Israel - Gaza: Roketi zarushwa juu ya anga ya mji mkuu wa Israel Tel Aviv huku watu wakikimbilia hifadhi

Maelezo ya video, Tazama Video: Roketi zarushwa juu ya anga ya mji mkuu wa Israel Tel Aviv huku watu wakikimbilia hifadhi

Raia wa Israel katika mji mkuu wa Tel Aviv walionekana wakikimbilia hifadhi baada ya ving'ora vya onyo kusikika.

Hamas ilisema imerusha "msururu wa makombora" juu ya mji mkuu wa Tel Aviv na Jerusalem.

Katika picha zilizoonekana kwenye mitandao ya kijamii, roketi zilionekana angani juu ya mji huo.

Ni tukio la hivi karibuni katika kuongezeka kwa mvutano kati ya Israel na Hamas.

Mapema siku hiyo, video iliyochambuliwa na BBC ilionekana kuonyesha shambulizi la anga kwenye kivuko cha Rafah kwenye mpaka wa Misri, ambapo ilitarajiwa usitishaji mapigano ungefanyika kwa raia wa Gaza na wale wa kigeni kuondolewa.