Urusi yatuma ujumbe wake wa kwanza katika mwezi baada ya miaka 47

Maelezo ya video, Tazama: Urusi yatuma ujumbe wake wa kwanza katika mwezi baada ya miaka 47

Urusi ilizindua ujumbe wake wa kwanza kwenda katika sakafu ya mwezi katika kipindi cha karibia nusu karne ili kuwa taifa la kwanza kutua kusini mwa eneo hilo.

Roketi inayoelekea katika eneo hilo iliruka kutoka eneo la Vostochny Cosmodrome mashariki mwa Urusi. Ncha ya kusini ya mwezi inadaiwa kumiliki maji.

Ujumbe huo wa Urusi unashindani na ule wa India ambao ulituma roboti yake mwezi uliopita ambayo tayari inazunguka katika mwezi.

Mkuu wa anga za juu wa Urusi aliambia Interfax kwamba roboti hiyo inatarajiwa kurudi tartehe 21 mwezi Agosti.

Kufikia mapema wiki hii chombo cha anga za mbali cha India kilitarajiwa kufika katika sakafu hiyo tarehe 23 Agosti.