Siku ya Ijumaa Kuu na siku kuu ya Pasaka zina maana gani?

Maelezo ya video, Fahamu maana ya siku ya Ijumaa Kuu na siku kuu ya Pasaka

Ijumaa kuu ni siku ambayo Wakristo duniani kote wanakumbuka kuteswa kwa Yesu kristo miaka mingi iliyopita.

Mchungaji wa Kanisa Kuu la Kilutheri Tanzania Usharika wa Kijitonyama Dkt. Eliona Kimaro anawakumbusha Wakristo duniani kote juu ya umuhimu wa siku hii katika imani ya Kikristo kama alivyozungumza na Scolar Kisanga.

Picha na Frank Mavura.