Africa Eye: Wachungaji wakorofi, miujiza ya uongo na mauaji
Kwa mamilioni ya Wakristo wa Afrika, Ukristo ni nguzo ya maisha yao. Lakini mlipuko wa wachungaji wakorofi wanaotumia imani ya wafuasi wao kwa maslahi ya kibinafsi wamewafanya wengi kutilia shaka imani yao.
Ripota wa Africa Eye Peter MacJob alisafiri hadi Uganda kukutana na familia ambazo zimepata hasara kubwa kutoka kwa wachungaji wakorofi, na wale ambao wameacha dini kabisa.
Kutokana na walaghai wanaocheza shere na imani ya mamilioni ya watu, ni nini mustakabali wa waumini nchini Uganda na kote barani Afrika?

