Vita vya Ukraine: Urusi yaanzisha mashambulizi mapya ya ndege zisizo na rubani huko Kyiv na Kharkiv, maafisa wasema

Ukraine imeshambuliwa tena na ndege zisizo na rubani za Urusi, maafisa wanasema, baada ya siku mbili za mashambulizi makubwa ya angani ya pande zote mbili.

Moja kwa moja

Lizzy Masinga

  1. Benjamin Kiplagat: Mwanariadha wa Uganda adungwa kisu hadi kufa nchini Kenya - ripoti

    Benjamin Kiplagat aliiwakilisha Uganda katika Michezo mitatu ya Olimpiki

    Chanzo cha picha, AFP

    Benjamin Kiplagat, ambaye ameiwakilisha Uganda kwenye Michezo mitatu ya Olimpiki, amepatikana akiwa amefariki nchini Kenya, huku ripoti za ndani zikisema kuwa alidungwa kisu.

    Kiplagat, 34, alifika nusu-fainali ya Olimpiki ya London 2012 katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi.

    Inasemekana alipatikana kwenye gari akiwa na majeraha ya kuchomwa kisu kifuani na shingoni, karibu na mji wa Eldoret nchini Kenya, unaojulikana kama kituo cha mazoezi ya wanariadha.

    Polisi wa Kenya wanasema wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo chake.

  2. Uchaguzi DRC 2023: Matokeo yatarajiwa hivi karibuni huku Rais Felix Tshisekedi akiongoza

    Mamilioni ya watu walipanga foleni kwa saa nyingi kabla ya kuweza kupiga kura

    Chanzo cha picha, AFP

    Matokeo ya uchaguzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yanatarajiwa hivi karibuni, huku Rais Félix Tshisekedi akifurahia kuongoza dhidi ya wagombea wa upinzani ambao wamedai uchaguzi urudiwe.

    Rais Tshisekedi amepata takribani 72% ya kura hadi sasa, na anaonekana kujiandaa kwa muhula wa pili.

    Uchaguzi wa Desemba 20 ulikumbwa na matatizo mengi ya vifaa. Ilibidi iongezwe hadi siku ya pili katika sehemu fulani za nchi.

    Takribani theluthi mbili ya vituo vya kupigia kura vilichelewa kufunguliwa, wakati asilimia 30 ya mashine za kupigia kura hazikufanya kazi, kwa mujibu wa waangalizi wa uchaguzi.

    Mamilioni ya watu walisubiri kwa saa nyingi kabla ya kupiga kura, huku wengine wakikata tamaa na kurudi nyumbani.

    Upinzani ulisema matatizo hayo ni sehemu ya mpango wa makusudi wa kuruhusu matokeo kuchakachuliwa ili kumpendelea Bw Tshisekedi.

    Mkuu wa tume ya uchaguzi hapo awali alisema wagombea wa upinzani wanataka uchaguzi mpya kwa sababu "wanajua walishindwa... ni walishindwa vibaya". Mkuu wa uchaguzi Denis Kadima alikiri kuwepo kwa dosari kadhaa lakini akasisitiza kuwa matokeo yaliyotangazwa hadi sasa yanaakisi matakwa ya watu wa Congo. Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta, tayari amechapisha ujumbe kwenye ukurasa wake wa X akimpongeza Bw Tshisekedi kwa kuchaguliwa tena.

  3. Meli ya kivita ya Marekani yadungua makombora ya Houthi kutoka Yemen katika Bahari Nyekundu

    USS Gravely ilidungua makombora mawili ya balistiki yaliyorushwa kutoka maeneo yanayodhibitiwa na Houthi nchini Yemen

    Chanzo cha picha, US NAVY

    Meli ya kivita ya Marekani imetungua makombora mawili yaliyorushwa kutoka Yemen, baada ya kuitikia wito wa msaada kutoka kwa meli iliyokuwa imepigwa katika Bahari Nyekundu.

    A US Navy admiral told AP it is the first successful strike since a global patrol was launched on 18 December.

    Amiri wa Jeshi la Wanamaji wa Marekani aliiambia AP kuwa ni shambulio la kwanza lenye mafanikio tangu doria ya kimataifa kuanza mnamo 18 Desemba.

    Wahouthi wamekuwa wakishambulia meli katika Bahari Nyekundu tangu Novemba.

    Kundi la waasi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran wamedai kuwa mashambulizi yake kwenye njia muhimu ya meli yanalenga meli zinazohusishwa na Israel, ili kukabiliana na vita huko Gaza.

    Meli ya kibiashara iliyoshambuliwa, Maersk Hangzhou, imesajiliwa kwa Singapore na inaendeshwa na kumilikiwa na kampuni ya Denmark, Kamandi Kuu ya Marekani (Centcom) ilisema katika taarifa.

    Centcom ilisema wakati meli hizo zilipokuwa zikiitikia wito huo, makombora mawili ya kuzuia meli yalirushwa kutoka maeneo yanayodhibitiwa na Wahouthi katika jozi za meli za jeshi la wanamaji la Marekani.

    USS Gravely iliharibu makombora ya masafa marefu, Centcom ilisema, na kuongeza kuwa ni "shambulio haramu la ishirini na tatu la Houthi kwenye meli za kimataifa" tangu 19 Novemba.

  4. Korea Kaskazini imesema itarusha satelaiti tatu mpya za kijasusi mwaka 2024

    Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alizungumza Jumapili wakati mkutano wa kila mwaka

    Chanzo cha picha, Reuters

    Korea Kaskazini inapanga kurusha satelaiti nyingine tatu za kijasusi mwaka ujao kama sehemu ya juhudi za kuimarisha jeshi lake, vyombo vya habari vya serikali ya nchi hiyo vimesema.

    Mwezi uliopita Pyongyang iliweka satelaiti ya kijasusi angani na inadai kuwa tangu wakati huo imepiga picha maeneo makubwa ya kijeshi ya Marekani na Korea Kusini.

    Akielezea malengo yake ya 2024, Kim Jong Un pia alisema kuwa shughuli zake na Korea Kusini zitapata "mabadiliko ya kimsingi".

    Na alisema hakuwa na namna ila kusonga mbele na matarajio yake ya nyuklia.

    Akizungumza katika mkutano wa mwisho wa mwaka wa Chama tawala cha Wafanyakazi cha Korea, Bw Kim alisema kuungana na Korea Kusini sasa haiwezekani tena.

    Alisema Seoul inachukulia nchi yake kama adui. Inaonekana kuwa ni mara ya kwanza kwa Bw Kim kusema jambo kama hilo na kuashiria mabadiliko rasmi katika sera, ingawa kiutendaji kumekuwa na matarajio madogo ya kuungana kwa miaka kadhaa, bila mafanikio na juhudi kidogo kufanywa.

    Uhusiano kati ya nchi hizo mbili uko katika hali mbaya.

    Mwezi uliopita, baada ya kurushwa kwa satelaiti ya kijasusi, Pyongyang ilivunja makubaliano na Seoul ambayo yalilenga kupunguza mvutano wa kijeshi.

    Korea Kaskazini pia iliendelea na majaribio ya mara kwa mara ya makombora yake mwaka mzima wa 2023 na mapema mwezi huu ilirusha kombora lake la juu zaidi la masafa marefu, na kukaidi vikwazo vya Umoja wa Mataifa.

    Kurushwa kwa kombora la balestiki linalovuka mabara, ambalo lina masafa ya kufika katika bara la Amerika Kaskazini, kulizua shutuma za mara moja kutoka Magharibi.

    Wakati huo huo Korea Kaskazini haijafurahishwa na Korea Kusini kuimarisha ushirikiano wa kiulinzi na Marekani, baada ya manowari ya Marekani yenye silaha za nyuklia kufika katika maji yake.

  5. Vita vya Ukraine: Urusi yaanzisha mashambulizi mapya ya ndege zisizo na rubani huko Kyiv na Kharkiv, maafisa wasema

    Urusi imekuwa ikiipiga Kharkiv katika siku za hivi karibuni

    Chanzo cha picha, Reuters

    Ukraine imeshambuliwa tena na ndege zisizo na rubani za Urusi, maafisa wanasema, baada ya siku mbili za mashambulizi makubwa ya angani ya pande zote mbili.

    Kuna ripoti za milipuko huko Kyiv na Kharkiv, ambapo meya alisema majengo ya makazi yameteketea.

    Moscow imekuwa ikilipiza kisasi dhidi ya mashambulio ya Ukraine kwenye mji wa mpakani wa Urusi wa Belgorod siku ya Jumamosi, na kusababisha vifo vya takribani watu 20.

    Hayo yanajiri baada ya Urusi kufanya mashambulizi kote Ukraine siku ya Ijumaa.

    Mashambulizi hayo, ambayo yalisababisha vifo vya watu 39, yalielezewa na Kyiv kama shambulio kubwa la makombora la Urusi hadi sasa.

    Mashambulizi ya hivi karibuni yalitokea Ukraine ilipoingia siku yake ya mwisho ya 2023.

    Mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine katika eneo linalozunguka mji mkuu wa Kyiv ilishirikiana Jumamosi kuzima shambulio la ndege zisizo na rubani za Urusi, utawala wa kijeshi wa eneo hilo ulisema kwenye Telegram.

    Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yameripotiwa katika mji wa kaskazini-mashariki wa Kharkiv, meya Ihor Terekhov alisema kwenye Telegram.

    "Katika usiku wa Mwaka Mpya, Warusi wanataka kutisha jiji letu, lakini hatuogopi - hatuwezi kuvunjika na hatuwezi kushindwa."

    Kiwango cha uharibifu hakiko wazi na hakuna majeruhi wameripotiwa bado.

    Mapema Jumamosi, shambulio la Urusi lilijeruhi 19 huko Kharkiv, serikali ya eneo hilo iliripoti.

  6. Habari, karibu katika taarifa zetu za moja kwa moja