Tazama: Meya wa Mexico akifunga ndoa na mamba katika tambiko la mavuno
Meya wa mji mdogo wa Mexico amefunga ndoa na mamba katika tambiko la zamani la ustawi. Alionekana akimbusu mnyama huyo, ambaye kinywa chake kulikuwa kimefungwa
Mamba huyo mwenye umri wa miaka saba, aliyepewa jina la utani la 'binti wa kifalme', anadhaniwa kuwakilisha mungu anayehusishwa na ardhi. Ndoa yake kwa kiongozi wa eneo hilo inaashiria kuunganishwa kwa wanadamu na Mungu.
Utamaduni huo unakisiwa ulianza karne nyingi kwa jamii za kiasili za Chontal na Huave katika jimbo la Oaxaca. "Ni muungano wa tamaduni mbili. Muungano wa Wahuave na Wachontales," Meya Victor Hugo Sosa aliwaambia waandishi wa habari.
Olivia Perez ,mwanamke aliyesimamia shughuli ya kumpamba mamba huyo kwa mavazi ya 'harusi' anasema :'Kwetu sisi mamba anawakilisha vitu vingi kwa sababu ni malkia.Binti mfalme anayeleta maji,mavuno mazuri na mvua'

