Mwaka mmoja tangu achukue mamlaka, je Rais Samia amefuata nyayo za Magufuli?
Mwishoni mwa juma hili itakuwa ni mwaka mmoja tangu Samia Suluhu Hassan ambae alikuwa Makamu wa rais wa Tanzania aliposhika hatamu za nchi hiyo kufuatia kifo cha mtangulizi wake hivyo kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza taifa hilo.
Aliapishwa, katikati ya kipindi cha janga la corona, mwezi Machi baada ya mtangulizi wake John Magufuli alipofariki ghafla alipokuwa madarakani. Na mara tu aliposhika uongozi , alinukuliwa akisema kuwa ‘‘yeye na Magufuli walikuwa kitu kimoja.’’
Lakini hatua zake Katika muda wa mwaka uliopita imedhihirisha mambo tofauti. Mwanahabari wa BBC Salim Kikeke alifanya mahojiano na Rais Samia kubaini mtazamo wake kwa miezi 12 iliyopita. Jiunge na Dira ya Dunia redio kwa mahojiano marefu ya Rais Samia mwendo wa saa kumi na mbili na nusu jioni ya leo na vilevile katika Dira TV saa tatu usiku.