'Tulipata habari mtu aliyekuwa anawania urais Marekani alikuwa amezaliwa Kenya'
Huku Idhaa ya BBC Swahili ikiidhimisha miaka 65 ya kuwepo hewani, Muliro Telewa ambaye pia anafikisha miaka 65 mwaka huu, ameifanyia kazi Idhaa ya BBC kwa miaka 25 kabla ya kustaafu.
Mwanahabari wetu @judith_wambare alimtembelea kwake nyumbani mjini Eldoret katika kaunti ya Uasin Gishu nchini Kenya na kutuandalia filamu hii.