujua," amesema Dkt Matiang'i.
Mwandishi wa BBC Odeo Sirari aliyepo mjini Kisumu, magharibi mwa Kenya hata hivyo anasema muda mfupi uliopita polisi wamekabiliana na vijana waliokuwa wakiandamana katika barabara ya Manyatta katika mtaa wa Kondele na eneo la Kibos.
Amepiga picha hizi:
Chebukati: Tutachunguza madai ya Nasa kuhusu udukuzi
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amewaambia wanahabari baadaye kwamba wamepata habari kuhusu tuhuma za muungano huo wa upinzani kwamba mitambo yao ya uchaguzi ilidukuliwa.
Amesema tume haiwezi kupuuza tuhuma kama hizo na kwamba maafisa wake watafanya uchunguzi kubaini iwapo kuna ukweli wowote katika madai hayo.
Hata hivyo alieleza imani yake kwamba mfumo wa uchaguzi unaotumiwa na tume hiyo ni imara na kwamba ulitumiwa na shughuli zote za awali, na sasa "imesalia shughuli ya mwisho" ya kupeperusha na kutangaza matokeo ya kura.
Matokeo ya urais ya hivi punde zaidi Kenya
Katika
matokeo ya vituo 38249 kati ya 40883:
Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana
kura 7,757,201 (54.4%)
Raila Odinga wa ODM ana kura 6,380,316
(44.74%)
Kura zilizoharibika kufikia sasa
ni 353,389.
Odinga: Mitambo ya tume ya uchaguzi ilidukuliwa
Mgombea urais wa muungano wa upinzani Nasa Raila Odinga amewaambia wanahabari kwamba wamepata habari kwamba mitambo ya Tume ya Uchaguzi IEBC ilidukuliwa na matokeo halisi kufanyiwa ukarabati.
Bw Odinga, akiandamana na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka, na viongozi wengine wakuu wa muungano huo, amesema wadukuzi walitumia taarifa alizokuwa nazo meneja wa teknolojia wa IEBC Chris Msando aliyeuawa wiki moja iliyopita kuingia katika mitambo ya IEBC.
Waziri huyo mkuu wa zamani amesema baada ya kuingia, wadukuzi walitumia programu fulani kuongeza matokeo ya Rais Kenyatta na kupunguza matokeo yake.
Amesema anaamini hilo lilifanyika katika kaunti zote na kwamba wagombea wa NASA katika nyadhifa nyingine waliathirika pia.
Bw Odinga, amesema huo ulikuwa "ulaghai wa hali ya juu".
Hata hivyo, ametoa wito kwa wafuasi wa muungano huo waendelee kuwa watulivu.
Bw Musyoka amesema anawashauri wafuasi wa muungano huo waendelee na shughuli zao za kawaida, ingawa huenda karibuni wakatakiwa kuchukua hatua.
Bw Odinga na Kalonzo wamekataa kusema ni hatua gani zaidi watachukua na badala yake wakasema wanasubiri kusikia ufafanuzi kutoka kwa IEBC kuhusu yaliyotokea.
Jubilee yasema madai ya upinzani hayana ukweli
Katibu mkuu wa chama cha Jubilee chake Rais Uhuru Kenyatta, Bw Raphael Tuju, ameambia wanahabari kwamba madai ya muungano wa upinzani Nasa kwamba matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi IEBC hayaeleweki si ya kweli.
Bw Tuju amesema upinzani unafaa kukubali kwamba haukufanya vyema katika uchaguzi uliofanyika Jumanne.
Amesema katika kaunti zote ambazo Bw Kenyatta alishinda mwaka 2013, hakuna kaunti hata moja ambayo ameipoteza kwa upinzani.
Badala yake, amesema chama hicho kilifanikiwa kupata uungwaji mkono maeneo ambayo hakikufanya vyema uchaguzi uliopita mfano Nyamira na Kisii, wakati huu Jubilee walifanya vyema.
Upinzani ulikuwa umelalamika kwamba IEBC imekataa kutoa Fomu 34A za kuthibitisha matokeo ya urais kutoka vituo vya kupigia kura.
Lakini Bw Tuju amesema: "IEBC wamewezesha maafisa wetu wa kiufundi kupata Fomu 34A. Wanazichunguza kwa makini. sible for our technical team to access Form 34A. Fomu hizo ambazo tunazo, Nasa wanazo na IEBC wanazo zinafaa kuwa na maelezo sawa."
Matokeo ya urais ya hivi punde zaidi Kenya
Katika
matokeo ya vituo 36659 kati ya 40883:
Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana
kura 7,461,933 (54.64%)
Raila Odinga wa ODM ana kura 6,079,136
(44.51%)
Kura zilizoharibika kufikia sasa
ni 353,389.
Yasemavyo magazeti nchini Kenya
Wakenya wanapoendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumanne, hivi ndivyo vichwa vya habari vya magazeti vinavyosema:
Matokeo ya urais ya sasa hivi
Katika
matokeo ya vituo 35095 kati ya 40883:
Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana
kura 7,163,684 (54.82%)
Raila Odinga wa ODM ana kura 5,794,443
(44.34%)
Kura zilizoharibika kufikia sasa
ni 338,584
Wasimamizi wa uchaguzi wasubiri kuwasilisha matokeo Kisumu
Mwandishi wa BBC Odeo Sirari, ambaye amekuwa katika mji wa Kisumu, magharibi mwa Kenya anasema wasimamizi wa uchaguzi katika eneo bunge la Kisumu ya Kati bado wanasubiri kupeperusha matokeo ya kura kutoka eneo hilo.
Pichani hapa chini ni masanduku ya kupigia kura yakiwa katika kituo cha kujumlishia matokeo cha eneo bunge hilo katika shule ya upili ya Lions High.