Malkia alazwa kwenye chumba cha kifalme kabla ya mazishi ya faragha ya familia

Ibada katika uwanja wa Windsor Castle ilikuwa hafla ya mwisho ya umma kabla ya Malkia kuzikwa karibu na mumewe, Mtawala wa Edinburgh.

Moja kwa moja

  1. Tunakomea hapo kwa leo. Kwaheri.

  2. Mazishi umma ya Malkia Elizabeth II ilivyofanyika

    Matukio ambayo tumeshuhudia leo huenda yakarudiwa kwa miongo kadhaa ijayo.

    Huu hapa muhtasari wa kile kilichotokea:

    • Siku ilianza na hitimisho la kipindi cha uongozi wa Malkia, na msafara wa jeneza lake kuelekea Westminster Abbey.
    • Ibada ya mazishi huko Westminster Abbey ilihudhuriwa na karibu watu 2,000 wakiwemo wakuu wengi wa nchi.
    • Msafara mkubwa kisha ulitembeza jeneza la Elizabeth II hadi Wellington Arch: Alama ya kihistoria yenye umuhimu wa ushindi katika historia ya Uingereza.
    • Malkia aliwekwa kwenye gari maalum la kubeba maiti na kuendeshwa hadi Windsor.
    • Msafara wa tatu wa siku ulimuonyesha tena Mfalme na washiriki wengine wa familia ya kifalme wakitembea nyuma ya gari la maiti la Malkia alipokuwa akipelekwa katika Kanisa la St George kwa ibada ya mwisho iliyohudhuriwa na watu 800.
    • Baadaye - saa 19:30 - Familia ya Kifalme itarudi kwenye kanisa kwa hafla ya faragha ambapo Malkia Elizabeth atazikwa kando ya marehemu mumewe, Duke wa Edinburgh.
    • Kipindi cha maombolezo ya kifalme kinaendelea kwa wiki nyingine - hadi mwisho wa tarehe 26 Septemba
  3. Katika Picha: Ibada ya mazishi ya Malkia ilisheheni ishara maalum

    Wabeba mizigo hubeba jeneza la Malkia ndani ya kanisa na chini ya kitovu kabla ya kuliweka kwenye ukumbi, ambapo Familia ya Kifalme iliketi kutazama ibada.

    Chanzo cha picha, PA Media

    Royal Family members at the service included (from left) the Duke of Sussex, Princess Charlotte, Prince George and the Prince of Wales

    Chanzo cha picha, PA Media

    Maelezo ya picha, Wanafamilia wa Kifalme waliokuwa kwenye ibada hiyo ni pamoja na (kutoka kushoto) Duke wa Sussex, PrBinti Mfalme Charlotte, Mwanmfalme George na Mtawala wa Wales.
    Bwana Chamberlain kwa sherehe anavunja fimbo yake ya ofisi na kuiweka kwenye jeneza

    Chanzo cha picha, PA Media

    Maelezo ya picha, Bwana Chamberlain kwa sherehe anavunja fimbo yake ya ofisi na kuiweka kwenye jeneza
    Taji ya Jimbo la Imperial inaonekana kwenye madhabahu ya juu baada ya kuondolewa kutoka kwa jeneza la Malkia na Mnara wa Taji.

    Chanzo cha picha, PA Media

    Maelezo ya picha, Taji ya Jimbo la Imperial inaonekana kwenye madhabahu ya juu baada ya kuondolewa kutoka kwa jeneza la Malkia na Mnara wa Taji.
  4. Matukio ya mazishi ya umma yakamilika

    Ibada ya mazishi ya Malkia sasa imekamilika, huku mpiga vyombo akicheza ala za Prelude na Fugue katika C minor na Johann Sebastian Bach.

    Hiyo inahitimisha ibada ya kujitolea katika Kanisa la St George's Chapel iliyohudhuriwa na karibu watu 800 pamoja na hafla za kitaifa za mazishi ya Malkia Elizabeth II.

    Wajumbe wa Familia ya Kifalme akiwemo Mfalme Charles III sasa watatoka kanisani na kwenda Windsor Castle yenyewe Lakini saa 19:30 jioni hii, Mfalme na ndugu zake watarudi kanisani kwa ajili ya mazishi ya Malkia Atazikwa karibu na marehemu mumewe, Duke wa Edinburgh. Maelezo ya ibada hiyo hayajawekwa wazi, huku Buckingham Palace ikiiita "tukio binafsi la kifamilia".

    Huku hayo yakijiri Mfalme Charles III na mke wake Malkia Camila wanazungumza na Askofu Mkuu wa Canterbury na makasisi nje ya kanisa wanapoondoka kwenye ibada.

  5. Malkia alazwa kwenye chumba cha kifalme

    Mwili wa Malkia umeshushwa kwenye chumba cha kifalme huku mpiga filimbi akipiga kwa huzuni Malkia ameshushwa polepole kwenye chumba cha kifalme kabla ya mazishi yake baadaye katika ibada binafsi ya familia.

    Mchungaji anasoma zaburi na sifa.

    Mfalme wa Silaha wa Garter kisha anatamka mitindo na vyeo vya Malkia - majina tofauti ambayo yalijulikana wakati wa utawala wake.

  6. Katika Picha: Ndani ya Kanisa la St George

    Ndani ya kanisa

    Chanzo cha picha, PA Media

    Kanisani

    Chanzo cha picha, pa

    Kanisani

    Chanzo cha picha, PA Media

    Kanisani

    Chanzo cha picha, PA Media

    fAMILIA YA MALKIA

    Chanzo cha picha, PA Media

  7. Ibada fupi ya kumuaga Malkia inaendelea Windsor muda huu

    IBADA YA MWISHO

    Ibada hii inayofanyika sasa katika Kanisa la St George ilikubaliwa na Malkia kabla ya kifo chake. Itaongozwa na David Conner, Dean wa Windsor.

    Ibada hiyo inaongozwa na Dean wa Windsor, David Conner.

    Maombi pia yatatoka kwa Rector wa Sandringham na Waziri wa Crathie Kirk - kanisa la parokia huko Scotland ambapo Familia ya Kifalme huabudu wakati ikiwa Balmoral.

    Pia kutakuwa na neno kutoka kwa Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby.

    Kwaya inayoimba ni ya Kanisa la St George.

  8. Mfalme na familia ya kifalme yajiunga na msafara

    Mfalme

    Wajumbe waandamizi wa Familia ya Kifalme sasa wamejiunga na msafara huo huku gari la maiti la serikali likikaribia Kanisa la St George.

    Mfalme Charles III, Princess Anne, Wakuu Andrew na Edward, pamoja na Wakuu William na Harry sasa wanatembea nyuma ya gari la maiti.

    Familia ya Kifalme
    Familia
  9. Ni nani wanaohusika katika msafara huu wa mwisho?

    Msafara

    Muundo huu hautofautiani na tulivyoona awali, ingawa ni mdogo kwa kiwango, kwa kuzingatia ukweli kwamba matukio ya mazishi ya siku hiyo yanakuwa ya ndani zaidi.

    Wanaoongoza msafara huo na wanaotembea mbele ya jeneza la Malkia ni washiriki baadhi wa Jeshi la Wapanda farasi na wengine, ikiwemo ngoma za Kikosi cha Scottland na Ireland na wahudumu wa binafsi wa Malkia

    Pembeni ya gari la kubebea maiti tunaona tena wabeba jeneza na hafla ya kusindikiza mwili Nyuma ya jeneza, kuna wanafamilia wa marehemu Malkia, Mfalme Charles III na Prince William, Mkuu mpya wa Wales

    Washiriki wa familia ya kifalme ikiwa ni pamoja na Mfalme mwenyewe watajiunga na maandamano katika eneo la kasri wakati Camilla, Malkia atafuata kwa gari pamoja na Catherine, Princess of Wales, Meghan, Duchess wa Sussex, na Sophie, Countess wa Wessex.

    Washiriki wengine zaidi wa Jeshi la wapanda farasi wanafuatia kwa nyuma.

  10. Mahali pa umuhimu maalum kwa Malkia

    Malkia

    Mazishi ya Malkia yatahitimishwa kwa ibada ya familia baadaye leo kwenye Windsor Castle.

    Ngome hiyo imekuwa ikikaliwa na wafalme 40 kwa karibu miaka 1,000 - na ilikuwa na umuhimu maalum kwa marehemu Malkia katika maisha yake yote.

    Akiwa kijana, Binti Mfalme Elizabeth wa wakati huo alitumwa kwenye kasri hilo wakati wa Vita vya Pili vya Ulimwengu huku London ikikabiliwa na tishio la kulipuliwa.

    Moto ulipozuka mwaka wa 1992, Malkia, aliyesifika kwa ukaidi, alionekana akiwa na hisia kali huku akitazama bila msaada.

    Malkia alitumia makao hayo makubwa kuwakaribisha wafalme wa ng'ambo na wakuu wa nchi katika kipindi chote cha utawala wake mrefu.

    Hivi majuzi, aliifanya kuwa nyumba yake ya kudumu wakati wa janga la coronavirus.

    Windsor
  11. Maelfu ya watu wakusanyika kwenye barabara ya kuelekea Windsor

    Wananchi wamekusanyika kwa maelfu kando ya njia ambayo msafara wa mazishi ya Malkia unaelekea Windsor. Umati wa watu ulitazama gari la serikali likipitia London, huku baadhi ya watu wakirusha maua kuelekea kwenye msafara huo.

    Msafara

    Chanzo cha picha, BB

    WATU
    Msafara
    Msafara
  12. Ni viongozi wapi wa Afrika wanahudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II?

    Viongozi kadhaa wa Afrika ni miongoni mwa mamia ya viongozi wa kigeni waliohudhuria mazishi ya Malkia wa Uingereza Elizabeth II mjini London.

    Takriban watu 2,000 wamekusanyika huko Westminster Abbey kwa mazishi yake ya serikali.

    Viongozi wa Afrika wanaohudhuria mazoshi hayo ni pamoja na Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, William Ruto wa Kenya, Nana Akufo-Addo wa Ghana, Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, Mfalme Letsie III wa Lesotho na Macky Sall wa Senegal, na mwenyekiti wa sasa wa Muungano wa Afrika.

    Pia kuna Paul Kagame wa Rwanda, mwenyekiti wa Jumuiya ya Madola, na Ali Bongo, Rais wa mwanachama mpya zaidi wa Jumuiya ya Madola, Gabon.

    Baadhi ya wanaharakati wa Sudan wamekosoa uamuzi wa kumwalika mtawala wa kijeshi wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.

    Rais wa Kenya William Ruto (aliyesimama nyuma) akiwasili Westminster Abbey
    Maelezo ya picha, Rais wa Kenya William Ruto (aliyesimama nyuma) akiwasili Westminster Abbey
    Rais wa Tanzania Suluhu Samia Hassan (kushoto) na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramapahosa (kulia)
    Maelezo ya picha, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kushoto) na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramapahosa (kulia)
    Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Abdel Fattah al-Burhan (wa pili kushoto)
    Maelezo ya picha, Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Abdel Fattah al-Burhan (wa pili kushoto)
  13. Njia ya mazishi ya Malkia kuelekea Windsor

    Malkia Elizabeth II anakaribia kupelekwa kwenye kasri lake pendwa la Windsor, na njia hiyo inatarajiwa kuwa na umati mkubwa wa watu kutoka kote nchini.

    Malkia Elizabeth II anakaribia kupelekwa kwenye kasri lake pendwa la Windsor, na njia hiyo inatarajiwa kuwa na umati mkubwa wa watu kutoka kote nchini.

    Baada ya kuondoka mnara wa Wellington, karibu na kona ya Hyde Park ya London, gari la kubebea maiti litatumia njia ya Apsley kufika South Carriage Drive, likisafiri magharibi kando ya Hyde Park

    Kisha litaelekea upande wa kushoto kuelekea Lango la Malkia na baadaye kugeuka kulia kuelekea Barabara ya Cromwell

    Hii inakuwa Barabara ya Talgarth (kupitia Hammersmith Flyover) na baadaye (baada ya Chiswick Flyover), Great West Road (A4)

    Njia kisha inapita kwenye Uwanja wa Ndege wa Heathrow na Barabara Kuu ya Kusini Magharibi (A30)

    Inayofuata: Barabara ya Staines (A30), Windsor Road (A308) na Barabara ya Albert ( A308)

    Baada ya lango la Shaw Farm, kutakuwa na msafara ambao unatumia njia maarufu ya kasri ya Long Walk - iliyopangwa kuanza saa 15:10 BST.

  14. Gari lililombeba Malkia laelekea Windsor

    .

    Gari maalum la kubeba maiti laelekea Windsor kwa ibada katika Kanisa la St Georges Chapel saa 16:00 BST.

    Takriban wageni 800 wanatarajiwa - kwa hivyo ni tukio la kiwango kidogo kuliko kile ambacho tumeshuhudia hivi punde huko Westminster.

    Baadaye jioni, Malkia atazikwa katika ibada ya kibinafsi ya familia ambayo itakuwa ya karibu zaidi.

    Gari linapoondoka mnara wa Wellington, washiriki wa gwaride wanatoa heshima ya kifalme na wimbo wa taifa unachezwa tena.

    Mfalme na mke wa Mfalme na washiriki wengine wakuu wa familia ya kifalme sasa watasafiri kwa gari.

  15. Katika picha: Familia ya Kifalme kwenye msafara wa kumuaga Malkia

    .
    .
    .
    .
    .
  16. Jeneza la Malkia lahamishiwa kwenye gari la kubebea maiti

    .

    Sasa shughuli nyingine inafanyika, huku wabebaji wakinyanyua tena jeneza la Malkia kutoka kwenye Gari maalum la Serikali na kuliweka kwenye gari la kubebea maiti.

    Sherehe hiyo inaundwa na kikosi cha kwanza cha Battalion Grenadier.

    Unaweza kufikiria wamekuwa wakifanya mazoezi ya kubeba na kuendesha shughuli hii.

  17. Msafara umefika mnara wa Wellington

    .

    Msafara sasa umefika mwisho baada ya kusafiri kwa takriban dakika 45.

    Kwa hivyo, ni nini umuhimu wa mnara wa Wellington?

    Hapo awali ulijengwa katika miaka ya 1820 kama lango la kasri la Buckingham lakini ulihamishwa hadi mahali lilipo sasa miongo sita baadaye, ikitumiwa kuashiria kushindwa kwa Duke wa Wellington kwa Napoleon.

    Moja ya tukio muhimu huko London, ni Pamoja na sanamu kubwa zaidi ya shaba huko Ulaya - inayoonyesha malaika wa amani.

    .
  18. Kengele kubwa yapigwa kote London huku mizinga ikifyatuliwa huko Hyde Park

    .

    Kengele kubwa yapigwa kote London huku mizinga ikifyatuliwa huko Hyde Park.

    Bado, sauti ya kengele kubwa inasikika katika eneo zima la katikati ya London.

    Inaingiliwa na sauti ya Kikosi cha Mfalme, Kikosi chenye kutumia Farasi cha Kifalme, kikipiga mizinga yao ya bunduki.

    Wao wapo Hyde Park.

  19. Wafanyikazi wamekusanyika nje ya kasri la Buckingham wakati jeneza linapita

    .

    Wafanyikazi wa kasri la Buckingham wamekusanyika mbele ya jengo wakati jeneza la Malkia Elizabeth II likipita katika ukumbusho wa Malkia Victoria.

    Mnara huo wa ukumbusho - ambao una urefu wa mita 25 na umejengwa kwa zaidi ya tani 2,000 za marumaru - uliwekwa mnamo 1901 kuashiria kifo cha nyanya ya Elizabeth.

  20. Malkia apita Mbuga za Kifalme kwa mara ya mwisho

    Msafara

    Msafara huu mkubwa wa jeneza la Malkia unaandamana kati ya Mbuga mbili za Kifalme za London kwenye njia ya kuelekea Wellington Arch.

    Upande wa kaskazini: Green Park, nafasi ya kijani ya ekari 40 iliyofunguliwa na Charles II mnamo 1668.

    Inajumuisha Ukumbusho wa Kanada, uliozinduliwa na Malkia katika 1994, ambayo inawakumbuka Wakanada milioni ambao walitumikia katika Vita viwili vya Dunia.

    Upande wa kusini: Hifadhi ya St James's, ndiyo kongwe zaidi kati ya Mbuga za Kifalme, iliyowahi kutumiwa kwa sherehe na mtangulizi wa Malkia, Elizabeth I.

    Hadi leo, ni sehemu inayopendwa na wakazi wa London na watalii - lakini leo kuna hali ya utulivu.