Ajali ya ndege ya Korea Kusini yaua 179, wafanyakazi wawili waokolewa

Familia za waathiriwa zimekusanyika katika uwanja wa ndege huku mamlaka ikichunguza chanzo cha ajali hiyo.

Muhtasari

  • Rais anayeondoka wa Georgia akataa kujiuzulu huku mrithi wake akiapishwa
  • Katika picha: Familia zinaomboleza huku wafanyakazi wakitafuta mabaki
  • Moshi ukifuka wakati ndege iliyoangua inaungua
  • Kaimu rais awasili eneo la ajali
  • Boeing yatoa rambirambi zake
  • Shirika la ndege la Jeju Air laomba msamaha kwa ajali
  • Hii inaweza kuwa ajali mbaya zaidi ya ndege nchini Korea Kusini
  • Takriban watu 120 wafariki katika ajali ya ndege Korea Kusini

Moja kwa moja

Na Asha Juma

  1. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu kwa leo. Kwaheri.

  2. Habari za hivi punde, Abiria wote na wafanyakazi wanne walifariki katika ajali ya ndege

    Tumepata uthibitisho kuwa watu 179 waliokuwemo kwenye ndege hiyo wamefariki.

    Kuna watu wawili walionusurika - wote ni wafanyikazi wa ndege ambao waliokolewa kutoka kwa mabaki na kupelekwa hospitalini.

    Hiyo ina maana kwamba abiria wote 175 wa ndege hiyo walifariki dunia katika ajali hiyo, pamoja na wafanyakazi wanne wa ndege hiyo.

  3. Rais anayeondoka wa Georgia akataa kujiuzulu huku mrithi wake akiapishwa

    .

    Chanzo cha picha, Reuters/EPA

    Maelezo ya picha, Mikheil Kavelashvili (kushoto) aliapishwa kama rais wa Georgia, Salome Zourabichvili (kulia) Rais anayemaliza muda wake

    Maelfu ya wananchi wa Georgia wameandamana katika mji mkuu wa Tbilisi huku rais mpya wa chama tawala cha Georgian Dream party akiapishwa.

    Mikheil Kavelashvili, mchezaji soka wa zamani, ameapishwa katika kipindi kigumu cha kisiasa nchini humo baada ya serikali kusitisha ombi lake la kujiunga na Umoja wa Ulaya.

    Georgian Dream kilishinda uchaguzi wa bunge mwezi Oktoba, lakini ushindi huo uligubikwa na madai ya udanganyifu ambayo tangu wakati huo yamesababisha maandamano mitaani.

    Rais anayemaliza muda wake Salome Zourabichvili alikataa kujiuzulu siku ya Jumapili, akisema ndiye "rais pekee halali".

    Akihutubia umati uliokusanyika nje, Zourabichvili alisema ataondoka ikulu ya rais lakini akamtaja mrithi wake kuwa haramu.

  4. Katika picha: Familia zinaomboleza huku wafanyakazi wakitafuta mabaki

    Siku nzima tumekuwa tukipokea picha mpya kutoka eneo la ajali huko Muan, Korea Kusini.

    Jamaa za waliofariki kwenye ajali hiyo wamekusanyika kwenye uwanja wa ndege.

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

  5. Moshi ukifuka wakati ndege iliyoangua inaungua

    Maelezo ya video, Picha za mashuhuda zinaonyesha wazima moto wakikaribia ndege inayoungua nchini Korea Kusini

    Tumepokea picha kutoka kwa mtu aliyeshuhudia, zikionyesha moshi ukifuka kutoka kwa ndege inayoungua, wazima moto wanapowasili kwenye eneo la tukio.

  6. Kaimu rais awasili eneo la ajali

    .

    Chanzo cha picha, EPA/Yonhap

    Kaimu Rais wa Korea Kusini Choi Sang-mok amefika katika eneo la ajali, ofisi ya rais inasema.

    Choi alitoa mwelekeo wa kutoa wafanyikazi, huduma ya afya na vifaa vya kusaidia katika juhudi za uokoaji, ofisi inasema.

    Serikali itafanya yote iwezayo kusaidia familia zilizofiwa, inaongeza.

    Choi aliteuliwa kuwa kiongozi wa muda wa nchi hiyo siku ya Ijumaa baada ya aliyekuwa kaimu rais kuondolewa madarakani kutokana na mzozo wa kisiasa unaoendelea.

  7. Boeing yatoa rambirambi zake

    Kampuni ya kutengeneza ndege ya Boeing imetoa rambirambi zake na kusema inawasiliana na Jeju Air ya Korea Kusini baada ya kutokea kwa ajali mbaya ya ndege.

    Ajali hiyo ilihusisha ndege aina ya Boeing 737-800, kulingana na Jeju Air.

  8. Shirika la ndege la Jeju Air laomba msamaha kwa ajali

    .

    Chanzo cha picha, EPA/Yonhap

    Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ndege la Jeju Air ameomba msamaha hadharani kwa waathiriwa wa ajali hiyo.

    Katika mkutano mfupi wa wanahabari, Kim E-bae na wakuu wengine wa kampuni waliinamisha vichwa vyao na kusema kuwaunga mkono wafiwa ndio kipaumbele chao kwa sasa.

    "Sisi Jeju Air tunainamisha vichwa vyetu kwa kuomba msamaha kwa kila mtu ambaye ameathirika katika tukio hili kwenye Uwanja wa Ndege wa Muan," inasema taarifa hiyo ambayo imetafsiriwa kwa Kiingereza.

    "Tutafanya kila tuwezalo kujibu tukio hilo. Tunasikitika kwa mfadhaika."

    Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana, lakini vyombo vya habari nchini humo viliripoti kuwa huenda ilisababishwa na ndege kukamatwa kwenye mfumo wa ndege hiyo.

    Ajali hii ya kwanza mbaya katika historia ya Jeju Air, mojawapo ya mashirika makubwa ya ndege ya bei ya chini ya Korea Kusini, ambayo ilianzishwa mwaka 2005.

  9. Hii inaweza kuwa ajali mbaya zaidi ya ndege nchini Korea Kusini

    Jean Mackenzie

    Mwanahabari wa Seoul

    Ajali hii si ya kawaida kwa Korea Kusini, ambayo imekuwa na rekodi nzuri ya usalama wa ndege katika miaka ya hivi karibuni.

    Ikiwa idadi ya vifo itathibitishwa, hii itakuwa ajali mbaya zaidi ya ndege kuwahi kutokea katika ardhi ya Korea Kusini.

    Inaonekana pia kuwa ajali mbaya pekee ambayo Jeju Air imepata katika historia yake ya karibu miaka 20.

    Jeju Air ndilo shirika maarufu la ndege la bei nafuu nchini Korea Kusini, lenye safari nyingi za ndege katika eneo lote la Asia.

    Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo alisema katika mkutano na wanahabari hapo awali shirika hilo la ndege halikuwa na historia ya ajali. Aliomba msamaha kwa familia za waathiriwa.

  10. Takriban watu 120 wafariki katika ajali ya ndege Korea Kusini

    .

    Chanzo cha picha, Reuters/Yonhap

    Ndege iliyokuwa imebeba abiria 181 imeanguka katika uwanja wa ndege kusini magharibi mwa Korea Kusini.

    Ajali hiyo ilitokea muda mfupi baada ya 09:00 saa za eneo - 00:00 GMT - wakati ilipokuwa ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muan.

    Picha zinaonekana kuonyesha ndege hiyo ikiteleza kutoka kwenye njia ya kurukia na kuangukia ukuta, kabla ya baadhi ya sehemu zake kuwaka moto.

    Shirika la Kitaifa la Zimamoto limethibitisha sasa kwamba watu 167 walifariki katika ajali hiyo ya ndege.

    Hapo awali, tulisikia pia kwamba wafanyikazi wawili wa ndege walipatikana wakiwa hai na kusafirishwa hadi hospitalini.

    Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Muan wa ukubwa wa kati ulifunguliwa mwaka wa 2007, na una njia za kwenda nchi kadhaa za Asia.

  11. Hujambo na karibu.