Kosovo: Waziri mkuu arushiwa maji bungeni kabla ya vita kuzuka kati ya wabunge

Maelezo ya video, Tazama: Vinywaji vyarushwa wakati rabsha zikizuka katika bunge la Kosovo

Wabunge walirushiana makonde baada ya Waziri mkuu wa Kosovo kurushiwa maji na picha yake kukatwa na mbunge wa upinzani ndani ya bunge la Kosovo.

Ghasia hizo zilizuka kufuatia mjadala mkali wa siku tatu kuhusu machafuko kaskazini mwa Kosovo.

Waziri Mkuu Albin Kurti alikuwa akihutubia bunge wakati ghasia hizo zilipozuka