Tazama: Vifaru vya Urusi vilivyoachwa kwenye eneo lililochukuliwa tena la Ukraine

Maelezo ya video, Tazama: Ukraine yakamata vifaru vya Urusi vilivyotelekezwa

Video inaonekana kuonyesha vifaru vya Urusi vilivyotelekezwa na vifaa vya kijeshi ambavyo vimekamatwa na wanajeshi wa Ukraine.

Jeshi la Ukraine linasema kuwa vikosi vyake vimechukua tena eneo kutoka kwa Urusi, na kufanya kuwa mafanikio yake ya kwanza katika kipindi cha miezi kadhaa.

Miji ya Izyum na Kupiansk, ambayo ni vitovu muhimu vya usambazaji wa vikosi vya Urusi huko Donbas, ilichukuliwa Jumamosi.

Mashambulizi ya Ukraine huko Kherson kusini yanaendelea.

Urusi bado inashikilia karibu moja ya tano ya nchi hiyo, lakini kujisalimisha kwa Urusi kunaonekana na wachambuzi wengi kama mafanikio muhimu sana kwa Ukraine.