Tazama wakati tetemeko kubwa la ardhi lilipokumba Morocco

Maelezo ya video, Tazama: Tetemeko kuu la ardhi la ukubwa wa 6.8 laikumba Morocco

Tetemeko la ardhi la kipimo cha 6.8 limekumba eneo la kati la Morocco na kuua takriban watu 296, wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo inasema.

Tetemeko hilo lilitokea saa tano na dakika kumi na moja usiku saa za ndani (22:11 GMT). Kulikuwa na mshtuko wa 4.9 dakika 19 baadaye.

Kitovu hicho kilikuwa katika Milima ya Juu ya Atlas, 71km (maili 44) kusini-magharibi mwa Marrakesh, kwa kina cha kilomita 18.5, Utafiti wa Jiolojia wa Marekani ulisema.

Picha hizi zinazotangazwa kwenye vyombo vya habari vya serikali zinaonyesha uharibifu huko Marrakesh baadaye.