Ukame Somalia: 'Chukueni hatua sasa au watoto 350,000 watakufa'

Maelezo ya video, Ukame Somalia: 'Chukueni hatua sasa au watoto 350,000 watakufa'

Huku Somalia ikikabiliwa na kile ambacho wataalam wanakiita ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika muongo mmoja, watoto wanabeba mzigo mkubwa zaidi.

Wazazi wanatatizika kuwalisha, huku karibu nusu ya watu walio chini ya umri wa miaka mitano nchini humo wakikabiliwa na utapiamlo ifikapo Juni.

Nimco Abdi anamweka kwa upole mtoto wake wa kike wa miezi sita kwenye beseni la plastiki lililowekwa kwa kamba za mkonge.

Yeye ni mdogo sana kwa umri wake. Macho yake yamezama, mifupa imetoka nje na ngozi yake imekunjamana na kupauka. Anaangua kilio dhaifu, kisichosikika huku Nimco akiinua mgongo wake.

Mercy Juma na taarifa zaidi