Marekani haina mipango ya kuuondoa utawala wa Urusi, asema Blinken

Marekani haina mbinu au mipango ya kuondoa uongozi wa Urusi , asema waziri wa Ulizni wa Marekani Antony Blinken alisema.

Moja kwa moja

  1. Mpaka hapa tumefika mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja, Asante

  2. Urusi haitafaulu kuigawa Ukraine na kuwa mataifa mawili , asema mkuu wa jeshi

    s

    Mkuu wa idara ya ujasusi ya Ukraine ameonya kuwa Urusi ina njama za kutumia “mbinu za Korea” kwa Ukraine hii ni baada ya kushindwa kuuteka mji mkuu na kuiangusha serikali halali iliyo madarakani.

    Mkuu huyo wa idara ya ujasusi Jenerali Kyrylo Budanov anasema Urusi inanjama za kuigawanya Ukraine kama vile Korea ilivyogawanyika na kuzaa mataifa mawili ya Korea Kaskazini na Korea Kusini.

    Jenerali Budanov anasema baada ya mshambulizi ya Urusi kushindwa kupata matokeo waliotarajia sasa Rais Vladimir Putin analenga maeneo yalio mashariki pamoja na yale ya kusini mwa Ukraine .

    ‘Anasema ikiwa Putin atafaulu kuunganisha maeneo hayo mawili basi huenda akajaribu kuchora mpaka wa kuimega sehemu hiyo kutoka kwa Ukraine -kwa kiasi fulani ni kama vile ilivyotokea baada ya vita vya Korea.

    Vita hivyo vilizaa Korea Kaskazini na Korea Kusini Lakini Jenerali Budanov anasema mpango huo wa Urusi kamwe hautafaulu.

    • Ukraine na Urusi: Vita ilivyoiweka njia panda Uturuki , mwanachama wa NATO na rafiki wa Putin
    • Fahamu mataifa 9 yenye uwezo mkubwa wa silaha hatari za nyuklia duniani
  3. Rais Macron: Kuongezeka kwa maneno kunaweza kuzuia vita visiishe

    m

    Chanzo cha picha, EPA

    Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaonya dhidi ya kuongezeka kwa maneno maneno juu ya vita vinavyoendelea nchini Ukraine.

    Maelezo hayo ameyatoa siku moja baada ya rais wa Marekani Joe Biden kumuelezea kiongozi wa Urusi Vladimir Putin kama mchinjaji na kusema hapaswi kubaki madarakani.

    Macron aliviambia vyombo vya habari vya Ufaransa kuwa lengo lilikuwa ni kusitisha mapigano nchini Ukraine na kisha kuwaondoa wanajeshi wa Urusi.

    Alisema hili halitawezekana kwa kuongezeka kwa maneno au vitendo.

    Mamlaka ya Marekani imekanusha kuwa Biden alikuwa akitoa wito wa mabadiliko ya utawala nchini Urusi kufuatia maoni yake ambayo hayajaandikwa wakati wa ziara yake nchini Poland.

    Macron amekuwa na mawasiliano na rais wa Urusi katika kipindi chote cha mzozo wa Ukraine na kusema kuwa atazungumza na Putin katika siku mbili zijazo ili kuandaa uondoaji wa raia kutoka mji wa bandari wa Mariupol ulioshambuliwa kwa mabomu.

    m

    Chanzo cha picha, Reuters

    • Zaidi ya Urusi na Ukraine: Mizozo 6 ya kivita ambayo inatokea ulimwenguni
    • Mzozo wa Ukraine: Ni vikwazo gani vilivyowekwa dhidi ya Urusi?
  4. Urusi inalenga kuigawa Ukraine katika sehemu mbili, idara ya kijasusi ya kijeshi ya Ukraine imesema

    mm

    Urusi inajaribu kuigawanya Ukraine katika sehemu mbili ili kuunda eneo linalodhibitiwa na Moscow baada ya kushindwa kuchukua nchi nzima, mkuu wa kijasusi wa kijeshi wa Ukraine amesema.

    Shirika la habari la Reuters linamripoti Kyrylo Budanov akisema katika taarifa yake kwamba Urusi inalenga "kuunda Korea Kaskazini na Kusini nchini Ukraine," na kuongeza kuwa hivi karibuni nchi yake itaanzisha vita vya msituni katika eneo linalothibitiwa na Urusi.

    • Vita vya Ukraine: Urusi inaweza kutumia silaha za nyuklia ikiwa itakumbwa na tishio la kuangamizwa kabisa: Kremlin
    • Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  5. Katika Picha: Maelfu ya Warusi waandamana Prague

    mm

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelfu ya raia wa Urusi eneo la Prague waliandamana katika jiji hilo wakipeperusha bendera na kushikilia mabango ya kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

    Wanaharakati kadhaa walimwaga rangi nyekundu, ikiashiria damu ya wale waliouawa katika vita hadi sasa, kwenye ngazi za ubalozi wa Urusi huko Prague.

    Wakiwa wamebeba mabango ya kumpinga Putin yaliyosema "Mzuieni Putin" na "Sitisha vita", waandamanaji walitembea katikati ya mji mkuu wa Czech.

    mm

    Chanzo cha picha, Getty Images

    mm

    Chanzo cha picha, Getty Images

    • Ukraine na Urusi: Ukraine yadai kuuawa kwa Jenerali mwingine wa Urusi
    • Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  6. Majenerali saba wa Urusi wamefariki Ukraine, asema afisa wa nchi za Magharibi

    mm

    Chanzo cha picha, Reuters

    Jenerali wa Urusi Luteni Jenerali Yakov Rezantsev, ambaye inasemekana alifariki Jumamosi, ndiye afisa wa cheo cha juu zaidi kuuawa, kulingana na wizara ya ulinzi ya Ukraine.

    Wataalamu wanasema ari ya chini kati ya wanajeshi wa Urusi imewalazimu maafisa wakuu kuwa mstari wa mbele.

    Mwandishi wetu wa masuala ya usalama Frank Gardner anasema vifo vilivyoripotiwa huenda vilitokana na majenerali kulazimika kuwa mbele katika mapigano ili kuwaondoa wanajeshi wao kutokana na kuzomewa.

    Mafumo wa kijeshi ya Kirusi huwa unasubiri amri kutoka juu.

    Afisa mstaafu wa Jeshi la Uingereza alisema vifo vya majenerali hao pia kumeonesha "mafanikio ya kiwango cha juu ambao unaweza kudhalilisha mfumo wa kijeshi wa Urusi".

    • Urusi na Ukraine: Je,Kwanini Moscow imeshindwa kudhibiti anga ya Ukraine licha ya kuwa na mojawapo ya jeshi Zaidi duniani la angani?
    • Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  7. Jimbo la Ukriane kupiga kura ya maoni ya kujiunga na Urusi

    Jimbo linaloungwa mkono na Urusi na ambalo limejitenga na kujiita Luhansk People's Republic lililo mashariki mwa Ukraine hivi karibuni linaweza kupiga kura ya maoni ya kuamua kujiunga na Urusi , kiongozi anaepigia jimbo hilo kujitenga Leonid Pasechnik amesema hayo, hii ni kwa muujibu wa shirika la habari (RIA).

    Jimbo hilo linaloungwa mkono na Urusi Mapema mwezi wa Februari Rais Vladimir Putin alitangaza kuwa anatambua uhuru wa majimbo mawili yalio kusini-mashariki mwa Ukraine ambayo yalijitenga.

    • Fahamu juhudi za kuwezesha ndege kutumia haidrojeni badala ya mafuta
    • Mzozo wa Ukraine: Hatua kali za usalama zinazotumiwa kumlinda Rais Putin
  8. Marekani haina mipango ya kuuondoa utawala wa Urusi, asema Blinken

    m

    Chanzo cha picha, Reuters

    Marekani haina mbinu au mipango ya kuondoa uongozi wa Urusi , asema waziri wa Ulizni wa Marekani Antony Blinken alisema.

    Katika hotuba yake mjini Warsaw siku ya Jumamosi , Rais Joe Biden alisema kuwa rais wa Urusi , Vladimir Putin, "hawezi kusalia madarakani".

    "Nafikiri rais , pamoja na Ikulu ya White House, ameelezea hili jana usiku , kwa njia rahisi ni hivi ,Rais Putin hawezi kuwezeshwa kuendeleza vita au kuishambulia Ukraine au yeyote yule ,Blinken amesema siku ya Jumapili , akiwa ziara yake Israel.

    "Kama unavyofahamu na kama mulivyotusikia tukisema mara kadhaa , hatuna mipango ya kubadilissha Utawala wa Urusi, au mahali popote pale..

    " Kwa hali hii , na kama ilivyo mara zote, nijukumu la watu wa taifa hilo, ni jukumu la raia wa Urusi wenyewe ," Blinken ameongezea.

    • Mzozo wa Ukraine: Marekani inapeleka silaha gani Ukraine na kwa kiasi gani
    • Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
  9. Rais wa Marekani: Putin hawezi kubaki madarakani

    m

    Maoni ya Rais wa Marekani Joe Biden kwamba rais wa Urusi Vladimir Putin "hawezi kubaki madarakani" yamesababisha ukosoaji mkubwa kutoka kwa mwanadiplomasia mkongwe wa Marekani Richard Haass.

    Maoni hayo "yalifanya hali kuwa mbaya zaidi na hatari zaidi," aliandika kwenye kurasa yake ya tweeter Bw Haass, ambaye ni rais wa Baraza la Mahusiano ya Kigeni la Marekani.

    "Hii ni dhahiri," aliongeza. "tofauti na kutengua uharibifu huo, lakini ninapendekeza wasaidizi wake wakuu wawafikie washirika wake na kuweka wazi kuwa Marekani iko tayari kukabiliana na serikali hii ya Urusi."

    Bw Haass alirejea kwenye mada hiyo baada ya Ikulu ya White House kuhitimisha matangazo ya Rais Biden, akisema: "Ikulu ya White House ikitoa wito wa mabadiliko ya serikali ya Putin.

    "Putin ataona kama uthibitisho wa kile anachoamini wakati wote. Ukosefu mbaya wa nidhamu ambao una hatari ya kuongeza wigo na muda wa vita."

    • Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • Urusi na Ukraine: Hujui kinachokuja - Joe Biden amwambia Putin
    • Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
  10. Habari...karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya BBC Swahili leo ikiwa tarehe 27.03.2022