Mwanajeshi mtoto wa zamani wa Liberia: 'Narudisha hisani kwa jamii'
Mwanajeshi mtoto wa zamani Morris Matadi anapigania kubadili mustakabali wa Libeŕia kwa kuanzisha shule ya watoto ambao wazazi wao, pia ni wanajeshi watoto wa zamani wanatumia madawa ya kulevya au wanalala mitaani.
Kwa Morris, shule ni fursa ya kurudisha hisani kwa jamii yake miaka 30 baada ya mzozo kumalizika na kuwapa kizazi kipya matumaini ya siku zijazo.