Tanzania yasisitiza msimamo wake kuhusu GMO

Imesem itaendeleza tafiti mbalimbali juu ya mbegu zilizobadilishwa vinasaba (GMO) ili kujifunza na kuijua zaidi.

Moja kwa moja

  1. Baada ya kukosolewa vikali waandaji wa Tuzo za Nobel waziondoa Urusi, Belarus na Iran

    Nobel

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Taasisi ya tuzo za Nobel imebatilisha uamuzi wake wa awali uliokosolewa sana wa kuzialika Urusi, Belarus na Iran kwenye sherehe za tuzo za mwaka huu huko Stockholm.

    "Tunatambua maoni na muitikio mkubwa nchini Sweden," Taasisi hiyo ilisema. Urusi na mshirika wake Belarus hawakualikwa mwaka jana kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, huku Iran ikiachwa nje kutokana na rekodi yake ya haki za binadamu. Ukraine ilikosoa uamuzi wa mwaka huu na kupongeza uamuzi mpya wa Jumamosi wa kuziondoa nchi hizo ikisema ni "ushindi kwa masuala ya binadamu".

    Sherehe ya tuzo hizo zinafanyika mjini Stockholm tarehe 10 Desemba - siku ya kumbukumbu ya kifo cha Alfred Nobel, mtu aliyeanzisha Taasisi hiyo.

  2. Israel kuwatimua wahamiaji wa Eritrea kufuatia ghasia za Tel Aviv

    Israel

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Israel inafikiria kuchukua hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwafukuza mara moja wahamiaji wa Eritrea waliohusika na ghasia mjini Tel Aviv siku ya Jumamosi.

    Takriban watu 170 walijeruhiwa katika makabiliano makali na polisi na mapigano kati ya makundi ya wafuasi na wapinzani wa utawala wa Eritrea.

    Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alisema wao hao wamevuka mipaka. Pia aliamuru mpango mpya wa kuwaondoa wahamiaji wote wa Kiafrika ambao aliwataja kama "wahamiaji haramu". Machafuko ambayo hayajawahi kutokea siku ya Jumamosi yalianza baada ya wanaharakati wanaoipinga serikali ya Eritrea kusema kuwa wameziomba mamlaka za Israel kufuta tukio lililoandaliwa na ubalozi wa nchi yao.

    Walivunja kizuizi cha polisi karibu na ukumbi huo, ambao pia uliharibiwa. Polisi waliokuwa wamejihami walirusha mabomu ya machozi, maguruneti na kufyatua risasi huku maafisa waliokuwa wamepanda farasi wakijaribu kuwasukuma waandamanaji hao.

    Uchunguzi umeanza kubaini iwapo matumizi ya silaha za moto yalikuwa ndani ya sheria.

  3. Ruto 'avunja itifaki' kwa kujiendesha mwenyewe kwa gari dogo la umeme

    Ruto

    Chanzo cha picha, Ruto Twitter

    Mkuu wa Nchi alichapisha video ya moja kwa moja ya dakika 2 akiendesha gari ya umeme aina ya MG Comet yenye viti viwili mpaka KICC ambapo maandalizi ya Mkutano wa Hali ya Hewa Afrika yalikuwa yakiendelea.

    Rais aliandamana tu na pikipiki chache za usalama, katika msafara wake wa kawaida huwa na magari zaidi ya 10 na pikipiki tano za usalama.

    Kwa itifaki Rais anapaswa kuendeshwa na kuandamana na ulinzi wakutosha kwa usalama wake.

    Msemaji wa Ikulu Hussein Mohammed, katika taarifa yake, alibainisha kuwa Mkuu wa nchi alifanya chaguo lisilopendeza la kuonyesha dhamira yake ya kubariki magari ya umeme.

    "Rais Ruto anaongoza kwa mfano, kujiendesha hadi KICC kwa gari la umeme ili kuungana na Vijana wa Afrika kuhusu tamko lao la hali ya hewa kabla ya Mkutano wa Kilele wa Hali ya Hewa barani Afrika hapo kesho," alisema Mohammed.

    Mkutano huo unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 4 hadi Septemba 6, 2023, ukijikita katika kushughulikia athari za kimataifa na za Kiafrika za mabadiliko ya hali ya hewa. Rais Ruto ambaye anatazamiwa kuwa mwenyeji wa wakuu 24 wa nchi, amethibitisha kuwa hatua za haraka zinahitajika ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  4. Tanzania yasisitiza msimamo wake kuhusu GMO

    Bashe

    Chanzo cha picha, Wizara Kilimo

    Serikali ya Tanzania imesisitiza kwamba nchi hiyo haipo tayari kutumia mbegu zilizobadilishwa vinasaba (GMO) kwa shughuli zake za kilimo kwa sasa.

    Hayo yamebainishwa leo Septemba 03, 2023 Ikulu na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe mbele ya waandishi wa habari kuelekea mkutano wa kimataifa kuhusu mifumo ya chakula (AGRF).

    Mkutano huo untarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 4 hadi 8, 2023, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na zaidi ya watu 3,000 kutoka nchi zaidi ya 70 duniani.

    Hata hivyo Waziri Bashe amesema Tanzania hawapingi wazo la kufanya utafiti kuhusu GMO ili kuangalia namna gani inaweza kunufaika na hilo na kukuza uzalishaji kwenye sekta ya kilimo nchini humo.

    Kuhusu kuanzisha maabara aliligusia pia mwezi Januari, 2023 wakati akizungumza na waandishi na wadau wa sekta ya kilimo kuhusu utekelezaji wa Agenda ya 10/30, ambapo Waziri Bashe alisema Serikali itatenga maabara mbili ili kuendelea kujifunza na kuepuka kutumia kitu wasichokijua.

    Alisema wataendeleza tafiti mbalimbali juu ya mbegu zilizobadilishwa vinasaba (GMO) ili kujifunza na kuijua zaidi.

    Kumekuwa na mjadala mkubwa duniani kuhusu matumizi na athari za GMO ambayo ni mazao yaliyobadilishwa vinasaba, au mazao yaliyoundwa na vinasaba vilivyofanyiwa uhandisi jeni.

    Wapo wanayoitaja ni salama na wapo wanaotaja kuwa na athari kwa binadamu, wanyama na mazingira kwa ujumla.

  5. Gitaa la mwaka 1961 lasakwa dunia nzima

    Höfner

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mpango wa kulitafuta ala maarufu zaidi duniani - gitaa asilia la Höfner la besi la msanii Paul McCartney.

    Mapngo huo unaoitwa The Lost Bass Project inatafuta maelezo kuhusu kile inachoeleza kama "besi muhimu zaidi katika historia".

    McCartney alinunua chombo hicho kwa dola $38 huko Hamburg, Ujerumani, mwaka 1961, lakini kilipotea miaka minane baadaye.

    Gitaa hilo lilitumika katika muziki wa miaka hiyo, ukiwemo vibao vilivyokuwa maarufu vya Love Me Do na She Loves You.

    Nick Wass anaongoza mradi wa utafutaji wa gitaa hilo la Höfner na ameungana na wanahabari wawili katika kujaribu kusaka "kitendawili kikubwa zaidi katika historia ya muziki wa rock and roll".

    Haijabainika ni nini kilitokea mpaka gitaa hilo kupotea, ambapo kiliwekwa kando baada ya kurekodiwa kwa filamu ya Get Back mnamo 1969.

  6. Kombe la EPL latua Kenya

    EPL in Kenya

    Chanzo cha picha, PCS

    Rais William Ruto amepokea na kulikaribisha kombe la ligi kuu ya England (EPL) nchini Kenya, katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Nairobi.

    Kombe hilo lilisindikizwa na nguli wa soka Jay-Jay Okocha.

    Baada ya kulipokea Rais Ruto alinukuliwa na vyombo vya habari vya ndani akisema: "Ligi kuu (EPL) inaleta msukumo kwa mamilioni ya wanasoka wanaochipukia kote duniani; Afrika, Kenya ikiwa ni miongoni mwao. Ni kivutio kikubwa cha soka".

    Wachezaji kadhaa wa Kenya wamewahi kuchezea ligi hiyo pendwa akiwemo nahodha wa zamani wa Harambee Stars, Victor Wanyama, ambaye alizichezea Southampton na baadaye Tottenham Hotspurs na Divock Origi aliyekipigia Liverpool, mtoto wa nyota wa zamani wa Harambee Stars, Mike Origi.