‘Siwezi kuona lakini napenda kutangaza mpira’
Kutana na mwanafunzi wa Darasa la tano Shaffih Seleman asiye na uwezo wa kuona lakini anapenda kutangaza mpira.
Ni kwa vipi anatangaza na ilikuwaje mpaka akatamani kutangaza mpira ilhali hawezi kuona?
Mwandishi wa BBC @frankmavura alimtembelea kijana Shaffih katika shule ya mseto Uhuru, Ilala jijini Dar es Salaam kujionea umahiri wa kijana huyu.