Tazama:Kisiwa kipya chaibuka baada ya mlipuko wa volkeno huko Japan
Picha za droni kutoka Japan zimenasa wakati adimu, wakati mlipuko wa ulipozua kisiwa kipya.
Mlima wa volkeno wa chini ya bahari ambao haukutajwa jina ulianza milipuko yake ya hivi punde tarehe 21 Oktoba.
Mapema mwezi wa Novemba, kisiwa kilikuwa na upana wa takribani mita 100 (futi 328) na urefu wa mita 20 (futi 66) juu ya bahari, kulingana na Yuji Usui, mchambuzi kutoka kitengo cha volkeno cha Shirika la Hali ya Hewa la Japan.
Aliongeza kuwa kisiwa kipya, nusu maili kutoka pwani ya kusini ya kisiwa cha Iwo Jima, tayari kilikuwa kimepungua kwa sababu ya uundaji wake "uliobomoka" ulifanya kiwe katika hatari ya mmomonyoko wa ardhi.

