Ngono kwa ajili ya maji: Wanawake na wasichana wanalipia huduma hii kwa gharama gani?

Maelezo ya video, Ngono kwa ajili ya maji

Mji mkuu wa Kenya, Nairobi, kwa sasa unakabiliwa na uhaba wa maji kutokana na sababu kama vile mabadiliko ya hali ya hewa na vifaa vya maji kuzeeka.

Wakaazi katika jamiivitongoji duni kama Kibera hulipa wachuuzi wa kibinafsi ili kupata maji, kumaanisha kuwa sasa wanadhibiti usambazaji na upatikanaji wa maji katika jamii. Hata hivyo, gharama ambayo wanawake na wasichana wanalipa ni kubwa mno zaidi ya kulipa pesa tu.

Video Producers: Njoroge Muigai, Azeezat Olaoluwa, Ann-Marie Yiannacou, Michael Onyiego