Moja kwa moja, Meli nyengine ya kubeba mafuta yashambuliwa katika mlango bahari wa Hormuz

Shirika la Uingereza la Operesheni za Biashara ya Baharini (UKMTO) limetangaza kuwa meli nyengine ya kubeba mafuta katika Lango la Hormuz imeshambuliwa

Muhtasari

  • Kampuni yatoa zawadi kumtafuta aliyeiba lori zima la bia
  • Mgomo wa wafanyakazi katika uwanja wa JKIA Nairobi wasitishwa
  • Aliyekuwa kiongozi wa genge la Crips apatikana na hatia ya mauaji ya Tupac Shakur
  • Meli nyengine ya kubeba mafuta yashambuliwa katika mlango bahari wa Hormuz
Ruka Video uendelee
  • xx
  • Besigye
  • .
  • xx
  • xx
  • xx
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • Dangote

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu

  1. Iran yaliandikia barua Baraza la Usalama kufuatia shambulio la Marekani mjini Lark

    Siku ya Jumatatu, balozi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, kupitia barua rasmi kwa Katibu Mkuu wa umoja huo, alilaani shambulio jipya la Marekani dhidi ya Kisiwa cha Lark na kuonya kwamba: "Marekani na pande zote zinazosaidia, kuwezesha, kuunga mkono, au kushiriki kwa namna yoyote ile katika maandalizi, utekelezaji, au kufanyika kwa vitendo vya uchokozi na vitendo vingine haramu vya Marekani, zitawajibika kikamilifu kwa matokeo mabaya ya vitendo hivyo haramu, ikiwa ni pamoja na uharibifu na hasara zote zinazotokana navyo, hasa madhara makubwa yaliyowapata wananchi wa Iran."

    Makao Makuu ya Jeshi la Iran pia yaliyaonya mataifa ya eneo hilo siku ya Jumatatu kwamba, iwapo mashambulio ya Marekani dhidi ya nchi hiyo yangeanzishwa au kufanywa kutokea katika ardhi yao, Jeshi la Iran lingejibu kwa kulenga "chanzo cha mashambulio hayo" kupitia operesheni za kijeshi.

    Barua ya Iran ya siku ya Jumatatu kwa Baraza la Usalama ilisema: "Iran pia inatoa wito kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama kuitaka Marekani kusitisha na kukomesha mara moja ukiukaji wake wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa pamoja na vitendo vyake vya uchokozi vinavyotishia uhuru wa usafiri wa majini na usalama wa baharini katika Ghuba ya Uajemi na Lango la Hormuz."

  2. Kampuni yatoa zawadi kumtafuta aliyeiba lori zima la bia

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kampuni ya kutengeneza bia ya Pabst Brewing Company imegeukia mitandao ya kijamii kuomba msaada wa kutafuta maelfu ya makopo ya bia yake ya Pabst Blue Ribbon (PBR) yaliyoibwa kutoka kituo cha usambazaji huko California.

    "TUMEIBIWA," kampuni hiyo ilitangaza. "Kwa mwizi huyo: hatukulaumu kwa kutaka kujivunia kwa marafiki zako kuhusu kiasi kikubwa cha bia ya PBR ulicho nacho, tunatamani tu ungeipata kwa njia halali na ya heshima."

    Kwa mujibu wa polisi, mtuhumiwa aliwasilisha nyaraka bandia katika kituo cha usambazaji cha Anheuser-Busch mjini Montclair na kufanikiwa kuondoka na mzigo wa bia wenye thamani ya dola za Marekani 25,000 (takriban pauni 18,500), ambao ulikuwa umepangwa kupelekwa San Diego.

    Pabst imesema "inafuatilia kwa karibu sana" tukio hilo ambalo imeeleza kuwa ni "la kushangaza na la kipuuzi", na sasa inatoa zawadi kwa yeyote atakayesaidia kupatikana kwa bia hiyo yenye uzito wa pauni 40,000 (sawa na kilo 18,144).

    Polisi wa Montclair walisema kuwa huo ulikuwa wizi wa pili kutokea siku hiyo hiyo katika kituo hicho hicho cha usambazaji. Wapelelezi wanachunguza iwapo matukio hayo mawili yalikuwa sehemu ya operesheni moja ya uporaji wa mizigo kwa kutumia nyaraka za udanganyifu.

    Katika tukio la kwanza, mzigo wenye thamani ya dola 45,000 (takriban pauni 33,000) uliokuwa ukielekea Tucson, Arizona, ulichukuliwa tarehe 17 Agosti lakini haukuwahi kufika ulipokusudiwa hata baada ya wiki mbili.

    Saa moja baadaye, polisi wanasema kuwa wezi walitumia nyaraka bandia kuchukua mzigo wa bia ya Pabst Blue Ribbon.

    "Wachunguzi wamebaini kufanana kwa matukio haya mawili," polisi walisema. "Taarifa zilizotolewa kuhusu kampuni ya usafirishaji, dereva na magari yaliyohusika zina dosari na tofauti zinazoshukiwa, na kwa sasa zinaendelea kuchunguzwa."

  3. Mgomo wa wafanyakazi katika uwanja wa JKIA Nairobi wasitishwa

    .
    Maelezo ya picha, Wasafiri walikwama katika uwanja wa JKIA kufuatia mgomo uliotatiza safari za ndege

    Wadau wa sekta ya uchukuzi, wakiongozwa na Waziri wa Uchukuzi Davis Chirchir, wanasema wafanyakazi wa sekta ya anga wamekubali kusitisha mgomo baada ya kufikia mwafaka wa kurejea kazini, hatua inayofungua njia kwa shughuli kurejea katika hali ya kawaida.

    Mgomo huo, ulioanza tarehe 30 Agosti 2026, ulisababisha ucheleweshaji wa zaidi ya saa sita na kufutwa kwa safari nyingi za ndege, na kuwaacha maelfu ya wasafiri wakiwa wamekwama.

    Wafanyakazi walilalamikia masuala ikiwemo makubaliano ya pamoja yaliyokwama, wasiwasi wa kuajiri wafanyakazi, na mapendekezo ya mabadiliko ya usimamizi wa uwanja wa ndege.

    Kufuatia makubaliano hayo Muungano wa wafanyakazi hao KAWU tayari umewataka kurudi kazini mara moja .

    "Tunasitisha mgomo wetu na kuwaomba wanachama wetu kuanza mchakato wa kurejesha shughuli na huduma katika hali ya kawaida," Ndiema aliambia mkutano na waandishi wa habari. "Kwa wale walio kazini, tunawaomba waanze kushughulikia safari za ndege." alisema Mkuu wa chama cha wafanyakazi wa sekta ya anga.

    Kwa sasa shughuli za uwanja wa ndege zinaendelea kurejea katika hali ya kawaida, ingawa abiria wanashauriwa kuthibitisha ratiba moja kwa moja na mashirika yao ya ndege.

    Mgomo huo, uliohusisha hasa maafisa wa kudhibiti usafiri wa anga siku ya Jumapili na Jumatatu, ulivuruga safari kadhaa za ndege zinazoingia na kutoka katika Uwanja Mkuu wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, huku ucheleweshaji ukisambaa hadi kwenye viwanja vya ndege vya kanda hiyo katika Afrika Mashariki na maeneo mengine.

  4. Aliyekuwa kiongozi wa genge la Crips apatikana na hatia ya mauaji ya Tupac Shakur

    .

    Chanzo cha picha, AFP via Getty

    Aliyekuwa kiongozi wa genge la uhalifu, Duane "Keffe D" Davis, amepatikana na hatia ya kupanga mauaji ya Tupac Shakur – hii ikiwa ni hukumu ya kwanza katika kesi ya muda mrefu ambayo haikutatuliwa na iliyowavutia mashabiki wa muziki wa hip-hop kwa karibu miaka 30.

    Baraza la wazee wa mahakama lilimkuta Davis na hatia ya shtaka moja la mauaji kwa kutumia silaha hatari kuhusiana na kifo cha nyota huyo wa rap, aliyeuawa kwa kupigwa risasi kutoka kwenye gari linaloenda kasi jijini Las Vegas mnamo tarehe 7 Septemba 1996.

    Akiwa amevaa suti nyeusi, mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 63 alisimama bila kuonyesha hisia zozote mahakamani huko Las Vegas wakati hukumu ikisomwa, kabla ya kusema kuwa atakata rufaa.

    Jamaa wa Shakur walishikana mikono, huku baadhi yao wakikumbatiana na kulia.

    Shakur alikuwa na umri wa miaka 25 alipouawa akiwa katika kilele cha taaluma yake kama mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa katika muziki wa rap.

    Amefanikiwa kuuza zaidi ya rekodi milioni 75 duniani kote.

  5. Meli nyengine ya kubeba mafuta yashambuliwa katika mlango bahari wa Hormuz

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Shirika la Uingereza la Operesheni za Biashara ya Baharini (UKMTO) limetangaza kuwa meli nyengine ya kubeba mafuta katika Lango la Hormuz imeshambuliwa.

    Kulingana na ripoti hiyo, meli hiyo ililengwa "wakati ikipita na kutoka katika Lango la Hormuz."

    Shirika hilo la Uingereza limesema tukio hilo lilitokea kilomita 31 mashariki mwa eneo la Khasab nchini Oman, likihusisha "makombora matatu ambayo hayakutambulika."

    Hakuna ripoti za majeruhi au vifo kutokana na shambulio hilo kufikia sasa.

    Saa moja kabla ya ripoti hiyo kutolewa, vyanzo vya habari visivyo rasmi nchini Iran viliripoti kuwa makombora matatu yalikuwa yamerushwa kutoka pwani ya kusini mwa Iran.

    Kama tulivyotangaza hapa muda mfupi uliopita, Mamlaka ya Uingereza ya Operesheni za Meli za Biashara ilitangaza tukio jingine la baharini siku ya Jumatatu, lakini ilibainisha kuwa tukio hilo katika Bahari ya Hindi lilitokea siku ya Jumapili, tarehe 30 Agosti.

  6. Natumai hujambo na karibu katika habari zetu za moja kwa moja