‘Zama Zama: Wahamiaji wanaotafuta riziki kwa njia hatari kwenye migodi Afrika Kusini

Maelezo ya video, ‘Zama Zama: Wahamiaji wanaotafuta riziki kwa njia hatari kwenye migodi Afrika Kusini

BBC Africa Eye inakutana na wahamiaji ambao wanahatarisha kila kitu kwenda chini ya ardhi katika machimbo ya dhahabu yaliyotelekezwa nchini Afrika Kusini.

Kila siku wanaenda kazini, hawajui kama watarudi nyumbani wakiwa hai.

Umaskini unawalazimisha chini ya ardhi kutafuta dhahabu. Wengine watakamatwa kwa uchimbaji haramu wa madini.

Wengine watakufa lakini wanalazimika kufanya kazi hii ili kujikimu kimaisha.