Video: Tazama wakati bosi wa mafia Matteo Messina Denaro alipokamatwa

Maelezo ya video, Tazama: Wakati Matteo Messina Denaro alipokamatwa huko Palermo, Sicily

Bosi wa mafia anayesakwa zaidi nchini Italia Matteo Messina Denaro amekamatwa huko Sicily baada ya kutoroka kwa miaka 30.

Video inamuonyesha akiongozwa hadi kwenye gari kutoka kliniki ya kibinafsi huko Palermo.

Anadaiwa kuwa bosi wa mafia maarufu wa Cosa Nostra.

Matteo Messina Denaro alihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2002 kwa makosa ya mauaji mengi.