Msanii wa TikTok Moya David1 anavyotumia usanii 'kuponya mioyo ya watu'

Maelezo ya video, Msanii wa TikTok Moya David1 anavyotumia usanii 'kuponya mioyo ya watu'

David Muchiri, almaarufu kama Moya David1 amepata umaruufu kupitia michezo yake ya uchokozi na pia kutumbuiza jamii na kuwapa maua na chokolet na hata pesai, lengo lake anasema ni “kuponya mioyo ya watu”.

Huku akiwa na karibu na wafuasi milioni moja wanaomfuata katika mtandao wa TikTok na michezo yake kupendwa na zaidi ya watu milioni 10, Moyes amekuwa jina tajika katika mitandao ya kijamii.

Mwanahabari wetu @judith_wambare alikutana naye, na kufahamu zaidi kuhusu maisha ya Moyes na changamoto anazopitia ili kuweka tabasamu katika nyuso za watu.