Tazama: Jengo laporomoka kutokana na mafuriko China

Maelezo ya video, Tazama: Jengo laporomoka kutokana na mafuriko ya China

Mamlaka ya China imeonya kuhusu "majanga mengi " mwezi ujao, huku mvua kubwa ikinyesha katika maeneo ya nchi.

Tahadhari ya hali ya hewa imetolewa kwa maeneo makubwa ya kati na kusini magharibi mwa China na maelfu ya watu wamehamishwa.

Jengo liliporomoka na mafuriko huko Chongqing. Wakati huohuo, katika jimbo la Henan, waokoaji walirekodiwa wakiwaokoa watu waliokuwa wamenaswa juu ya gari katikati ya mkondo wa maji.