Sababu za Familia ya Magdalena kuficha maradhi ya Fibroids
Mwogeleaji Magdalena Moshi ambaye amewakilisha Tanzania mara tatu kwenye michezo ya Olimpiki anataka utamaduni wa kukaa kimya kuhusu maswala ya afya ya uzazi barani Afrika ukomeshwe.
Hii ni baada ya kufanyiwa upasuaji wa dharura ambapo alitolewa kilo 3.7 za uvimbe kwenye mfuko wa uzazi, yaani fibroids.
Ni baada ya matitabu tu Magdalena, 32, aliweza kugundua maradhi hayo yamewaathiri wanawake wengine katika familia na hata kusababisha vifo lakini hakufahamishwa kwa sababu ni mwiko katika jamii yao kuzungumzia wazi maswala ya afya ya uzazi.
BBC Michezo Afrika ilimtembelea Magdalena mjini Adelaide, Australia anakoishi kusikia hadithi yake.