Saratani: 'Nilienda kwa waganga kabla ya kwenda kutibiwa hospitali'
Imani potofu katika jamii zinachangia kuongezeka kwa wagonjwa wa saratani haswa wanawake katika ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.
Wataalamu wa tiba ya saratani wanasema kuwa wagonjwa wengi hufika hospitalini wakiwa kwenye hatua ya juu kwa maana ya kuchelewa tiba.
Kila mwaka Hospitali ya ukanda huo, Bugando iliyopo mkoani Mwanza imekuwa ikipokea wastani wa wagonjwa 400 wa saratani ya kizazi kwa mwaka ambao ni asilimia 30% ya wagonjwa wapya wanaofika katika hospitali hiyo kupata tiba.
Mwandishi wa BBC @lasteck2023 alifika mkoani Mwanza na kuandaa taarifa hii.
Video: Nicholaus Mtenga